Elections 2010 CHADEMA inajiandaaje kwa uchaguzi wa serikali za mitaa 2014?

Nicky82

JF-Expert Member
Mar 14, 2009
941
64
Mara nyingi tumewasikia viongozi wa CHADEMA wakisema kuwa wanakijenga chama na kukiandaa kushika dola baada ya kushinda uchaguzi mkuu wa 2015, lakini hawasikiki wakielezea kwa msisitizo ulio sawa kuhusu uchaguzi wa serikali za vijiji/mitaa wa 2014.

Katika uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka 2009, CHADEMA walilalamika kuwa wagombea wao wengi walikosa sifa za kushiriki uchaguzi ule kwa sababu utaratibu wa uchaguzi uliwataka wagombea wachaguliwe katika ngazi za vijiji na mitaa wanakoishi, huko ambako katika maeneo mengi CHADEMA hawana matawi/ofisi za chama na hivyo kutoa nafasi kwa wagombea wengi wa CCM kupita ama bila kupingwa au kushinda kwa kishindo na overall ya matokeo kuipa CCM usindi wa 97% nchi nzima.

Nilifikiri lile lingekuwa somo kwa CHADEMA kujipanga kwa ajili ya uchaguzi wa 2014, lakini wengi wa viongozi wanahubiri uchaguzi wa 2015 wakisahau umuhimu wa uchaguzi wa serikali za mitaa wa 2014
Itakuwa kazi ngumu sana kwa CHADEMA kushinda mwaka 2015 ikiwa kama watashindwa kufanya vizuri kwenye uchaguzi wa 2014. Sababu ziko wazi;

Kwanza, kuruhusu kushindwa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa 2014 kutawavunja nguvu wafuasi wao, na itawapa CCM nguvu ya campaign huku ikiwaaminisha watu kuwa kama CHADEMA wameshindwa kutawala vijiji basi hawawezi kutawala majimbo/taifa
Pili, mara nyingi tumeshudia CHADEMA na vyama vingine vya upinzani vikinyimwa maeneo hata ya kufanyia mikutano yao ya kampeni, au mikutano yao kuhujumiwa. Lakini kama wao ndo watakuwa watawala wa hayo maeneo itakuwa rahisi wao kuzuia na kupambana na hujuma zozote, na kinyume chake ni kuwa kama watashindwa basi kwenye hayo maeneo, wimbo wa hujuma utaendelea kusikika.
Tatu, tumeshuhudia CHADEMA ikikosa wasimamizi wa vituo vya kupigia kura sababu ya kukosa kuwepo kwa watu wenye kulisimamia hili. Lakini uwepo wa serikali inayoongozwa na chama chao itasaidi kuognize watu wa kwenda kusimamia vituoni.
Nne, Uhujumu wa matokeo hufanyika kirahisi pale ambapo hakuna mtu wa kusimamia kile kilicho hesabiwa kuwa ndo kama kile kinachowasilishwa, pia hata katika usimamizi wa kuwachagua wasimamizi wasidizi wa tume, uwepo wa uwakilishi wa chama katika maeneo husika utasaidi kupunguza hatari ya kuchomekwa kwawasimamizi wasio waminifu watakaokuwa na nia ya kupendelea chama tawala

Nawashauri CHADEMA badala ya kuconcentrate kwenye uchaguzi wa 2015, ni vema wakaelekeza nguvu zao kwenye uchaguzi wa 2014, kwa kufanyia kazi yale mapungufu yaliyowaengua mwaka 2009 kwa kuhakikisha wanajenga na kuimarisha matawi kuanzia ngazi ya vijiji/mitaa kwani mfumo huu ndo umekuwa mtaji mkubwa wa CCM na kwa kufanya hayo automatically watakuwa wanajenga mfumo kwa ajili ya kutimiza azma yao ya kuchukua nchi 2015.

Ni wakati sasa wa kila mbunge mchaguliwa na mteuliwa kuhakikisha anaimarisha chama jimboni kwake na mkoa wake ili kukipa chama mfumo imara wenye nguvu kuanzia ngazi ya mashina, vinginevyo itakuwa ngumu sana kushinda 2015.

Angalizo
Ili kushinda uchaguzi ni lazima chama kiwe na mfumo tangu ngazi ya shina.
Wengine wanaweza wakafikiri kuwa wimbi la 2015 huenda likafanana na 2010, lakini tukumbuke kuwa mazingira ya wimbi la ushabiki na mvuto aliokuwa nao mgombea wa CHADEMA mwaka 2010 yanaweza kuwa tofauti na mwaka 2015.......hivyo ni wajibu wa chama kujijenga kimfumo kuanzia ngazi ya shina, na kazi hii ilipaswa kuanza miezi 9 iliyopita...........yawezekana imeshaanza lakini kasi yake haitoshi inabidi kuongezwa.

Wananchi wanapaswa kuandaliwa kushika madaraka kwa chama chao kuanzia ngazi ya vijiji/mitaa na ndipo sasa kazi ya kushika dola itakuwa rahisi. Wakijisahau, kuna hatari ya kufika 2015 na chama kikaonekana bado hakina uwezo wa kuaminika kupewa dola.
 
Afadhali wewe umeleta kitu cha maana, kuna watu wanapumbazwa na urais kwa sifa za ujana. On records power will intoxicate the best hearts, as wine the strongest heads. No man is wise enough to be trusted with unlimeted power.(C. C. Colton) vijana chadema ni muda kujenga chama. Hadith za kikwete kutupumbaza ni ujinga kama ujinga mwingine.
 
kwa taarifa yako kuna mikakati inaendelea kiataifa na ngazi za chini.
leo timu ya chadema mkoa wa dodoma inaanza opereshen katika wilaya za mpwapwa na kongwa baada ya kumaliza kwenye wilaya nyingine.
fuatilia kaka.
 
Nimekuelewa mkuu ila nazani umepitiwa kidogo.chama kinajijenga vizuri na kwa kasi nzuri kama utakumbuka weekend hii dr slaa alikuwepo hapa jf na kujibu maswali.alisema kwamba alikuwa kisarawe akifanya mikutano na kuzitaja kata alizotembelea.pili operation sangara kanda za nyanda za juu kama iringa,mbeya na ruvuma ilikuwa na lengo la kukijenga cha ndio maana walifanya mikutano mpaka vijijini.mwisho operation sangara itakayo anza mikoa ya dodoma na singida kwa mujibu wa dr. Lengo ni hilo hilo.usihofu uchaguzi huo mapambano yatakuwa makali kwani ndani ya miaka3 ijayo chama kitajengeka vizuri.
 
Nimekuelewa mkuu ila nazani umepitiwa kidogo.chama kinajijenga vizuri na kwa kasi nzuri kama utakumbuka weekend hii dr slaa alikuwepo hapa jf na kujibu maswali.alisema kwamba alikuwa kisarawe akifanya mikutano na kuzitaja kata alizotembelea.pili operation sangara kanda za nyanda za juu kama iringa,mbeya na ruvuma ilikuwa na lengo la kukijenga cha ndio maana walifanya mikutano mpaka vijijini.mwisho operation sangara itakayo anza mikoa ya dodoma na singida kwa mujibu wa dr. Lengo ni hilo hilo.usihofu uchaguzi huo mapambano yatakuwa makali kwani ndani ya miaka3 ijayo chama kitajengeka vizuri.

Majibu yako umeyatoa kijuujuu sana kana kwamba suala hili ni dogo. Mimi nipo katika moja ya majimbo yaliyotwaliwa na CDM 2010, tatizo lililopo ni kuwa kwa muda mrefu uliopita imefanikiwa sana kujenga mfumo wa kumgeuza Mbunge kuwa omba omba wa miradi ya maendeleo kwa ajili ya jimbo lake na kuitumia miradi hiyo kama rushwa kwa wananchi wa jimbo lake ili achaguliwe tena. Majukumu halisi ya Mbunge yanafafanuliwa na ibara 63 (2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yaani "Kuismamia na Kuishauri Serikali".

Ili Mbunge aweze kuisimamia Serikali ni lazima atumie muda mwingi kusoma nyaraka mbali mbali, kukagua miradi na utekelezaji wa Serikali sio katika jimbo lake tu, kwa kuwa anaposimama bungeni anawawakilsha watu wajimbo lake katika kuisimamia Serikali katika nyanja zote na kwa ujumla wake wote.

Mbunge anapogeuka kuwa omba omba wa miradi ya maendeleo toka Serikalini tena akiwaomba Mawaziri ambao kimantiki anawajibika kuwasimamia, hili ni tatizo kubwa sana lakimfumo katika Tanzania. Kwa hali hiyo ili mtu aweze kujinadi kugombea ubunge badala ya kuonyesha uwezo wake kusimamia raslimali za tifa na Serikali atajinadi kuyafahamu sana matatizo ya Jimbo fulani la uchaguzi tu. Na kuwa akipapata wadhifa huo atajishughulisha kutatua matatizo ya jimbo husika na kuiacha Serikali, viongozi na watumishi wake wakiwa hawana usimamizi wowote. Katika hali ambapo wabunge wa CCM ni wengi bungeni na karibu wote kabisa huu ndio mtizamo wao ni dhahiri kuwa ndio maan Serikali ya Tanzania haina usiamamizi wowote, raslimali za Tanzania zilizo lukuki haina usimamiz wowote n.k

Kama binadamu mbunge akichaguliwa, atapenda kuchaguliwa tena na tena, na kwa kuwa watanzania walio wengi hawana elimu ya uraia kuwawezesha kupima yupi mbunge bora kwa maana ya kutimiza ibara ya 63 (2) ya Katiba, wananchi huwapima wabunge kwa idadi ya miradi ya maendeleo iliyoletwa jimboni kwao. Kwa maneno mengine watanzania walio wengi hutarajia rushwa ya maendeleo kutoka kwa wabunge badala ya kupata haki yao ya maendeleo kutoka Serikalini.

Kwa kuwa watanzania wasomi na wasio wasomi wameishi katika mfumo huu wa Kifisadi kwa muda mrefu, ili vyama vya upinzani viweze kushinda nafasi za ubunge iliwalazimu wagombea wake kuimba nyimbo watanzani walio wengi wanazotaka kusikia nazo ni kutoa ahadi za kuleta hiki na kile.

Kwa kiwango fulani baada ya watanzania kuichoka CCM waliwachagua wabunge kutoka vyama hivyo ikiwemo CDM. Jambo la hatari ni kuwa watanzania hawa bado hawajapatiwa elimu ya uraia kumtambua yupi mbunge bora kwa maana ya kutimiza majukumu ya kibunge ya kuisimamia Serikali, hivyo wanaendelea kuwapima wabunge kwa rushwa za miradi ya maendeleo inayokuja jimboni hata kama upatikanaji wake ni wa kutia shaka k.m Wizi wa EPA, RADA, MEREMETA n.k. Athari za Bunge la Tanzania kujaa wabunge omba omba wa maendeleo badala ya wasimamizi wa Serikali ni kutokuwajibika kwa watumishi, wizi wa mali ya umma, rushwa raslimali za Tanzania kukosa usimamizi na Tanzania na wananchi wake kuendelea kuwa maskini hata baada ya miaka 50 katika nchi ilijaaliwa sana na mwenyezi mungu.

Cha kusikitisha CDM imeshindwa kujifunza kutokana na kuporomoka kwa vyama vya NCCR, CUF huko nyuma, hivyo inashindwa kujikita katika kuwapatia watanzania elimu ya uraia ili watambue haki zao za kikatiba za kupata maendeleo na sio kutegemea hisani ya mbunge anayeshindwa kutimiza jukumu la kuisimamia Serikali na kugeuka omba omba wa miradi ya maendeleo ili aitumie kama rushwa kwa wananchi ili achaguliwe tena.

Katika jimbo nililopo ambalo mbunge ni kutoka CDM wanachi wengi hususan wasomi ambao ungetarajia watafahamu vyema ibara ya 63 (2) ya Katiba, licha ya kuona kazi kubwa ya usimamizi wa Serikali anayofanya mbunge wa jimbo hili huko bungeni wameanza kuhoji wapi miradi ya maendeleo? Ni haki yao kwa kuwa ndizo ahadi zilizotolewa katika mazingira niliyoyataja hapo juu.

Ni vyema DR Slaa Katibu Mkuu wa CDM na Kamati Kuu yake wakaliona hili na mara moja wakabuni mpango wa utoaji elimu ya uraia hususan kuhusu suala hili kwani bila ya kufanya hivyo ipo hatari CCM kutumia udhaifu huo kuisambaratisha CDM katika uchaguzi wa mitaa wa 2014 na Mkuu wa 2015 kwa wagombea wa CDM kushindwa kutekeleza ahadi zao.

Mfano wa hali hii ni hatua ya Rais Benjamin Mkapa kutumia ilani ya CCM ya 1995 kuomba urais iliyokuwa na ahadi kibao na aliposhionda hakuchelewa kuwaeleza wananchi ukweli kuwa ilani hiyo haitekelezeki na akaanza kutekeleza mipango yake kama Rais, akalipa madeni, Serikali yake ikaamnika kwa wafadhuili na nje ikapata misaada na mikopo nakufanikiwa kuimarisha uchumi wa nchi. CHADEMA IGENI MFANO HUO SEMENI UKWELI NA TOENI ELIMU YAURAIA ILI KUWAKOMBOA WATANZANIA WAJUE KUWATAMBUA NA KUWAPIMA WABUNGE BADALA YA KUKA KIMYA.
 
Back
Top Bottom