CHADEMA imezindua Mkakati wa Kuwatetea Lowassa,Rostam na Chenge! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA imezindua Mkakati wa Kuwatetea Lowassa,Rostam na Chenge!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mlengo wa Kati, Apr 20, 2011.

 1. Mlengo wa Kati

  Mlengo wa Kati JF-Expert Member

  #1
  Apr 20, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 2,733
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Chama Cha Demoktasia na maendeleo kimejikuta kikitetea mafisadi ambao CCM imetangaza kuwatosa! Chadema badala ya kubeza kwa miaka mingi kuwa CCM haina ubavu juu ya mafisadi hao sasa haiamini kile kinachotokea na badala yake wameanzisha mkakati wa kusema Mafisadi hao wana onewa! Pia wamekua wakisema siku zote CCM ilikua wapi kuwatimua! Lakini ikumbukwe kitendo cha Kikwete kwenda kuwa nadi watuhumiwa hao majimboni mwao Chadema ili pata agenda kwa mgombea wao wa Urais Dr Slaa kusema CCM inakumbatia mafisadi! Chadema kusema siku zote CCM ilikua wapi kuwatimua mafisadi wanatoa fursa ya kuwatetea mafisadi! Kwa hili nasimama upande wa CCM kuwaunga mkono kwa hatua hii ya kupambana na Ufisadi! Pia naona suala la Ufisadi iwe vita ya Utaifa na sio Chama kimoja cha siasa,naona Chadema ina hisi imenyang'anywa agenda ya Ufisadi na CCM! Leo gazeti la Tanzania daima linalo milikiwa na Mbowe nimeonesha taswira ya Chadema kuwatetea mafisadi hao kama CCM ina waonea! Hata JF nayo imegawanyika kwa baadhi ya wajumbe kubeza juhudi za CCM lakini kubwa ni chuki tu walio nayo kwa CCM bila kujali hatua hii mhimu ya kupambana na ufisadi. Na wengine wanasema CCM itagwanyika,jambo ambalo kwa utalaamu wa kisiasa kundi hili la akina lowassa,Rostam na Chenge lina nuka kwa jamii hivyo hawana ujanja wa kukubalika iwe kuanzisha chama au kuhamia vyama vingine!

  My take: chadema iwe makini na jambo hili lasivyo itaonesha taswira ya yake kwa umma!
   
 2. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #2
  Apr 20, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Huyo JK mwenyewe FISADI. Atawaambiaje wenzie waondoke CCM yeye abaki??? Kwa usafi upi alio nao JK??? Anatakiwa aonyeshe njia yeye kwanza. Vinginevyo bdo ana2fanyia usanii.
   
 3. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #3
  Apr 20, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  mjomba mi cjaelewa vizuri nan anawatetea mafisadi mbna sijaona wapi kina RA AC na EL wamerudisha kadi ya chama.. CHUKUA HATUA
   
 4. Mlengo wa Kati

  Mlengo wa Kati JF-Expert Member

  #4
  Apr 20, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 2,733
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Umechelewa kuamka,ikifika mchana utaelewa tu!
   
 5. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #5
  Apr 20, 2011
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Hii twisting ya ukweli isnt working at all.Chadema unayozungumzia ni hii iliyoibua kashfa dhidi ya Lowassa,Rostam,Chenge na mafisadi wengineo,au Chadema nyingine ya kufikirika?

  Hivi ni utetezi kwa mafisadi kuihoji CCM kwanini Kikwete alipanda majukwaani akiwa na Lowassa,Rostam na Chenge na kuwatetea huku akidai ni watu safi,then leo anadai ni mafisadi?Kwa wanaofahamu lugha vizuri,hapo subject ni Kikwete na utetezi wa mafisadi ilhali object ikiwa mafisadi waliowahi kutetewa lakini sasa wanadaiwa kutoswa.Underlined points ni pamoja na usanii wa Kikwete,Kikwete kama sehemu ya ufisadi,involvement yake katika kukomaa kwa mafisadi,nk nk

  Only way mtu ataambiwa anawatetea Lowassa,et al ni atakapotamka kuwa HAWANA HATIA,au HAWAJATIWA HATIANI,au kama alivyosema Sophia SImba,niTETESI SI AMBAZO HAZIJATHIBITISHWA.Sasa kwanini msimlaumu Sophia Simba mje kuirukia Chadema?

  Hapa kunachofanyika ni upuuzi uleule wa kupinduapindua maneno.Kwamba CCM wanapohojiwa iweje Chadema iliposema Lowassa nawenzie ni mafisadi,CCM ikawatetea,lakini leo inaunga mkono position ya Chadema (bila aibu wala kutoa credit kwa Chadema)...jibu la CCM ni kuwa Chadema sasa inawatetea mafisadi!!!

  Anyway,kuilaumu CCM na wafuasi wake (including vibaraka lukuki waliomwagwa hapa JF) ni kama kupoteza muda vile kwani Chama hicho kilishapoteza mwelekezo zamani hizo,na sasa ni kama kipofu anayetafuta paka mweusi kizani ilhali paka huyo hayupo.Ukskia kauli za Nape,January Makamba na Mukama,utagundua hawana jipya zaidi ya mwendelezo wa anachofanya JK: AHADI JUU YA AHADI.Ungetegemea watu hawa wanaodai kuwa wamejivua gamba la ufisadi wangekuja na vision mpya,ya kumjali Mtanzania wa kawaida,lakini all they talk is about themselves.Wamekuwa so obsessed na madaraka na hadhi ya chama kuliko thamani ya wananchi wa kawaida.

  Umaarufu na support kwa Chadema from common man on street ni focus ya chama hicho kwa wnanchi,kuzungumzia matatizo yao badala ya majigambo kuwa ooh tuna sera hii au ile,ooh tumepigani uhuru,oooh amani na utulivu.That's talking about oneself and forgetting kuwa taifa ni watu na si mtu au taasisi moja tu.

  End of the day,you'll run out of steam.Huku mpambane na Chadema,huku mpambane na the so-called magamba,mtamudu?
   
 6. Consigliere

  Consigliere JF-Expert Member

  #6
  Apr 20, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,071
  Likes Received: 7,553
  Trophy Points: 280
  Kama CCM imejaribu kufanya jambo ambalo linalenga kuleta muafaka wa kijamii, kwa nini isipongeze kwa hatua hiyo? Kama tutaamua kujivalisha unafiki na kujitia upofu wa kutoona jambo ambalo lipo dhahiri sidhani kama tutafika kule ambak tumekuwekea matamanio ya siku moja kukufikia.
  Sidhani kama miongoni mwetu kuna mtu aliemsafi kwa kiwango kinachohitajika, na sielewi ni gauge ipi tunaitumia kupima na kuwapata watu wale tunaodhani kuwa ni wasafi.
  Kuna watu wamejichagulia tabia ya kupinga kila kitu kifanywacho na watu walio upande wasio utaka wao, hapo tutakuwa hatujifunzi kitu wala hatujiandaa na mafanikio ya baadae, ieleweke kuwa CCM peke yake bila ushirikiano toka kwa watu walio na itikadi ya vyama vingine haiwezi kuongoza nchi hii, vivyo kwa CDM, sasa sioni kwanini tusijengee ustaarabu katika kukosoana na kushaurina, badala yake tunajikita katika kudharirishana na kutiana maudhi, mbinu ambayo hutumika pale ambapo malengo ni kuangamizana na si kusaidiana kurekebishana.
  Tuache tabia ya kubuni na kuunga unga taarifa ambazo mwisho wake ni kuchafuana kusiko na tija, kama wote lengo letu ni kusimama kama taifa moja imara katika nyanja zote za kijamii, yatupasa tushirikiane, tuwe wazi kiutambuzi kuwa pamoja na kelele zote CDM pia wana nafasi kubwa ya kushindwa kutimiza au kuyafanyia kazi yale wanayoyaahidi kwa wananchi kama vile ambavyo CCM inavyoshindwa.
  Tuwe wakweli na kutambua mchango wa kila kundi katika kuijenga nchi yetu. Hakuna kundi la malaika miongoni mwetu, makundi yote yanaundwa na raia/binaadam dhaifu wenye mioyo na miili yenye asili na tabia za umimi, uchoyo, majivuno, tamaa, ubaguzzi,dharau,kukata tamaa, chuki,kuzaliwa, kuumwa kuishi na kufa.
  Kama kuna watu wa kundi au chama fulani kinaundwa na watu wasio na tabia nilizozitaja hapo juu na wajitokeze.
   
 7. m

  mao tse tung Member

  #7
  Apr 20, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [​IMG] Mlengo wa Kati

  Today 10:29 AM
  #1 [​IMG]
  [​IMG] Senior Member [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG]


  Join Date : 16th February 2011
  Posts : 164
  Thanks46Thanked 34 Times in 18 Posts

  Rep Power : 21  [​IMG] CHADEMA imezindua Mkakati wa Kuwatetea Lowassa,Rostam na Chenge!

  Chama Cha Demoktasia na maendeleo kimejikuta kikitetea mafisadi ambao CCM imetangaza kuwatosa! Chadema badala ya kubeza kwa miaka mingi kuwa CCM haina ubavu juu ya mafisadi hao sasa haiamini kile kinachotokea na badala yake wameanzisha mkakati wa kusema Mafisadi hao wana onewa! Pia wamekua wakisema siku zote CCM ilikua wapi kuwatimua! Lakini ikumbukwe kitendo cha Kikwete kwenda kuwa nadi watuhumiwa hao majimboni mwao Chadema ili pata agenda kwa mgombea wao wa Urais Dr Slaa kusema CCM inakumbatia mafisadi! Chadema kusema siku zote CCM ilikua wapi kuwatimua mafisadi wanatoa fursa ya kuwatetea mafisadi! Kwa hili nasimama upande wa CCM kuwaunga mkono kwa hatua hii ya kupambana na Ufisadi! Pia naona suala la Ufisadi iwe vita ya Utaifa na sio Chama kimoja cha siasa,naona Chadema ina hisi imenyang'anywa agenda ya Ufisadi na CCM! Leo gazeti la Tanzania daima linalo milikiwa na Mbowe nimeonesha taswira ya Chadema kuwatetea mafisadi hao kama CCM ina waonea! Hata JF nayo imegawanyika kwa baadhi ya wajumbe kubeza juhudi za CCM lakini kubwa ni chuki tu walio nayo kwa CCM bila kujali hatua hii mhimu ya kupambana na ufisadi. Na wengine wanasema CCM itagwanyika,jambo ambalo kwa utalaamu wa kisiasa kundi hili la akina lowassa,Rostam na Chenge lina nuka kwa jamii hivyo hawana ujanja wa kukubalika iwe kuanzisha chama au kuhamia vyama vingine!

  My take: chadema iwe makini na jambo hili lasivyo itaonesha taswira ya yake kwa umma!
  wewe ulitaka CHADEMA wawasifie CCM.kazi ya CDM ni kuonyesha maovyo ya CCM sii kuisifia ukutaka wakusifia kazi za ccm hii ni kazi ya CUF,NCCR,TLP,UDP na kile chama cha dovutwa ambao ni vibaraka wa ccm
   
 8. Msarendo

  Msarendo JF-Expert Member

  #8
  Apr 20, 2011
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 9,148
  Likes Received: 3,337
  Trophy Points: 280
  Naunga mkono hoja.
   
 9. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #9
  Apr 20, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,277
  Trophy Points: 280
  Kweli Mkapa hakutukana pale aliposema Watanzania ni wavivu wa kufikiri. ukitaka kuwajuwa mafisadi waote wakubwa soma list of shame ya mwembe yanga, jina namba ni la JK, sasa kama wao wanataka kutufanyia usanii watanzania kwa kuwatoa hao watatu kama ng'ombe wa kafakara kuna ubaya gani basi Rostam na Lowasa wakijisalimisha CHADEMA (lakini sio kujiunga na chama) wakatusaidia kusema kile wanachokijuwa na wakasurrender evidence document za kagoda kwa CHADEMA then ukweli ujulikane, hata mimi nawachukia watu wanafki kama tuliiba wote basi tufe wote, au tukomae tuu tuweke pamba masikioni. kwani mmesahau Mkapa alivyokuwa anamtetea Sumaye kwamba Watanzania tuna wivu wa kike? sitetei wezi naomba nieleweke usitafute utukufu kwa damu za wenzako. mimi sidanganyiki kama sio Lowasa kujiuzuru uwaziri mkuu serikali nzima ya JK ilikuwa inakwenda na maji. je leo tumuone Mwakyembe mbaya kwa kulificha jina la JK kwenye kashfa ya Richmond? tujifunze kuzisoma siasa kwa nyakati na timing zake. Kwa faida ya Chadema Lowasa ni link muhimu kwa sasa. lakini si kuwa mwanachama.
   
 10. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #10
  Apr 20, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Ni kweli uyasemayo, pamoja na yote na hisia ulizoonyesha katika suala hili.... kuna vitu vya msingi nadhani bado chama tawala katika nchi yetu lazima kibebe lawama zote na majukumu ya kila kianachotokea katika matukio yanayotokea saiv hapa kwetu.
  Ni kweli chama hicho kimewahi kufanya mambo ya maana sana kwa nchi hii hiyo hamna anayeweza kukataa, lakini nao hawana sababu ya kusimanga watu na hilo sababu wao waliyafanya hayo mema kwakuwa lilikuwa jukumu lao la msingi, na wananchi hawalazimiki kushukuru kwa chochote kwani ni haki yao kutendewa mema na serikali yao.

  Unazungumzia kuwa tupongeze kwenye hatua waliyochukua juu ya ufisadi (kuvua gamba)... ndugu yangu hii itakuwa ni unafiki uliokithiri, sababu utakuwa hujamtendea haki mkulima na mfanyakazi wa kawaida eti ajitokeze kupongeza kujivua gamba kwa chama, ambapo zaezi lenyewe limehusisha kiini macho kwa wajumbe wa 3 tu (EL,RA & AC), nasema kiini macho sababu wajumbe hao bado ni wanachama hai tena bado wamo NEC, pia nasema itakuwa hujawatendea haki wakulima na wafanyakazi sababu tatizo lao wao sio mafisadi binafsi kama hayo magamba yanayodaiwa, tatizo kuu hapa ni mfumo wa ufisadi ambao upo toka serikali ya mtaa/kijiji hadi serikali kuu... Nakubali miongoni mwetu hamna mtu aliyekamilika japo wapo wenye uthubutu wa kuwanyooshea wenzao vidole bila wewe kuweza kuwanyooshea vidole, watu hao wapo... ila tusiende huko, bado nipo kwenye hili la mfumo wa kifisadi. Wazarendo kadhaa wakashauri japo turekebishe sheria ya TAKUKURU ili kuipa nguvu na meno zaidi (kuitoa kwenye ofisi ya rais) hamna aliyesikiliza, hata Dr Hosea analilalamikia suala hili (Wiki leaks alituja hilo)
  Sasa ndugu yangu kwa hili unataka mkulima na mfanyakazi apongeze nini hapo? Nini kimefanyika kwakweli??
  Unasema watu wamejichagulia kupinga kila kinachofanywa, sidhani kama watu wanapinga kila kinachofanywa ila watu tunapinga mengi yanayofanywa na kila jambo husika linalopingwa watu wanatoa hoja za kupinga na wanasuggest njia zenye maana zaidi na zenye manufaa ya wazi zaidi kwa watu wote lakini seikali hizi hazisikii la mtu awe mtaalamu au mwanaharakati, rejea masuala ya umeme na tanesco yetu, kupanda kwa gharama za maisha (bei ya mafuta), hata la muswada wa marekebisho ya katiba (badala ya katiba mpya).... pia kubwa zaidi nakupa mfano mmoja wa namna tunavyotelekeza wataalamu wetu na vipaji vyao..... kwenye Gazeti la Raia Mwema la Aprl 6. ukurasa wa 12 kuna stori ya Dr Mselly Nzotta, mtanzania anayetamba uko Sweden kwenye masuala metallurgy ( teknolojia ya vyuma), kajaribu kuja hapa kuleta utaalamu hamna wa kumpokea, wakati chuma kule liganga tunampa mchina bila wataalamu wazawa wa kutosha, huo ni mfano mmoja tu kwenye eneo hilo moja.
  Ifike sehemu tuanze kuwa watu wa kufikiria makubwa kwa nchi yetu sababu nchi hii Mungu aliiumba ili liwe taifa kubwa sana ndio maana akaipa utajiri wote kuliko nchi zote duniani, kwa maana hiyo ni lazima tuache siasa nyepesi za kinafiki za kusifiana kijingajinga tu wakati tunapiga hatua moja mbele na kurudi kilomita nzima.
  Tukiringanisha potential za nchi kwa maana ya resource za kila namna na hapa tulipo baada ya miaka 50 ya uhuru, ukweli ni kwamba hamna kinacho fanyika na viserkali vyetu hivi vya watu wenye mawazo madogo wasioona mbali!
   
 11. Viper

  Viper JF-Expert Member

  #11
  Apr 20, 2011
  Joined: Dec 21, 2007
  Messages: 3,665
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  nakubaliana na wewe... uliposema juhudi za kupigana na ufisadi isibaki kaika chama bali iwe kwa taifa zima!!...
   
 12. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #12
  Apr 20, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  You are part of twisters or spinner mafisadi watachukiwa, watashambuliwa na CDM mpaka kieleweka. Kama unawaomba CDM ipunguze kasi wewe ndiye unatikiwa uwe makini na ushauri wako
   
 13. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #13
  Apr 20, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  poleni sana ndio siasa hiyo
   
 14. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #14
  Apr 20, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,971
  Likes Received: 2,967
  Trophy Points: 280
  Naomba unijuze hatua ip waliyochukua ya kupambana na mafisad, hii ya kuwapa siku 90 wamalizie wizi wao???????????????..
   
 15. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #15
  Apr 20, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,971
  Likes Received: 2,967
  Trophy Points: 280
  mikakati gani CCM waliyofanya ya kukomesha na kupambana na mafisad????. Kwangu naona usanii mtupu. Mfano: mwanzoni waliwapa muda a kurudisha fedha wizokwiba (EPA), msimu huu wamewapa siku 90(approx 3 months) wamalizie kufisad, then wajiondoe wenyewe,(tunataka waondolewe na si kujiondoa, kwann wanatumia polite language ktk swala kama hilo?, huu ni udhaifu).
  Huu ndio mkakati unaousifia????????.
   
 16. Mzee Wa Rubisi

  Mzee Wa Rubisi JF-Expert Member

  #16
  Apr 20, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,754
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Mbona CCM aiwataji kwa majina mafisadi hiyowapa siku 90 kujiondoa kwa chama.?
   
 17. kanta

  kanta JF-Expert Member

  #17
  Apr 20, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 343
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  We jamaa unachekesha sana,yaani umekubali kabisa kwamba CCM wamejivua Gamba,hilo ni changa la macho tu hamna lolote.Shetani ni shetani hata akija kwa sura ya malaika.Unatakiwa ufikirie kabla ya kuandika cause walichofanya CCM ni upuuzi mtupu.Huwezi kuwaadhibu kwenye chama halafu uwaache waendelee kuwa Serikalini,wanaendelea kupeta.Lingine ni kwamba GAMBA ni mfumo hivyo huwezi kulitoa kwa kuwaondoa kina Makamba tu ndo maana CHADEMA hawakubaliani hicho kiini macho.CCM wanapaswa kujivua GAMBA kwa kuondo viongozi wabovu waliopo serikalini,kuonyesha nia ya kweli katika kupambana na Rushwa,kupunguza matumizi makubwa yasiyo na msingi wowote, na kuweka misingi mizuri kwa ajili ya maendeleo,kusimamia na kuhamasisha uwajibikaji.Hayo ni macheche tu ambayo walipaswa kuyafanya kuenyesha kuwa WANAJIVUA GAMBA.
   
 18. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #18
  Apr 20, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  Rostam, Lowassa na Chenge walikuwa ni facilitators lakini yupo aliyenufaika na EPA ambaye ni Kikwete. Na incvumbent Presideny aliyeriuhusu uchafu huo Mkapa. CHADEMA inataka kuprove kuwa hata Mwalimu Nyerere was wrong katika kutuchagulia Benjamin Mkapa for presidency. Toka lini kujivua gamaba kukaanzia katika kiwiliwili nai lazima ianze kichwani na kichwani ni marais Mkapa na Kikwete
   
 19. Y

  Ye Nyumbai Senior Member

  #19
  Apr 20, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 125
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sawa EL,RA,AC kweli ni mafisadi lakini mbona ccm wasiwatoe wengine akiwepo Mzee Mkapa na Kikwete?Mafisadi ni wengi ndani ya chama cha magamba wawtoe hadharani nao tuwajue.
   
 20. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #20
  Apr 20, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Slaa yeye mwenyewe fisadi. nendeni kwenye kamusi ya kiswahili tafuteni nini maana ya neno fisadi , utakuta imeandikwa ' ni mtu anae chukua wake za watu'
   
Loading...