CHADEMA ikifa Taifa litafaidi nini? Sisi wengine tutafaidi nini?

Paul Alex

JF-Expert Member
Jul 14, 2012
4,240
9,527
Sawa tuseme Chadema ni chama kibaya sana!
Tuseme kinatetea mabeberu!
Tuseme Lissu ni adui wa nchi!
Tuseme ni chama cha Mbowe!

Hayo mengine tulishasema!

Jiwe amepolarise system yote ya CCM!
Pale lumumba au Chamwino, kwa sasa hakuna wa kumwambia kitu!
Mkapa hayupo.
Mwinyi yuko kwenye mfuko.
Kikwete hajielewielewi, hajui hata leo ni lini.
Kuna nini tena?
Namkubali mzee, ni master wa siasa za kihuni.

Eenhee! CHADEMA haipo tena!
Hesabu zake zimeshakamilika.
Kundi la kina Mdee litapewa uongozi wa chama.
Watahamishiwa account ya chama.
The rest itakuwa kama story ya Maalim na Prof.
Chadema imefika mwisho.

Sisi wapenzi washabiki tunafaidikaje na hizi siasa za kihuni?
Maana tumetumika na tunatumika kuzihalalisha.
Sioni mwisho mwema, 2025 mzee haendi mahali na hakuna wa kumwambia kitu!

Tutakutana tena hapa kufanya kilio cha pamoja.
Sibariki kifo cha demokrasia.
Sina cha kufanya kwa sasa ila ndio basi tena!
Kwaheri Tanzania ya Nyerere, kwaheri Tanzania ya heshima!
Karibu Tanzania ya Magufuli.
 
Lengo la Jiwe ni kipindi cha 2020 - 2025 kwenda ajenda bungeni ya kutoa kipengele cha ukomo wa nafasi ya kugombea urais ili awe rais hadi umauti wake.

Yote anayofanya ni kuelekea huko. Baada ya figisu figisu hizi mwaka 2022 utaona wananchi wanaandamana Dodoma wakiomba wabunge wajadili kuondoa ukomo wa urais. Baada ya maandamano ya muda mrefu utasikia anasema anakubaliana na mawazo ya wananchi lakini halikuwa lengo lake.
 
Watakuja wapinzani wengine mpka wawe kwenye nafasi ya kuchukua nchi muda utakua ushaenda ...Mpka ule utabiri wa Makonda utimie Rais wa kutoka upinzani yuko chekechea anasoma
 
Upinzani ni Iman huwez mbadilisha mtu utaua chadema lakin iman ya Upinzani bado ipo...
ona Uganda Bob wine kaja juzi tu lakini ana nguvu ya Umma...
Hata Tanzania ni swala la muda tu watu watachoka...
 
Sababu ya kuwa mpinzani nikuwa siamini kabisa kuwa maendeleo chanya yanaweza kuletwa na chama kimoja kuwa madarakani kwa miaka 60. Chama kinapokosa upinzani na msukumo wa kukosolewa hufanya kazi kwa uadilifu. CCM imekosa uadilifu na mpaka sasa 60% wanaishi katika absolutely poverty.

Niliona kampeni za Tundu Lissu na niliamini kuwa anaweza kufungua ukurasa wa pili wa siasa katika nchi yetu. Sijakata tamaa kumpa support Tundu Lissu. Tunapotia wakati mgumu sana kisiasa.
 
Huwezi kumwambia adui yako "Nikifa utafaidika vp." Jukumu lake ni kukumaliza kama ambavyo wewe jukumu lako ni kummaliza ila umeshindwa.
 
U have gone too far mkuu, Jambo hili ni proove ya blander ccm, cdm kitawasamehe kina mdee pia kwa kukuza mgogoro na kidhibiti hiki ccm wataomba suluhu ikibidi kutoa viti 10 maalumu JPM kwa CDM.
 
Siasa sio uadui, ni mchezo kama ulivyo mpira wa miguu!
Ukiua timu pinzani zote utacheza na nani?
Huwezi kumwambia adui yako "Nikifa utafaidika vp." Jukumu lake ni kukumaliza kama ambavyo wewe jukumu lako ni kummaliza ila umeshindwa.
 
Utatokea upinzani mwingine halisi imara zaidi, hiyo ndio faida tutakayoipata kama wananchi.
Haiwezekani kusiwe na upinzani ila ni wa aina gani na unaongozwa na watu gani ndio tatizo.
Naamini utatokea upinzani imara zaidi kama CDM ikifa.
 
Siasa sio uadui, ni mchezo kama ulivyo mpira wa miguu!
Ukiua timu pinzani zote utacheza na nani?

Siasa sio sawa na mpira wa miguu. Siasa unaweza kucheza mwenyewe bila mpinzani, for instance, China.

Kama CDM wanataka waendelee kubaki relevant kwa hisani ya mpinzani wao basi wanastahili kufa na kupotea kabisa. Nia ya chama cha siasa popote pale ni kushika dola na kupoteza wengine wote, huu ndo ukweli wenyewe japo sio rahisi katika nchi nyingi. Hata CDM wenyewe hili ndo lengo lao kuu japo hawajafikia.

Sisemi kwamba nataka upinzani ufe au upinzani hauna maana bali nasema matamanio halisi ya vyama vya siasa vyote.
 
Utatokea upinzani mwingine halisi imara zaidi, hiyo ndio faida tutakayoipata kama wananchi.
Haiwezekani kusiwe na upinzani ila ni wa aina gani na unaongozwa na watu gani ndio tatizo.
Naamini utatokea upinzani imara zaidi kama CDM ikifa.

Huo upinzani umeshindwa kutokea mpaka cdm ife kwanza?
 
Sawa tuseme Chadema ni chama kibaya sana!
Tuseme kinatetea mabeberu!
Tuseme Lissu ni adui wa nchi!
Tuseme ni chama cha Mbowe!

Hayo mengine tulishasema!

Jiwe amepolarise system yote ya CCM!
Pale lumumba au Chamwino, kwa sasa hakuna wa kumwambia kitu!
Mkapa hayupo.
Mwinyi yuko kwenye mfuko.
Kikwete hajielewielewi, hajui hata leo ni lini.
Kuna nini tena?
Namkubali mzee, ni master wa siasa za kihuni.

Eenhee! CHADEMA haipo tena!
Hesabu zake zimeshakamilika.
Kundi la kina Mdee litapewa uongozi wa chama.
Watahamishiwa account ya chama.
The rest itakuwa kama story ya Maalim na Prof.
Chadema imefika mwisho.

Sisi wapenzi washabiki tunafaidikaje na hizi siasa za kihuni?
Maana tumetumika na tunatumika kuzihalalisha.
Sioni mwisho mwema, 2025 mzee haendi mahali na hakuna wa kumwambia kitu!

Tutakutana tena hapa kufanya kilio cha pamoja.
Sibariki kifo cha demokrasia.
Sina cha kufanya kwa sasa ila ndio basi tena!
Kwaheri Tanzania ya Nyerere, kwaheri Tanzania ya heshima!
Karibu Tanzania ya Magufuli.
Chadema haifi itaendelea kuwepo usipotoshe.Tulianza na NCCR-Mageuzi 1995, ikaja CUF ngangari 2000, ikaja Chadema 2015 na 2025 NCCR-Mageuzi itakuwepo tena na wengine wanasubiri. Huo ndiyo ukweli Chadema mkicheza karata vibaya hawa 19 wataenda NCCR-Mageuzi wakaungane na kina Selasini na Anthony Komu
 
Maono yangu yanasema hawa 19 wataita wanachama wengine, watachagua uongozi wao, uongozi utatambuliwa na msajili.
Watapewa account na mali za chama.
Yatakayofuata ni ya Maalim na Prof. Chadema kwaheri!

Back
Top Bottom