Chadema imeishinda CCM

Stephano

Member
Dec 30, 2008
27
4
Wadau kuna hoja kwamba nchi kuingia kwenye mgao ni sehemu ya ushindi wa CHADEMA dhidi ya CCM ambao wamefanikiwa kuisambaratisha CCM na kuifanya kipoteze muelekeo kiasi cha kusababisha CCM kugawanyika na kushambuliana wao kwa wao na kisha kushindwa kufanya maamuzi yenye maslahi kwa taifa hadi kufikia hali hiii ya mgao. imekaaje hii?
 
Hili sio kweli. Haya mambo ya mgawo wa umeme yamekuwapo miaka nenda rudi. Vyanzo vya nishati ya umeme tunavyo vingi sana. Kwa mfano: tukiamua kujenga kituo cha kuzalisha umeme pale Stiegler gorge nasikia tutapata zaidi ya 3,000 MW. Sasa hivi mahitaji ya Tanzania hayazidi 800 MW. Nionavyo huu uvivu ndani ya viongozi serikalini kufanya maamuzi yenye faida kwa ajili ya nchi yetu.
 
Hiyo haijakaa vizuri. CHADEMA ingeshinda kama mgao ungekuwa unawaumiza wanaCCM tu. Hu mgao ni maumivu kwa Watanzania wote. Ushindi huwa unasheherekewa na hapa hamna cha kusheherekea. Tumeshindwa wote kwa kukipa chama cha wababaishaji ridha ya kutuongoza.

.
 
Hili sio kweli. Haya mambo ya mgawo wa umeme yamekuwapo miaka nenda rudi. Vyanzo vya nishati ya umeme tunavyo vingi sana. Kwa mfano: tukiamua kujenga kituo cha kuzalisha umeme pale Stiegler gorge nasikia tutapata zaidi ya 3,000 MW. Sasa hivi mahitaji ya Tanzania hayazidi 800 MW. Nionavyo huu uvivu ndani ya viongozi serikalini kufanya maamuzi yenye faida kwa ajili ya nchi yetu.

Na hiyo Serikali ni ya chama gani kama si CCM?
 
CCM na Serikali yake wameshindwa kuamua ni nini kifanyike Tanzania ili tuondokane na uhaba wa nishati ya umeme.

Wengi wa viongozi wao wanakazania mitambo ya dizeli na gesi ili inunuliwapo wapate commission. Ni ufisadi wao unatukwamisha na kwa kuendelea na mgao tutaangamia.

Mafisadi wanajua kwamba mitambo ya kutumia maji kama ya maporomoko ya Stieglars' Gorge itawakoseshea mlungula kwa miaka mingi.

Hakuna njia ya Tanzania kujikwamua kutoka katika janga hili la mgawo wa umeme ila kuwatoa CCM madarakani. Na ni Chadema wameonyesha ni wabunifu, ni jasiri kutumia raslimali zetu kwa maslahi yetu na ni wazalendo walio na huruma na wananchi wanyonge wanaoteseka kwa kukosa ajira na huduma za kiafya etc.

Hakuna ubishi. Chadema imeshinda CCM kwa ubunifu, uzalendo, kwa ujasiri ktk kutumia raslimali kwa maslahi ya wananchi na, zaidi ya yote, kwa kutokuwa mafisadi.
 
Hili sio kweli. Haya mambo ya mgawo wa umeme yamekuwapo miaka nenda rudi. Vyanzo vya nishati ya umeme tunavyo vingi sana. Kwa mfano: tukiamua kujenga kituo cha kuzalisha umeme pale Stiegler gorge nasikia tutapata zaidi ya 3,000 MW. Sasa hivi mahitaji ya Tanzania hayazidi 800 MW. Nionavyo huu uvivu ndani ya viongozi serikalini kufanya maamuzi yenye faida kwa ajili ya nchi yetu.

Mkuu inaonyesha hujamwelewa mtoa mada, amesema hamuoni kama chadema imeichanganya ccm mpaka kufikia kushindwa kukaa pamoja na kutoa maamuzi ambayo yangeiepusha nchi katika giza? tunajua kuwa uwezekano wa kuwa na umeme hata wa kuuza nje tunao sana tu, lakini huoni kama wanashindwa kufanya maamuzi kutokana na kuchanganywa na chadema?
 
Siyo uvivu mzee, kama ingekuwa uvivu basi mahela yote yangekuwa bado yapo kule hazina, BOT etc... NI WIZI MZEE. nNa ndiyo maana kazi hazijafanyika na hela zimeibiwa....
 
Hivi tunazijua sera za chadema kuhusiana na maswala ya nishati na madini ,manake ccm ni marehemu wako ndani ya masanduku ni wakufukiwa tuu,nchi yenye vijito mito bahari na gesi bado inaingia gizani halafu watu wanapanda ndege kwa kodi yetu wakizunguka dunia nzima kujisherehesha tuu ,ni vile watanzania tumezubaa tungeamua wote kwenda kulala pale mlangoni ikulu mpaka mashine ya IPTL iwashwe ,wanatufanya tunakula mlo moja kwa siku kwa sababu icecream zetu hazigandi tukauza
 
sisi ccm tuacheni tu jamani...nchi hii tumeipata kwa taabu sana hatukuwa hivi tafadhari........tuacheni tugawane maana hii ni nchi yetu wapinzani mtaishia kupiga makelele tu....sisi uchaguzi ukifika tunaelekea zetu vijijini ambako tuna wapiga kula wengi tunagawa kanga,kofia,yeboyebo,na pipi kwa watoto ili tupigiwe kura ili tuendelee kula....chadema sisi hawatuchanganyi mambo ya ufisadi tumeanza zamani ila tulikuwa tunaogopana sana tofauti na sasa ambapo tumekaa vikao vya kuwaruhusu wanachama wetu kusulubiana wao kwa wao..hayo yote ni kuimarisha nchi na uongozi.........jamani sisi ccm madini yetu,kila kitu ni chetu msituulize iwapo mikataba tuliyoingia ni mizuri au mibaya nyie jalini shughuri zenu tuacheni tulivyo na mtukome na pia hatutaki mtugombanishe na chadema kwani wale ni marafiki zetu na baadhi ya viongozi wake ni mamruki ambao tumewapandikiza ili kuudhoofisha upinzani ndio maana tunaamua kuwaachia majimbo mengine
SISI CCM TUNASEMA TUACHENI TUFAIDI MATUNDA YA JASHO LETU......
 
Mkuu inaonyesha hujamwelewa mtoa mada, amesema hamuoni kama chadema imeichanganya ccm mpaka kufikia kushindwa kukaa pamoja na kutoa maamuzi ambayo yangeiepusha nchi katika giza? tunajua kuwa uwezekano wa kuwa na umeme hata wa kuuza nje tunao sana tu, lakini huoni kama wanashindwa kufanya maamuzi kutokana na kuchanganywa na chadema?

King Louis wa Ufaransa aliondolewa enzi hizo shauri ya boflo ( mikate ) sembuse umeme.
 
Wadau kuna hoja kwamba nchi kuingia kwenye mgao ni sehemu ya ushindi wa CHADEMA dhidi ya CCM ambao wamefanikiwa kuisambaratisha CCM na kuifanya kipoteze muelekeo kiasi cha kusababisha CCM kugawanyika na kushambuliana wao kwa wao na kisha kushindwa kufanya maamuzi yenye maslahi kwa taifa hadi kufikia hali hiii ya mgao. imekaaje hii?
Hujaeleweka? je hayo ndiyo malengo ya mwaka huu ya Chadema?..
 
Back
Top Bottom