Uchaguzi 2020 CHADEMA hofu yatanda: Wajuta kumpendekeza Lissu kuwa mgombea Urais, Nyalandu ana ukwasi na sifa za kupeperusha bendera yao

OTTER

JF-Expert Member
Feb 20, 2016
476
331
Baada ya wajumbe kutathini mwenendo wa namna bw. Lissu anavyotafuta wadhamini huko mikoani, hofu na giza kuu limetamalaki hapo UFIPA, baada ya kuona muda wote Lisu ni mtu wa kutukana Serikali iliyopo madarakami na kushawishi wananchi waingie barabarani pindi jina lake lisiporudi kwa ajili ya kampeni ya kuwania urais wa JMT.

Wajumbe wamethibitisha kuwa yawezekana huyu ana agenda yake aliyotoka nayo huko kwa mabeberu, kwani haiwezekani ahofie jina lake kukatwa, mbona wengine hawana hofu kama ACT, CUF, CCM, n.k. na wanatafuta wadhamini huko mikoani kimyakimya.

Hofu inakuwa yawezekana kwa matendo yake anayoyafanya wakati wa kutafuta wadhamini anajua dhahili atakosa sifa za kuteuliwa hivyo nafanya hivyo kuitishia NEC ili wasifanye maamuzi ya kuteua kwa kufuta misingi, sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa kwa kumuogopa Lisu afanyiwe anavyotaka yeye ateuliwe hata kama hana sifa.

Wajumbe wameona mwenendo huo wa kuhamasisha vurugu kwa ajili ya uvunjifu wa amani wanajuta wanaona ni heri wangeendelea na Bw. Nyalandu ambaye alikuwa mshindi wa kwanza kwenye kura za maoni, kwani anazo sifa za kufanya kampeni za ustaarabu zisizo kuwa na chuki miongoni mwa Watanzania.

Pia wanasema chama hakina pesa za kukodi helcopter kutoka Kenya, ya kumzungusha nchi nzima na kuwalipa waandishi wa habari kwa muda wa siku sitini na kulipia Redio na TV. wanahofu ya mgombea wao kutopata mvuto kwa wananchi wa Tanzania bara na visiwani. Mwenyekiti wao alisikika akisema ni heri wangempitisha BW. NYALANDU yeye anaukwasi ambao unaweza kufanya kampeni bila wasiwasi wowote na kuwalipa waandishi na TV zote kwa kipindi chote cha kampeni. Wanajipanga kupitisha bakuli kwa wananchi ili wanusulu kampeni zao.
 
Rubbish mtu msomi hawezi kuandika pumba hizi!! Hiki kipindi andikeni Sera za vyama vyenu ili tujue nini mda mtawafanyia wananchi!!hizi propaganda za kitoto kujustify uongo kuwa ukweli mtanzania gani atawaelewa?

Sent from my SM-G920F using JamiiForums mobile app
Mkuu kuwa mpole, wakati wa kuelezea sera bado. Subiri kipenga kipulizwe. Mumeshikwa pabaya
 
Yale mabilioni ya Akina Lijuakali na wabunge wengine waliokuwa wanakatwa na chama yako wapi? Itakuwa mwemyekiti mbowe alishayatia mfukoni kitamboo
 
Screenshot_20200816-164514.png
 
Yale mabilioni ya Akina Lijuakali na wabunge wengine waliokuwa wanakatwa na chama yako wapi? Itakuwa mwemyekiti mbowe alishayatia mfukoni kitamboo
Kwa sasa wanajuta sana, alikuwa anawakata bila kujua kama huko mbeleni kuna kazi kubwa inayohitaji pesa. Sasa wanafikilia kuwachangisha raia wapate pesa za Coverage kwenye media na magazeti.
 
Kila tunapowambia kuwa wagombea wa upinzani ni wajasiriamali hawaelewi, Watanzania wazalendo hawawezi kuuza nchi.
 
Nahisi imefika muda sasa mods muanze kuondoa watu humu jamii forum ili neno THE HOME OF GREAT THINKERS liendelee kubaki na thamani ..hivi mtu km aliyepost huu uchafu na yy ni member...sasa hapo unasoma ili upate mawazo gani ...kwa sbb yote aliyoandika ukiwa na kichwa kisafi hakuna hata moja lenye uhalisia..propaganda km za kunadi kiranja mkuu wa shule
Naunga mkono hoja.
 
Mkuu Otter, hili jinamizi liwatatesa sana. Kama ktk kutafuta tu wadhamini ni hivi! Je! Kampeni zikianza si itakuwa ni balaa kabisa.
Mbenge, hao unao waona ni mashabiki tuu, hakuna mpiga kura. Wapiga kura wapo wametulia nyumbani wanaendelea kulinda visu vyao visiibiwe, wazee wameviweka kibindoni wanawaangalia tuu. tukutane 28 oktoba hapo ndipo mtajuta na kusaga meno
 
Back
Top Bottom