Chadema imekosa hoja za kupambana na CCM na kwa mantiki hii wamekubali matokeo mapema

Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
8,708
5,711
Wahenga walishasema asiyekubali kushindwa si mshindani. Ila kukubali kushindwa hata kabla mtanange haujapigwa ni ishara mbaya sana.

Chadema kama chama kikuu cha upinzani sasa kinaonyesha dalili zote kuwa kimenyoosha mikono juu. Kama ni vitani sasa wameka silaha chini na wameshakuwa mateka.

Maana ili uweze kukichachafya chama kilichoshika dola lazima kifanye makosa ili upate hoja za kukishambulia na kukikosoa.

Lakini toka JPM aingie madarakani wapinzani wamekosa kabisa wapi wataikosoa serikali ya CCM, Maana huko nyuma ajenda ambayo walizoea kuikamata na kujipatia umaarufu ni ufisadi.

Nashangaa sana mpaka sasa wanashikilia kidedea hoja ya upotevu wa tril 1.5 na kutaka kujipatia umaarufu wakati PAC walitoa majibu bungeni kuwa kulifanyika maridhiano ya kimahesabu na hakuna ufisadi uliofanyika.

Nashangaa pia kuona wafuasi wa Chadema na wanachama wake wanapinga serikali kutekeleza miragi kama SGR, JNHPP, ujenzi wa miundo mbinu kama madaraja na barabara na wanajitoa akili kichwani kuwa hii miradi itakuwa na manufaa makubwa kwa taifa letu.

Lazima watambue kuwa ni kwa kuwa na kiongozi ambaye ana uzalendo wa hali ya juu ndio maana haya mambo yanafanyika. Maana kama mtu ana nia ya kufanya ufisadi alafu yupo ikulu nani atamzuia. Maana hata hiyo tri 6+ inayojenga JNHPP angeliamua kuihamishia Uswisi nani angelijua!
 
chagu wa malunde,

Chama cha matapel tu kile acha mbowe apige pesa huko huku watu wakiamini kuwa ni shujaa, Yule jamaa anachoongea kwenye mikutano yake na uhalisia wake kimatendo tofauti kabisa.

Hizo tuhuma zote wanasosema akina Waitara na Lijualikali kuhusu, ufisadi wa mbowe usifikir wanamzingizia ndiyo ukweli.

Ukitaka ujuwe Mbowe ni nani waza kugombania uenyekiti ndiyo utajuwa nguvu zake.




Sent using Jamii Forums mobile app
 
chagu wa malunde,

Chadema kwisha chali kabisa inasubiri kuzikwa october 2020. Chama gani kimejaa watukana matusi kama kina mdude na yule newton sijui nani wa temeke. Eti ukikosa hoja kupinga hoja unatukana matusi. Uongo na ubaradhuli kupinga mazuri ili eti ccm isipendwe. Wamekosea kudhani chama cha upinzani lazima lengo la kwanza ni kushika dola kumbe unaweza kuunga mkono mambo ya msingi na maendeleo.

Chama kimekusanya wenye hasira kwa kutumbuliwa kwa kila aina ya ufisadi na uzembe halafu kinalazimisha kuendesha dola wala hakipo madarakani. Ndio unaona kila rais akitoa muelekeo wa jambo muhimu hapohapo mbowe anajidai eti kuhutubia na yeye taifa. Ingetosha kuishia hapo mbaya wanalazimisha hoja zao kwa kujidai ndio wanajua na kejeli nyingi kwa rais wa jamhuri hadi utajua wametumwa na mtu.
 
Swali tena? Hoja ni nini mpaka useme kwamba CHADEMA wamekosa hoja na kwako wewe CHADEMA ni nini?
Mkuu usitake kukwepa ukweli mmekosa masuala ya msingi ya kuibana serikali. Yaani leo hii mnakomalia suala la tril 1.5? Wakati mwenyekiti wa PAC ni mbunge wa Chadema!
 
Mkuu usitake kukwepa ukweli mmekosa masuala ya msingi ya kuibana serikali!
Kwanza CHADEMA haina sababu ya kuibana serikali kwa kuwa serikali ni ya Watanzania. CHADEMA inapambamba na CCM ambayo ndiyo inayoiongoza serikali kwa niaba ya Watanzania.

Unaposema kiujumla kwamba CHADEMA imekosa hoja ya kuibana CCM ni kama vile CHADEMA ina jambo moja tu inayoisimamia!!
 
Kwanza CHADEMA haina sababu ya kuibana serikali kwa kuwa serikali ni ya watanzania. CHADEMA inapambamba na CCM ambayo ndiyo inayoiongoza serikali kwa niaba ya watanzania.

Unaposema kiujumla kwamba CHADEMA imekosa hoja ya kuibana CCM ni kama vile CHADEMA ina jambo moja tu inayoisimamia!!
Kwani nini hasa kuwa na mfumo wa vyama vingi? Ni kuhakikisha chama dola kinatekeleza ilani yake. Kama kikifeli ndio opposition inakosoa. Sasa CCM haijafeli.
 
CCM ni chama dola? Mbona kama unachanganya mambo. Unajua maana ya chama dola?

Turudi kwanza kwenye swali langu la msingi kwanza. Hoja ili iwe hoja inatakiwa iwe na sifa gani??
We hujui kama Ccm imekamata dola?
Hoja ni jambo la msingi linalotakiwa kuhojiwa ili kupata majibu.
 
We hujui kama CCM imekamata dola?
Kwa ivo CCM kukamata dola ndiyo kunaifanya iwe chama dola? Halafu nyie ndiyo watetezi wa CCM humu JF ambao hata hamjui maana ya "chama dola".

Hoja ni jambo la msingi linalotakiwa kuhojiwa ili kupata majibu.
Kwa ivo kama jambo la msingi ni kujenga daraja yule atakayeuliza litajengwa lini tayari ana hoja?? Kwenu nyinyi CCM hiyo ndiyo maana ya hoja?
 
Back
Top Bottom