CHADEMA ifanye nini kujikwamua ilipozama? ushauri wenu ni muhimu

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
17,506
15,999
Naam, hata kama waswahili husema 'adui yako muombee njaa' lakini kwenye hili la Chadema kuzama kwenye 'matope' ya kisiasa linahitaji mjadala mpana wenye lengo la kutoa maoni yenye tija ili wajikwamue walipokwama.

Zinahitajika hoja jadidi na sio vijembe au kumshambulia mleta hoja.

Nawasilisha.
 
Hawa jamaa walifeli toka walipo anza kukumbatia walio waita mafisadiii. hadi leo wanajuta kwa kile walichokifanyaaa.

Waliahidi na kufurahia kwamba watawapelekea maendeleo ya speed kwa majiji walikoshinda, mpaka sasa majiji hayo yanasikitishaaa.

Wao imebakia kufanya dilution kila jambo jemaa analofanya raisi
Kwa sasa yaaanii kama vile sasa hawana lakufanyaaa . speed ya jpm imewaharibia kila kitu.
Kwa kweli ni shiida tuuu.
 
Kuwasaidia zaidi ni CCM kuongeza yale magogo mazito aina ya MAGUFULISM ili chadema izame kabisa, chama cha siasa kimekosa sura ya kitaifa...!
 
Wanaweza kuiga kutoka kwa CCM yaani kujivua gamba....wawaondoe mafisadi kwenye safu ya ukuu wa chama....Fisadi hatakiwi kupewa hifadhi.

Mbowe ajiuzulu uwenyekiti au ikishindikana kabisa ajiite kiongozi mkuu wa chama kama zitto.

Wampigie magoti Dr Slaa arejee kwenye nafasi yake.

Tundu lissu awe katibu mwenezi wa chama.
 
Chadema haijakwama. Walio kwama ni maCCM ambao wamepitisha sheria mbovu za madini bungeni, kisha serikali yao kusaini mikataba mibovu halafu leo wanajaribu kutuongopea watanzania kwamba wapinzani ndo wanashirikiana na wawekezaji kutuibia madini yetu. maCCM yanahitaji kukwamuliwa kifikra. Wanatia huruma.
 
Tunaomba matokeo ya utafiti unao onyesha wamezama au na wewe unaleta porojo za mtaani kama wenzio
Jikite kwenye hoja, tatizo kubwa lililopo ufipa siku hizi ni kupinga kila kitu hivyo hata ukipewa utafiti utaupinga tu.
 
Chadema haijakwama. Walio kwama ni maCCM ambao wamepitisha sheria mbovu za madini bungeni, kisha serikali yao kusaini mikataba mibovu halafu leo wanajaribu kutuongopea watanzania kwamba wapinzani ndo wanashirikiana na wawekezaji kutuibia madini yetu. maCCM yanahitaji kukwamuliwa kifikra. Wanatia huruma.
Mdudu hali ni ngumu kweli hapa ufipa, kwani jana Kubenea aligeuka mtetezi wa Prof.Muhongo bungeni licha ya kumtukana mfulululizo kwa miaka kadhaa kupitia kijarida chake.
 
Naam, hata kama waswahili husema 'adui yako muombee njaa' lakini kwenye hili la Chadema kuzama kwenye 'matope' ya kisiasa linahitaji mjadala mpana wenye lengo la kutoa maoni yenye tija ili wajikwamue walipokwama.

Zinahitajika hoja jadidi na sio vijembe au kumshambulia mleta hoja.

Nawasilisha.
Mbona utoi jibu umetumia utafiti gani kujua chadema imezama nasubiri jibu
cc
Wakudadavuwa
 
Ustaarabu katika jamii yetu ya kiTanzania unarejea kwa speed nzuri kabisa, yale ya hovyo yanamezwa na ustaarabu.

Hii inachangiwa na namna kiongozi wa nchi (Rais) anavyosimamia misimamo yake. Sera inatekelezeka, pia maumivu yapo kwa kila familia kwa sasa, tuvumilie siku hazigande.

Ni jukumu la kila mzalendo kusema AHSANTE CCM KWA KUTULETEA DEREVA MWENYE UHAKIKA WA KUTUFIKISHA ABIRIA WAKE.

MUNGU AKUPE AFYA NJEMA RAISI WETU, TANZANIA YETU, MAENDELEO YETU, MCHANGA WETU, MADINI YETU.
 
Jikite kwenye hoja, tatizo kubwa lililopo ufipa siku hizi ni kupinga kila kitu hivyo hata ukipewa utafiti utaupinga tu.
Nijikite kwenye hoja ya kufikirika iyo ni akili au matope,tupe sababu za kuona iyo ni hoja ya msingi usilete maneno kama unautafiti sema na leta kusema ukiletwa utakataa tu uko unanijibia!!!
Nawatu wanasema wewe ni mbunge mbunge unae kurupuka kwa maneno bila chanzo wewe ni hatari kwa taifa hili na nyie ndio mnaongezaga zile ndio bila kufikili
 
CCM WANAWEWESEKA SANA. KIJANA MDOGO WA UDSM AMEANDIKA KITABU CHAKE,POLISICCM KM 100 WAMEKUJA KUMKAMATA, TENA NA MAGARI YA KUWASHAWASHA
DAWA YENU INAKUJA. Uliza Nn kiliwapata madikiteta uchwara wote duniani. Time will tell
 
Wewe umeshakuwa kituko kabisa. Chadema ndiyo imezama kwenye tope au CCM ndiyo unayoizungumzia? Chama kilichoshindwa kuisimamia serikali, chama kilichogeuzwa cha mwenyekiti pekee ni chama au kikundi?
Kushindwa kwa serikali iliyoko madarakani ni dalili za chama tawala kutotimaza majukumu yake. 2016/17 Budget imetekelezwa chini ya 50%, bado serikali imeshindwa kutoa ajira hivyo rate ya unemployment kupanda kwa kasi. Huduma za afya sasa hivi ni mbovu pengine kuliko wakati wowote tokea tupate uhuru, ndio, tuliokuwepo tokea awamu ya kwanza hatujawahi ona chanjo za watoto zinakosekana katika vituo vya afya. Achana na hii hali ya chajo hata za mbwa vichaa tuu. Sasa hivi kuna CCM Kinana na CCM Magu.
 
Tume huru idaiwe mapema ccm itoke vinginevyo watanzania mtapata tabu sana.
 
Mnamuombea adui njaa mtangoja sana. Chadema inazidi kuchana mawimbi kwa mkia wa chuma
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom