CHADEMA ikigundulika mnadanga, kwenye hili hamtapona

Kumekuwa na maneno kwamba uchumi unaenda vibaya na kwamba kuna mtikisiko wa uchumi. Hizi habari zimeenea hasa katika mitandao huku mamlaka rasmi zikikana taarifa hizo.

Siyo hivyo tu lakini hata wataalamu wa maswala ya fedha, uwekezaji na uchumi hatujawasikia wakilizungumzia hili.

Siyo hao tu lakini hata kurugenzi za fedha za CHADEMA hazijaongea lolote kuhusu hili swala.

Sasa angalia madhara ya haya maneno:

=>Watu waliotaka kuwekeza ziada ya akiba yao katika biashara wanaogopa kufungua biashara kwa sababu ya hayo maneno.

=> Baadhi ya wanafunzi waliotaka kujiunga na masomo ya chuo kikuu wamebadili kozi hasa wale ambao wanaona kozi hizo hazitakuwa na manufaa katika uchumi ukiodorora. Mfano kozi kama za usimamizi wa biashara(Finance, Accounting, Marketing, HRM,), banking, engineering kama civil. Kumbuka hawa watu walizipenda hizo taaluma lakini hawawezi kusoma kitu ambacho hawakuwa na manufaa nacho iwapo mdororo wa uchumi utatokea.

=> Watu walioajiriwa hasa katika sekta binafsi wanafanya kazi kwa msongo wa hali ya juu. Wangine wanaogopa kupoteza ajira wakati wengine wana hofu ya biashara zao kufirisika. Sasa hii inapelekea watu kufanya maamuzi kulingana na taarifa hizi ambazo wengine hatuamini kama ni za kweli au za uongo.

Sasa sheria ya tatu ya Newton ya mwendo inasema: "to every action there is equal and opposite reaction".

Watu mtakaoweza kuwalaghai hao hao watakuwa kinyume chenu iwapo itagundukika maneno yenu yalikuwa ni uongo na nia yenu ilikuwa ovu. Watu watakosa imani na nyie.
Hii inamadhara yale yale kwa CCM hasa pale itakapogundulika walidanganya uma na kuisababishia nchi kuangukia mdororo wa uchumi.
Nashauri ruzuku za vyama ziondolewe ili pesa hizo zisaidie kuinua uchumi.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom