CHADEMA imewasaliti wafiwa wa Arusha? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA imewasaliti wafiwa wa Arusha?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by muhogomchungu, Jan 28, 2011.

 1. muhogomchungu

  muhogomchungu JF-Expert Member

  #1
  Jan 28, 2011
  Joined: Jan 9, 2011
  Messages: 375
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Baada ya siku 3, yalifanyika hitma ya marehemu. licha ya kuwa chadema sio chama cha kidini, lkn utu ni bora kuliko kitu, lkn kuna taarifa kwamba Chadema hawakumuwakilisha kiongozi yoyote katika kisomo kile. yaani vijana wanasema wameingia mitini tofauti na mazishi . jee mazishi kwa kuwa yakiangaliwa na mabolozi wa kimataifa kupitia redio na tv? kwa kuwa yalilelenga kuwaonyesha Chadema wameonewa? kuonyesha chadema imeshiriki kikamilifu.
  lkn swala la kuwafariji wafiwa sio kwa Pesa, kanga na Vitenge kwani waswahili wamesema Bora utu kuliko kitu.kama kweli chadema imesusa kisomo jee nini ilikuwa ya kushiriki mazishi?
  jee tutegemee nini baada ya miezi 6 kama hawa mashujaa hawatashaulika na chadema
  Kwani chadema haina viongozi wenye imani sawa na marehemu na kuwaakilisha? au ndio chadema sio chama cha kidini? jee inamaana hakuna kiongozi wake anaeishiriki katika missa?
  [​IMG]
   
 2. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #2
  Jan 28, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Gazeti lingine la HabariLeo ila safari hii lile linalotumia uji. Eeehh, leta umbea.
   
 3. M

  Mwera JF-Expert Member

  #3
  Jan 28, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 968
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  tatizo hamtaki kuambiwa ukweli,
  akukosoae anakupenda anataka ujirekebishe
   
 4. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #4
  Jan 28, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Du, ni kweli hata hivyo.

  Hebu tuanze basi kwanza na CCM waliosaliti taifa zima kwa karibia zaidi ya miaka 50 hivi sasa ndipo tukaeneze zaidi mapenzi yetu kwa vyama vingine vilivyokuja majuzi tu!!!
   
 5. Mtumiabusara

  Mtumiabusara JF-Expert Member

  #5
  Jan 28, 2011
  Joined: Nov 18, 2009
  Messages: 473
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33

  Hivi hitima huwa inafanyika baada ya siku 3? Hebu tueleweshe

  Pili je Chadema walipelekewa taarifa wakakataa kuhudhuria? lete taarifa kamili usitoe malalamiko kama huna details
   
 6. N

  Nonda JF-Expert Member

  #6
  Jan 28, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  muhogomchungu,
  Leo umekuja na hasira...umeanza na
  "Waziri wa CUF Zanzibar abariki upigwaji mwandishi wa channel ten " halafu "CHADEMA imewasaliti wafiwa wa Arusha?"

  CCM hawajafanya kosa lolote au baya lolote linalostahili sisi kulijua? Tuletee taarifa za upande wa CCM pia!
  Vizuri kukosoa upinzani lakini huwatendei haki wananchi kama hukosoi CCM ambayo ndiyo inayotuzidishia ugumu wa maisha kila leo.
  Au yote wayafanyayo CCM ni mazuri kwako?
   
 7. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #7
  Jan 28, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Nilidhani hitma hufanyika baada ya siku 40 au siyo?
   
 8. muhogomchungu

  muhogomchungu JF-Expert Member

  #8
  Jan 28, 2011
  Joined: Jan 9, 2011
  Messages: 375
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwani mazishi chadema walaikwa? kama mtu kafariki kwa ajili yao. mpaka aalikwe, wao si ndio wenyewe . au wamesusa tu kwa kuwa haitakuwa na faida kisiasa kwao. lkn huu ni usaliti mkubwa. sidhani kama ingalikuwa missa wangalingoja mwaliko
   
 9. muhogomchungu

  muhogomchungu JF-Expert Member

  #9
  Jan 28, 2011
  Joined: Jan 9, 2011
  Messages: 375
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hiyo ni arubaini sio kisomo.
   
 10. c

  carefree JF-Expert Member

  #10
  Jan 28, 2011
  Joined: Dec 19, 2010
  Messages: 265
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Bora uanze kutumia viazi vitamu uchungu wa hogo unakuharibu akili , ulitakiwa uhoji kwa nini serikali haikugharamia maziko ya iliyowauwa au kwako kosa ni yule cdm ambayo ilijitolea bila kuombwa wala kulazimishwa kuchukua jukumu la kusimamia maziko na watawapa wafiwa msaada wa kisheria walipwe fidia kwa vijana wao kuuwawa au kipengele cha mwisho ndio kimekuongezea uchungu wa hogo
   
 11. D

  DENYO JF-Expert Member

  #11
  Jan 28, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 699
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  wewe muhogomchungu ni vema wakati huu kwa mauaji ya arusha uliza wauaji wako wapi? Ukitaka kuandika saana uliza andenyenge bado yuko arusha anafanya nini? Kama unataka kuandika zaidi hebu andika kuhusu hizi sekondari za kata -nikupe mfano mbezi inn -kati ya wanafunzi 320 waliomaliza kidato cha nne -200 wamepata zero kabisa, 115 wamepata div iv,
   
 12. M

  Msindima JF-Expert Member

  #12
  Jan 28, 2011
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Hivi mleta mada alikua analenga nini sijaelewa, mbona nahisi kama imekaa kidini-dini?
   
 13. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #13
  Jan 28, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,604
  Likes Received: 4,725
  Trophy Points: 280
  Watu wa mihadhara hao, hamuwawezi kutwa nzima kubishana halafu wanataka maendeleo.
   
 14. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #14
  Jan 28, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Viongozi wa Chadema wana matatizo binafsi ni wapenda sifa ,hawana vitendo endelevu ,wakiona hili halina nguvu wanazua jingine ili kujijengea umaarufu ,wananchi wengi wameanza kuwasitukia.
   
 15. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #15
  Jan 28, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,604
  Likes Received: 4,725
  Trophy Points: 280
  Mwanaume kuwa mbeya haipendezi.
   
 16. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #16
  Jan 28, 2011
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Ndugu yangu tunaomba ufafanue vizuri hiki kitu unachokisema. ni nini ambacho Chadema hawakushiriki na hicho kitu kikoje? ukisema hitma, kisomo na arobaini sidhani kama vinaeleweka kwa kila mtu. Kila dini au kabila linaweza kuwa na utaratibu wake na utamaduni wake ambao wengine wanaweza kuufahamu au wasioufahamu na wanaweza kushirikishwa au la.

  Malalamiko yako yameanza tu katikati wakati hata watu wengine wanashindwa kukuelewa kwamba unazungumzia nini hasa.
   
 17. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #17
  Jan 28, 2011
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Ni kweli unachokisema ila wewe binafsi ni mbinafsi mkubwa. Chadema ni chama kinachoundwa na watu. wewe uko wapi kwa maana ya chama chako, je ubinafsi huo kwako huko haupo? Jaribu kulinganisha basi
   
 18. m

  mob JF-Expert Member

  #18
  Jan 28, 2011
  Joined: Dec 4, 2009
  Messages: 2,027
  Likes Received: 510
  Trophy Points: 280
  tujiulize mambo haya.
  je walitoa taarifa kwa viongozi husika
  pili je waliwashirikisha viongozi wote wa kitaifa

  kama hayo majibu yangeweza kujibiwa ndio tuanzae kuwalaumu viongozi wetu wa juu kwa kutofika hapa.ila kuna mabo yanafanyika ikitegemea kila mtu aanajua.
   
 19. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #19
  Jan 28, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Ahsante kwa kukubali kuwa nikisemacho ni kweli.
  Chadema ni chama kinachoundwa na watu kama vyama vingine ,mimi sina Chama kwani Chama kinawahusu viongozi wa Chama tu awe mdogo au mkubwa, kwa upande wangu mimi ni mpiga kura nilie huru ,kura yangu naipeleka pale ambapo ninaona pataniletea matumaini ya maisha mazuri na ya amani ,hivyo ushawishi unaojengwa na hao wenye vyama ndio unaonifanya nitoe maamuzi yangu kila baada ya miaka mitano.
   
 20. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #20
  Jan 28, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Jambo la kujitolea sio ungojee ushirikishwe ,wewe ni kiongozi ulitakiwa wewe uwepo mstari wa mbele aidha uwe unafuatilia ,sio ungojee kuletewa taarifa.
   
Loading...