CHADEMA ina washabiki wengi, Haina wapiga kura wengi

BAK: Umefanya uchunguzi japo kidogo?

Haya matokeo ya uraisi KAWE

DAR ES SALAAM
MANISPAA YA KINONDONI
KAWE
Candidate
Political Party
Number of Votes
Percentage Votes
KIKWETE JAKAYA MRISHO
CCM
45,321 48.81
SLAA WILLIBROD PETER
CHADEMA
40,794 43.94
LIPUMBA IBRAHIM HARUNA
CUF
4,563 4.91
RUNGWE HASHIM SPUNDA
NCCR-MAGEUZI
485 0.52
KUGA PETER MZIRAY
APPT - MAENDELEO
229 0.25
MGAYWA MUTTAMWEGA BHATT
TLP
37 0.04
DOVUTWA YAHMI NASSORO DOVUTWA
UPDP
25 0.03
SPOILT VOTES1,389 1.5
TOTALS 92,843 100

Hivi ni kweli Halima Mdeee alimzidi Dk Slaa!!!!!!!!!.
 
Hivi ni kweli Halima Mdeee alimzidi Dk Slaa!!!!!!!!!.

DAR ES SALAAM
MANISPAA YA KINONDONI
KAWE
Candidate
Political Party
Number of Votes
Percentage Votes
MDEE JAMES HALIMA
CHADEMA
43,365 43.17
ANGELA CHARLES KIZIGHA
CCM
34,412 34.26
MBATIA JAMES FRANCIS
NCCR-MAGEUZI
11,970 11.92
MAPEYO SALIMU SHAABANI
CUF
9,121 9.08
GRACE MAHAMUDU RENDI
UDP
673 0.67
NATHANIELI MANASE MLAKI
APPT - MAENDELEO
375 0.37
RICHARD PIUS MAHALAKA
UPDP
215 0.21
STEPHEN FEDRICK KATUMBI
TLP
215 0.21
MICHAEL BERNARD NDERUMAKI
SAU
50 0.05
SPOILT VOTES 51 0.05
TOTALS 100,447 100

Hapo Kawe Mwanachama mmoja anachagua Rais tofauti na Mbunge tofauti sasa huyu ni mwanachama wa chama fulani au?
 
Ndio maana matokeo ya uraisi yalichelewa kutolewa. Sasa naelewa. Huu uzi uifadhi vizuri, uurudishe 2016 January.
 
Ndio maana matokeo ya uraisi yalichelewa kutolewa. Sasa naelewa.
Kila kitu kikitokea unasema unaonewa! Nikama mtu anayemwambia mwenzake. Ukiniacha unaniogopa ukinipiga unanionea. Which is Which?
 
Kuna ukweli katika thread yako na hii ni challenge kubwa kwa VIONGOZI wa CDM.

Ni kweli CDM ina wapenzi wengi kuliko CCM. Lakini wengi wa wapenzi wa CDM hawana vitambulisho vya kupigia kura. Ni jukumu la vinonzi wa CDM KWANZA kuishinikiza NEC kulifanyia marekebisho daftari la kudumu la wapiga kura.

Kama NEC itakubali kulifanyia marekebisho daftari la wapiga kura. Kazi ya PILI ya viongozi wa CDM ni kufanya kila inaloweza kuhakikisha kuwa WAPENZI na WANACHAMA wao wanajiandikisha kwenye daftari la wapiga kura na kutuza kadi zao.

Kama hilo litafanyika jukumu la TATU ni 2015, ambapo viongozi wa CDM wafanye kila wanaloweza kuhakikisha kwamba WAPENZI na WANACHAMA wao wanakwenda kupiga kura 2015 na kuzilinda.

Kama hayo MATATU wataweza kufanya viongozi wa CDM, Mark my words comes 2015, CCM kitakuwa chama KIKUU cha UPINZANI. Ila kama mojawapo kati ya mambo hayo MATATU hayatafanyika CCM watashinda 2015.

Kwahiyo the ONUS is in CDM leaders.
 
Hayo ni mawazo ya ukweli kabisa.
 
Hata wanachama wa CHADEMA ni wengi kuliko wa magamba.Mwombe msajili wa vyama vya siasa akupe update.

Kuna ukweli mkuu, manake kila mahali ilipofika M4C wanaccm wengi walijivua gamba. Mfano wilaya ya Ngorongoro peke yake wanachama zaidi ya 4,000 walijivua gamba na kujiunga na CDM.
CHADEMA imeweza kuwavua gamba mpaka wanaccm mashuhuri kama akina James Ole Milya na madiwani wengi kutoka CCM. CCM mpaka sasa hawajafanikiwa hata kumshawishi balozi wa CHADEMA kuweza kuvaa gamba!

Mungu Ibariki CHADEMA
Mungu Ibariki Tanganyika
Mungu Ibariki Tanzania ya watu waliostaarabika
 
Hii ni kweli na sio uongo. CHADEMA kusema kweli imeteka watu wengi na kujiibulia washabiki wengi sana. Bali inawapiga kura wachache.

Unajua kura ni siri: Mtu anaweza akamshabikia mgombea fulani lakini ikifika wakati wa kupiga kura palepale ana badili na kumchagua mwingine, halafu akitoka anaendela kukushabikia.

!
Hii ndio inayo wacost CHADEMA itabidi wabadili mfumo si kufurahia ushabiki wa watu. Wawatake watu wawe na vitabulisho vay kupiga kura. pili wawaombe watu waende kupiga kura.

Au mnaonaje?

Ni kweli kabisa, hata hata tukikumbuka kule Arumeru Mashariki hivi majuzi tu, walikuwa na washabiki wengi lakini wapiga kura wachache kuliko CCM. Gamba zito @ work
 
Mbona 2010 tulipiga kura na Dr akashinda ama hzo kura zilipigwa na majini na si wapiga kura wa kawaida

Chunga kauri zako mkuu.
 
Plz jaribu kunielewa mimi nimesema hali halisi ilivyo. Kuwa watu wengi wanashabikia mikutano mizuri ya CHADEMA, huku hawana hata vitambulisho vya kupiga kura. Nikasema inabidi wabadili namna ya kuongea na watu. Na kura ya mtu ni siri na si kila anayekushabilkia ndie atakupigia kura!
Think!

Katika SPIN DOCTOR wa Magamba at least wewe unaweza kujenga hoja lakini unashindwa kuwa COHERENT.

Unasema kwamba mashabiki wengi wa CDM hawana vitambulisho vya kupiga kura. I agree with you. Viongozi wa CDM inabidi walifanyie hili kazi. Kuhakikisha MASHABIKI wao wanajiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura.

Halafu pili unasema kura ni SIRI sio kila mtu anyekushabikia atakupigia. That is where your arguments becomes flawed. Hao mashabiki wengi unaowasema hawana vitambulisho vya kupiga kura, then watawezaje kupiga kura in the first place? Therefore tatizo sio CDM inavyoongea na watu kama unavyotaka tuamini. CDM inavyoongea na watu is FINE ndiyo maana inapata mashabiki wengi kama wewe mwenyewe ulivyokiri.

Tatizo kama nilivyosema ni viongozi wa CDM kuwafanya hao mashabiki wake wengi kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura na siku ya kupiga kura waende kuipigia CDM kura, CCM itakuwa haina chake tena.
 
Wewe kijana mdogo: Ninaweza kuwa na kitambulisho kabisa na nikakupigia kelele Pawaaaaa! lakini mwisho wa siku kupiga kura ni mimi mwenyewe.
 
Hii ni kweli na sio uongo. CHADEMA kusema kweli imeteka watu wengi na kujiibulia washabiki wengi sana. Bali inawapiga kura wachache.

Unajua kura ni siri: Mtu anaweza akamshabikia mgombea fulani lakini ikifika wakati wa kupiga kura palepale ana badili na kumchagua mwingine, halafu akitoka anaendela kukushabikia.

Hii ndio inayo wacost CHADEMA itabidi wabadili mfumo si kufurahia ushabiki wa watu. Wawatake watu wawe na vitabulisho vay kupiga kura. pili wawaombe watu waende kupiga kura.

Au mnaonaje?

Kimsingi CDM wanawapenzi wengi na washabiki wengi kuliko wapiga kura kama ikitokea kuwa tupige kura leo. Lakini hii haimaanishi kuwa CDM inawapiga kura chache kuliko vyama vingine. Kabisa inawezekana kwa wale waliojiandikisha, ikitokea firsa ya kupiga kura leo na uwanja ukawa tambarare, basi CDM wanaweza kuwa na % (asilimia) kubwa ya wapiga kura watakao wachagua.

Kimantiki, nia na sababu ya kupiga kura sasa imeongezeka maradafu kulinganisha na miaka 2 iliyopita, na hii imeletwa na vuguvugu lililozidi kuchochewa moto na CDM, hivyo basi kuna kundi kubwa la wapenzi na washabiki (niaminivyo mimi) ambao hawakuona sababu ya kujiandikisha kupiga kura kipindi kilichopita, hawakuwa wametimiza umri wakati hou, lakini kwa sasa hamasa iko juu. Hivyo basi, hoja yako itakuwa na mashiko kuwa kuna kundi kubwa nje linalotegemea kujiandikisha ili kuwapa kura CDM. Kwa mtizamo wangu, washabiki waipendao CDM lakini wasiokuwa tayari kuipa kura ni hoja yenye mashiko mepesi ambayo imeshuhudiwa katika chaguzi mbalimbali.
 
Plz jaribu kunielewa mimi nimesema hali halisi ilivyo. Kuwa watu wengi wanashabikia mikutano mizuri ya CHADEMA, huku hawana hata vitambulisho vya kupiga kura. Nikasema inabidi wabadili namna ya kuongea na watu. Na kura ya mtu ni siri na si kila anayekushabilkia ndie atakupigia kura!
Think!

Funguka. Uchaguzi ukiitishwa leo, huwezi kwenda kujichongea kadi ya mpiga kura eti kwa sababu unapenda kuipigia kura ccm au cdm. Kimsingi, ilipaswa daftari la mpiga kura liwe linahhuishwa kila unapokuwepo uchaguzi mdogo/mkubwa ili kuwapa wananchi haki yao ya kikatiba.
 
Je CHADEMA wamefanya nini sasa katika hili? Bali wanapiga kelele tu kwenye majukwaa.
 
ni kweli mkuu, na tatizo kubwa ambalo mimi naliona na bado lipo labda litamalizwa na M4C ni wanachama ambao mwisho wa siku ndiyo watakuwa mawakala na kulinda kura, CCM ni majambazi ukiwapa dakika 5 kwenye kituo wana kumaliza...namini 2015 tutakuwa na wakala kila kituo na kusimamisha diwani,mbunge kila kata na jimbo..

M4C ni nini kirefu chake
 
Hao Magamba waelewe kuwa kuna idadi kubwa ya vijana waliotimiza miaka 18 wanasubiri kwa hamu kubwa sana kujiandikisha kwenye hilo daftari la wapiga kura, mimi mwenyewe nasubiri mchakato huo uanze ili 2015 tuungane pamoja tuweke utawala mpya. Hizo longolongo za huyo sijui Anaeli ndo atajua sisi ni mashabiki au la!! Arumeru viongozi wenu walijiamini kwa hilo sana kwamba vijana wengi ni washabiki tu hawana shahada za kupiga kura, hata sisi wanachuo wa chuo kikuu cha Tumaini Makumira ambao hatukupiga kura tuliwahamasisha watu wajitokeze kukipa kura CHADEMA kwa kuwa sisi hatukuwa na haki ya kupiga kura kama sheria inavyoelekeza kwa kuwa hatukujiandikisha ktk jimbo hili, tulilinda kura za waliojitokeza kupiga hadi tukamwondoa SIOI SUMARI NA MAGAMBA wenzake akina Wassira na Lusinde aliyekuja kutukana na katibu wenu mwenezi Nape, Mkapa, Lowassa na wengine kawaulizeni jinsi walivyotoroka usiku wa manane baada ya kugundua kuwa hawanachao. So subirini mtauona moto wake 2015.
 
Hao Magamba waelewe kuwa kuna idadi kubwa ya vijana waliotimiza miaka 18 wanasubiri kwa hamu kubwa sana kujiandikisha kwenye hilo daftari la wapiga kura, mimi mwenyewe nasubiri mchakato huo uanze ili 2015 tuungane pamoja tuweke utawala mpya. Hizo longolongo za huyo sijui Anaeli ndo atajua sisi ni mashabiki au la!! Arumeru viongozi wenu walijiamini kwa hilo sana ila hata sisi wanachuo wa chuo kikuu cha Makumira ambao hatukupiga kura tuliwahasisha watu wajitokeze kukipa kura CHADEMA tulilinda kura za waliojitokeza kupiga hadi tukamwondoa SIOI SUMARI NA MAGAMBA wenzake waliotoroka usiku wa manane baada ya kugundua kuwa hawanachao. So subirini mtauona moto wake 2015.

Kwenye KATIBA tunabadili nchi yetu inakuwa ya kifalme
 
Back
Top Bottom