CHADEMA iliyoshindwa kujifanyia mageuzi inatuaminishaje tukiwapa nchi watafanya mageuzi?

Uvimilivu una kiasi. Uvimilivu bila kiasi ni ujinga. Lazima utofautishe wapi pa kuvumilia na wapi pa kusema ukweli. Yani Makamu mwenyekiti wa CHADEMA apigwe risasi; Msaidizi wa mwenyekiti auwawe na mwili wake usijulikane ulipo; Mwenyekiti wa CHADEMA abambikiwe kesi ya ugaidi na wabunge 19 Viti maalum wateuliwe bila baraka za chama. Nani anaweza kuvumilia, was Kwanza anayetakiwa kuwa na uvimilivu wakisiasa ni CCM. Kama CCM haina uvimilivu wa kisiasa hakuna chama Cha siasa Cha upinzani kitachokuwa na uvimilivu.
Tuache visingizio yaani chadema ingekaza kidogo tu ingetoboa ila sasa tatizo ni wabishi balaa
 
Tunashuhudia wafuasi wa CHADEMA humu mitandaoni wakiwa na imani kubwa sana na chama chao huku wakiwaamini viongozi wao mithili ya miungu watu kwamba eti tukiwapa ridhaa ya kuongoza nchi basi watafanya mambo makubwa kwelkweli.

Mbaya zaidi ni kwamba hata inapotokea failure ya mtu binafsi ndani ya serikali wao utawasikia wanalaumu akili za wanaccm.

Niwaambie ukweli tofauti kati ya ccm na CHADEMA ni ndogo kwa sababu kiongozi huandaliwa na mifumo ya malezi na makuzi elimu uzoefu pamoja na uwezo binafsi.

Kwa mantiki hiyo sitarajii jipya lolote kwa kuwa mifumo iliyowaandaa ccm ndiyo huwaandaa CHADEMA .

Nafasi pekee ambayo wangeitumia ni uwezo binafsi ambao nao sioni kama wanao maana tangu niifahamu CHADEMA haijabadili kitu chochote zaidi ya KUONDOA ukomo wa mwenyekiti.
Hapo ndipo uwezo wako wa kufikili ulipoishia??
 
Back
Top Bottom