CHADEMA ikifanikiwa kuwashawishi wanawake, CCM itayeyuka kama barafu juani! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA ikifanikiwa kuwashawishi wanawake, CCM itayeyuka kama barafu juani!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gosbertgoodluck, Jan 23, 2011.

 1. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #1
  Jan 23, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  WanaJF na hususan viongozi wa CHADEMA,

  Ninaandika thread hii nikiwa serious kabisa. Nimetazama mikutano mingi ya CHADEMA na ya CCM na kubaini tofauti kubwa ya mahudhurio ya wanawake. Ni jambo lisilopingika kwamba watu wanaojaa sana kwenye mikutano ya CCM ni wanawake. Kinyume chake, watu wanaojaa sana kwenye mikutano ya CHADEMA ni wanaume, wazee na vijana. Mfano mzuri ni mkutano uliofanyika Mabibo. Ukiangalia kwa makini utabaini kuwa ninachoongea kina ukweli ndani yake.

  Ndugu zangu viongozi wa CHADEMA, tusibeze umuhimu wa wanawake katika ukombozi wa taifa letu kutoka kwenye makucha ya chama kinachowahifadhi na kuwapalilia mafisadi. Lazima iwekwe mikakati ya sayansi jamii ya namna ya kubadili fikra potofu walizopandikiza CCM kwenye vichwa vya mama zetu kiasi cha kuamini kuwa bila CCM amani ya nchi hii itatoweka. Akina mama wengi (na siwalaumu kwa hilo) ni wahanga wa vurugu zinazotokea maeneo mengi Duniani. Wengi wao ni waoga. Wanaona bora waendelee kuteseka na hali ya mbaya ya maisha lakini siyo kwa vurugu za kubakwa, kupigwa risasi na kuishi kama wakimbizi ugenini, n.k. Wenzenu wa CCM wameiona hiyo 'potential' na wamebuni 'injili ya vitisho' na wanaihubiri barabara kila wanapopata fursa hiyo adhimu.

  Ushauri wangu kwa viongozi, wanachama na wapenzi wa CHADEMA, waanze mara moja kupanga mikakati ya kubadili fikra ya kundi hili kubwa la wapiga kura. Tusibeze hata mara moja umuhimu wa kundi hilo katika ukombozi wa nchi yetu. Kazi kubwa imefanyika ya kumobile watu lakini bado kuna kazi nyingine ya kumobilize akina mama.

  Hilo likifanyika, CCM itachinjiliwa mbali na kuzikwa maana hata mbinu zao za kuchakachua matokeo hazitafua dafu, itayeyuka kama barafu juani.
   
 2. V

  Vumbi Senior Member

  #2
  Jan 23, 2011
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 191
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Well said, viongozi wa CDM kama mpo hapa JF tafadhali lifanyie kazi.Vijana wa kike waliopo mashuleni na vyuoni kama tukiwapata kwenye chama watakuwa na impact kubwa sana kwenye kukiimarisha chama vilevile watakuwa mabalozi wazuri wa kuwashawishi wanawake wengine kujiunga na CDM. Lazima mfahamu kuwa CCM imeshaona umuhimu wa vijana na inatumia njia mablimbali kuhakikisha inawateka.
   
 3. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #3
  Jan 23, 2011
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Uliyosema ni kweli.

  Katika siasa, huwezi kuwavuta wafuasi kwa nguvu bali unavutia kwako kutokana na sera zako. CHADEMA inatakiwa itafsiri sera zake kwa lugha zaidi sana kufikia interest za wanawake. Wanawake wana tabia ya kuheshimu status quo sana, kwa hiyo ni lazima CDM wajifunze kuonyesha jinsi gani status quo siyo nzuri kwa wanawake wa Tanzania katika mazingira ya leo.

  Nilivyomwangalia Dr Slaa kwenye ule mdahalo wa ITV, aliweza sana kuunganisha kwa ufanisi mkubwa sana sera za CHADEMA na maslahi ya vijana na Tanzania kwa jumla, lakini nadhani hakulenga kudni la wanawake wa Tanzania kwa jumla. Ni muhimu wakati huu CHADEMA iweke makundi matatu ya kufikia, wanawake, vijana, na wanaume katika viwango vyote vya elimu.
   
 4. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #4
  Jan 23, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu sijui mnakumbuka wakati wa kampeni kuna ahadi moja ilitolewa na CCM ya kuwanunulia wanawake bajaji ili ziwasaidie wakati wa kwenda kujifungua.

  Sisi tuliibeza ahadi hiyo kwani tulijua ni kebehi kwa akina mama zetu. Lakini ukitulia na kufikiri na kupata picha halisi ya mateso wanayopata akina mama ikiwemo hilo la kukosa huduma za uzazi, utaona kuwa CCM walitumia mwanya huo kuvuta hisia za akina mama. Nimeongea na akina mama kadhaa mitaani wengi wao wanasema ni bora chama kinachozungumzia angalau matatizo ya akina mama kuliko chama kisichogusia kabisa masuala ya akina mama. Hii ni changamoto kubwa kwa CHADEMA.

  Inawezekana sera za CHADEMA zinamgusa mwanamke vizuri kuliko CCM lakini tatizo linaweza kuwa ni kutoziongelea sera hizo majukwaani kwa lugha nyepesi inayoeleweka kwa wanawake.
   
 5. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #5
  Jan 23, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Kuna msemo unasema "ukimwelimisha mwanamke, umeelimisha jamii nzima"
  Nakubaliana na mtoa mada kwa asilimia mia.
   
 6. Joss

  Joss JF-Expert Member

  #6
  Jan 23, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 729
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Pointi nzuri,

  Kama CHADEMA watafanikiwa kuwa na kiongozi wa ngazi ya juu kama m/kiti au makamu m/kiti,katibu mkuu au naibu k/mkuu ambaye ni mwanamke, halafu wakawa na mpango maalum wa kuwakomboa wanawake kifikra na kivitendo kama kurusha vipindi vya kuwaelimisha wanawake katika tv, kuhusu maisha bora yanavyoweza kupatikana kwa kupitia nguvu ya wanawake pamoja na umuhimu wa siasa safi.

  Ikiwezekana waanzishe mfuko maalumu wa wanawake ambao utakuwa unatumika kusaidia mahitaji mbalimbali ya wanawake kama uzazi mahospitalini n.k. Labda hiyo itasaidia.
   
 7. V

  Vancomycin Senior Member

  #7
  Jan 23, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 171
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mtoa mada nakubaliana na wewe ila napenda nitoe mtazamo wangu wa kisayansi.

  Inaelezwa kuwa wanawake hutumia both cerebral cortex hemispheres katika kufikiri lakini wanaume hutumia left cerebral hemisphere na kutafsiriwa kuwa kwa mwanamke mwenye umri sawa na mwanaume utaona mwanamke huweza kufikiri kwa haraka na kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja.

  Wanasaikolojia wameenda mbali nakueleza kuwa wanawake kwa kiasi kikubwa huendeshwa kwa hisia zaidi tofauti na wanaume ambao wenyewe wamesimama katika facts.Kwa sababu hii unaweza shangaa aidha wanavutiwa tu na rangi,namna mtu anyoongea,sura nk. tofauti na wanaume ambao wanasimamia facts.

  Mfano sehemu kubwa ya watu wanaoibiwa kwa kulaghai ni wao hata michezo kama kekundu. Kwa hiyo si ajabu kwa kundi hili kubaki nyuma. Kwa kuelewa hili na kwa sababu CHADEMA kinaendeshwa kisayansi wanahitaji kutumia saikolojia na elimu kwani elimu ndiyo kila kitu.

  Baraza la wanawake lina kazi ya kufanya kwa pamoja na jumuiya nyingine katika kuwafikia wanawake wote. Si wao tu pia liwe jukumu la kila mpenda mabadiliko kuwaelimisha kwani ni dada zetu, mama zetu, wake zetu na hata marafiki zetu.
   
 8. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #8
  Jan 23, 2011
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Napendekeza tuliooa tuwahamasishe wake zetu kuwa wana CDM hai, wawalike marafki zao kujiunga na Chadema.

  Nikiwa eneo la kikazi kuanzia sasa ntaanza kuwahoji wanawake wana mtazamo gani kuhusu siasa ya Tz.
   
 9. bullet

  bullet JF-Expert Member

  #9
  Jan 23, 2011
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 959
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Ni kweli wanawake ni watu muhimu katika kuleta mapinduzi ya nchi yoyote! lakini turn up yao katika siasa imekuwa ni ndogo, mfano hata pale Nkurumah kwenye mdahalo wa katiba wanawake walikuwa wachache sana mpaka mama Nkya akalalamika! Something ought be done!
   
 10. m

  mzambia JF-Expert Member

  #10
  Jan 23, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  kweli kabisaaaa
   
 11. Ngalikivembu

  Ngalikivembu JF-Expert Member

  #11
  Jan 23, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 1,908
  Likes Received: 355
  Trophy Points: 180
  CDM iwe na kitengo maalum cha wanawake ili 2015 tuwateke.Ahadi wanazopewa hawatekelezewi.Lakini niwakumbushe wan CDM kuwa wasifanye makosa ya kutoanza kampeni za vijijini mapema.wasisubiri had uchaguzi unakaribia.huu ni wakati wa kujipanga.waje huku vijijini waongeze wanachama.
   
 12. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #12
  Jan 23, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Hamna washawishi wazuri kwa wanawake kama wanawake wenzao..ni swala la imani!Ndo maana mke wa kikwete alikua active wakati wa kampeni..ile iliwavuta wanawake wengi sana..hata wasioelewa faida na hasara za kuchagua ccm!Nawashauri CDM wawatumie vizuri wanawake ambao tayari wamepata mwamko wa ukombozi kuwashawishi wale ambao bado!!Ukombozi daima!
   
 13. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #13
  Jan 23, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Mbona umechelewa ndugu yangu!! Wengine kazi hiyo tumemaliza zamani sana kabla hata ya uchaguzi uliopita. Mimi binafsi nyumba yangu nzima tunaiunga mkono cdm. Tena basi, mke wangu ndiye yupo mstari wa mbele kushawishi wanawake wenzie waisupport cdm.
   
 14. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #14
  Jan 23, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Asante sana kwa kufafanua zaidi kwa mtizamo wa kisayansi. Ni matumaini yangu kuwa viongozi wa cdm watayafanyia kazi seriously mawazo ya wachangiaji wa hoja hii.
   
 15. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #15
  Jan 23, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,421
  Likes Received: 436
  Trophy Points: 180
  jana wakati wa kuweka mikakati kuzindua tawi chuo cha mipango diwani aliyechakachuliwa wa kata ipagala bibi kunti alilitoa hilo kama angalizo!
  vijana wakshidi kuwa wao na magfrnd wao wote sasa ni chadema.pia watalipa kipaumbele.mkurugenzi wa orgnzni kigaila ambaye alikuwa mgeni rasmi amelichukua angalizo!
   
 16. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #16
  Jan 23, 2011
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Hoja safi.
  Si lazima kujenga hoja yenye kubeba uongo na janja kama ya Bajaji.

  Hata Ishu ya katiba tu inaweza kujengewa hoja ya kuwavutia wanawake.

  Kwa mfano ukijengwa msisitizo kuonyesha ni jinsi gani Katiba iliyopo kwanza inavywanyanyasa zaidi wanwake na watoto kabla ya kuwabana wanaume. Hoja ya namna hiyo ni lazima italeta mwammko na mvuto kwa wanawake walio wengi.

  Hoja si tatizo namna itolewavyo ndiyo tatizo. Hoja ya kujenga mvuto kwa wanawake wote nchi nzima ni jambo la lazima kabisa.
   
 17. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #17
  Jan 23, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,421
  Likes Received: 436
  Trophy Points: 180
  mie pia nshahona gwanda.leo nimewaahidi wife na vibinti vyangu vyote wakapime yao. tukitoka wote kihivyo ni simulation nzuri
   
 18. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #18
  Jan 23, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Ni kweli, cdm isitumie mbinu ya mafisadi ya kuwaahidi wanawake mambo yasiyotekelezeka. Ahadi lazima ziwe practically possible kutekeleza.
   
 19. 22nd

  22nd JF-Expert Member

  #19
  May 8, 2011
  Joined: Aug 1, 2010
  Messages: 498
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Wale wa mujini: so called high class-bongo daresalama
  Most of them(nadhani nimeeleweka) wanaishi kutegemea mafisadi,wanafanywa vimada,inamaana huyu fisadi akianguka na maisha ya huyu mwanamke yameisha, kwahiyo usitegemee mwanamke wa hivi akaipa support Chadema. coz all mafisadi na wezi ni CCM.kwahiyo lazima huyu mwanamke apalilie anapokula kwa kuisupport CCM.
  UNABISHA?????

  Wale wa mujini: so called watoto wa vibosile
  Toka anavaa nepi baba yake au mama yake yupo ccm na anaona hayo maisha mazuri yanatoka na baba au mama kuwa fisadi wa ccm, hivi unategemea mtu kama huyu kuipenda Chadema? na ikumbukwe kwamba huyu mtoto wa kibosile ana mashoga zake iwe wenzangu na mimi au wavibosile pia ambao wanampa support.

  UNABISHA?????????

  Wa uswahilini:
  Wanaridhika ukiwapa kanga na kofia za kuziba jua,na hongo ya hapa na pale ili uipe support ccm, nothing else, they dont care about future,wengi wao vilaza ambao wamemaliza darasa la saba au zero ya form four anasubiria mume aolewe, au amebahatika kuolewa anasubiria mume atoke kibaruani alete ugali.
  siku yake nzima anaimalizia kibarazani kupiga umbea na kugombana na majirani.

  Wa vijijini:
  The same as uswahilini,wanachojali ni kwamba leo wameshiba,hawajui kesho itakuaje.mawazo mgando,wanaogopa eti vita, amani itaisha(amani my foot).

  NANI ANABISHA???

  WANAOIPENDA CCM:
  Only independent women,amemaliza vidato lakini elimu yake haimsaidii kwa chochote,hapati kazi,na wale waliopata kazi wanauchungu wa kulipa kodi then hela zinaliwa na mafisadi na wao kuishia gizani na maji yasiyokuwa na uhakika.barabara mbofu mbofu.

  I HATE CCM,I wish to kill them one by one
  my little secret,please dont share(nafurahi kweli nikisikia kiongozi wa ccm amefariki,either na ajali au na ugonjwa).

  sorry kama nimemkwaza mtu
   
 20. Nsiande

  Nsiande JF-Expert Member

  #20
  May 8, 2011
  Joined: Jul 27, 2009
  Messages: 1,649
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Huh ! The fact that we don't like CCM doesn't necessarily guarantee our love for CDM...I don't dig either but commend CDM kwa yooote mema na wakiendelea hivyohivyo kura yangu wanayo! Heck in 2000 I voted for CUF ! I have never voted for CCM!!
   
Loading...