Chadema huu ni msimu wa kilimo, waache watu walime kwanza! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema huu ni msimu wa kilimo, waache watu walime kwanza!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nyami2010, May 5, 2011.

 1. Nyami2010

  Nyami2010 JF-Expert Member

  #1
  May 5, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 227
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Bila ushabiki wowote wa kisiasa, ninawasihi na kuwashauri CHADEMA muwaache watu walime huu ni msimu wa kilimo.


  Kama nyote mjuavyo, nchi yetu inategemea kilimo tena cha jembe la mkono. Hiki ni kipindi cha kilimo na mvua zinanyesha karibia nchi nzima hususani mikoa ya Nyanda za kati, Magharibi na Nyanda za Juu Kusini, hivyo wananchi wetu wako busy sana na kilimo ambacho ndiyo baba na mama yao. Nyanda za Magharibi na Juu Kusini, ghala la Taifa. Mnatupeleka wapi????

  Je CHADEMA hamuoni kama munawaharibia wakulima ratiba yao ya kukimbizana na mvua zisizotegemewa? Wenzetu kila mwisho wa mwezi munakunja takribani TSh 12M+, watendeeni haki wakulima mnaojaribu kuwatetea. Tafadhari fanyeni maandamano na mikutano yenu kipindi cha kiangazi baada ya mavuno!
   
 2. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #2
  May 5, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Huu mwezi sio wa kilimo,watu washalima tokea disemba(december),mtoto wa makamba,na february,sasa hivi wanasubiri kuvuna tu.Kwa hiyo tafuta propaganda nyingine(interejensia).
   
 3. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #3
  May 5, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,843
  Likes Received: 472
  Trophy Points: 180
  Wewe ni mwanasiasa usituyeyushe, tena wewe ni CCM, inaonekana uko mbali sana na swala la utawala bora.Wakulima tunajua wanawajibu wa kulima, lakini pia wana haki ya kujua nini kinachojili katika maendeleo ya nchi yao; kisiasa na kiuchumi pia, kwa maana nyingine wanahaki ya kupata habari kwa uwazi( transparency). Ni bahati mbaya sana chama tawala hakiko tayari kuwa wazi katika utoaji habari.CDM wanafanya kile ambacho CCM hawataki kukifanya.Watanzania wana haki ya kujua kwamba uchumi wa nchi umeyumba, kuna ufisadi, na wanahitaji kuwa na katiba mpya.Yote haya wanapaswa kuhabarishwa bila kujali ni muda gani wanahabarishwa, wana haki ya kupata habari hata wakati mvua inanyesha na wao wakanyeshewa ili mradi ujumbe uwafikie usiwapangie muda baaaanaaaa!!!!!!!.GO DR.SLAAAAAAAA
   
 4. z

  zamlock JF-Expert Member

  #4
  May 5, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  wewe ni ccm tena mboga nane mezani sisi ambao hata atujui leo tule nini ndio tunaoangaika acha uchizi sisi tunapambana kukomboa taifa wewe unaleta mzahaa
   
 5. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #5
  May 5, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  teh! Hata wakilima soko hawana teh! Chadema kafanyeni mambo!
   
 6. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #6
  May 5, 2011
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Kwa taarifa yako Siasa hazina musimu! Huu ndi wakti mzuri wa kukibomoa CCM kwa kuwatapeli Wadanganyika na sera mbovu,za uongo na zisizotekelezeka za ETI KILIMO KWANZA!

  Hakuna cha Kilimo Kwanza wala Kilimo Pili,ni UFISADI NA KUJIVUA MAGAMBA KUSIKOTEKELEZEKA. Bajeti inasema KILIMO KWANZA kimetengewa Tshs.400 milioni kwa nchi nzima, CHAI ya WIZARA Tshs.30 Bilioni kwa mwaka mzima.

  Badilisheni kauli mbiu iwe kwamba;CHAI KWANZA na KILIMO MWISHO! Itakuwa ikitoa picha halisi kabsaaaaaaa!
   
 7. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #7
  May 5, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Tumia akili kabla hujaleta upupu wako hapa, jana kupitia TBC CCM mlifanya maandamano huko rukwa kama sikosei je watu warukwa si wakulima, je maandamano huchukua siku ngapi? mpaka uhofie wananchi kuhalibiwa ratiba yao sana maana unaonyesha unawajari sana je umeboresha bei ya mazao yako maana kumbukumbu zinaonyesha wakishavuna huwa mnazuia magari kwenda kubeba mazao yako ilikupeleka sehemu ambayo wananunua kwa bei nzuri sijui mnataka wasafirishe kwa kubeba begani, je ni wakati gani wafaka wakufanya maandamano...
   
 8. M

  Mbwazoba Member

  #8
  May 5, 2011
  Joined: May 5, 2011
  Messages: 93
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Toa mifano ya namna hizo tsh12 zinavyopatikana na kwa akina nani,pia wewe uliyesema wewe hujui kesho ikoje fafanua ww ni mkazi wa nyanda hizo?....hebu acheni ushabiki wenu humu ongeeni vitu kwa kujenga hoja...huyu kiporo amesema ni msimu wa kilimo, nilitegemea afafanue ni kilimo gani cha mazao yapi maeneo yapi hasa, kisha ww unaepinga upinge kwa ufafanuzi huohuo.
   
 9. F

  FJM JF-Expert Member

  #9
  May 5, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145

  CHADEMA haimlazimishi mtu yeyote kuja kwenye mikutano/maandamano yake. Hakuna fuso zinazopita kusomba watu na kuwapeleka kwenye maandamano. Watanzania wa leo wana uwezo wa kuuamua nini cha kufanya na wakati gani wafanye - tuache kulishana matapishi.
   
 10. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #10
  May 5, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  hawajamaa wana hangaika na kidude cha Thanks na like nilitaka nikugongee
   
 11. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #11
  May 5, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hivi GDP inapanda kwa asilimia ngapi vile?
   
 12. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #12
  May 5, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hivi yale magari chakavu (scrap) Mbowe anataka kuwauzia CDM kwa shs ngapi vile ? nikumbushe gazeti langu silioni hapa
   
 13. Tuyuku

  Tuyuku JF-Expert Member

  #13
  May 5, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 3,149
  Likes Received: 1,407
  Trophy Points: 280
  mtoa hoja umekurupuka kwa ushabiki. Huu siyo msimu wa kulima, wala kung'oa maharage, wala kuchimba viazi, wala kuvuna mkoani Mbeya. Waacheni watu wapaze sauti zao. Ambaye ameridhika na mfumo wa sasa asiwarubuni wengine.
   
 14. F

  FJM JF-Expert Member

  #14
  May 5, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  2005 GDP growth rate ilikuwa north of 6.4% sasa hivi hata hiyo 6% ni mgogoro. IMF wame-downgrade majigambo ya 7% pamoja na kwamba Mkullo anajitahidi ku-spin growth rate. Yote tisa assume GeniusBrain GDP iko juu(!) je kwa nini mishahara siku hizi inatoka kwa kusuasua? pia huwezi kuangalia GDP in isolation bila kugusia infalation rate. I have no doubt inflation rate ni 'double digit' lakini kuna 'utalaam' maalum wanautumia hawa wakubwa ndio maana wanatuambia ni single digit!
   
 15. m

  mkulimamwema Senior Member

  #15
  May 5, 2011
  Joined: Apr 14, 2011
  Messages: 153
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Msimlaumu eti hao ndio vijana wa Msekwa wametumwa kuiua JF,mimi namshangaa huyu babu si ajifunze computer aje apambane na vijana wanao tumia akili humu ndani kuliko kupoteza pesa zetu za kodi kuwalipa watu kama hawa
   
 16. Najijua

  Najijua JF-Expert Member

  #16
  May 5, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 1,029
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Ndio kipindi kizuri wakawaeleze jinsi wanavyonyonywa katika bei za mazao zao, wakaeleze jinsi serikali ilivyowatenga katika kununu mazao yao ,ni wakati muafaka wa kwenda kuwaeleza ufisadi wa vocha za pembejeo, ni wakati muafaka wa kwenda kuwaeleza jinsi serikali inavyowafungia macho walanguzi wa mazao yao na wengine wakiwa ni wao au waliowapa fedha wao, wacha waende sasa ni wakati muafaka wa kuwaeleza baada ya miaka 50 ya Uhuru hawasthili kutumia jembe la mkono tena bali CCM inafurahia kuwaona wakiendelea kuwa maskini wakati wao wanatenga mabilioni ya kununulia chai na taarifa za utekelezaji wa ilani ya CCM


   
 17. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #17
  May 5, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,003
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  duh!! ha ha haaaa!!! kali ya siku, ntafanya kazi kwa furaha leo.
   
 18. M

  Mr.Mak JF-Expert Member

  #18
  May 5, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 2,635
  Likes Received: 496
  Trophy Points: 180
  kuhusu msimu wa kilimo hapana kwani sidhani kama watafanya mikutano asubuhi na mapema, najua watakuwa wanafanya mchana, halafu ni just siku moja katika kila sehemu watakazopita. Ila tu mimi sijajua mara hii Heading ya Maandamano ni ipi? Chama cha magamba style ya kuongeza wanachama ni kurudi nyumba kumikumi ama cdm ni kwa maandamano zote ni style za kila mmoja kufikia malengo. Ila sisi ambao hatuna vyama tungeomba yote hayo yafanyike kwa kheri na amani na kuheshimiana.utu wa mtu uheshimiwe kama anahatia hasira tusizimalize kwa kumtukana majukwaani, kama wapiganaji wetu wanakuwa na data na wanasheria wa kujitegemea tunao kwanini tusiwapeleke mahakamani? au wanasheria wetu wa kujitegemea ni magumashi?
   
 19. J

  JABEZ Member

  #19
  May 5, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Harakati za ukombozi haziwezi kusubiri mvua ziaache kunyesha. Tutapambana na mafisadi wakati wa mvua, wakati wa jua na wakati wa mavuno mpaka kieleweke
   
 20. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #20
  May 5, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,640
  Likes Received: 1,429
  Trophy Points: 280
  Kama ulivyojielezea hapo kwenye kijani... basi watanzania nao wanahitaji kujua kwa nini mpaka leo miaka 50 ya uhuru bado wanatumia jembe la mkono. CDM wanaenda kuwaeleza watu yaliyojiri mpaka leo wanatumia jembe la mkono katika karne hii ya sayansi na teknolojia.

  nikianza na wewe unaweza kutupa sababu ya sisi kutegemea jembe la mkono mpaka leo?
   
Loading...