mkalamo
JF-Expert Member
- Sep 7, 2013
- 319
- 345
Katika siku za hivi karibuni Chama cha Demokrasia na maendeleo, kupitia viongozi, wanachama na washabiki wake kote nchini, waliutangazia umma kuwa hawatashiriki uchaguzi wowote kama hakutakuwa na tume huru ya Uchaguzi.
Mbaya zaidi ikakinyooshea kidole chama cha ACT Wazalendo, kilichoshiriki katika chaguzi za marudio kwenye majimbo ya Buhingwe na Muhambwe na kueleza kuwa chama hicho kinatumika kuisafisha CCM kutokana na makando kando ya uchaguzi wa 2020.
Kama haitoshi wakawaonya hata wananchi walioamini kuwa ni wapiga kura wasioweza kuipigia CCM wasiende kumchagua mgombea wa ACT katika chaguzi hizo kwa kuwa chama hakitambui juu ya uchaguzi huo.
Ikumbukwe katika majimbo hayo ya Buhigwe na Muhambwe CCM ndiyo waliokuwa wanawakilisha awali na nguvu yoyote ya upinzani ilikuwa inaiminya CCM kupata ushindi,lakini Chadema wakasusa na wakazuia watu wao wasipige kura.
Kiufupi waliwaambia CCM sisi hatushiriki na kura zetu hatuwapigii wapinzani wengine ili CCM ishinde.
Leo haijatimia hata miezi miwili katika jimbo la Konde kisiwani Pemba ambako kulikuwa na Mbunge anayetokana na ACT Wazalendo kabla ya kukutwa na umauti Chadema imesimamisha mgombea kwa lengo la kwenda kupambana na ACT na kuipa afueni CCM inayohaha kulitwaa jimbo hilo.
Maswali yangu Kwa wanachadema ni haya:
1. Je, tume huru imepatikana?
2. Lengo la ushiriki wa Uchaguzi huo ni lipi zaidi ya kuisaidia CCM jimbo la Konde?
3. Kwanini hawakushiriki uchaguzi wa Muhambwe na Buhigwe ambako CCM ilikuwa inatetea majimbo hayo,tofauti na sasa ambako Konde ACT ndiyo inatetea jimbo hilo?
Ni lini Chadema itaacha kuwapelekesha wanachama wake kama mazuzu kwa kuwaaminisha ambavyo haviaminiwi na viongozi wao?
CC Freeman Mbowe, Heche, Msigwa, Maria Sarungi.
Zaidi, soma: CHADEMA wachanganyana uchaguzi jimbo la Konde, Wadai Mgombea hawajampitisha wao