CHADEMA ina ma 'thinkers' na 'Strategists' Wazuri sana, soma hapa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA ina ma 'thinkers' na 'Strategists' Wazuri sana, soma hapa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ibange, Nov 27, 2011.

 1. i

  ibange JF-Expert Member

  #1
  Nov 27, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 1,545
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Katika vitu ambavyo chadema imefanikiwa ni kuwa na watu wenye fikra za kisiasa na wanazitumia kujenga na kufanya strategies kubwa. Nilikuwa na mkuu mmoja wa chadema nikamuuliza ana maoni gani kuhusu gamba la Lowassa. Yeye alichosema ni kwamba kimkakati chadema wanamuunga mkono Lowassa akiwa ndani ya ccm na wapo tayari kumsaidia apitishwe kugombea urais.

  Faida za Lowassa kugombea ni mbili. Kwanza itakuwa ngumu sana kwa ccm kumuuza kwani wao wenyewe ndio waliosema kuwa ni fisadi na gamba na ipo kwenye record. Pili, ndani ya ccm kuna makundi hasimu sana kiasi kwamba watu kama akina Sitta hawawezi kubaki ndani Lowassa akigombea. Hivyo ccm itagawanyika mapande na itakuwa faida kubwa kwa chadema.

  Na mbaya zaidi wanahofia atalipiza kisasi kwa wana ccm waliokuwa wanampinga hivyo watakuwa tayari kuona chadema ikishinda kuliko kushinda Lowassa. Wanachosema ambacho hata mimi nakiona hivyo, ccm watapata faida sana kama akiteuliwa kugombea mtu msafi na ambaye hana makundi.

  Naomba niliyezungumza nae asinilaumu kwa kuanika mikakati ya chadema, ni kwa ajili ya mjadala tu
   
 2. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #2
  Nov 27, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Kuna Kipindi niliomba sana Makamba aendelee kuwa Katibu Mkuu wa CCM, ili Pumba zake ziendelee kuwafanya wananchi waichukie CCM!
  Lowassa atahitaji kampeni za CHADEMA ili apitishwe kuwa Mgombea urais wa CCM!
   
 3. apolycaripto

  apolycaripto JF-Expert Member

  #3
  Nov 27, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 637
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Hizi ni hisia zako tu na wala si za kiongozi mmoja wa CDM!CCM hawawezi kuwa wajinga kiasi hicho hasa linapokuja suala la U-rais.
   
 4. i

  ibange JF-Expert Member

  #4
  Nov 27, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 1,545
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Swala ambalo huelewi ni kamba hakuna mtu ndani ya ccm atakayeweza kumzuia Lowassa. Nitajie mwana ccm mmoja ambaye ana nguvu kuliko Lowassa kwa sasa
   
 5. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #5
  Nov 27, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Kwa hali tuliyo nayo na ugumu wa maisha uliopo kinacho shinda ni nguvu ya pesa ni mara chache sana mtu kushinda ktk hali kawaida pasipo njia ajabu kama za kutumia pesa.

  EL pesa anayo hata wale mahasimu wake wakipewa pesa tu watalegeza msimamo kama tunavyo soma magazetini kuwa pesa zimemwagwa Dodoma kiasi kwamba hojaya kumvua nafasi zake chamani hazikuzaa matunda

  Nenda uendako pesa inanguvu watu hutumia umasikini huu tulionao kujipatia uongozi
  Sidhani kama yeye atashindwa kutumia pesa ili hali zipo
   
 6. Godlisten Masawe

  Godlisten Masawe Verified User

  #6
  Nov 27, 2011
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 739
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Lowasa akipitishwa kugombea urais kwa tiketi ya c.c.m itakua faida sana kwa CDM
   
 7. kichomi

  kichomi JF-Expert Member

  #7
  Nov 27, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 511
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mpaka dakika hii ni kitendawili kikubwa sana ndani ya CCM,kuhusu mgombea wao wa urais 2015 maana kuna mgawanyiko sasa hatujui sijui watawasimamisha wagombea wawili,yaani namaanisha CCM original na CCM fake maana ndani ya CCM kunawanaotaka kulipiza visasi na wanao ogopa kulipizwa visasi sasa sijui nani ataibuka kidedea hapo,ngoja tusubili tuone.
   
 8. nditolo

  nditolo JF-Expert Member

  #8
  Nov 27, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 1,335
  Likes Received: 300
  Trophy Points: 180
  Lowassa atasaidia mabadiliko ya kudumu kwani ndo itakuwa mwisho wa ccm. Kwani mpaka sasa anatuhumiwa kuwaroga Mwandosya, Mwakyembe so kifupi hata kampeni ikiwa atapitishwa itakuwa kukanyaga Mbeya ni vigumu sana, au akifika huko atauwawa.
   
 9. Vato

  Vato JF-Expert Member

  #9
  Nov 27, 2011
  Joined: Feb 15, 2009
  Messages: 230
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 33
  Hiyo inaitwa adui muombee mabaya ikiwemo njaa.
   
 10. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #10
  Nov 27, 2011
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,781
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  BONGE LA MOVIE!Na mgombea binafsi awe Chenge vijisenti!!!!!!!!!!!!!
   
 11. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #11
  Nov 27, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  mimi nitamtetea lowasa mpaka siku naingia kaburini,naombeni mnipe ufisadi wa lowasa ili niwape ufafanuzi kuna thread moja hapo nyuma nimeichangia na kama chadema tutajidanganya kwa lowasa itakula kwtu,
  ccm isimamishe mtu yeyote si lowasa kwani atatusumbua sana.
  huyu mtu ni jakob zuma.
   
 12. n

  nyandaojiloleli JF-Expert Member

  #12
  Nov 27, 2011
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 206
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  LOWASA ndiye mwenye nguvu kwenye CCM hakuna mwingine maana anavyojiandaa na kuwahadaa watu ili aonekane msafi.
   
 13. m

  msafi Senior Member

  #13
  Nov 27, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 192
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  ni ukweli ulio wazi, pamoja na kashfa zilizokuwa zinamwandama EL, makundi hasim ccm waliongeza chumvi mno juu ya el kuwa fisadi, hususani nape. nakubaliana na wengine kabisa kuwa el ni tishio kwa cdm,maana huyu jamaa mbali ya nguvu ya fedha lakini ana maaamuzi, tofauti na rahisi wa sasa,
   
 14. Leonard Robert

  Leonard Robert JF-Expert Member

  #14
  Nov 27, 2011
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 9,146
  Likes Received: 2,465
  Trophy Points: 280
  CHADEMA haina siasa za kuvizia kama wengi wanavyo zani.
   
 15. Papa D

  Papa D JF-Expert Member

  #15
  Nov 27, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 687
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  nafikiri wakti unaandika hayo ulikuwa umebanwa kuharisha!! kwa hiyo ukaandika huku unawaza choo kipo wapi!!!!!
  CDM has great thinkers but the Lowassa things is non of their plans! Lowassa is never a threat or a strategy to them!
  Ningekuambia aliye strategy kwao ila kwa kuwa umeanza kwa pumba ........... BASI NA UBAKI VIVYO HIVYO!!!
   
 16. Borakufa

  Borakufa JF-Expert Member

  #16
  Nov 27, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 1,503
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ama kweli
   
 17. j

  jigoku JF-Expert Member

  #17
  Nov 27, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,347
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  Hakuna cha EL wala nani mnaemuona ana nguvu ndani ya CCM,kwanza mtueleweshe hizo nguvu mnazozungumzia ni nguvu zipi?za ufisadi au?kwa picha hii ya juzi kule dodoma nadhani wananchi wanaojihurumia hawatakuwa tayari kuiunga mkono CCM,maana ushahidi umetolewa wazi na EL mwenyewe ya kwamba kumbe hata JK ni fisadi,kwa hiyo ccm kwngu ni chama kinachosubiri kukata roho,ni chama cha kulea na kutetea mafisadi,wote ni wachafu hao hata mkinitajia nani naona ni the same.Kuweni na kumbumkumbu ya matukio ya kifisadi na athari zilizosababishwa na matokeo ya ufisadi huo kwa taifa letu kisha ndo tuanze kufikiri nani agombee wapi na kwa nafasi ipi.
   
 18. Kisima

  Kisima JF-Expert Member

  #18
  Nov 27, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 3,768
  Likes Received: 2,228
  Trophy Points: 280
  Czan kama hılı nı jıpya sana!
  Sıtegemeı anguko la CCM kwa mgombea awaye yoyote yule!
  Muundo na utaratıbu mzıma wa upıgajı kura ndanı ya Nchı yetu nı kıtendawılı kıgumu kwa chama chochote cha upınzanı kuchukua madaraka.
  Kwa mfano, ktk chaguzı zote Zanzıbar CUF walıshında, ndg zangu wana JF wote nı mashahıdı jınsı chaguzı zıle zılıvyoenda na ubabe wa CCM kujıhalalıshıa ushındı kwa nguvu ya dora!
  Mahubırı ya free and faır electıon katıka ukanda wa Afrıka na Mıddle East yatachukua zaıdı ya mıongo kadhaa kwa watawala wanaohodhı madaraka kukubalıana na dhana nzıma unless mzımu wa watu wazalendo kama Mwl JK Nyerere uwatembelee.
  Hasa kwa Taıfa kama Tanganyıka amabalo asılımıa kubwa ya wananchı hawajuı elımu ya uraıa, waoga na watu wanaokumbatıa amanı ılıyopotoshwa n akuhongwa kanga,kofıa chumvı n.k
  Tutavuja mate sana humu JF lakn nawahakıkıshıa mabadılıko ya kwelı hayataletwa na katıba mpya wala sıasa ya vyama vıngı zaıdı ya mıongo mıtatu ıjayo!
  Vıngınevyo vıjana wazalendo wa Nchı hıı waongoze mapınduzı ya kwelı!
   
 19. A

  Ame JF-Expert Member

  #19
  Nov 27, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 3,352
  Likes Received: 659
  Trophy Points: 280
  Siyo aliyekwambia tu bali hata roho mtakatifu hakubaliani na huo uhuni wako; mtu anakuamini anakwambia secreat yake wewe unai expose ili tu upate tija kwa nafsi yako duuh ningekuwa mm ndo huyo siku nyingine ningekuwa nakuingiza chaka tu ili uwe unaaibika kila siku!
   
 20. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #20
  Nov 27, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,578
  Likes Received: 18,521
  Trophy Points: 280
  Rais 2015 atatoka Kaskazini!.
   
Loading...