Chadema huu ni msimu wa kilimo, waache watu walime kwanza!

Bila ushabiki wowote wa kisiasa, ninawasihi na kuwashauri CHADEMA muwaache watu walime huu ni msimu wa kilimo.

Kama nyote mjuavyo, nchi yetu inategemea kilimo tena cha jembe la mkono. Hiki ni kipindi cha kilimo na mvua zinanyesha karibia nchi nzima hususani mikoa ya Nyanda za kati, Magharibi na Nyanda za Juu Kusini, hivyo wananchi wetu wako busy sana na kilimo ambacho ndiyo baba na mama yao. Nyanda za Magharibi na Juu Kusini, ghala la Taifa. Mnatupeleka wapi????

Je CHADEMA hamuoni kama munawaharibia wakulima ratiba yao ya kukimbizana na mvua zisizotegemewa? Wenzetu kila mwisho wa mwezi munakunja takribani TSh 12M+, watendeeni haki wakulima mnaojaribu kuwatetea. Tafadhari fanyeni maandamano na mikutano yenu kipindi cha kiangazi baada ya mavuno!

Kipindi cha kiangazi pia watakuwa busy kuvuna,kula na kuuza. Muda muafaka wa maandamano ni sasa.
 
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO,(TWANGA KOTEKOTE) We (NYAMI2010) bado ile nafasi ya Chama Cha Mapapa unashikilia?? Naomba ufanyie usemi huu kazi mapema iwezekanavyo"Chukua Chako Mapema" kwani mwisho wenu waja miaka inahesabika. Shwain wewe!!!! KILIMO UNAJUA MAJIRA YAKE??
 
Chama Cha Magamba (CCM) muna vioja juzi hapa na magari ya kifahari meupeeeeeeeeeeeeee mumepitia mikoa kadhaaa mukiwatambulisha viongozi wenu wapya kwani wakati huo mvua zilikuwa hazinyeshi,mikoa wanayopiata CHADEMA sasa hivi iko kwenye big five wanalipa na kuzalisha ziada inayotutosheleza nchi nzima lakini serikali ya CCM inashindwa kuwatafutia soko we bwana vipi
 
Kwenye bendera ya chama cha magamba kuna alama ya jembe la mkono! huwezi kuleta mabadiliko ya kilimo kwa kutegemea jembe la mkono! CHADEMA go go go....!
 
Siasa ni kilimo,azimio la iringa mwaka.......
lazima huwatakii mema wakulima wa nyanda za juu kusini,ninachokiona katika hoja zako ni kutaka kuwanyima wakulima taarifa sahihi kuhusu maisha yao na kilimo au kuendelea kubaki watwana katika nchi yao,msimu huu ndio unafaa kuongea na wakulima,halafu tutaongea nao tena msimu ujao kabla hawajapanda,tutajadiliana na wakulima ktk msimu unaouita wa kilimo badala ya kuwatenga.
 
Msimu wa kilimo ni kuanzia kuandaa shamba hadi kuvuna na kuuza!

Aliyeshiba hamjui mwenye njaa. Hao wote walioko kwenye huo msafara ni nani kati yao hapati mshahara utokanao na kodi za hao wakulima?

Mbona wao waheshimiwa wabunge wanapokuwa Bungeni hawabusumbuliwi hadi Bunge liishe? Mbona wafanyakazi na watumishi wengine hawasumbuliwi wanapokuwa kazini kwao? Au ni kwa vile wananchi wetu hawawezi kuingia hapa JF kujisemea?

Hatuwezi kuendelea kuwasumbua watu wetu hususani kama ni kipindi cha kilimo kama hichi, PERIOD! Mikutano na maadamano kwa watu wetu yawe kwenye off season.
 
oh,kumbe ni kilimo cha msimu Eeh? Basi hii ndiyo sababu inayopelekea Chadema kuandamana.hatukustahili kutegemea kilimo cha msimu wa mvua,tulistahili kuwa nasera nzuri ya kilimo cha umwagiliaji ili tupate mazao ya kutosha>gharama za maisha ziko juu kutokana na mfumuko wa bei za vyakula.Asante,nimekupa ufunuo tu mkuu
 
hata uchaguzi na kampeni tusiwe tunafanya kwa vile miaka yote kuna misimu ya kilimo.

Bila ushabiki wowote wa kisiasa, ninawasihi na kuwashauri CHADEMA muwaache watu walime huu ni msimu wa kilimo.

Kama nyote mjuavyo, nchi yetu inategemea kilimo tena cha jembe la mkono. Hiki ni kipindi cha kilimo na mvua zinanyesha karibia nchi nzima hususani mikoa ya Nyanda za kati, Magharibi na Nyanda za Juu Kusini, hivyo wananchi wetu wako busy sana na kilimo ambacho ndiyo baba na mama yao. Nyanda za Magharibi na Juu Kusini, ghala la Taifa. Mnatupeleka wapi????

Je CHADEMA hamuoni kama munawaharibia wakulima ratiba yao ya kukimbizana na mvua zisizotegemewa? Wenzetu kila mwisho wa mwezi munakunja takribani TSh 12M+, watendeeni haki wakulima mnaojaribu kuwatetea. Tafadhari fanyeni maandamano na mikutano yenu kipindi cha kiangazi baada ya mavuno!
 
iwe wakati wa kiangazi wakati wa mvua harakati zitaendelea maana huu ndo wakati wa mabadiliko!!!!!!!!!!!! mabadiliko yasubiri kiangazi!!!!!!!!!!!!!!!! mbona ninyi baada ya kujivua magamba mnaendelea kujitangaza kila mkoa kuwa mmejivua magamba na mnaendelea kustawi kama mafisadi zaidi????????????
 
Watakuja na majembe mkutano ukiisha waende shambani.Hata hivyo kukosa shamba siku moja hakuwezi kuua kilimo.
 
Msimu wa Kilimo ni kuanzia maandalizi ya shamba hadi kuuza mazao. Kilimo hufanyika muda wote, asubuhi hadi jioni na pengine usiku kufuatana na aina ya kilimo. Mfano wakulima wa tumbuku ni takribani masaa yote 24.

Hakika, katika Nyanda za Juu Kusini na Magharibi hichi ni kipindi cha Kilimo. Mazao mengi kama vile mahindi na maharagwe (chakula kikuu) ndiyo tunaanza kuvuna, japo mvua zinatusumbua sana.

Chondechonde, siyo kwamba hatupendi au hatutaki mikutano na maandamano halali, bali wito wangu ni kuwa tupeni muda hususani tunapokuwa katika kipindi cha kilimo kama hiki. Njooni Julai hadi Septemba katikati.

Maswali manne madogo:
1. Ni nani kati ya hao walioko kwenye msafara wa viongozi wa CHADEMA hapati mshahara utokanao na kodi za wakulima?
2. Kama kweli CHADEMA wanapinga ufisadi, mbona sijasikia Mbunge yeyote miongoni mwao anayesemea unono wa mshahara wa Mbunge wa Tanzania?
3. Kweli hamjui kuwa mshahara mmoja wa mbunge kwa mwezi ni sawa na mishahara ya walimu takribani 70 wa shule za msingi hapa nchini?
4. Mbona wabunge wote pamoja na hao makamanda walipopewa pay cheque za shilingi milioni tisini (Sh 90,000,000/-) za kununulia magari walinyamaza?

Watanzania tutakapo amka, hakuna cha CHADEMA, CCM wala uchafu wowote ni kutwangana tu! Mungu Ibariki Tanzania!
 
Mafisadi wanavyokwapua kila kitu serikalini hivyo wakulima watakua wamepata kweli kitu pembejeo muhimu shambani, kutembelewa na bwana shanba asiyekua hata na baiskeli, au mazao yake ya msimu uliopita tangu ukopwe na gala la serikali kuhifadhi nafaka kuendelea kutegemea hadi siku akina RACHEL watakapoamua kurejesha japo kidogo sehemu ya mali waliojitwalia visivyo halalii.

Haya ndio mambo mazito ambayo kila leo CHADEMA kinajadili na wakulima huko mikoani kwenye mikutano yake. Je, na hayo pia CDM bado isubiri mpaka kipindi cha uchaguzi????????????

CHADEMA si chama cha uchaguzi tena ujue.
 
Siasa haifanyiki wakati wa kilimo tu ndugu yangu,kama ni hivyo basi, hata campaign za udiwani,ubunge na uraisi zingesitishwa.Zaidi ya hilo misimu inatofautiana toka eneo moja hadi jingine.kwa mfano nyanda za juu kusini kwa sasa watu wanavuna na kula kwa mafanikio yako.Hakuna kulala!!hasa kwa kipindi hiki cha mafisadi ni kupiga tu siasa pamoja na kilimo na kuchapa kazi kwa kiwango cha juu!!!!
 
kupigania haki ya kweli, ukandamizaji, uozo n.k hakuna majira wala msimu

fikiri kabla ya kubandika post
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Mwenye kuleta hii THREAD ni vema ukatuomba radhi kwa hoja yako kuonekana kupoteza nguvu kulingana na michango yetu hapo juu hivyo usikalie tu kimya pls.
 
Bila ushabiki wowote wa kisiasa, ninawasihi na kuwashauri CHADEMA muwaache watu walime huu ni msimu wa kilimo.

Kama nyote mjuavyo, nchi yetu inategemea kilimo tena cha jembe la mkono. Hiki ni kipindi cha kilimo na mvua zinanyesha karibia nchi nzima hususani mikoa ya Nyanda za kati, Magharibi na Nyanda za Juu Kusini, hivyo wananchi wetu wako busy sana na kilimo ambacho ndiyo baba na mama yao. Nyanda za Magharibi na Juu Kusini, ghala la Taifa. Mnatupeleka wapi????

Je CHADEMA hamuoni kama munawaharibia wakulima ratiba yao ya kukimbizana na mvua zisizotegemewa? Wenzetu kila mwisho wa mwezi munakunja takribani TSh 12M+, watendeeni haki wakulima mnaojaribu kuwatetea. Tafadhari fanyeni maandamano na mikutano yenu kipindi cha kiangazi baada ya mavuno!

Any time is tea time. Any time is maandamano time. Hkuna kulala hadi kieleweke. CDM chapa mwendo.:happy:
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom