CHADEMA, hivi hamjaona kama Hayati Magufuli ni fursa kwenu hata kama alikuwa adui yenu?

abdulhamis

JF-Expert Member
Aug 2, 2019
1,175
2,000
Habari Wadau,

Nimekuja kuwauliza Chadema na vyama vingine vyote vya Upinzani, je ni kweli wanaitaka nchi!? Na je, ni kweli walikua wanataka kutukomboa, kama ni kweli basi kifo cha Hayati Magufuli inaweza ikawa Fimbo nzuri kwao ya kumuulia nyoka ikitumika akili tu.

Chadema na vyama vingine vya Upinzani Nadhan mmeona msiba wa Mpendwa wetu Magufuli Watanzania Walivyokua wanalia kwa uchungu. Niwaulize uchungu ule mnahisi hatuwezi kuwasaidia? Nasema hivyo kwasababu kama mtamtumia vizuri hata zile nguvu za umma mlizokua mnazitaka mtazipata kwa Asilimia Mia.

Ila naona kama vile hamko tayari sababu Badala ya kumuandaa kama njia ila mnashirikiana na Watu wasiompenda kama nyinyi kumchafua. Mkumbuke mkimchafua akachafuka hamtoweza kumtumia tena na huenda waliopo mkashindwa kuwatoa sababu mmeshamchafua wa mwanzo na kusema kuwa wa pili ni mzuri ambaye mtashindana naye tena na kwenye ushindani atasema Mimi ni mzur hata Chadema walisema.

Mimi Binafsi niko tayari kuwaunga mkono ili kiwe kama kisasi kwao wazee wa Bandari ya Bagamoyo na yule wa hiii serikal ni Awam ya Sita kiukweli nimeichukia CCM kwa sababu ya Magufuli na sababu izo Zipo negative na positive.

Kwa sababu kama Magufuli alikua Mbaya kwanini wasiseme kipindI hajafa? Kua alikua anatudanganya Watanzania

Pili Magufuli kama hakua mchafu kama ninavyoamini kwanini wamchafue kwa Maslahi yao

Pia Kuna Mawil kwa Chadema huenda moja likatokea

1) Huenda Chadema wakapewa wanachotaka wakaamua kuwatelekeza wtz na Matatizo yao na kubaki kupiga kelele tu

2) Wakaamua kupambana kuchukua nchi

Ivyo ngoja tuone, wakati utaamua
 

Mawazo2

Member
Dec 10, 2020
11
45
Dah! Sijiu nimeamka vibaya..! hapa sjaelewa kabisaa!!

Anataka kutaka nini kwetu Huyu mwenzetu? Mliomwelewa mtujuze
Anataka CHADEMA wamsifie sana Magufuli kama ndo Rais wa wanyonge, na kwa hiyo CHADEMA wajipambanue kwa wanyonge na wafuasi wote wa Magufuli, wapingane na wale wanaombeza na kumchafua Magufuli, lengo ni CHADEMA kuchukua hao wafuasi wote kama mtaji wao mkubwa kwenye uchaguzi wa 2025 ili wachukue nchi kama kweli wako serious na kama kweli wanaitaka nchi na kama kweli wana nia ya kuwakomboa wanyonge wa Tanzania. Mimi ndivyo nilivyojaribu kumwelewa Mtoa mada.

Maoni yangu binafsi:-
1. Vyama Mbadala (vyenye mawazo mbadala, siyo vizuri kuwa wapinzani na wasiwe wapinzani wanakosea wakikubali kuwa hivyo) vijenge taasisi/vyama imara vyenye misingi imara ya demokrasia. Chama kisiwe na sura au mwelekeo wa ukanda, udini, ubinafsi, ukabila, au hata ukoo wa kurithishana kuanzia kwa mwanzilishi ndo Mwenyekiti atoke huko huko miaka nenda rudi, na ukomo wa muda wa mwenyekiti haujulikani, kuna wengine Mgombea Urais ni huyo huyo kwa miaka 30, etc. Wawe na mifumo ya uwazi ya uchaguzi na uongozi ambayo ni bora zaidi ya ile chama Tawala, ili wawe mfano wa kuigwa na kuwashawishi watu makini kuwa wao (vyama mbadala) wana vitu vya ziada vizuri zaidi ya vile vya Chama Tawala, na hivyo nishawishike nikihame chama fulani, nije chama kingine.

2. Chama Mbadala lazima kiwe na mrengo wa kisiasa na kimaendeleo ambao una agenda ya kudumu, chama kinajijenga kuongeza Wataalam wabobezi katika nyanja nyingi muhimu, chama kinafanya utafiti wa kina na kuja hoja na nzito na facts na takwimu, n.k na siyo hoja za kuandia majukwaani.

3. Chama Mbadala kinapaswa kujipa malengo ya muda mrefu huku kikijijenga na kufanya maandalizi ya kutosha miaka kadhaa kabla ya mwaka wa uchaguzi mkuu, badala ya kusubiria Wagombea urais,ubunge na udiwani wahame vyao au chama tawala kipindi cha kampeni za uchaguzi mkuu.

Kama mambo hayo hayatazingatiwa, sahauni kuichukua nchi! Mifano ipo mingi hata kwenye Club za soka. Bila uwekezaji wa kutosha, bila kujenga club imara kiuchumi na mifumo imara na endelevu ya uongozi, makuzi ya wachezaji na wataamu muhimu, na malengo na maandalizi thabiti, ni ndoto kuchukua ubingwa na kuendelea kuwa bingwa na kutawala soka la nchi husika.
 

wakuja town

JF-Expert Member
Oct 26, 2020
875
1,000
Kati ya ma prezdaa wote, aliekuwa wa ovyo tz na dunia nzima ni jiwe, mwamba alikuwa kituko cha kushangaza sana, angalau mh rais wangu samia suluhu anaanza kuturudishia heshima ya nchi yetu iliyokuwa inaelekea shimoni
 

Kihava

JF-Expert Member
May 23, 2016
4,420
2,000
Dah! Sijiu nimeamka vibaya..! hapa sjaelewa kabisaa!!

Anataka kutaka nini kwetu Huyu mwenzetu? Mliomwelewa mtujuze
Masalia wa mwendazake hawaeleweki ndugu yangu. Wao siku zote mbaya wao ni Chadema. Sielewi Chadema ilimfanya nini mwendazake na wafuasi wake. Huwa hawajiamini kabisa mbele ya Chadema au mwana Chadema. Wapo tayari kumuua asionekane kabisa au kumfilisi kabisa. Kwa kweli huwa najiuliza sipati Jibu la nini hasa Chadema ilikifanya kwa mwendazake na wafuasi wake. Anayejua anisaidie maana siyo kwa chuki hii.
 

Kihava

JF-Expert Member
May 23, 2016
4,420
2,000
Madalali wa AstraZeneca na mabeberu hawawezi kamwe kufungamana na Mzalendo Magufuli.
Tukiwaomba mtutajie beberu mmoja tu ambaye Tanzania haina shirika naye hamtaji. Mwendazake kaenda zake na akili za wengi
 

Kihava

JF-Expert Member
May 23, 2016
4,420
2,000
hapo walipo wanaogopa kuchanika msamba,hawaelewi waende wapi.

kumkana hayati hadharani ni kupingana na wananchi,kumuunga mkono ni kumeza matapishi.siasa ngumu sana mkuu.

basi wamekuwa fisi.
Mbona wamemkana hadharani Mwendazake na wananchi hatujapingana nao? Kwani hukumsikia Mbowe juzi? Mwendazake hakuwa binadamu wa kawaida. Binadamu gani hana utu? Anapenda kuona mwenzake anateseka.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom