CHADEMA imeupokea ushauri wa CCM na kuufanyia kazi... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA imeupokea ushauri wa CCM na kuufanyia kazi...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by VUTA-NKUVUTE, May 9, 2012.

 1. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #1
  May 9, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,868
  Likes Received: 6,566
  Trophy Points: 280
  CCM,ikiona inaikomoa na kuidhihaki CHADEMA,ilikiita chama hicho kikuu cha upinzani nchini-'chama cha msimu'.Ikawataka viongozi wa CHADEMA waimarishe chama chao hasa vijijini.CHADEMA wakasikia.Wakafanyia kazi.Sasa hivi hawashikiki.CCM wamebaki kuweweseka.Hapakaliki,hapaliki.CCM inazidi kudorora.Kama ni mgonjwa anaomba asali.

  Inavyoenea CHADEMA ni zaidi ya kimbunga.Sasa ni mtaa kwa mtaa,kijiji kwa kijiji,kata kwa kata,tarafa kwa tarafa,wilaya kwa wilaya na Taifa kwa ....I see!.Mimi pia nimejikuta nipo ndani ila kadi tu ndio sina.Sikumbuki ni lini na ni vipi wamenipata hawa Makamanda.CHADEMA si mchezo...........
   
 2. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #2
  May 9, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,196
  Likes Received: 1,977
  Trophy Points: 280
  CCM walikuwa wanafikiri itawawia ngumu kwa CDM kufahamika vijijini kumbe huko ndio rahisi kuliko hata mjini sasa hivi CDM inasambaa kama moto wa petrol CCM hata vijijini wanashindwa kwenda kwa kuogopa kupopolewa na mawe wamebakia kubeba dhambi ya kuua na kuwakatakata kwa mapanga viongozi wa CDM lakini hiyo haitazuia kuchimba kaburi lao
   
 3. s

  slufay JF-Expert Member

  #3
  May 9, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,372
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  CDM acheni kujifariji ninyi ni chama cha msimu ,,, CCm ni chama babu kubwa yenye tawi hadi maporini,,, Mfano mzuri enzi za mzee wa kiraracha ..... atawabomoa ZZZk halafu last MBOWEEEEEEEEEEEEEE
   
 4. H

  Honey K JF-Expert Member

  #4
  May 9, 2012
  Joined: Sep 14, 2008
  Messages: 629
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hah kwa taarifa tu ushauri wa CCM kwa Chadema haukuwa wa kukurupuka, ulimaanisha tunafurahi wamefuata ushauri hata kama kuna mahali wameteleza....MTUNGI UUFINYANGE MWENYEWE UKUPE TABU KUUVUNJA UKITAKA? ITAKUWA MAAJABU SANA, UCHONGE MWENYEWE KINYAGO KISHA KIKUTISHE MPAKA UNA KIMBIA... CDM fikirini mara mbili njia mliyofuata.   
 5. RUBERTS

  RUBERTS Senior Member

  #5
  May 9, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 136
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  We Nnauye Jr huko ni kuweweseka. Tatizo lako unakuwa mnafiki kupindukia. Kuwa mkweli bwana. Mwanasiasa makini ni yule anayekuwa mkweli daima. Wewe ni kijana lkn bado umekumbatia kasumba za kizamani za kukwepa ukweli. Zama hizo zimekwisha. Kizazi hicho kimepita. Siasa hizo hazina mshiko kwa sasa. Huko ni kujipa matumaini yasiyokuwepo. Kama unaogopa kutoa ukweli basi kuwa kimya. Hiyo ndo inaweza kuwa busara ya kukulinda anglau.
   
 6. d

  dguyana JF-Expert Member

  #6
  May 9, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 426
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kweli NAPE unaweweseka brother. Yaani 3d unaanzisha mwenyewe then unachangia mwenyewe. Da jiangalie kaka proganda zako za kizamani siku hizi watu tunajua kusoma na kuandika.
   
 7. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #7
  May 9, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,782
  Likes Received: 2,392
  Trophy Points: 280
  ccm inakufa vibaya sana kuliko chama cha KANU kenya!JK anaingia madarakani 2005 gas ilikua sh 18000 leo sh 58000 Kg15
   
 8. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #8
  May 9, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  hivi wewe kwa nini huimbi taarabu..maana maneno yako ni mipasho tupu.....hivi CCJ inaendeleaje
   
 9. Alfred Daud Pigangoma

  Alfred Daud Pigangoma Verified User

  #9
  May 9, 2012
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,778
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Join Date : 14th September 2008
  Posts : 288
  Rep Power : 552
  Likes Received296
  Likes Given0
  Inavyoonekana Nnauye jr, una matatizo ya akili tena akili mgando! jitafakari umekuwa member wa JF kwa muda mrefu sasa lakini kila unalolisema humu ndani ni MPUMBA * MAPOVU + KIDUMBWENDUMBWE = MZOGA-CCM. Ndo maana hata jamaa zako hawajawahi kukuunga mkono japo kwa kukupa "LIKE". Shame on U!!!!!:israel:
   
 10. Adolph

  Adolph JF-Expert Member

  #10
  May 9, 2012
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 870
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 45
  hivi wewe kijana mara ya mwisho kupima akili zako ilikua lini?hembu kacheki inawezekana uvuvuzela wako wa kujifanya unaponda magamba matatu wameshakuozesha akili na hujijui..kusoma huwezi hata kuona huoni????
   
 11. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #11
  May 9, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Acheni kujifariji kama askari wa Saddam.
  Hali ye ccm ni mbaya na inazidi kuwa mbaya.

   
 12. mbogo31

  mbogo31 JF-Expert Member

  #12
  May 9, 2012
  Joined: Nov 28, 2008
  Messages: 687
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Nilikuwa anagalau bado nafikiri wewe ni kijana makini napengine bado unajifunza na ungeweza kuwa kiongozi bora huko tuendako lakini kwa kauli yako hii nimekushusha sana, wewe kama kiongozi tena wa juu wa ccm hukupaswa kutoa kauli hii, yaani kwa kauli hii unadhirisha hujuma zote wafanyiwazo Chadema zinatoka kwenu, yaani umedhihirisha kitu kikubwa sana, siku nyingine fikiri kabla hujakurupuka.
   
 13. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #13
  May 9, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,736
  Likes Received: 1,447
  Trophy Points: 280
  Nape siamini,
  Umeendelea kuuthibitishia umma pasipo shaka kuwa CCM mliifanya nchi hii kuwa ni personal property. Kwamba mnaweza kuivunja/kubomoa amani na umoja wa kitaifa mkipenda.....maana ndio mambo mnayojisifia (kimakosa) kuwa mliyajenga.

  Nikutahadharishe kwa hizo mbinu na mikakati yenu michafu haitakuwa rahisi, na mtalipa gharama kubwa tu. Mark it!
   
 14. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #14
  May 9, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Nape na CCM wamevaa miwani ya chuma kama ya Mubarak!
   
 15. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #15
  May 9, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kama tu mwigulu naye alivyoilinganisha ccm na barcelona huku cdm akisema ni manyema fc kwenye uchaguzi wa arumeru mashariki.Na kweli ccm tuliuona ubarcelona wenu,ongezeni bidii kuichafua cdm lakini ukumbuke nyuki huwa hakumbatiwi...
   
 16. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #16
  May 9, 2012
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,288
  Likes Received: 597
  Trophy Points: 280
  You sound like you're comfortable and pleased with the outcome of your advice to CDM, are you?
   
 17. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #17
  May 9, 2012
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Siku zote serekali ya ccm imepewa msaada wa kuendeleza vyama vya siasa nchini kwahiyo hawana ubavu wa kuvivunja,maana waliotoa msaada wao wanaangalia pia,usitudanganye kuwa una ubavu wa kuvivunja hivi vyungu maana vimeshakomaa na vimekuwa vigumu sana kiasi kwamba ili uvunje na wewe utaumia bro,Kinyago unaweza ukakichonga mwenyewe lakini ukikiweka mahali pabaya ukakiangukia kitakujeruhi na huna cha kukifanya zaidi ya kukitupa.tetetete.
   
 18. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #18
  May 9, 2012
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,555
  Likes Received: 4,683
  Trophy Points: 280
  Hivi ni wewe Nape wa CCM au kuna mtu anatumia ID yako, mbona hoja zako hazilingani na wadhifa wako. Yaani umekuja kimipasho zaidi kuliko kujenga hoja.
   
 19. Bitende

  Bitende Member

  #19
  May 9, 2012
  Joined: Aug 20, 2011
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu ni kweli unayo yasema moto wa chadema unakasi ya ajabu ambayo hata ccm hawakutegemea maana jana nilienda kutafuta chakula cha usiku mida ya saa 3 bar nikamkuta mama mmoja kajifunga bendera ya chadema mabegani akiandikisha wanachama wapya nakutoa kadi kwa tshs.1,500.kwa mara ya kwanza nilizani ni mawakara wa tigo lakini niliposogea nikakuta ni mwana mama wachadema.nawapongeza kwakasi hiyo hakuna kulala kweli mpaka kieleweke kweli KAHAMA CHADEMA MMEJIPANGA KWA KASI YA MABADILIKO.
   
 20. Marunda

  Marunda Senior Member

  #20
  May 9, 2012
  Joined: Mar 3, 2010
  Messages: 115
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Nape, Ni vema kabla ya kuandika fikiri impact ya sentense zako. Tanzania sio mali ya CCM na nchi ni ya wantanzania wote. CCM haina mamlaka ya kuendelea kuongoza nchi kama wananchi hawahiitaji!! Na kumbuka wenye nchi hii ni pamoja na wanaJF.

  Kwa umri wako na utashi ulionao hukutakiwa kuandika sentense za namna hii. Kumbuka kwamba bado una safari ndefu katika umri wako na katika siasa za Tanzania. Ni vema kutulia na kusoma alama za nyakati na usikurupuke. Shame on you!!
   
Loading...