CHADEMA iliyoshindwa kujifanyia mageuzi inatuaminishaje tukiwapa nchi watafanya mageuzi?

The Phylosopher

JF-Expert Member
Mar 11, 2015
1,015
2,000
CCM ipo madarakani kwa sababu ni chama dola. Huwezi kutofautiana CCM na fola. Ndio maana Jaji Mkuu Ramadhani aligombea kupitia CCM; IGP Mahita aligombea ubunge huko morogoro kupitia CCM; Afande Tibaigana pia; General Mboma aligombea Mbeya Vijijini kipindi Fulani akashindwa kwa tiketi ya CCM bila kumsahau Hassy Kitine Mkurugenzi wa TISS amewahi kuwa mbunge wa CCM na mwisho Salim Jecha mwenyekiti wa Time ya uchaguzi Zanzibar aligombea urais kupitia CCM. Siku CCM ikijitenga na dola ndio utakuwa mwisho wake.
Kwa hizi hoja zako ilikuwaje chadema wakashinda kura million 7 kasoro
 

The Phylosopher

JF-Expert Member
Mar 11, 2015
1,015
2,000
Uvimilivu una kiasi. Uvimilivu bila kiasi ni ujinga. Lazima utofautishe wapi pa kuvumilia na wapi pa kusema ukweli. Yani Makamu mwenyekiti wa CHADEMA apigwe risasi; Msaidizi wa mwenyekiti auwawe na mwili wake usijulikane ulipo; Mwenyekiti wa CHADEMA abambikiwe kesi ya ugaidi na wabunge 19 Viti maalum wateuliwe bila baraka za chama. Nani anaweza kuvumilia, was Kwanza anayetakiwa kuwa na uvimilivu wakisiasa ni CCM. Kama CCM haina uvimilivu wa kisiasa hakuna chama Cha siasa Cha upinzani kitachokuwa na uvimilivu.
Tuache visingizio yaani chadema ingekaza kidogo tu ingetoboa ila sasa tatizo ni wabishi balaa
 

Mchokolo

JF-Expert Member
Oct 24, 2021
222
500
Tunashuhudia wafuasi wa CHADEMA humu mitandaoni wakiwa na imani kubwa sana na chama chao huku wakiwaamini viongozi wao mithili ya miungu watu kwamba eti tukiwapa ridhaa ya kuongoza nchi basi watafanya mambo makubwa kwelkweli.

Mbaya zaidi ni kwamba hata inapotokea failure ya mtu binafsi ndani ya serikali wao utawasikia wanalaumu akili za wanaccm.

Niwaambie ukweli tofauti kati ya ccm na CHADEMA ni ndogo kwa sababu kiongozi huandaliwa na mifumo ya malezi na makuzi elimu uzoefu pamoja na uwezo binafsi.

Kwa mantiki hiyo sitarajii jipya lolote kwa kuwa mifumo iliyowaandaa ccm ndiyo huwaandaa CHADEMA .

Nafasi pekee ambayo wangeitumia ni uwezo binafsi ambao nao sioni kama wanao maana tangu niifahamu CHADEMA haijabadili kitu chochote zaidi ya KUONDOA ukomo wa mwenyekiti.
Hapo ndipo uwezo wako wa kufikili ulipoishia??
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom