CHADEMA ijitafakari upya ni dhahiri kuna kitu hakipo sawa ndani ya chama

Dam55

JF-Expert Member
Oct 8, 2015
3,565
2,000
Ujumbe wangu ni mfupi tu kwa viongozi wa chama kikuu cha upinzani CHADEMA.

Jitafakarini upya kuhusu mwenendo wa chama, mifumo ya uongozi, sera za Chama, namna mnavyoshughulika na masuala ya ndani ya chama, masilahi ya mtu mmoja mmoja chamani, umoja wa chama n.k. Haya mambo yaangaliwe kwa jicho la tatu.

Ni dhahiri sasa kuwa hawa wabunge,madiwani na wanachama wenu wanao hama chama kila siku si kwa sababu wananunulia kama mnavyoamini/kuaminisha watu, kutakuwa na tatizo la kiuongozi.

Katika hili wala msitafute mchawi, ni ninyi wenyewe ndio sababu na msipo badilika mtaendelea kupoteza watu wengine makini chamani.

Hivi karibuni mmekuwa mkifanya maamuzi ya kushangaza sana kwenye mambo ya msingi mfano.

Kumchagua Lissu kuwa makamo mweyekiti wakati mtu hayupo hata nchini na anadai hatorudi nchini kuhofia usalama wake.

Alafu yeye ndio makamo mwenyekiti, katika hili mmekosea sana. Sijui kama wote mlikubaliana hili sina hakika.

Uamuzi wa kuondoka bungeni kisa Covid-19, huu uamuzi kwa asilimia mia moja mlikurupuka haukuwa uamuzi sahihi na sina hakika pia kama ulikubaliwa na wengi ndani ya chama.

Tuhuma za ubadhilifu na ufisadi ndani ya chama, hili nalo ni tatizo kubwa sana hili ambalo linaendelea kuota mizizi ndani ya chama mfano mweyekiti anatuhumiwa kwa matumizi mabaya na upotevu wa bil 8.

Malalamiko ya wabunge kukatwa mishara yao kwa kiwango kikubwa, hili pia linawaumiza wengi ndani ya chama.

Kujiingiza kwenye kesi zisizokuwa za lazima na kutia hasara chama, mfano kufanya fujo gerezani kule segerea.

Kauli zisizokuwa na mipangilio mfano kauli ya mch Msigwa kusema kuwa alimsingizia kinana ujangili, anaomba radhi inamaana kuna mengi pia waliwasingizia viongozi wa serikali? Ester Bulaya kuwatumikia mabeberu n.k

Kuja na majina ya uteuzi mifukoni, ubabe wa mwenyekiti n.k

Kutokuwepo kwa Uhuru wa maoni ndani ya chama, mwenyekiti kudaiwa kuwaburuza tu wajumbe kwenye maamuzi.

Matamko wanayo yatoa hasa kwenye kipindi hiki cha Janga la Covid-19.

Hayo yote yanaweza kuwa sababu ya mpasuko wa chama kwa wale wenye nia ya mabadiliko ya kweli wanaweza kukihama chama na wala si kununuliwa kama inavodaiwa sasa.

Niwakati sasa wakukaa pamoja muyaangalie madhaifu yenu muone wapi mnakosea ili msizidi kupoteza Imani kwa watanzania.
 
Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
38,262
2,000
Watanzania acheni kuwa wajinga,hizi ni siasa chafu kuelekea uchaguzi mkuu wa baaae mwaka huu.

Uelewe tu,ilii kufanikisha mpango huu, na kuhalalisha hii hamahama,ni lazima watafute sababu na sababu ndio hizi za kumchafua Mbowe kama mwenyekiti na huo uzushi mwingine.

Lengo hapa ni kutaka kuia CHADEMA(hawataweza maana wameshashindwa) kama chama kikuu cha upinzani na kuifanya NCCR kuwa chama kikuu cha upinzani kwa faida ya CCM.

Mpango huu huenda ndio msingi wa Spika kuwabeba wabunge wa CHADEMA waliovuliwa ubunge kuendelea kuingia Bungeni,Wabunge ambao wanaohamia NCCR kukamilisha mpango wao.

Watu wa vijijini ndio wanaoweza kudanganywa na propaganda hizi za CCM na inashangaza hata wewe wa mjini unadanganyika unless na wewe ni gamba unaendeleza tu propaganda za CCM.

Hakuna chama ambacho viongozi wake hawana mapungufu na kama utasema CCM ndio kuko safi,basi nakushauri uende Mirembe ukachekiwe.

Waulize tu hao CCM baada ya kamati ilioundwa kuchunguza mali za chama chao nani kawajibishwa au nani kawajibika kufuatia ripoti za CAG zinazoonyesha madudu ya CCM.

Kama wewe kweli si CCM,basi wewe ni miongoni mwa watu katika lile kundi la watanzania wanaoweza kurubuniwa na propaganda za CCM kila mwaka wa uchaguzi ikiwemo hata kupewa kofia na vitenge na kuona CCM ndio inafaa.

CCM ndani ya hii miaka mitano mmeshindwa kutekeleza ahadi zenu kama ile ya milioni 50 kwa kila kijiji,kuboresha masilahi ya watumishi,mmevuruga biasha ya korosho,n.k na mmejikita katika maendeleo ya vitu na kusahau maendeleo ya watu na sasa mnaona kuna hatari kubwa inawakabili katika uchaguzi hivyo ponepone yenu ni kutumia mabavu kujaribu kuua upinzani mnasahau kustawi kwa upinzani ni matokeo ya nyie mliopewa dhamana kushindwa ku-deliver na huu ndio msingi wa nguvu ya upinzani hapa nchini na ni sababu kuu ni kwanini upinzani kamwe hauwezi kufa.

Mtahangaika sana!!
 
chagu wa malunde

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
4,210
2,000
Ujumbe wangu ni mfupi tu kwa viongozi wa chama kikuu cha upinzani CHADEMA.

Jitafakarini upya kuhusu mwenendo wa chama, mifumo ya uongozi, sera za Chama, namna mnavyoshughulika na masuala ya ndani ya chama, masilahi ya mtu mmoja mmoja chamani, umoja wa chama n.k. Haya mambo yaangaliwe kwa jicho la tatu.

Ni dhahiri sasa kuwa hawa wabunge,madiwani na wanachama wenu wanao hama chama kila siku si kwa sababu wananunulia kama mnavyoamini/kuaminisha watu, kutakuwa na tatizo la kiuongozi.

Katika hili wala msitafute mchawi, ni ninyi wenyewe ndio sababu na msipo badilika mtaendelea kupoteza watu wengine makini chamani.

Hivi karibuni mmekuwa mkifanya maamuzi ya kushangaza sana kwenye mambo ya msingi mfano.

Kumchagua Lissu kuwa makamo mweyekiti wakati mtu hayupo hata nchini na anadai hatorudi nchini kuhofia usalama wake.

Alafu yeye ndio makamo mwenyekiti, katika hili mmekosea sana. Sijui kama wote mlikubaliana hili sina hakika.

Uamuzi wa kuondoka bungeni kisa Covid-19, huu uamuzi kwa asilimia mia moja mlikurupuka haukuwa uamuzi sahihi na sina hakika pia kama ulikubaliwa na wengi ndani ya chama.

Tuhuma za ubadhilifu na ufisadi ndani ya chama, hili nalo ni tatizo kubwa sana hili ambalo linaendelea kuota mizizi ndani ya chama mfano mweyekiti anatuhumiwa kwa matumizi mabaya na upotevu wa bil 8.

Malalamiko ya wabunge kukatwa mishara yao kwa kiwango kikubwa, hili pia linawaumiza wengi ndani ya chama.

Kujiingiza kwenye kesi zisizokuwa za lazima na kutia hasara chama, mfano kufanya fujo gerezani kule segerea.

Kauli zisizokuwa na mipangilio mfano kauli ya mch Msigwa kusema kuwa alimsingizia kinana ujangili, anaomba radhi inamaana kuna mengi pia waliwasingizia viongozi wa serikali? Ester Bulaya kuwatumikia mabeberu n.k

Kuja na majina ya uteuzi mifukoni, ubabe wa mwenyekiti n.k

Kutokuwepo kwa Uhuru wa maoni ndani ya chama, mwenyekiti kudaiwa kuwaburuza tu wajumbe kwenye maamuzi.

Matamko wanayo yatoa hasa kwenye kipindi hiki cha Janga la Covid-19.

Hayo yote yanaweza kuwa sababu ya mpasuko wa chama kwa wale wenye nia ya mabadiliko ya kweli wanaweza kukihama chama na wala si kununuliwa kama inavodaiwa sasa.

Niwakati sasa wakukaa pamoja muyaangalie madhaifu yenu muone wapi mnakosea ili msizidi kupoteza Imani kwa watanzania.
Wameshachelewa. Na laana ya Dk slaa inawatafuna. Chama kinamaliza uhai wake bunge likivunjwa.
 
technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
9,612
2,000
Siasa tupu Jiwe alitenga bil 5 kila mwezi toka mwaka 2016 ili kuua upinzani, Mbowe ana mapungufu mengi ila jiwe ni kirusi hatari kwa usitawi wa democrasia TZ! Watakao baki chadema ndio wanaume na ndio watakuwa watu wa kuaminika zaidi. nguvu inayotumika ni kubwa.
 
Sidhani kama umenielewa mkuu
 
Dam55

JF-Expert Member
Oct 8, 2015
3,565
2,000
Watanzania acheni kuwa wajinga,hizi ni siasa chafu kuelekea uchaguzi mkuu wa baaae mwaka huu.

Uelewe tu,ilii kufanikisha mpango huu, na kuhalalisha hii hamahama,ni lazima watafute sababu na sababu ndio hizi za kumchafua Mbowe kama mwenyekiti na huo uzushi mwingine.

Lengo hapa ni kutaka kuia CHADEMA(hawataweza maana wameshashindwa) kama chama kikuu cha upinzani na kuifanya NCCR kuwa chama kikuu cha upinzani kibaraka kwa faida ya CCM.

Mpango huu ndio msingi wa Spika kuwabeba wabunge wa CHADEMA waliovuliwa ubunge kuendelea kuingia Bungeni,Wabunge wa CHADEMA wanaohamia NCCR kukamilisha mpango wao.

Watu wa vijijini ndio wanaoweza kudanganywa na propaganda hizi za CCM na inashangaza hata wewe wa mjini unadanganyika unless na wewe ni gamba unaendeleza tu propaganda za CCM.

Hakuna chama ambacho viongozi wake hawana mapungufu na kama utasema CCM ndio kuko safi,basi nakushauri uende Mirembe ukachekiwe.

Waulize tu hao CCM baada ya kamati ilioundwa kuchunguza mali za chama chao nani kawajibishwa au nani kawajibika kufuatia ripoti za CAG zinazoonyesha madudu ya CCM.

Kama wewe kweli si CCM,basi wewe ni miongoni mwa watu katika lile kundi la watanzania wanaoweza kurubuniwa na propaganda za CCM kila mwaka wa uchaguzi ikiwemo hata kupewa kofia na vitenge na kuona CCM ndio inafaa.
Utetezi kama huu kwasasa hauna mashiko, huu sio wakati wa kushupaza shingo wakati vitu vinaonekana wazi mkuu, wanatakiwa kuchukua hatua haraka kama chama makini
 
Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
38,262
2,000
Utetezi kama huu kwasasa hauna mashiko, huu sio wakati wa kushupaza shingo wakati vitu vinaonekana wazi mkuu, wanatakiwa kuchukua hatua haraka kama chama makini
Nyie endeleeni kubebwa na dola na ndio maana hata kiongozi wa CHADEMA ngazi ya mtaa/kata akitaka kuitisha mkutano anadhibitiwa na dola.

Siasa za ushindani zimewashinda ila kutwa kujimwambafai!!

Pathetic creatures!!
 
Pakawa

JF-Expert Member
Mar 11, 2009
6,109
2,000
Kila chama kina mapungufu
Hao wanawake wawadanganye wajinga wenzao
Ni tamaa zao wasilete visingizio

Ni wachumia tumbo Wabinafsi wanachowaza ni PESA period
Mwenye nia njema na nchi yupo Chadema na ACT wengine ni maslahi zaidi point blank period!

Wasitukoroge kama walivyojikoroga nyuso bana!
 
Donald Marcus Hemu

Senior Member
May 14, 2019
165
250
Nilishasema hiki chama kinaitaji service kubwa mno ili kurudi kwenye hadhi na ubora wake kuanzia oil, rims, tyres, hadi engine vinahitajika vipya hivi vilivyopo hamna kitu naiman mwaka huu watapiga hatua nyingi sana kurudi nyuma
 
FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
18,867
2,000
Kinachonipa wasiwasi ni namna Lumumba wanavyoshadadia mambo ya CDM, Spika wa Bunge kila kikicha laizma amtaje Mh. Mbowe, Pole pole naye ambaye hajulikani kama ni kijana ama mzee na yeye anamshambulia Mbowe wakati CCM kuna matatizo kibao kwanza hawakumfukuza Membe bila kufuata taratibu na katiba ya chama chao na nasikia watu wa kusini wameapa kumrudisha ama majimbo ya kusini yote CCM inafutika.

Hoja hapa shughulika na ya kwako, ya mwenzako yanakuhusu nini? Pilipiki zipo mtaa wa pili wewe unawashwa washa kwa namna gani wakati upo mtaa wa saba?
 
Dam55

JF-Expert Member
Oct 8, 2015
3,565
2,000
Kila chama kina mapungufu
Hao wanawake wawadanganye wajinga wenzao
Ni tamaa zao wasilete visingizio

Ni wachumia tumbo Wabinafsi wanachowaza ni PESA period
Mwenye nia njema na nchi yupo Chadema na ACT wengine ni maslahi zaidi point blank period!

Wasitukoroge kama walivyojikoroga nyuso bana!
Usizidishe sana ushabiki mkuu.
 
Dam55

JF-Expert Member
Oct 8, 2015
3,565
2,000
Nyie endeleeni kubebwa na dola na ndio maana hata kiongozi wa CHADEMA ngazi ya mtaa/kata akitaka kuitisha mkutano anadhibitiwa na dola.

Siasa za ushindani zimewashinda ila kutwa kujimwambafai!!

Pathetic creatures!!
Ungenielewa usinge andika hivi, ukweli ni kwamba hiki chama kisipofanya marekebisho kwenye baadhi ya mambo basi tutendelea kuilalamikia dola kila siku.
 
Karne

JF-Expert Member
Jun 13, 2016
4,146
2,000
CHADEMA inaongozwa na malaika ile so chama kiko perfect hakijawahi kukosea chochote bali serikali ya CCM na hao wanaohama ndo tatizo.😁!

"Ukipata mtu wa kumrushia lawama juu ya matatizo yako wala hutojihangaisha hata kufikiri nje ya hapo"
 
Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
38,262
2,000
Utetezi kama huu kwasasa hauna mashiko, huu sio wakati wa kushupaza shingo wakati vitu vinaonekana wazi mkuu, wanatakiwa kuchukua hatua haraka kama chama makini
Vipi kila chama ambacho wanapeana sumu kutaka kumua kiongozi wao?
 
Scale199

Member
May 3, 2020
23
75
Ungenielewa usinge andika hivi, ukweli ni kwamba hiki chama kisipofanya marekebisho kwenye baadhi ya mambo basi tutendelea kuilalamikia dola kila siku.
Ww akili yko ni ndgo sana Kama kweli unaamn chadema kuna shida pawepo na tume huru ya uchguzi afu huyu alyshka inchi kwa miaka mitano ya njaaa kwa watumishi uone kma atttoboa Jana naona Rc singida anawatshia watumishi kshabkia upinzan ujinga mtupu iyo n siasa brother cdm ikftika hiii inchi ttapitia wkt mgum ktkua hkuna wa kmnyooshea kidole jiwe probably atabadili katiba atawale milele am expect kwnn antumia nguvu kuufuta upinzan kias hiki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom