Chadema inachukua hatua gani dhidi ya diwani aliyekutwa na silaha ya kivita ak 47? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema inachukua hatua gani dhidi ya diwani aliyekutwa na silaha ya kivita ak 47?

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by WATANABE, Apr 21, 2011.

 1. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #1
  Apr 21, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  Ni ukweli kuwa vyama vya siasa vimeundwa na binadamu, hivyo kuwepo au kutokuwepo kwake kunategemea akili za binadamu. Tofauti na ardhi na vyote vilivyomo ambavyo kwa pamoja hujulikana kama nchi, vilivyoumbwa na mwenyezi mungu.

  Hivyo Tanzania itaendelea kuwepo hata kama vyama vyama vya siasa vitaendelea kuwepo au kufutika kabisa. Hivyo mantiki na busara inanielekeza kuwa nchi ni bora kuliko chama.

  Kutokana na ubovu wa sheria zetu, watawala wetu wa CCM wanatulazimisha watanzania wote tunaotaka kushiriki kwa namna moja au nyingine katika uongozi wa nchi yetu kupitia katika vyama vya siasa. Awali chama kilikuwa kimoja tu yaani TANU na baadaye CCM hivyo wengi wetu tulilazimka kuwa katika chama hicho. Ujio wa vyama vingi kidogo kidogo ukaanza kutoa uhuru wa mawazo, maoni na kupingana bila kupigana na leo ndio tulipo katika mhjadala wa katiba mpya.

  Kwa kuwa vyama vya siasa navyo hubuniwa na kuongozwa na binadamu mara nyingi udhaifu wa binadamu ndani ya vyama vya siasa hususan viongozi mara nyingi hukiganda chama husika kama ambavyo CCM ilivyogandwa na ufisadi baada ya kuchelewa kuwashughulikia watu wenye tuhuma za ufisadi ndani ya CCM.

  Tukio la hivi karibuni la Diwani wa chama chetu wa CHADEMA kukutwa na silaha ya kivita AK 47 haliwezi kupita hivi hivi kwa watu wazima wenye mapenzi mema na nchi yetu ambao kila kukicha tunapoteza raslimali na muda kupambana na vitendo viovu ndani ya jamii yetu.

  Naomba kuuliza uongozi wa CHADEMA unachukua hatua gani dhidi ya Diwani wetu alikutwa na silaha ya kivita? Kutokana na ufisadi uliotalamaki ndani ya CCM tumepata taabu sana kuikuza CHADEMA ili angalau sauti za watanzania wanyonge ziweze kusikika. Hivyo hatuwezi kuvumilia mambo ya kuoneana haya na kukaa nyumba moja aina ya watu kama diwani huyu. Kwa kuwa hizi ni tuhuma nzito, hata kama Serikali imeamua kumsamehe naomba sisi wanachama wa CHADEMA tusimsamehe. Hakuna kutafuta ushaidi wala nini, ni yeye mwenyewe aliyjiweka katika mazingira ya kuchafuaka hivyo ang'oke kwa kuwa ametuchafua wote.

  Nashauri hakuna kuhurumia kata itapotea wala nini atakiwe ajihudhuru mara moja au afukuzwe na uchaguzi mdogo ufanyike hata tukipoteza kata hiyo potelea mabili ilikuwa ni katika jitihada za kulinda maadili mema.

  Naomba kuwasilisha!!!!
   
 2. Mch.A.Mwasapile

  Mch.A.Mwasapile Member

  #2
  Apr 21, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Watamwongezea Guruneti na Mabuldoza ya kupigania
   
 3. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #3
  Apr 21, 2011
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Umeambiwa ametumia silaha hiyo kuua mtu?Usikurupuke kumhukumu mtu bila kuwa na taarifa kamili.Kwa mfano,tatizo sio kuwa na silaha bali ni kama anamiliki silaha hiyo kihalali.

  Pili,kwa mtizamo wako,umiliki wake wa silaha unahusiana vipi na udiwani wake?

  Tatu,wenye mamlaka ya kumchukulia hatua diwani huyo (iwapo itabainika anamiliki silaha hiyo kinyume cha sheria) ni vyombo vya dola.
   
 4. Mch.A.Mwasapile

  Mch.A.Mwasapile Member

  #4
  Apr 21, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [font=&quot]kavue gamba[/font][font=&quot][/font]
   

  Attached Files:

 5. Elungata

  Elungata JF-Expert Member

  #5
  Apr 21, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 28,045
  Likes Received: 8,534
  Trophy Points: 280
  Hvi nayo AK47 ni tishio kiivo.mbona zimetapakaa,angekutwa na RPG ningeona ajabu.hyo ni bunduki tu kama M16,uzi machinegun.suala hapa anamiliki kihalali kama siyo WHY alikua nayo.ama naye alikua mzee wa kupiga night
   
 6. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #6
  Apr 21, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,319
  Likes Received: 439
  Trophy Points: 180
  Hata mzee maokola majogo former minister of defence alikuwa nayo
   
 7. The Prophet

  The Prophet JF-Expert Member

  #7
  Apr 21, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 682
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  inaonekana umejiunga JF baada ya CCM kujivua gamba. karibu sana. hili ndiyo jamvi.
   
 8. h

  hoyce JF-Expert Member

  #8
  Apr 21, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 1,119
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Hata waliomchagua wanajua kuwa anamiliki AK47. Isitoshe kwa wakurya kuwa na mashine ndio uanaume bila kujali ni halali au la. Kazi yake ni kuibia ng'ombe au kupambana na wezi wa ng'ombe, kama sivyo wakurya tujuzeni
   
 9. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #9
  Apr 21, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Nashauri waiachie sheria ichukue mkondo wake
   
 10. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #10
  Apr 21, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  Yaani siamini kama mpaka leo kuna mambumbumbu wa sheria kiasi hiki. Ile kukutwa na silaha usiyo kuwa na kibali nayo ni kosa la jinai. Kwani ufisadi wa RA. EL ulikuwa na mahusino gani nyadhifa zao za uongozi na CCM?

  Ujinga huo wa kujali zaidi mahakama za kisheria tu na kupuuza mahakama za umma ndio uliowagharimu CCM. Ndio maana mara kwa mara CHADEMA hususan DR Slaa anasema "kushitaki kwa wananchi". Mahakama za wananchi hazitumii ushahidi wa kimahakama bali wa kimazingira. Endapo leo CHADEMA inaweza kuvumilia kuwa na kiongozi anayemiliki silaha kinyume cha sheria kesho ikipata madaraka viongozi wake watamiliki vngapi haramu?


  Je CHADEMA ikishitakiwa katika mahakama ya umma kama yenyewe inavyofanya kuhusinana kumfumbia kiongozi anayemiliki silaha kinyume cha sheria nini kitatokea?
   
 11. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #11
  Apr 21, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  Vipi kisiasa. Kama CHADEMA inaweza kuwa na diwani anyemiliki silaha kinyume cha sheria, tena ya kivita. Where does it get the moral authority kukemea maovu katika kambi zingine kam vile za CCM?
   
 12. kisururu

  kisururu JF-Expert Member

  #12
  Apr 21, 2011
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 332
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Sheria ichukue mkondo wake,akikutwa kweli na makosa atahukumiwa na atakua tayari ameshatolewa kwenye udiwani na hataweza kugombea tena
   
 13. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #13
  Apr 21, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  Kisias vipi? Tuendelee kuwa na mtu anyemiliki silaha isivyo halali. Huo ujasiri wa kukemea maovu kwa wengine tutaupata wapi?
   
 14. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #14
  Apr 21, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 160
  Silaha imekamatwa katika ofisi za CHADEMA au shamba la Diwani? Wala hakuna siasa upande wa CHADEMA ujiulize upande wa CCM kwa kuwa aliyemkamata nayo ni MKUU WA MKOA na sio POLISI
   
 15. mwanaone

  mwanaone JF-Expert Member

  #15
  Apr 21, 2011
  Joined: Apr 2, 2011
  Messages: 635
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 180
  acheni ushabiki wa mandazi. sisi tumechagua kuwa wanachadema kwa kuamini ni chama chenye kufuata haki. so alichofanya huyo diwani ni kosa la jinai na ukiondoa sheria ambazo anapaswa kuchukuliwa na serikali. chadema kama chama kinatakiwa kimchukulie hatua za kinidhamu kwa kukiaibisha chama na wananchi waliomchagua. yeye huyo diwani alikuwa anatakiwa awe mstari wa mbele kuwashawishi wananchi wanaomiliki silaha kinyume cha sheria kuzisalimisha polisi na sio yeye kuwa mfano mbovu kwa kumiliki silaha kinyume cha sheria. so tunasubiri tuone viongozi wetu wa chadema ni hatua gani watazichukua ili iwe mfano kwa wengine.
   
 16. a

  adobe JF-Expert Member

  #16
  Apr 21, 2011
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 1,666
  Likes Received: 290
  Trophy Points: 180
  Chadema ndo mahakama???...................na je wale vigogo woote wanaotuhumiwa kutishia wengine wakiwa ndani ya ccm itawafanyaje? Mwanza,dsm na wale ccm walotumwa kummaliza mengi kwa kumpachika mwanae madawa nao je? Chenge aliyeua akiwa mjumbe wa ccm nec je? Na wengineo wengi bila kumsahau jk na babu seya
   
 17. mbogo31

  mbogo31 JF-Expert Member

  #17
  Apr 21, 2011
  Joined: Nov 28, 2008
  Messages: 687
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Swali;

  Kwa nini mkuu wa mkoa achunguze na baadae aamue kumsamehe!!? kuna kitu kimejificha tuchunguze kwanza halafu tutoe uamuzi.

  Kama anamiliki kihalali poa, ila kama hamiliki kihalali na ameshakamatwa basi waliomkamata ndio wanajua sheria inasemaje.
   
 18. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #18
  Apr 21, 2011
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Vipi kuhusu CCM iliyopitisha mgombea ambaye aliongoza kura za wauza/wanunua viungo vya albino Kigoma?
   
 19. Dr wa ukweli

  Dr wa ukweli JF-Expert Member

  #19
  Apr 21, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 892
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  mmmmmmmmmmmmmmm hapo tu ndio patamu
   
 20. W

  WildCard JF-Expert Member

  #20
  Apr 21, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Kuna jimbo moja hukohuko Mara Mbunge kwa tiketi ya CCM ni jambazi wa siku wa silaha na funguo bandia. Madiwani wa jimbo hilo wa CCM wengi ni wezi na wafadhili wakubwa wa wezi wa mifugo.
   
Loading...