Uchaguzi 2020 CHADEMA inahitaji kuwezeshwa kifedha maana tofauti na CCM inayotumia rasilimali za Serikali kufanya kampeni haina pa kushika

CreativityCode

Senior Member
Aug 8, 2020
158
653
Nimeona wachache wakibeza CHADEMA kuchangisha fedha kwenye mikutano yake ya kampeni sidhani ikiwa wako makini.

Ila ukweli ni kwamba watu wote wanaopenda mabadiliko ya kweli ambayo kwa hakika kwa kipindi hiki anayeweza kuyaleta ni Tundu Lissu pekee.

Wala siyo Magufuli kwa maana tumekwisha muona kwa miaka 5 yote na bado ameendelea kuahidi yaleyale ambayo kwayo maisha ya watu yamekuwa magumu na haki ya kuishi na uhuru wa kuongea ukiminywa ili yeye pekee aonekane mbele ya wananchi

Wala siyo Membe maana ana kila elements za CCM

Wala siyo Lipumba maana ni mamluk

SASA WEWE USIPOMCHANGIA LISSU NA CHADEMA WADHANI FEDHA ZA KAMPENI ZITATOKA WAPI? NAWASIHI NDUGU ZANGU WAPENDA HAKI TUICHANGIE CHADEMA ILI TUNDU LISSU AWEZE KUWAFIKIA WAPIGA KURA WENGI ZAIDI.

MWISHO NAWAOMBA CHADEMA MUWEKE NA ACCOUNT YA BENKI ILI TULIO NJE YA NCHI NASI TUCHANGIE

NI HAYO TU, USIKU MWEMA
 
Bavicha huwa wanatamba Mbowe ni tajiri tangu enzi za Nyerere lakini kila unapofika uchaguzi Chadema huwa hoi sana kipesa kwenye kampeni!!

Mfano uzinduzi wa kampeni leo ni hovyo kabisa na ni dhahiri chadema hawana pesa.

Je utajiri wa Mbowe una manufaa gani kwa Chadema??
 
Licha ya kwamba wananchi wamepigika lakini leo nimeona wakijitoa,mwenye mia mbili mwenye elfu tano mwenye elfu kumi wote wanatoa
 
Jamani ruzuku yote inapelekwa Ogaden? CCM hawaombi lakini watu wanawachangia wenyewe jana Dodoma walipata mamilioni
 
CDM wahuni wahuni tu, tukiwachangia buku buku zetu tukija kuomba mahesabu na maelezo ya pesa Mbowe anakuwa mkali na manyumbu wanatukana tu, sasa mchangiane humo humo ndani ya Saccos, mle mlipopeleka mboga.
 
CCM wana hela za mwenge walizobana, wana trilioni 1.5 walizogoma kukaguliwa, wana hela walizopiga kwa manunuzi ya ndege na miradi mbalimbali ya rais, wana hela walizogoma kuwapa wafanyakazi nyongeza za mishahara, wanachangisha wafanyabiashara wakubwa na wa kati, wamechangisha machinga Sh. 20,000 bila kifungu chochote cha sheria, n.k.

Wafanyabiashara wakubwa wanaogopa kuonekana wanaisaidia CHADEMA kwa kuogopa kuhujumiwa na hata kufilisiwa na serikali ya ccm hata wakati huu wa kampeni. Hivyo basi Watanzania wa kawaida wapenda haki hatuna budi kuwachangia CHADEMA hata Sh. 500 ili ujumbe wa Uhuru, Haki na Maendeleo ya watu ufike kwa Watanzania wote.
 
Hela za ruzuku
Hela za michango ya wabunge kila mwezi
Hela sa uanachama
Hela za wahisani

zote zimeenda wapi mpaka mnaomba michango sasa. Hivi miaka yote 5 tulikua tunajipanga kweli au tulitegemea kupata mgombea tajiri tena
 
Ccm walidhani baada ya kumfilisi mbowe na chadema lissu atakosa hela za kampeni.Tutaendekea kumchangia.juzi nimechangia laki na nitaendelea.ccm wao wanachota hazina
 
Hela za ruzuku
Hela za michango ya wabunge kila mwezi
Hela sa uanachama
Hela za wahisani

zote zimeenda wapi mpaka mnaomba michango sasa. Hivi miaka yote 5 tulikua tunajipanga kweli au tulitegemea kupata mgombea tajiri tena
Mkuu wanaojua yaliyotendwa na jpm kwa wapinzani kwa miaka mitano, tutawachangia.we kalale
 
Mmekula bilioni moja michango ya makato toka kwa wabunge, malizaneni na takukuru kwanza.

pia kama chama makini ruzuku ya kila mwezi mnapeleka wapi?

TUKUTANE OCTOBER, ACHENI LONGO LONGO.
FB_IMG_1598719257064.jpg
 
Mkuu wanaojua yaliyotendwa na jpm kwa wapinzani kwa miaka mitano, tutawachangia.we kalale
waliyotendewa ina uhusiano gani na fedha za ruzuku michango ya wabunge etc? maana hata hela za Matibabu ya Lisu ni sisi tulichangia
 
Bavicha huwa wanatamba Mbowe ni tajiri tangu enzi za Nyerere lakini kila unapofika uchaguzi Chadema huwa hoi sana kipesa kwenye kampeni!!

Mfano uzinduzi wa kampeni leo ni hovyo kabisa na ni dhahiri chadema hawana pesa.

Je utajiri wa Mbowe una manufaa gani kwa Chadema??
we kweli hamnazo, Trump mwenyewe na mabilioni yake anachangiwa itakuwa Mbowe??.
Uchaguzi mkuu ni gharama kubwa.
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom