CHADEMA Inaongoza nchi Indirectly

PHILEMAN

Member
Oct 22, 2011
44
10
Sura ya 1 Ibara ya 1(4) ya Rasimu ya Katiba Mpya inasema ''Tanganyika itaitwa jimbo la Tanganyika na Zanzibar itaitwa jimbo la Zanzibar na kila jimbo litaongozwa na Gavana'' Hii ni sera ya CHADEMA ya Majimbo. Cha Kushangaza Mwenyekiti wa Tume alisema Tume haijapendekeza Serikali ya Majimbo. Nimeamini CHADEMA ndio inaongoza nchi indirectly.
 
hata hii katiba mpya ilikuwa sera ya CDM tena ya kwanza kabisa katika ilani yao ya uchaguzi ya 2010. Inaruhusiwa copy /paste cha msingi tu mambo yawe mazuri kwa manufaa ya watanzania wote.
 
Sura ya 1 Ibara ya 1(4) ya Rasimu ya Katiba Mpya inasema ''Tanganyika itaitwa jimbo la Tanganyika na Zanzibar itaitwa jimbo la Zanzibar na kila jimbo litaongozwa na Gavana'' Hii ni sera ya CHADEMA ya Majimbo. Cha Kushangaza Mwenyekiti wa Tume alisema Tume haijapendekeza Serikali ya Majimbo. Nimeamini CHADEMA ndio inaongoza nchi indirectly.
Hata katiba mpya yenyewe haikuwepo kwenye Sera za CCM ndiyo maana hata waziri wa sheria yule mwanamama sijui anaitwaga nani alishatoa tamko la Serikali hadharani kwamba Serikali ya CCM haina mpango wa kuandika katiba mpya kwani iliyopo haina matatizo lakini baadaye wakaona sera zao ni za kipumbavu ikabidi warudi nyuma waangalie sera za Chadema then Rais akaamua huu mchakato uanze mara moja.

Via Mobile
 
Haijawahi tokea chama cha upinzani makini kama cdm hapa nchini,mnaosema cjui hata nccr enzi za mrema ilikuwa kama cdm mnaota ndoto za mchana na hata cuf haijawahi ifikia cdm labda kwa zenji,bahati nzuri since then nilkuwepo,ushauri mwingi wa cdm unafanyiwa kazi na serikali hii indirect,pia kila linaloanzishwa na cdm na ccm wanaiga,while kipindi kile ccm haikuwahi kuiga chochote toka vyama vikubwa kama nccr na cuf na wala haikuwa kukosa usingizi kama inavyokoseshwa na cdm.

slaa leo akiwa morogoro kesho kutwa nape na kinana wako moro,sugu akiwika mbeya kesho kutwa wako hapo,sasa enzi za cuf na nccr haya yalitokea? think
 
Hii Nchi inaongozwa na CDM kwasababu muda mrefu unatumiwa na viongozi wa CCM kuiongelea CDM badala ya maendeleo
 
hapo imeongoza je sasa kwa hiyo watu waliotoa maoni yao yakakubalika, pia nao wanaongoza serikali au??
 
Sura ya 1 Ibara ya 1(4) ya Rasimu ya Katiba Mpya inasema ''Tanganyika itaitwa jimbo la Tanganyika na Zanzibar itaitwa jimbo la Zanzibar na kila jimbo litaongozwa na Gavana'' Hii ni sera ya CHADEMA ya Majimbo. Cha Kushangaza Mwenyekiti wa Tume alisema Tume haijapendekeza Serikali ya Majimbo. Nimeamini CHADEMA ndio inaongoza nchi indirectly.

mkuu, mbona unapotosha? soma hapa chini
SURA YA KWANZA
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
SEHEMU YA KWANZA
MIPAKA, ALAMA, LUGHA, UTAMADUNI NA TUNU ZA TAIFA
Jamhuri ya
Muungano 1.-(1) Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Shirikisho lenye
mamlaka kamili ambayo imetokana na Muungano wa nchi mbili za
Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ambazo kabla
ya Hati za Makubaliano ya Muungano ya mwaka 1964 zilikuwa nchi
huru.
(2) Jamhuri ya Muungano ni Shirikisho la kidemokrasia
linalofuata mfumo wa vyama vingi vya siasa, usawa wa binadamu,
kujitegemea, utawala wa sheria na kuheshimu haki za binadamu.
(3) Hati ya Makubaliano ya Muungano iliyorejewa katika Ibara
ndogo ya (1), ndio msingi mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
na Katiba hii, kwa kadri itakavyorekebishwa, itakuwa ni mwendelezo wa
Makubaliano hayo.
Eneo la
Jamhuri ya
Muungano
2. Eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo lote la Tanzania Bara
ikijumuisha sehemu yake ya bahari na eneo lote la Zanzibar ikijumuisha
sehemu yake ya bahari.
Alama na Siku
Kuu za Taifa 3.-(1) Alama za Taifa ni:
(a) Bendera ya Taifa;
(b) Wimbo wa Taifa; na
(c) Nembo ya Taifa,
kama zitakavyoainishwa katika sheria itakayotungwa na Bunge.
(2) Siku Kuu za Kitaifa zitakuwa ni:
(a) Siku ya Uhuru wa Tanganyika, itakayoadhimishwa tarehe 9
Disemba;
(b) Siku ya Mapinduzi ya Zanzibar, itakayoadhimishwa tarehe 12
Januari;
(c) Siku ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar,
itakayoadhimishwa tarehe 26 Aprili; na
(d) Siku Kuu nyingine zita
ri ya Muungano itaenzi na kuzingatia Tunu za Taifa
zifuatazo:
(a) utu;
(b) uzalendo;
(c) uadilifu;
(d) umoja;
(e) uwazi;
(f) uwajibikaji; na
(g) lugha ya Taifa.
SEHEMU YA PILI
MAMLAKA YA WANANCHI, UTII NA HIFADHI YA KATIBA
Mamlaka ya
wananchi 6. Jamhuri ya Muungano ni nchi inayofuata misingi ya
demokrasia inayozingatia haki ya kijamii, na kwa hiyo:
(a) wananchi ndio msingi wa mamlaka za nchi, na Serikali
itapata madaraka na mamlaka yake kutoka kwa wananchi
ambao kwa umoja na ujumla wao wanaimiliki na kuipatia
Katiba hii uhalali;
(b) lengo kuu la Serikali litakuwa ni maendeleo na ustawi wa
wananchi;
(c) Serikali itawajibika kwa wananchi; na
(d) wananchi watashiriki katika shughuli za Serikali kwa
mujibu wa masharti ya Katiba hii.
Watu na
Serikali 7.-(1) Muundo wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano na vyombo
vyake, katika uendeshaji na utekelezaji wa shughuli zake utazingatia
azma ya kukuza umoja wa kitaifa na kudumisha heshima ya Taifa.
(2) Kwa madhumuni ya masharti ya Ibara ndogo (1), mamlaka
ya nchi na vyombo vyake vinawajibika kuelekeza sera na shughuli zake
zote kwa lengo la kuhakikisha kwamba:
(a) utu na haki nyingine zote za binadamu zinaheshimiwa na
kuthaminiwa;
(b) sheria za nchi zinasimamiwa na kutekelezwa;
(c) Serikali itahakikisha kuwa shughuli zinazofanywa
zinatekelezwa kwa njia ambazo zitahakikisha kwamba
utajiri wa Taifa unaendelezwa, unahifadhiwa na
unatumiwa kwa manufaa ya wananchi wote kwa jumla na
pia kuzuia mtu kumnyonya mtu mwingine;
(d) ardhi ikiwa rasilima
u, heshima na haki nyingine zote za binadamu
zinahifadhiwa na kudumishwa kwa kuzingatia mila na
desturi za kitanzania na kwa kufuata mikataba mbalimbali
iliyoridhiwa na Jamhuri ya Muungano;
(h) mamlaka za nchi zinatoa fursa na haki zilizo sawa kwa
wananchi wote, wanawake na waume, bila ya kujali rangi,
kabila, nasaba, dini au hali ya mtu;
(i) aina zote za dhulma, vitisho, ubaguzi, unyanyasaji,
rushwa, uonevu au upendeleozinaondolewa nchini;
(j) utajiri wa rasilimali na maliasili za Taifa unaelekezwa
katika kuleta maendeleo, kuondoa umaskini, ujinga na
maradhi; na
(k) nchi inatawaliwa kwa kufuata misingi ya demokrasia na
kujitegemea.
Mamlaka na
utii wa Katiba 8.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya Katiba za Washirika wa
Muungano kwa mambo yasiyo ya Muungano, Katiba hii itakuwa sheria
kuu katika Jamhuri ya Muungano.
(2) Mtu yeyote, chombo, taasisi, jumuiya na wakala wowote wa
mamlaka ya nchi na mamlaka binafsi zinao wajibu wa kuzingatia
masharti ya Katiba hii na kuyatii.
(3) Sheria yoyote, mila, desturi au uamuzi wowote wa chombo
cha dola, ofisa wa Serikali au mtu binafsi ni sharti ufuate na kuendana na
masharti yaliyomo kwenye Katiba hii na kwamba, sheria, mila, desturi
au uamuzi wowote ambao hautawiana au kwenda sambamba na masharti
ya Katiba hii utakuwa batili.
Hifadhi ya
Katiba 9.-(1) Mtu au kikundi cha watu hakitachukua au kushikilia
mamlaka ya nchi isipokuwa kwa mujibu wa Katiba hii.
(2) Kitendo chochote kinachokiuka masharti ya Ibara ndogo ya
(1) ni batili na ni kitendo cha uhaini kama itakavyoelezwa katika sheria
za nchi.
(3) Kwa madhumuni ya kuhifadhi masharti ya Ibara ndogo ya (1)
na (2), Serikali itaweka utaratibu wa kuisambaza Katiba hii kwa
wananchi na kuiweka katika mitaala ya elimu ili kuwezesha wananchi
kuifahamu, kuilinda na kuitii.
 
mkuu, kwanza ibara ya kwanza haina kipengele cha 4. ina vipengele vitatu tu
 
Hata katiba mpya yenyewe haikuwepo kwenye Sera za CCM ndiyo maana hata waziri wa sheria yule mwanamama sijui anaitwaga nani alishatoa tamko la Serikali hadharani kwamba Serikali ya CCM haina mpango wa kuandika katiba mpya kwani iliyopo haina matatizo lakini baadaye wakaona sera zao ni za kipumbavu ikabidi warudi nyuma waangalie sera za Chadema then Rais akaamua huu mchakato uanze mara moja.

Via Mobile

unatupotosha mkuu kwani sote tunafahamu ni jinsi ganinrais alivyoplay role kuhakikisha kuwa tanzania inakuwa na katiba mpya
 
sura ya 1 ibara ya 1(4) ya rasimu ya katiba mpya inasema ''tanganyika itaitwa jimbo la tanganyika na zanzibar itaitwa jimbo la zanzibar na kila jimbo litaongozwa na gavana'' hii ni sera ya chadema ya majimbo. Cha kushangaza mwenyekiti wa tume alisema tume haijapendekeza serikali ya majimbo. Nimeamini chadema ndio inaongoza nchi indirectly.
acha uongo iyo rasimu haisemi hivyo
 
unatupotosha mkuu kwani sote tunafahamu ni jinsi ganinrais alivyoplay role kuhakikisha kuwa tanzania inakuwa na katiba mpya

Sasa mbona kwenye Ilani ya chama chake cha ccm , hakuna andiko kuhusiana na Katiba Mpya ? Bali ukiondoa Unafiki wako utagundua kuwa hiyo imo kwenye Ilani ya uchaguzi ya Cdm ! Sasa wadau wakisema Jk anatekeleza ilani ya Cdm utabisha kivipi ?
 
vijana wa bar ya vichaa mna tabu sana, hivi hiyo katiba umeisoma peke yako??? au kipengele hicho umekiona peke yako??? hakuna mahali pameandikwa jimbo la tanganyika wala jimbo la znz..ni uzuzu kuwadanganya wenzako
 
Sasa mbona kwenye Ilani ya chama chake cha ccm , hakuna andiko kuhusiana na Katiba Mpya ? Bali ukiondoa Unafiki wako utagundua kuwa hiyo imo kwenye Ilani ya uchaguzi ya Cdm ! Sasa wadau wakisema Jk anatekeleza ilani ya Cdm utabisha kivipi ?
naona unajifariji na kujipa matumaini hewa...ccm ndio baba mwenye nyumba, nyie okoteni makopo huko
 
Sura ya 1 Ibara ya 1(4) ya Rasimu ya Katiba Mpya inasema ''Tanganyika itaitwa jimbo la Tanganyika na Zanzibar itaitwa jimbo la Zanzibar na kila jimbo litaongozwa na Gavana'' Hii ni sera ya CHADEMA ya Majimbo. Cha Kushangaza Mwenyekiti wa Tume alisema Tume haijapendekeza Serikali ya Majimbo. Nimeamini CHADEMA ndio inaongoza nchi indirectly.
kanywe chai pengine akili itafanya kazi sawa sawa mana njaa imekufanya uanze kuzusha yasiyokuwepo kwenye rasimu
 
Kweli hata kipindi kile CHADEMA walipoweka shinikizo bungeni hata wakatoka nje, waziri wa sheria alikuwa Celina Kombani akachemsha kwa kupingana kauli na rais. CHADEMA walikwenda ikulu wakaongea na rais umuhimu wa katiba mpya mpaka kimeeleweka!
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom