Francis12
JF-Expert Member
- Sep 30, 2016
- 7,533
- 22,276
Kaimu Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika anazungumza na vyombo vya habari muda huu.
Kaimu Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika John amelitaka Jeshi la Polisi kutoa kauli juu ya watu 40 waliokamatwa kwenye maandamano ya chama hicho February 16, 2018.
Mnyika amesema kama Polisi wakishindwa kuwapa dhamana na kuwatolea ufafanuzi ifikapo kesho basi wapelekwe Mahakamani.
Mnyika amesema Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, CHADEMA, kina taarifa za baadhi ya watu wanadhamiria kuwabambikizia kesi ya mauaji dhidi ya mwanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji, Akwilina Akwilina, pamoja na kesi ya kufanya maandamano bila ya kuwa na kibali cha jeshi la polisi.
Tunataka Kauli kutoka Serikalini kuhusiana na watu wetu kukamatwa na kushindwa kupelekwa Mahakamani je! Polisi wamepewa agizo na Serikali au laaa? na kama hawatatoa Kauli yoyote basi tutaifungulia mashtaka Serikali kwa kukiuka Sheria. Kaimu Katibu Mkuu Bara CHADEMA , John Mnyika.