CHADEMA ina washabiki wengi, Haina wapiga kura wengi

Hii ni kweli na sio uongo. CHADEMA kusema kweli imeteka watu wengi na kujiibulia washabiki wengi sana. Bali inawapiga kura wachache.

Unajua kura ni siri: Mtu anaweza akamshabikia mgombea fulani lakini ikifika wakati wa kupiga kura palepale ana badili na kumchagua mwingine, halafu akitoka anaendela kukushabikia.

Hii ndio inayo wacost CHADEMA itabidi wabadili mfumo si kufurahia ushabiki wa watu. Wawatake watu wawe na vitabulisho vay kupiga kura. pili wawaombe watu waende kupiga kura.

Au mnaonaje?

Sasa mbona unaongea majungu ya CCM. Hebu tupe data zako umezipataje?
 
mara chadema chama cha kaskazini,mara chadema chama cha wambulu,mara chadema chama cha kidini,mara chadema chama cha wahuni.
Mara chadema chama cha wachochezi.
Ukijumuisha hizi kauli utaona chadema ni chama cha makundi yote ya kijamii.

Nimekugongea like mkuu, umenena vyema!
 
Kwa kukuthibitishia Washabiki wa chadema sasa hivi wanafanza kweli ni matokeo ya Igunga,Arumeru,Kule Mbeya vijijini,Chato,Segerema, Kote huko wanazoa tuu uongozi zidi ya CCM ndio ushabiki mzuri unashabikia na kuhakikisha unawapa uongozi kwa kupiga kura na kulinda kura
 
Ni kweli CDM inakubalika zaidi kuliko CCM katika maeneo mengi ya nchi hii. CDM ina nguvu kubwa mikoa ya Mbeya, Rukwa, Mwanza, Shinyanga, Mara, Arusha, Kilimanjaro, Iringa, Ruvuma, Dar es salaam, Manyara na Kagera. Pia inakubalika kwa kiasi kikubwa Singida, Tanga, Morogoro na Dodoma. Mikoa ya kusini nao wameanza kubadilika. Si kweli kwamba watu wanaoshabikia CDM hawakipigii kura CDM wakati wa uchaguzi. Ukweli ni kwamba CCM wamekuwa wakiiba kura za CDM kwa kushirikiana na tume ya taifa ya uchaguzi. Inaonekana wewe ni mwana-CCM unayetaka kuhalalisha wizi wa kura unaofanywa na CCM.

Kwa kuwa daftari la wapiga kura litafanyiwa marekebisha kabla ya uchaguzi mkuu ujao, vijana wengi ambao ni wanachama wa CDM watajiandikisha kupiga kura; na mwisho wa CCM kutawala utaanza 2014 katika chaguzi za serikali za mitaa na baadaye 2015 kitakuwa chama cha upinzani. Mbinu chafu za CCM na usalama wa taifa(usalama wa CCM na ndugu zao) hazitafua dafu kwani CDM kitakuwa na mtandao nchi nzima ambapo vijana watalinda kura.
 
Matokeo ya tume ya magamba ya uchaguzi baada ya kuchakachuliwa.


BAK: Umefanya uchunguzi japo kidogo?

Haya matokeo ya uraisi KAWE

DAR ES SALAAM

MANISPAA YA KINONDONI
KAWE
Candidate

Political Party

Number of Votes

Percentage Votes
KIKWETE JAKAYA MRISHO

CCM
45,321
48.81
SLAA WILLIBROD PETER

CHADEMA
40,794
43.94
LIPUMBA IBRAHIM HARUNA

CUF
4,563
4.91
RUNGWE HASHIM SPUNDA

NCCR-MAGEUZI
485
0.52
KUGA PETER MZIRAY

APPT - MAENDELEO
229
0.25
MGAYWA MUTTAMWEGA BHATT

TLP
37
0.04
DOVUTWA YAHMI NASSORO DOVUTWA

UPDP
25
0.03
SPOILT VOTES
1,389
1.5
TOTALS
92,843
100


 
Ilikuwa hivi:
"...ccm haina mpinzani,..... ikaja ccm nambari wani, ........ikaja ccm wako vijijini (mtaji wa kura).... na sasa wameishiwa sera wakuja na CDM haina wanachama wengi..."

Therefore, CCM ni mufilisi, now dead and soon watakuwa mzoga
 
Inawezekana ni kweli kwa sasa ili before next election mashabiki zaidi ya 80% watakuwa wapiga kura
Ni kweli kabisa, na mfano hai ni mimi mwenyewe. Kwa takribani chaguzi kuu mbili zilizo pita nilikuwa mwanachama wa ccm lakini sikuwahi kuona umuhimu wa kupiga kura kwa sababu nilijua kwamba napoteza muda wa kufanya shughuli zangu tu. Lakini 2015 nitapiga kura, na ni lazima nipige kura kwa sababu msukumo uliojengeka akilini mwangu ni kuiangusha ccm. Nina uhakika kwa sasa hivi tunapoelekea 2015 watu wengi wanamsukumo kama wangu ni wengi sana kwa sababu watu wengi ninaowajua wanaonyesha wazi kwamba wamechoshwa na ccm tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma.
 
kweli kabisa mkuu! Na wengi kwenye mikutano sidhani hata kujiandikisha kupiga kura kama huwa wanajiandikisha
 
Ndiyo maana ilishinda Arumeruuu.......ahaaaaa kumbe ina washabiki tuu ...basi washabiki wake ni wazuri
 
kura watu wanapiga sema uchakachuaji ndo umekithili sana kwa hawa wenzetu wa chichiemu
 
Sasa matokeo ya CHADEMA yako wapi? ili tupate ushahidi?

Matokeo gani ya CHADEMA? Ushahidi gani tena unaoutaka zaidi ya ushahidi wa kuchakachua matokeo uliofanywa na magamba kwa kushikiana na tume ya uchaguzi wa magamba? Magamba walijua wamepigwa mueleka katika majimbo mengi na hata kura za Urais ndio maana wakachakachua matokeo. Tume ilidai matokeo ya uchaguzi wa Rais yangetangazwa baada ya masaa 24 tangu kumalizika upigaji kura, baada ya kuona msanii ana hali mbaya wakayachelewesha ili wapate muda wa kuchakachua.
 
Wana jf habari
Kwanza niseme mimi ni mwanachadema ila nasikitiswa na jinsi wanachadema wenzangu wa humu jf wanavyojibu maswali magumu kwa majibu mepesi.Nimewahi kusoma mada nyingi tu zinazowatahadharisha viongozi wa Chadema madhara ya kutokwenda vijijini kupiga kampeni,pia mimi niliwahi kuandika humu nikieleza jinsi kataya ngu nzima isivyo na kiongozi hata mmoja lakini ukisoma maneno ya wachangiaji yanakatisha tamaa, wengine watakuambia wewe sio mzalendo, wengine watakuambia chukua hiyo nafasi wewe,wengine wanasema kama wanachama wapo hakuna tatizo. Sasa ukiangalia majibu haya huoni mtu mwenye uchungu wa kweli na chama halafu huwezi kuona hata mchangiaji mmoja anaeumia kwa titizo hilo la viongozi wetu halafu wachangiaji wengi wako mjini na huenda hata hao huko vijijini kwao hakuna viongozi wa chama sasa mimi najiuliza, tunaposeta chadema itashinda tunatumia tathmini ipi,iliyopatikana kwa toka kwa viongozi gani, katagani ina wanachama wangapi, katagani imetekwa na ccm ili chama kiongeze nguvu pale, sasa kama hayayote hatuyajui tunategemea ushindi kutoka wapi?pia ikumbukwe kuwa vijijini ndio kuna wapiga kura wengi pia hukohuko ndiko watu wanakodangganyika haraka zaidi kutokana na uelewa wao mdogo. mwisho niombe kila mwanachadema tujitahidi kuwahimiza viongozi wetu kupeleka nguvu vijijini Tunamuoni kamanda mawazo alivyoiacha familia yake na kuhamia huko kanda ya ziwa na ani-apita kata kwa kata kijiji kwa kijiji.
 
Ningekuelewa kuwa CHADEMA inapendwa na watu wengi, ina mashabiki wengi lakini haina wanachama wengi ukilinganisha na magamba!

Lakini kama ulivyosema kura ni siri, tuambie hizo kura za siri ni za nani?
Arumeru mashariki kwa mfano, CHADEMA hawakuwa na hata mwenyekiti wa mtaa, hizo kura za siri za wanachama wa ccm ndiyo iliyokipa ushinda CHADEMA.

Igunga CHADEMA hawakuwa hata wanachama, lakini kwenye uchaguzi ule walipata kura zaidi ya 23,000, pungufu ya kura 2000 au 3000 ya kura walizopata CCM.

Hivyo unatakiwa ueleweke mkuu siyo unakurupuka kupost!


........

Sawa MKUU umenena. Kwenye mfumo wa vyama vingi SI LAZIMA ukipigie chama chako ILA yule mgombea UNAYEMKUBALI (Unaye-Mshabikia). Hivyo "Pool" la wapiga kura ni la wote.
 
Back
Top Bottom