CHADEMA imekiri kufadhiliwa kutoka nje ya nchi katika shughuli zake za kujijengea uwezo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA imekiri kufadhiliwa kutoka nje ya nchi katika shughuli zake za kujijengea uwezo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Uhalisia Jr, Sep 13, 2012.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Uhalisia Jr

  Uhalisia Jr Senior Member

  #1
  Sep 13, 2012
  Joined: Sep 10, 2012
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimekiri kufadhiliwa kutoka nje ya nchi katika shughuli zake za kujijengea uwezo.

  Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt Willibrod Slaa alisema hayo jana katika semina iliyoshirikisha baadhi ya viongozi wa chama hicho na wageni kutoka shirika la Chama cha Kikristo cha Ujerumani (CDU) la Konrad Adenauer Stiftung (KAS).

  Kwa mujibu wa Dkt. Slaa, CHADEMA na KAS, wamekuwa na ushirikiano wa karibu kwa miaka sita sasa na ushirikiano huo umelenga zaidi kukuza demokrasia nchini.

  Dkt. Slaa alidai kuwa CHADEMA ni chama chenye uwazi kwa kila mtu na katika uhusiano wao na KAS, hakiletewi fedha moja kwa moja kwa ajili ya operesheni au maandamano, ila kujijenga kiuwezo.

  "Kwa sasa kumekuwa na propaganda zinazoenezwa kwamba CHADEMA wanapata mabilioni ya fedha kutoka kwa wafadhili, hii si kweli, ila wanatujengea uwezo na si kutufadhili kampeni. Napenda kusema propaganda za aina hii zimepitwa na wakati na wote watakaozifanya tutawafungulia kesi," alisema Dkt. Slaa.

  "Wanaosema kwamba CHADEMA wanapokea mabilioni nao wanashirikiana na mashirika ya aina hiyo yenye mrengo mmoja na ni utamaduni duniani kote, vyama vyenye mrengo mmoja kushirikiana, hivyo hii dhana isipotoshwe," alidai.

  Pamoja na kusema kuwa KAS haitoi fedha moja kwa moja kwa CHADEMA kwa ajili ya maandamano na kampeni, lakini Dkt. Slaa alidai kuwa shirika hilo huwasaidia wastani wa Sh milioni 60 kwa mwaka kwa ajili ya machapisho na kutoa elimu.

  Pia alisema kipo chama cha Uholanzi ambacho hakukitaja jina, lakini akakiri kuwa huwafadhili Sh milioni 20 kulingana na idadi ya wabunge walio bungeni.

  Pamoja na kusema kuwa ni kawaida kwa vyama vya mrengo mmoja kusaidiana duniani, Dkt. Slaa alisema chama hicho cha Uholanzi kinachowasaidia, pia hufadhili CCM fedha zaidi ya zinazopelekwa CHADEMA kutokana na chama hicho tawala kuwa na idadi kubwa ya wabunge.

  Nape ashitakiwa

  Dkt. Slaa alidai kwamba kwa kuanzia wameamua kumshitaki Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.

  Kwa mujibu wa madai ya Dkt. Slaa, tayari CHADEMA imefungua kesi namba 186 ya mwaka 2012, katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam dhidi Nape, ambaye anadaiwa alitamka CHADEMA kufadhiliwa kutoka nje.

  Dkt. Slaa alidai kuwa kesi hiyo itakapokuwa ikiendelea, wataongeza watu wengine walioeneza kauli hiyo.

  Semina ya KAS

  Akizungumzia semina ya kujenga uwezo iliyotolewa jana kwa makada wa CHADEMA, Dkt. Slaa alisema imelenga kuangalia wanavyoweza kuleta uchumi wa soko utakaoshirikisha watu walio katika ngazi za juu na chini.

  Lengo la kushirikisha watu hao wa tabaka mbalimbali kwa mujibu wa Dkt. Slaa, ni ili raslimali za nchi zitumike kwa faida ya Watanzania wote ambapo pia mgeni kutoka KAS ambaye alipata kuwa Naibu Waziri wa Uchumi na Maendeleo wa Ujerumani, Klaus-Jurgen Hedrich atatoa mada.

  Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe alisema ili uchumi uwe endelevu, lazima wananchi wapewe haki na kuruhusu sekta binafsi kusimamia uchumi na si rahisi kusimamia uchumi kwa sera za kijamaa.

  via HabariLeo

  Source: wavuti - wavuti
  MY TAKE!

  Kila mtanzania anaefuatilia siasa za Tanzania anamfahamu ndugu NAPE NNAUYE tangu alipokua UVCCM na hatimae ukuu wa wilaya. Mabadiliko yake hasa alipokua mkuu wa wilaya ilibidi mtambue kua kelele alizokua akipiga UVCCM ilikua ni kutokana na kutaka kutimiza ndoto flani aliokua nayo, na pindi alipoona mwanga (Baada ya kua m/wilaya) mtazamo ukaanza kuota kutu. Hii ni kwa kua anajaribu kuonyesha ukweli ulio nyuma ya pazia tangu enzi za waliomlea (CCM).

  Kukimbizana na mtu kama huyu mahakamani ni kupoteza muda kwani mi ninamfahamu kama mtu wa maneno mengi hasa linapokuja suala la FEAR OF THE UNKNOWN.......
  CHADEMA endelezeni kile mnachoamini kitatutoa katika hali hii tuliyonayo na Watanzania wataamua katika sanduku la KURA katika chaguzi, CCM sera ni ileile iliyomtoa Rostam katika siasa(MAJI TAKA) japo si muumini wa kigezo hiki.

   
 2. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #2
  Sep 13, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,615
  Likes Received: 396
  Trophy Points: 180
  Nape tunamshughulikia kortini ila Nchembe tutadil nae jimboni.
   
 3. Mingoi

  Mingoi JF-Expert Member

  #3
  Sep 13, 2012
  Joined: Jul 21, 2012
  Messages: 10,408
  Likes Received: 1,877
  Trophy Points: 280
  Funguka Dr taja na huyo mfadhili mwengine isije ikawa hao wa uholanzi ni chama cha kutetea mapenzi ya jinsia moja.
   
 4. MAFILILI

  MAFILILI JF-Expert Member

  #4
  Sep 13, 2012
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 1,884
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Kwenye ukweli, uwongo unawekwa pembeni. CDM ni chama cha KIKRISTO, WAISLAM hamna chenu CDM
   
 5. m

  mtznunda Senior Member

  #5
  Sep 13, 2012
  Joined: Sep 15, 2011
  Messages: 143
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  said arfi,chiku abwao,abdallah safar,zitto na wengine kataka yangu mnasubiri nn tena hilo lipo wazi halihitaji tochi.mrengo mmoja hao(deception)
   
 6. Uhalisia Jr

  Uhalisia Jr Senior Member

  #6
  Sep 13, 2012
  Joined: Sep 10, 2012
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Lete facts kuprove unachokisema kaka sio kama ulivyochangia, unaonekana uko katika msitu wa kilichojazwa kichwani mwako na hata kushindwa kufikiria. Hii hua kasumba ya mtu asiekua na uwezo wa kufikiri kwa kukosa elimu na huchukua mambo kama anavyoambiwa hata na mtoto aliemalixza darasa la 7.

  Open your mind and be neutral kujua mambo haya.
   
 7. S2dak_Jr

  S2dak_Jr Senior Member

  #7
  Sep 13, 2012
  Joined: Jul 15, 2012
  Messages: 198
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Viroba vya saa moja asubuhi vinafanya kazi.

  Hujaliona lile la kusajili meli za waislamu wenzenu mpaka Obama akawapiga mkwara.
   
 8. MAFILILI

  MAFILILI JF-Expert Member

  #8
  Sep 13, 2012
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 1,884
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Hilo liko wazi CDM ina mlengo wa KIKRISTO, Dr Slaa kaapa kutekeleza matakwa ya KANISA maishani mwake
   
 9. Mu-Israeli

  Mu-Israeli JF-Expert Member

  #9
  Sep 13, 2012
  Joined: Mar 21, 2012
  Messages: 2,456
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Mimi naona tungeanzia kwa mfadhili huyu hapa kwenye picha.
  Angalia vizuri picha hii ambayo JK yuko na mfadhili. JK anashirikiana na mfadhili huyu !!
  Unamfahamu vizuri mfadhili huyu ?? Basi hebu angalia vizuri hapo kwenye maandishi ya rangi ya blue !!
  Hapo vipi ?? (Hii kauli ya "Hapo Vipi ??" ni kwa hisani ya Edward Lowassa !!
   

  Attached Files:

 10. Kalumbesa

  Kalumbesa JF-Expert Member

  #10
  Sep 13, 2012
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,009
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Samahani wanajukwaa naomba kuuliza eti source ya habari ni gazeti la HABARI LEO au UHURU?
   
 11. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #11
  Sep 13, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,082
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 0
  Kwa kukiri tu Slaa baada ya Nape kutangaza hadharani, Nape kisha shinda kesi, Chadema waandae kulipa gharama za kesi na kumlipa fidia Nape. Piga pangua, wala kujidai kukiri sasa hivi hakusaidii kitu.

  Siku zote huwa tunasema humu, hiki chama kina ufadhili wa kidini ya Kikristo, watu wanakuja juu, Nape katekenya watu wameachia.
   
 12. cacico

  cacico JF-Expert Member

  #12
  Sep 13, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 8,392
  Likes Received: 127
  Trophy Points: 160
  Job true true!
   
 13. Mingoi

  Mingoi JF-Expert Member

  #13
  Sep 13, 2012
  Joined: Jul 21, 2012
  Messages: 10,408
  Likes Received: 1,877
  Trophy Points: 280
  Bado shirika la Jesuits (Society of Jesus),mayor wa london na Sabodo, sorry nilijua nae ni mzungu kumbe ghaba choli.
   
 14. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #14
  Sep 13, 2012
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Dokta Slaa mbona unaanza kuchanganyikiwa hata mahakamani ujafika si mmefungua kesi mkipinga Chadema hawana wafadhili kumbe Nape yupo sahihi.
   
 15. yaser

  yaser JF-Expert Member

  #15
  Sep 13, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 1,375
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  kiukweli chadema sasa msitaje hawa wafadhili hadharan coz mtapoteza wanachana wenu.hawa wazungu tena wakristo kwa nchi km tanzania c nzur sana kupublish.halafu mzungu cku zote ana kamsemo kake anasema "no economic aid without political interest" sasa hapa watanzania tuwe macho zaid kuliko tulivyokua macho kwenye tukio la mwangosi.kila hatua lazma tulifuatilie icje ikawa heri ya ccm walivyouza nchi yetu kuliko watakavyokuja kugawa hawa cdm.
   
 16. S2dak_Jr

  S2dak_Jr Senior Member

  #16
  Sep 13, 2012
  Joined: Jul 15, 2012
  Messages: 198
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hebu jaribuni kumuelewa Dr. Slaa. Hakusema kuwa KAS ni wafadhili wa CDM bali wanawawezesha katika seminars kwa kuleta wataalamu wa kutoa mada.
   
 17. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #17
  Sep 13, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 10,995
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Na walaaniwe wote wenye maneno,fikiri finyu kama hii ya kwako!


   
 18. m

  mamajack JF-Expert Member

  #18
  Sep 13, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,163
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  hakuna chama kisichokuwa na wafadhili au marafiki,tunachotaka nape atudhihilishie ni yale mapesa ya kutishia kuuza nchi,hiki ndo tunasubiri huko mahakamani,kama ni pesa ya kuendeleza chama,hata magamba wanapata pesa nyingi kuliko chama chochote,sie tunachotajka kukiona ni hicho cha kutishia nchi kuuzwa,and nape alisema anaweza kuprove maana ana vidhibitisho,subiri mahakama ifanye kazi yake.hatutaki akiri dhaifu kuiongoza akiri imara,
   
 19. Kakende

  Kakende JF-Expert Member

  #19
  Sep 13, 2012
  Joined: Aug 18, 2012
  Messages: 2,734
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mimi nina wasi wasi na elimu tunayopewa watanzania, kwanini mnapandikiziwa udini nanyi mnakubali? Hivi sabodo alipowafadhili CHADEMA yeye ni mkristu? mbona hamkusema kuwa CHADEMA ni chama cha waislam kwa kuwa sabodo ni Mwislam?
   
 20. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #20
  Sep 13, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,082
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 0
  Nape kisha shinda kesi, hilo hamkwepi hata mseme nini.
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...