Mafanikio ya chadema katika uchaguzi huu makubwa na yanastahili kupongezwa na kila mtanzania anayeitakia mema nchi hii. Hakuna kificho kuwa Chadema wamedhulumiwa ushindi; hata sisi wanaccm tunayoitakia mema nchi yetu tunaona aibu kutembea vifua wazi kusheherekea ushindi huu. Hii ni sawa na baba kusheherekea arusi ya mtoto shoga aliyepata mume. Hii ni fedheha kubwa kwa kiongozi aneyejinadi kuwa ni mwanademokrasia kila kona ya dunia. Siasa ni ushindani; lakini hatuna ulazima wa kuendesha nchi kama hatuwezi. Watanzania wanachodai ni maendeleo, wale wanaccm mliokimbilia pilau na fulana uchaguzi umekwisha shangwe zenu zimeishia wapi? Kumbukeni Raisi bora ni yule anayewajali wananchi wake kwenye kipindi chote cha utawala na si kwenye uchaguzi tu! CCM inaongozwa na kikundi cha wahuni kwa manufaa ya familia zao na marafiki zao; JK hakubaliki, tumechoshwa na kauli za ccm imeleta amani, hii karne ya 21 acheni kutuongoza kwa siasa za karne ya 20. JAMBO FORUM HONGERA KWA UTANDAWAZI. "WE ARE ALL FIGHTING FOR COMMON CAUSE REGARDLESS OF OUR POLITCAL VIEWS". GODBLESS TANZANIA.