Chadema huu ndio wakati muafaka kufungua televisheni ya cdm %100

commonmwananchi

JF-Expert Member
Mar 12, 2011
3,377
1,952
Sasa ni dhahiri kabisa kwamba serikali ya CCM imekuja na mkakati maalumu wa kuivuruga Chadema,
Ninapata ujasiri wa kuyasema haya kwa sababu matukio yanayotokea sehemu mbalimbali nchini kuanzia morogoro,Iringa,Arusha,Mwanza na kauli tunazozisikia kutoka kwa wana CCM wenyewe ni dhahiri kuwa kuna mpango maalum wa kuitega CDM iinngie katika mtego wa kuonekana kama ni chama chenye vurugu na hivyo tupelekee kufungiwa kufanya siasa za mikutano kwa sasa.

Pia kule Arusha wamefanya mkakati wa kuligawa eneo maarufu kwa mikutano ya hadhara la viwanja vya NMC kwa kuwapatia wamachinga.ili tu kwa sababu mahali pale hukusanya umati mkubwa wa wafuasi wa CDM na pamejiptia umaareufu kama Chadema square jijini arusha.

CDM ni vema viongozi mkaliona hili mapema,na mkajiandaa kwa kuwa na njia mbadala na pana zaidi ya kuwafikishia ujumbe wapenda demokrasia ya kweli nchini,kwa wakati muafaka.na pia kuweza kuyafafanua yote yale ambayo mnakuwa mmezuiwa kuwafikishia wananchi kwa wakati,na au mkizuiwa kufanya mikutano

Kama tumepata helikopta,inakuwaje viongozi mnashindwa kuliona hili.

Mbona kuna vituo lukuki nchini kwa sasa vya televisheni na vinajipatia umaarufu na ni vya taasisi ndogo kabisa kuliko CDM.

CCM wao wanayo TBC ambayo wanaitumia kinyume na katiba kwani kile ni chombo cha walipa kodi nchini na hakikupaswa kubagua ni nani apewe habari zipi na kwa wakati gani.lakini mambo yanaenda ndivyo sivyo na imegeuka kuwa TBCCM na hilo halina ubishi na kama kuna anayebisha akamuulize Tido mhando yaliyompata baada ya kuwabishia wakubwa.

My take:ni wakati sasa wa cdm kujipanga na kumpata kada wa CDM akafungua kituo chake cha redio na tv,kwa maslahi ya wengi.maana sidhani kama chama kama chama kitapewa nafasi hiyo na ccm.kama ilivyo Star TV na kada wa ccm Diallo.

VIVA CHADEMA NA M4C
 
[h=5]Zitto Kabwe
[/h][h=5]Narudia, mwaka 2015 sitagombea Ubunge. Nitafanya kampeni ya Urais, ama mimi kama mgombea wa chama changu CHADEMA au kama mpiga debe wa mgombea wa chama changu. Miaka 10 ya Ubunge inatosha na kwa ngazi hiyo ni vema niwaachie wengine wasukume mbele gurudumu la maendeleo ya Jimbo na mkoa wetu. Huu ndio uamuzi wangu wa mwisho na nimeshawaeleza wananchi wa Jimbo langu na mkoa wa Kigoma toka mwaka 2005.

[/h]
 
[h=5]Zitto Kabwe
[/h][h=5]Narudia, mwaka 2015 sitagombea Ubunge. Nitafanya kampeni ya Urais, ama mimi kama mgombea wa chama changu CHADEMA au kama mpiga debe wa mgombea wa chama changu. Miaka 10 ya Ubunge inatosha na kwa ngazi hiyo ni vema niwaachie wengine wasukume mbele gurudumu la maendeleo ya Jimbo na mkoa wetu. Huu ndio uamuzi wangu wa mwisho na nimeshawaeleza wananchi wa Jimbo langu na mkoa wa Kigoma toka mwaka 2005.

[/h]

Hii haihusiani na nilichowakilisha achas umagamba wako wewe.
UNAWEZA KUNUNUA WATU LAKINI HUWEZI KUNUNUA HESHIMA YAO
 
Hili linawezekana ukizingatia mbunge wangu mh. Philemoni ndessamburo (ndesapesa) yeye binafsi anamiliki helkopta zaidi ya moja na radio moshi fm.
Nadhani hili jambo dogo wakiliamulia.
 
Zitto Kabwe


Narudia, mwaka 2015 sitagombea Ubunge. Nitafanya kampeni ya Urais, ama mimi kama mgombea wa chama changu CHADEMA au kama mpiga debe wa mgombea wa chama changu. Miaka 10 ya Ubunge inatosha na kwa ngazi hiyo ni vema niwaachie wengine wasukume mbele gurudumu la maendeleo ya Jimbo na mkoa wetu. Huu ndio uamuzi wangu wa mwisho na nimeshawaeleza wananchi wa Jimbo langu na mkoa wa Kigoma toka mwaka 2005.


Ritz bwana. hii hoja umeishadadia sana. enhee inatufundisha nini?
 
Sioni sababu ya chadema kuwa na tv yao binafsi wakati ya taifa ipo. Mbona baadhi ya mikutano yao huwa inarushwa ?

Near by Isanga Mbeya
 
Back
Top Bottom