CHADEMA inafanya kosa la msingi kutenganisha madai ya Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
10,242
2,000
Nimewasikiliza viongozi wa CHADEMA, wamefungua battle mbili katika madai yao, Battle ya kwanza ni tume huru ya uchaguzi, na battle ya pili ni katiba mpya.

Kisha wamegawana majukumu, Baraza la Wanawake wamewapa jukumu la kupigania Tume huru ya uchaguzi, Baraza la vijana wamewapa jukumu la kupigania katiba mpya.

Kwa kweli sikutegemea kama CHADEMA wanaweza kufanya blunder kama hii, Yaani badala ya nguvu zote kuzielekeza kwenye ajenda moja tu ya kudai katiba mpya, wao wanaigawagawa hiyo nguvu kwenye kupigania vitu viwili.

Kitendo cha kuwapa akina mama kupigania kitu kingine maana yake ni kuwa umeondoa nguvu yao kwenye kupigania katiba mpya

Hili kosa ambalo CHADEMA wanalifanya sasa, litatuchelewesha zana kwenye madai yetu ya msingi ya katiba mpya na athari zake ni hizi zifuatazo
1. kufifisha sauti na nguvu moja kwenye kudai jambo kubwa zaidi na linaloungwa mkono na watu wengi zaidi yaani Katiba mpya

2. Kuwachanganya wananchi wasijue, Ni kitu gani haswa Chadema wanakipa priority, Je ni tume huru ya uchaguzi au katiba ambayo ikipatikana ndani kutakuwa na tume huru ya uchaguzi?

3. Hii kitendo cha kupigania tume huru ya Uchaguzi pararrel na kupigania katiba mpya kumeanza kuwafanya wananchi wadhani kuwa mapambano halisi ya CHADEMA ni kupigania tume huru ya uchaguzi ili waingie madarakani tu ila hii ya kujifamya kudai na katiba mpya ni zuga tu kwa wananchi wadhani wako serious na kudai katiba mpya

4. Kitendo cha kudai tume huru sambamba na katiba mpya, kumeanza kugawa public opinion, watu wameanza kusema eti tupate tume huru ya uchaguzi kwanza ili hiyo tume huru ndo ije isimamie mchakato halali wa kura za maoni kipindi cha mchakato wa katiba mpya utakapokuwa umefikia phase ya kura za maoni. Wakati tjere is no way unaweza kupata tume huru ya uchaguzi bila kufanya mabadiliko ya katiba ya sasa itakayowahusisha CCM ambao ndo majority bungeni. Sasa binge hili la CCM linawezaje kulia time jiru ya uchaguzi?. Kwa mistake hii ya CHADEMA, Wananchi wameanza kugawanyika!

USHAURI WANGU
Kuanzia sasa CHADEMA iwe na Ajenda moja tu, nayo ni KATIBA MPYA. Ndani ya katiba mpya tutapata tume huru ya Uchaguzi.

Kama CHADEMA ikipewa tume huru ya Uchaguzi kabla ya Katiba mpya nayo hatuwezi kuiamini kutuletea katiba mpya baada ya kunufaika na chaguzi, Kwa hiyo Sisi Wananchi tunataka kusikia Sauti moja tu sasa ya KATIBA Mpya. Nje ya sauti hii, tutafikiri kuwa wanasiasa wanapigania madaraka tu

Chadema isifanye kosa kuseparate ajenda hizi mbili, Isimamena kudai katiba mpya, katiba mpya ndiyo itakayotupa tume huru ya uchaguzi na si vinginevyo!
 

adolay

JF-Expert Member
Dec 8, 2011
12,035
2,000
Ndani ya rasmu ya katiba mpya pendekezwa ya Warioba

Uchaguzi wa haki kwa tume huru imo.
 

Nkanini

JF-Expert Member
Jun 6, 2017
2,360
2,000
Kweli kila mtu now tumepata our voices back,mkuu mtoa hoja wewe sio msemaji wa watanzania na pia sio msemaji wa CDM nani na kwa ushahidi upi umeyaona hayo ya CDM kutenganisha madai yao?

Uongo ni zaidi ya uchawi sio vema kueneza uongo mkubwa kama huu,ulichokileta hapa ni unafiki mkubwa na uchoyo wa ukweli,uhuru wa Haki ndio unatakiwa na uhuru huu unacover mambo yote kuanzia katiba hadi kwenye tume ya uchaguzi inayotakiwa kuwa independent na impartial
 

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
10,242
2,000
Kweli kila mtu now tumepata our voices back,mkuu mtoa hoja wewe sio msemaji wa watanzania na pia sio msemaji wa CDM nani na kwa ushahidi upi umeyaona hayo ya CDM kutenganisha madai yao?uongo ni zaidi ya uchawi sio vema kueneza uongo mkubwa kama huu,ulichokileta hapa ni unafiki mkubwa na uchoyo wa ukweli,uhuru wa Haki ndio unatakiwa na uhuru huu unacover mambo yote kuanzia katiba hadi kwenye tume ya uchaguzi inayotakiwa kuwa independent na impartial
Labda hujafuatilia maagizo ya Chama kwa baraza la vijana na baraza la wanawake la chama
 

F9T

JF-Expert Member
Dec 26, 2015
1,673
2,000
Hiyo paragraph ya pili kutoka mwisho umenichekesha Sana . yaani huwaamini chadema Kama wanaweza kuileta katiba mpya endapo wataingia madarakani, wakati huo unawataka waidai kutoka kwa ccm.
 

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
10,242
2,000
Hiyo paragraph ya pili kutoka mwisho umenichekesha Sana . yaani huwaamini chadema Kama wanaweza kuileta katiba mpya endapo wataingia madarakani, wakati huo unawataka waidai kutoka kwa ccm.
Wanasiasa siyo wa kuwaamini moja kwa moja.

Wanatutia wasiwasi wanaposeparate agenda mbili moja ya kuwarahisishia kupata madaraka na nyingine ndo comprehensive yenye mambo yetu wananchi.

Sasa swala ni kwa nini kama hata wao wataipata tume huru ya uchaguzi kupitia katiba mpya kwa nini waidai separately?
 

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
4,699
2,000
Nimewasikiliza viongozi wa Chadema, wamefungua battle mbili katika madai yao, Battle ya kwanza mi tume huru ya uchaguzi, na battle ya pili ni katiba mpya...
Chadema wako sawa lakini kwa muda tu. Lengo kwa sasa ni kuongea na Raisi Samia na mpango ni kwamba wakienda na katiba Mama anaweza kukataa kwa sasa lakini akakubali tume huru.

Lakini wakienda na tume huru pekee watakuwa wameanzia chini sana kwenye madai. Hii ni njia ya majadiliano na kwa sasa lengo sio watu ni Raisi. Lakini baada ya kukutana na Raisi watabadilisha na kuwa na kitu kimoja.

Warioba na tume walikosea pale walipo weka kipaumbele kwenye serikali tatu hii haitaweza kukubaliwa na ndiyo tatizo kubwa zaidi.
 

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
10,242
2,000
Chadema wako sawa lakini kwa muda tu. Lengo kwa sasa ni kuongea na Raisi Samia na mpango ni kwamba wakienda na katiba Mama anaweza kukataa kwa sasa lakini akakubali tume huru. Lakini wakienda na tume huru pekee watakuwa wameanzia chini sana kwenye madai. Hii ni njia ya majadiliano na kwa sasa lengo sio watu ni Raisi. Lakini baada ya kukutana na Raisi watabadilisha na kuwa na kitu kimoja. Warioba na tume walikosea pale walipo weka kipaumbele kwenye serikali tatu hii haitaweza kukubaliwa na ndiyo tatizo kubwa zaidi.
Wewe unafikiri CHADEMA wakipewa tume huru ya uchaguzi, watakumbuka hata kudai katiba mpya as long as wanachokitaka kwenye uchaguzi wanakipata?

Ndiyo maana sisi wananchi tunaanza kuwa na wasiwasi kwa nini CHADEMA haiwi na Battle moja tu ya kudai katiba mpya, kwa nini Wafungue na ya tume huru ya uchaguzi ambayo kimsingi ndo lulu kwa wanasiasa?

Sisi wananchi tunataka Katiba mpya hiyo ndani yake ndo itakuwemo tume huru ya uchaguzi
 

F9T

JF-Expert Member
Dec 26, 2015
1,673
2,000
Wanasiasa siyo wa kuwaamini moja kwa moja.

Wanatutia wasiwasi wanaposeparate agenda mbili moja ya kuwarahisishia kupata madaraka na nyingine ndo comprehensive yenye mambo yetu wananchi.

Sasa swala ni kwa nini kama hata wao wataipata tund huru ya uchaguzi kupitia katiba mpya kwa nini waidai separately?
Hoja yako uko sahihi kuwa ndani ya katiba mpya ,tume huru itapatikana . sikupingi kwa hilo. Lakini kwa mwanasiasa hivyo ni vitu viwili tofauti kabisa. Tena kwa mwanasiasa ukimuuliza kipi kianze atakwambia ianze kwanza Tume huru.
 

Tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
42,836
2,000
Wanasiasa siyo wa kuwaamini moja kwa moja.

Wanatutia wasiwasi wanaposeparate agenda mbili moja ya kuwarahisishia kupata madaraka na nyingine ndo comprehensive yenye mambo yetu wananchi.

Sasa swala ni kwa nini kama hata wao wataipata tund huru ya uchaguzi kupitia katiba mpya kwa nini waidai separately?

Bila kupinga haya maelezo yako, je ni kweli wametanganisha hayo mambo mawili? Kama ni kweli wametanganisha hayo mambo mawili, basi waache mara moja.
 
  • Thanks
Reactions: F9T

Mr Dudumizi

JF-Expert Member
Sep 9, 2020
1,395
2,000
Kweli kila mtu now tumepata our voices back,mkuu mtoa hoja wewe sio msemaji wa watanzania na pia sio msemaji wa CDM nani na kwa ushahidi upi umeyaona hayo ya CDM kutenganisha madai yao?uongo ni zaidi ya uchawi sio vema kueneza uongo mkubwa kama huu,ulichokileta hapa ni unafiki mkubwa na uchoyo wa ukweli,uhuru wa Haki ndio unatakiwa na uhuru huu unacover mambo yote kuanzia katiba hadi kwenye tume ya uchaguzi inayotakiwa kuwa independent na impartial
Hii ndio demokrasia inayopiganiwa na chadema juu ya uhuru wa kuongea na kutoa mawazo? Kwamba mtu akiongea kinyume na kiongozi/ viongozi wa chadema anaonekana muongo hata kama alichoongea kina tija?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom