CHADEMA ina mpango wa kupeleka wabunge wa Viti Maalumu kuchukua nafasi za Mdee na wenzake 18

CDM haili najisi, kukubali kushiriki jambo lolote lile lililotokana na ubedhuri wa uchaguzi ule ni sawa na kula kibudu. Msimamo ni uchaguzi urudiwe kukiwa na Tume huru ya uchaguzi.
 
Nadhani unaeumia ni wewe. Seems ulitamani sana viongozi wa CHADEMA waendelee kususa to prove a point. Bahati mbaya huna clue chama kinaendeshwaje
Mkuu kama negotiation zimefunguliwa kuna haja ya Kuendelea kususa? Maana najua main idea ya kugoma kushiriki chaguzi ni kutaka reforms ya sheria za uchaguzi sasa kama suluhu imeanza kupatikana kwa kuanza na mazungumzo na Rais (by the way haikuwezekana kwa miaka 6 sasa) je kuna haja ya kuweka mgomo? Utakua unagomea nini sasa?

Yaani unagoma kufanya kazi mpaka ule.....then Masufuria yanaandaliwa na moto unawashwa bado tu unaendeleza mgomo? Unataka nini sasa hapo?
 
Mkuu maadam Rais ana nia ya dhati kuleta muafaka wa kisiasa sioni haja ya kuendelea kususa. Ya JPM aliondoka nayo, wao wakubaliane tu kubadili mfumo wa uchaguzi then 2025 ndio tuta evaluate.

Hata JPM pamoja na ubabe wote aliachia yale makontena wakati wa mazungumzo ili kuonyesha goodwill na kuaminiana kwenye kutafuta muafaka.

Sidhani kama kuna haja ya kususia ushiriki kwa Rais ambaye anatafuta maridhiano maadam hakuwa JPM tuichukulie kama a new beginning.
CCM ni ile ile, leo mtamuachia huyu kesho ataibuka mwingine arudie ujinga wa mwendazake, kama Chadema wakienda bungeni wahakikishe kwanza wanapewa Tume Huru vinginevyo ni kujidanganya tu, na Mbowe keshasema bila Tume Huru hawashiriki uchaguzi, tuepuke kero km hizi next time.
 
Hili anajua zaidi Chairman na Katibu. According to CAG, mpunga unaingia kwenye account kama kawaida tu.

Politics waachieni politicians!
Hapana hii si kweli CHADEMA hawajaingiziwa maana hawakupeleka hata account rasmi ya chama ilipohitajika.

Ruzuku yenyewe ni chini ya million 100 sioni kma ni hela ya kuwafanya wa risk reputation.
 
CHADEMA hawana haja na Halima mdee na wenzake hao ni wabunge wa Ndugai na mwenyekiti wa malaika,CHADEMA inahaja na kuheshimiwa kwa katiba.
 
Hao akina Mdee wakitolewa huko Bungeni basi kisiasa watakuwa wamekufa, maana watashambuliwa kila kona na mashabiki wa CDM, kama kuna mabingwa wa kuchafua watu hapa nchini hamna anawafikia CDM, may be Nape anawafuatia, ila kwa mbali sana. Babu Slaa na ubishi wake wote aliwakimbia CDM, akaona bora akawe meneja wa Supermarket, CDM wana midomo michafu sana, watakupa kila aina ya majina. Haya Mzee Mdee karibu mtaani uje ukinywe kikombe ulichojiandalia mwenyewe.
Kwanini mnamuita mzee mdee
 
Chadema walisema hawatambui uchaguzi wa mwaka 2020 ila sasa wanataka kupeleka majina tena?😂

Chadema kwenye hela hawawezi kuruka, hawawezi.

Sasa wameruka ruka weee sasa wanakaa.

Kwa hiyo ule uchaguzi wanautambua na wanakiri kua walishindwa kwa haki, sio?

Nilijua mbele ya hela chadema sio kitu, si chochote si lolote. Ona sasa wametepeta
 
CDM haili najisi, kukubali kushiriki jambo lolote lile lililotokana na ubedhuri wa uchaguzi ule ni sawa na kula kibudu. Msimamo ni uchaguzi urudiwe kukiwa na Tume huru ya uchaguzi.
Anachopanga Mbowe huna ubavu wa kupinga
 
sasa mumeshikwa pabaya ...mae tulieni tumimine DAWA iwangie vizuri.. shwain nyie

Tatizo mnadhaniaga the way chadema kila mtu anasharubu basi ndio mpaka taasisi nyingine nazo ziko hivyo,

Mlisema after hotuba ya mama wabunge watatolewa mbona mpaka leo hii wapo bungeni?
 
Serikali haitaki maridhiano yoyote na vyama vya siasa, rais ametoa nafasi ya kuongea nao na kuwasikiliza, ni kama rais anavyoongea na walemavu au wafanyabiashara ndogo ndogo

Maridhiano ya chadema kwa ajili ya kitu gani? Wananguvu gani sasa hivi?

Ela tu ya kuajili wafanyakazi wa Office hawana, chadema sio threat tena
Wewe unatakaJe lakini !!.
Kwanini unaamini ktk faraka zaidi ya maridhiano ?!. Kwanini unaumia !!
 
Kwa mujibu wa gazeti la RAIA MWEMA la leo 28 April, CHADEMA inataka Mdee na wenzie waondoke/waondolewe Bungeni mara moja ili chama kiweze kupeleka orodha ya wabunge wa viti maalumu kuchukua nafasi ya wale imposters

Msimamo huu mpya wa CHADEMA ni wa kumtambua Rais aliyepatikana kutokana na uchaguzi wa Oct 28 mwaka jana na kupokea ruzuku inayotolewa na Serikali.

Well, it was just a matter of time

View attachment 1766204
Watapelekaje wakati wazito wanakumbatia Covid-19 bungeni?
 
Watapelekaje wakati wazito wanakumbatia Covid-19 bungeni?

Ndugai na kiti chake wanakumbatia wale watu katika ile hali ya kujustify walichokifanya.

Msimamo wa CHADEMA seems ni katika kile kinachoitwa kussupport efforts za Mama za kuleta maelewano ya kisiasa. Kama ule mkutano wa wanasiasa na Rais utafanyika kweli baada ya CHADEMA kuandika barua kwa Rais kuomba audience, moja ya compromise nadhani itakuwa ni kuwatosa akina Mdee.

Hii ni hatua nzuri japo imechelewa na lazima nidhamu ya kuheshimu institutions ijengwe kwa vitendo
 
Back
Top Bottom