CHADEMA: Hiki ndicho kitakachotumaliza!

Mtani wangu, mwenyewe ndiyo nilikuwa naanza kupasha moto mwili, teteteee....

Dahh, nyie watu hasa wewe na Chris Lukosi , nafikiri ni Chadema kwa ndani ila basi tu.

Ningelikuwa CCM, ningelitangaza muondolewe mapema sana kwani nikiwasoma sawasawa..... mmekaa Kifipa.

Ila nakiri kuwa, mnasaidia mijadala mingi ijadiliwe sana. Vinginevyo ingelikuwa kama miezi kadhaa nyuma watu wakaanza kuona JF inakufa vile. Mmetengeneza balance nzuri kati ya CCM na Chadema. Endeleeni kuwa wapinzani wa Chadema na kuifunda kuwa na yenyewe siku ikitawala, wapinzani watawakaanga kwelikweli. PAMOJA SANA Watani wangu.
Hahahahahahaahahaa

Sikonge mbona unatumia bomu kuua mbu?

Hahahahahahahhahahaha

Basi yaishe...
 
Last edited by a moderator:
Mtani wangu, mwenyewe ndiyo nilikuwa naanza kupasha moto mwili, teteteee....

Dahh, nyie watu hasa wewe na Chris Lukosi , nafikiri ni Chadema kwa ndani ila basi tu.

Ningelikuwa CCM, ningelitangaza muondolewe mapema sana kwani nikiwasoma sawasawa..... mmekaa Kifipa.

Ila nakiri kuwa, mnasaidia mijadala mingi ijadiliwe sana. Vinginevyo ingelikuwa kama miezi kadhaa nyuma watu wakaanza kuona JF inakufa vile. Mmetengeneza balance nzuri kati ya CCM na Chadema. Endeleeni kuwa wapinzani wa Chadema na kuifunda kuwa na yenyewe siku ikitawala, wapinzani watawakaanga kwelikweli. PAMOJA SANA Watani wangu.

Chadema ni chama kinachoendeshwa katika misingi ya kilaghai.
 
Last edited by a moderator:
Hivi we unataka kuzunguka nini, nani asiyejua na akili zake timamu kuwa CCM hawalali kuangalia watasambaratisha vipi CDM, kwa mantiki hiyo lazima tu tuwaangalie sana kwenye nafasi ya first suspect.
Ebo, akina Mwigulu, Wassira hawalali kwa ajili ya CDM we unajifanya huoni. CHADEMA komaeni tu inaelekea kila mbinu sasa zinagonga, ushindi unakaribia........
tunakushukuru sana .
 
inawezekana kwa upande fulani ukawa sawa , lakini kuna ushahidi wa maneno na matendo kwamba ccm wanahusika , bomu la arusha ni uthibitisho , ukubwa wa cdm mitaani unaiogopesha sana ccm , rejea maneno ya jk kwenye vikao vyao dodoma , hujuma zipo , hebu waangalie masalia waliko hivi sasa ! nakuhakikishia bila hujuma ccm hairudi madarakani 2015 ng'oo !
 
Yaani kila kitu kinachotokea ndani ya Chama, hatuna hata muda wa kufanya uchunguzi, moja kwa moja tunakimbilia tu ni CCM.

  • Kila tukikubwa na Tatizo lolote bila hata uchunguzi na tafakuri ya kina;haraka tunakimbilia ni CCM tu hao!.
  • Mtu akitukosoa kwa lolote bila hata kulitafakari kwa makini kwanza; haraka tunakimbilia lazima katumwa tu na CCM huyo.Wala hata hatuna muda wa kutafakari hoja yake na kuipima misingi na mantiki yake!.
  • Mtu akilalamika kidogo tu ndani ya chama kwamba kuna jambo haliendi sawa, moja kwa moja tunakimbilia mbona huyu katumwa na CCM na kesha hongwa wala hata hatuangalii analalamikia nini!.
  • Mtu akijitokeza tu na kutoa wazo linaloonekana kutofautiana na baadhi ya watu basi utasikia kesha hongwa huyo, kazi ya CCM hiyo na kinachofuata ni kejeli!
Amin! Amin nawaambia: Kwa kusoma mazingira tu, Utaratibu huu ndio utakaotumaliza!. Kuna jambo linatufunga macho na tunashindwa kuona mbele katika mwanga bora. Jambo hilo si jingine zaidi ya kujiaminisha kwamba tuko “Absolutely perfect” Wakati watu wengine wote nje ya CHADEMA, au hata baadhi ya wanachadema wenzetu Wako “Absolutely wrong” na kudhani kuwa hali hiyo ni “constant " kana kwamba ni hali ya kimaumbile! kitu ambacho kiuhalisia si kweli. Hali hii inatuponza na itatusababishia masikitiko makubwa sisi wenyewe na Watanzania wanaoitegemea CHADEMA na hatmae kwa taifa zima.

Hivi inawezekana je mwanao akiugua homa; haraka tu wewe unasema ni jirani, mwanao akilalamika njaa ;unakimbilia ni jirani kamtuma, akisema anataka kusoma arts na si sayansi ;unasema lazima katumwa na jirani, akiuliza sasa baba kwa nini tusifungue duka badala ya kununua bajaji; unasema atakuwa katumwa na wenye maduka jirani wanaogopa ushindani: Yaani bila hata kutafakari na kuopata muunganiko wa kimantiki!

Inaniuma sana katika hili kwa kuwa muaminifu tu. Ni mfano wa mtu mwenye tongo tongo usoni. Ni vigumu kwa mtu mwenye kujiona, ila mwezake anaweza kumuona kiurahisi.Sasa kama anaemuona akimuambia "Ndugu yangu una uchafu usoni" mwenye uchafu anakuwa mkali kweli!, kitakachotokea watu watanyamaza tu!. Hata hivyo kunyamaza kwao
hakutasababisha uchafu ule kwenye uso wa ndugu yao kuondoka (ikiwa upo). Hatimae kila watakakopita; jamii yote itakuwa inauona hali aliye nao hauoni!, alieongozana naye naye atakuwa anauona ila kwa kuwa akisema anagombezwa basi ataamua kukauka kana kwamba haoni.Mwishowe walioongozana wote wataishangaza jamii itakayokuwa inawatazama.

Ni bora tukaamua kuondoa "impurities" ambazo tayari ziko kwenywe vichwa vyetu, ili tuweze kupokea maarifa zaidi na mapya kutoka nje ya vichwa vyetu wakati huo huo tukipata fursa ya kusoma kutoka kwenye uzoefu wa watu wengine.


Na ili kujua ni kwa jinsi gani tatizo hili ni kubwa; utaona hata kwenye uzi huu, kuna watu bila hata kusoma uzi wote, watakurupuka na kuanza kusema "Wewe sio CCM kweli!" "Umetumwa!" "unatumika!" n.k

Mkuu betlehem ni sawa na unampigia Mbuzi gitaa, vijana/wafuasi wengi wa CHADEMA ni kama misukule! Hawasikii wala hawaoni, na hawataki kusikia wala kuona!
 
Last edited by a moderator:
betlehem kwa upande mmoja namlaumu sana Zitto sababu kama kiongozi wa taasisi hakutakiwa kutoa ajenda zozote zinazohusu chama chake kwenye media kukashfu viongozi wenzake au kutoa hoja zinazokinzana .Mfano alipoto maelezo kuwa amemuandikia barua Katibu Mkuu wa CDM kuhoji uhalali waripoti iliyopo kwenye mtandao,hivi alishindwa nini kwenda ofisini na kukaa na viongozi wenzake wakajadili na kukubaliana nini cha kufanya.Hata Zitoo pia ameasisi misuguano mingi ndani ya CDM kwa kujion yu bora kuliko wengine kwa hilo lazima ajifunze na aliombee radhi.Na kama hakuwa teambuilder basi hastahili kuwepo kwenye team ya uongozi ni vyema akae pembeni na awe mwanachama wa kawaida,kama kiongozi wa chama cha siasa kwa kweli hafai.Pia ningependa kuwashauri CDM wasimfukuze uanachama adhabu waliyompa ya kumnyang'anya vyeo vyake inatosha kama mtu wa kujifunza basi atajifunza.a mwisho CDM inatakiwa ipokee changamoto hizi kwa hekima,ni kweli si kila jambo adui yako amesababisha ila kutokana na tabia na mwenendo wa binadamu ambaye anamawazo tofauti na mwingine lakini mawazo haya yatolewe mahali panapofaa.
 
Mkuu Tetty nimejizuia sana kujibu baadhi ya hoja au kuwauliza baadhi ya watu maswali kwa sababu maalum.Hata hivyo naona najizui lakini nashindwa.Hebu naomba nikuulize walau machache kwa niaba ya wenzako ambao wamekuwa wakirudia rudia hoja kama ya kwako.
namlaumu sana Zitto sababu kama kiongozi wa taasisi hakutakiwa kutoa ajenda zozote zinazohusu chama chake kwenye media kukashfu viongozi wenzake
Hivi unaweza ukanipa walau kauli moja aliyoitoa zitto kwenye media akimkashifu si kiongozi tu wa chama bali hata mwanachama yeyote? Hivi sio kina Lema ambao wamekuwa wakimchafua zitto kwa ushahidi ulio wazi kabisa nasi tukidakia kuendelea kumtukana zitto? Ndugu yangu Tetty tuwe waaminifu na waadilifu katika hili tafadhali!
au kutoa hoja zinazokinzana .
Kwa mfano hoja gani inayokinzana ambayo zitto katoa.Tuwe realistig tafadhali
Mfano alipoto maelezo kuwa amemuandikia barua Katibu Mkuu wa CDM kuhoji uhalali waripoti iliyopo kwenye mtandao,hivi alishindwa nini kwenda ofisini na kukaa na viongozi wenzake wakajadili na kukubaliana nini cha kufanya.
Mkuu kuna jambo kubwa hapa limejificha katika jambo hili.Ni kawaida katika chama chetu, likitokea jambo linalochafua chama au kiongozi mkubwa wa chama asubuhi,basi jioni jambo hilo lishatolewa ufafanuzi. Katika hali ya kusikitisha sana ni kwamba ripoti lile ilikuwa inasamba kwa zaidi ya wiki mbili ,ikijadiliwa mtandaoni na hakuna kiongozi wa chama alie toa kauli yeyote.Chakusikitisha zaidi ni kwamba viongozi waandamiziwalikuwa wanai like! na kulike hoja zilizokuwa zikimkandia zitto, huku wakijua dhahiri ripoti hiyo ni ya kutunga.Mkuu Tetty naomba nisifunguke zaidi kama nilivyosema hapo mwanzo kwamba sipendi kufunguka sana kwenye jambo hili.Tutosheke tu kuelewa kwamba suala la Zitto ni zaidi ya kile tunachokiona mtaani.
Hata Zitoo pia ameasisi misuguano mingi ndani ya CDM kwa kujion yu bora kuliko wengine
Kwa kuwa realistic, ni wapi zitto kasema yeye ni bora kuliko wenzake? au wanaosema anajiona bora, wanatumia kigezo gani? tuwe makini tusije tukaonekana kwamba tatizo letu ni wivu kwa mtu kwa kuwa tumeona anamafanikio fulani!
kwa hilo lazima ajifunze na aliombee radhi.
Hebu toa jambo moja concrete, toa ushahidi wake kwaba zitto ndio kafanya, toa vielelezo thabiti na kisha ndio pendekeza aombe msamaha.Kwa kipindi chote nimeona hoja zinajengwa hewani.Nimemfatilia zito katika matamshi yake.Kwa hakika sijasikia akitukana mtu zaidi ya kujitetea na kulalamia anavyoumia Tetty tuwe wakweli. Ushawahi kusikia Zitto Akitukana mtu?
Na kama hakuwa teambuilder basi hastahili kuwepo kwenye team ya uongozi ni vyema akae pembeni na awe mwanachama wa kawaida
,Mkuu hapa ndipo tutakapoonekana na kujivua nguo kabisa juu ya ajenda inayotuongoza.Kweli chadema tumechagua kueleke njia hii? Mimi sijui bwana!
kama kiongozi wa chama cha siasa kwa kweli hafai
.Mkuu hii hoja yako unaijenga kutokea hewani ndugu. Hebu jaribu kuwa neural kwanza halafu ndo utizame mambo.Tatizo ni kuanza kutizama tatizo wakati ushafanya conclusion; ni lazma ulazimishe mambo ili yaende kwenye conclusion unayotaka.
Pia ningependa kuwashauri CDM wasimfukuze uanachama adhabu waliyompa ya kumnyang'anya vyeo vyake inatosha kama mtu wa kujifunza basi atajifunza.
Hivi kwa ni kikuuliza kwamba kwa sasa Zitto anafundishwa nini na kwa nini na nikikuambia uje na vielelezo vya wazi kuthibitisha kauli yako unaweza kufanya hivyo? Mwisho, ningependa kukukumbusha tu kwamba uzi huu hauhusiani na zitto na kitendo cha watu kukazana kumchomekea zitto hapa , kinatupa picha fulani, picha inayonipa shida sana.
 
Last edited by a moderator:
inawezekana kwa upande fulani ukawa sawa , lakini kuna ushahidi wa maneno na matendo kwamba ccm wanahusika , bomu la arusha ni uthibitisho , ukubwa wa cdm mitaani unaiogopesha sana ccm , rejea maneno ya jk kwenye vikao vyao dodoma , hujuma zipo , hebu waangalie masalia waliko hivi sasa ! nakuhakikishia bila hujuma ccm hairudi madarakani 2015 ng'oo !
Mkuu; tunatengeneza fallacy kwa makusudi hali tunajua.Kwa sasa naamini miongoni mwa nyuzi ambazo ni rahisi kueleweka ni pamoja na hii. Kusema eti kwa kuwa CCM wamekuwa wanahujumu CHADEMA, wakati fulani sasa basi kila jambo linalotokea ndani ya CHADEMA tukimbilie kuishutumu CCM, ni sawa na kusema; "kwa kuwa watu wanaokuwa wabunge wakati mwengine huwa mawaziri, basi kila tukiona mtu kawa mbunge basi tuhubiri lazima atakuwa waziri huyu" halafu mfano tunaotoa tunasema "mbona Pinda amekuwa mbunge na akawa waziri" n.k.Au kwa kuwa watu wengi wanapata uongozi kwa rushwa, kila mtu akipata uongozi tunasema rushwa hiyo! tukiulizwa kuwa kwa nini? tunasema kwa kuwa fulani na fulani walipita kwa rushwa basi itakuwa ni rushwa tu hiyo hiyo! CHADEMA tumefika huku??

 
Acha ulongo weye siyo chadema wala nini itakuwa ccm wameshakutumia pesa,kachukue pesa kwa ZITTO PESA
Wewe nina uhakika kwa 100% kwamba unafanya makusudi.Hakuna haja ya mimi kutumia akili nyingi kukuelewesha.
 
betlehem naweza kusema asante kwa clarification,unajua kuna wakati huwezi kuwaelewa wanasiasa,kuna maeneo ambayo Zitto kama Zitto naweza kusema hasa pale ambapo atoa lawama kwa viogozi wenzake ambapo yeye naye ni part and parcel ya uongozi,pili kutumia media ambazo hazimjengi badala yake zinambomoa .Na kwa sasa ninaona taabu kujibu au kutetea chama sababu sijui nani wa kuamini.Still thanks for clarification & information.
 
Back
Top Bottom