Wakudadavuwa
JF-Expert Member
- Feb 17, 2016
- 17,506
- 15,997
Naam, nilipotea hapa jukwaani ili kuweza kutekeleza majukumu yangu kulitumikia taifa ambapo nililazimika kusafiri mikoa kadhaa ikiwamo Arusha,Kilimanjaro,Manyara,Dodoma, Singida, Tabora,Kigoma, Mwanza,Shinyanga, Mara, Geita na Simiyu. Katika tathmini yangu ya awali ni kwamba pasi na shaka yoyote vyama vya upinzani vikiongozwa na Chadema havina uwakilislishi wala uhai wa wanachama wenyeji wa mikoa hivyo. Ofisi zimefungwa tokea baada ya kumalizika uchaguzi mkuu mwaka 2015.
Wakati ninajiandaa kutoa tathmini kamili, nilikuwa nina swali moja tu; je hili la kuboresha ofisi na uwezo wa kitaasisi linahitaji kibali cha serikali? Nimejiuliza hivyo sababu kama Chadema haifanyi mikutano ni dhahiri matumizi ya ruzuku yangeelekezwa huku kwenye mashina.
Kuna wana Chadema wowote wanaofikiria kuhusu hili jambo? nini matumizi ya ruzuku?
Tujenge hoja kwa upendo.