Chadema huu ni wakati wa kukibomoa chama cha magamba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema huu ni wakati wa kukibomoa chama cha magamba

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Dangire, Apr 24, 2012.

 1. Dangire

  Dangire JF-Expert Member

  #1
  Apr 24, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 209
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Katika tasnia ya 'mawasiliano ya kikampuni (corporate communication) kuna dhana moja muhimu sana ambayo inahamasisha makampuni kuitumia mwanya uliojitokeza kwa wakati fulani ili kuipa mafanikio zaidi (publicity). Dhana hii inakwenda kwa almaarufu "OPPORTUNE MOMENT". Dhana hii hutumika hasa inapotokea jambo lolote kwa wakati fulani ambalo limevuta hisia au limewagusa wananchi walio wengi km vile milipuko ya mabomu (mbagala, g'mboto), mafuriko, nk. Katika kipindi hiki, wataalamu wa mawasiliano kwa makampuni hukitumia katika kuushawishi uongozi wa makampuni kwenda kutoa misaada mbalimbali ya kidinadamu, n.k. huku kukiwa na both overt and covert goals.

  Ni katika kipindi hiki makampuni hutumia kujiimarisha hasa pale ambapo kampuni ilikuwa inayumba kimwonekano, nk.

  Katika tasnia ya siasa za nchi yetu, wakati huu tulionao, kwangu mimi ni opportune moment muhimu sana kwa maendeleo ya chama ambacho, kwa miaka ya hivi karibuni kimeonesha kubeba matumaini makubwa sana ya wananchi wa Tanzania. Naizungumzia CHADEMA. Wakati huu umegubikwa na sintofahamu katika chama cha magamba (CCM) ambayo haijatokea kwa kipindi kirefu ndani ya chama hicho. ambapo, wanachama wa chama hicho wameonekaka kukatishwa tamaa na mambo yanavyoendeshwa ndani ya chama chao na hata serikali yao.

  wanazungumzia ufisadi uliokithiri, ugawaji wa vyeo kwa kujuana, kushindwa kuwajibika kwa kwa wananchi na kukithiri kwa umasikini nchini. wamebaini kuwa chama chao hakina dhamira ya dhati kuwakomboa watanzania toka katika maadui wakubwa watatu / ujinga, umasikini na maradhi. wamechoka. wamekata tamaa. wanachungulia nje. wanatafuta pa kukimbilia.

  Ni katika hali hii, kama ilivyoripotiwa katika vyombo vyetu vya habari kuwa viongozi maarufua na maelfu ya wanachama wa ccm wameanza kukihama chama hicho na kujiunga na chadema. hii ni habari nzukwa wapenda maendeleo na mageuzi wote wa nchi yetu kwani angalau sasa tumeanza kuuona mwisho wa utawala wa magamba. mwisho wa udhalimu, ufisadi, uonevu, na rushwa. mwanga wa mabadiliko unaangaza katika nchi yetu.

  Ni katika hili, ninauomba uongozi ufanye sasa hima kuzunguka nchi nzima kuzidi kuueleza uma uozo wa ccm na liserikali lake. ni wakati wananchi wanahitaji maelezo machache kuongeza katika sehemu ya taarifa ambazo tayari wanazo, ili watoke katika vifungo vyao (kuwa ccm ndio mkombozi wao) na kuiona nuru hii inayongaa tayari kwa kuikomboa nchi hii toka kwa makaburu weusi (ccm).

  Bungeni, wabunge wa ccm wanadiriki hata kukitabiria kushindwa chama chao katika uchanguzi mkuu ujao. baadhi yao sasa wanaonekana wasaliti wa chama chao. yaani, kwa ccm, ni bora uwe msaliti wa wananchi wako kuliko kukisaliti chama!!!!!!! ama kwe hawapaswi kuendelea uiongoza nchi hii. wamechoka kabisa.

  Ni wakati wa kuwaeleza wanaccm na wananchi kwa ujumla kuwa sasa ni wakati muaafaka wa kuhamia 'airtel' (chama cha ukombozi) na kuachana na mitandao ya hovyo.

  CHADEMA JUU!! DR. SLAA ENDELEA NA KAZI HIYO NJEMA KANDA YA ZIWA.MAKAMANDA WENGINE WAPELEKE MASHAMBULIZI KANDA ZINGINE ZILIZOSALIA.


  KAZI KWENU VIONGOZI.
   
 2. S

  Shambano Member

  #2
  Apr 24, 2012
  Joined: Apr 21, 2012
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Naunga mkono hoja, umeichambua vizuri na inaeleweka. Kazi kwenu Kamanda Mbowe, Dr. wa ukweli (siyo wa heshima), Lema, Zito, Mnyika, Mdee, Sugu pamoja na makamanda wote wa ukweki tupeni laha watanzania
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  Apr 24, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,437
  Likes Received: 19,791
  Trophy Points: 280
  sema hawa magamba ni wezi sana ..chadema inabidi sasa hivi iwe na wataalamu wa kuzuia wizi wa kura
   
Loading...