CHADEMA hii si ile iliyokuwa enzi za Dkt. Wilbroad Slaa

Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
112,251
2,000
Hayo ni maoni na imani yenu chadema, lakini kwa kuwa wananchi wanaendelea kuiunga mkono CCM.

Chadema hamuungwi mkono na wananchi sababu ya kuishi kibange bange.
Hata hotuba zenu majukwaani hamna pozi.

Mnaongea kama ma MC!
Tangu lini wananchi waliwahi kuiunga mkono ccm?

Wananchi wanahitaji katiba mpya mnawapiga virungu na wengine mnawapa makesi.

Mmerogwa sana nyinyi mbogamboga.
 

Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
112,251
2,000
Hayo ni maoni na imani yenu chadema, lakini kwa kuwa wananchi wanaendelea kuiunga mkono CCM.

Chadema hamuungwi mkono na wananchi sababu ya kuishi kibange bange.
Hata hotuba zenu majukwaani hamna pozi.

Mnaongea kama ma MC!
Wewe mwenyewe ni mvuta bhangi
 

Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
112,251
2,000
Hata Mbowe aliwahi kutamka hivyo akimwambia Slaa,kwamba mzee atupishe.
Kibri ya pesa ya Lowassa ikiwa imemjaa kicjwani na rohoni.
Leo hii anajutia usiku na mchana.

Endeleeni kukaririshana ujinga tu.
Kajinyonge basi
 

residentura

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
4,729
2,000
Maisha ya mwaka 1977, sio maisha ya leo. Mahitaji, changamoto na hata tekinolojia ni tofauti. Ulimwengu unabadilika hivyo, yafaa kubadilika kuendana nayo
Kwa hiyo kama juzi hakukuwa na ushoga,leo upo, nawe utabadilika na kuwa shoga!!??
 

Mr Dudumizi

JF-Expert Member
Sep 9, 2020
1,800
2,000
Kwahiyo miradi yote hiyo katumia mshahara wake?

Hujui hizo ni kodi za wananchi wa Tanzania?

Hivi nyinyi nani kawaroga hadi kutojua nini maana ya....kajenga.....
Ya bora umekiri mwenyewe kuwa hayati Magufuli alitumia kodi za wananchi kujenga miradi mikubwa yenye tija na faida kwa nchi. Sasa kuna yule mwenyekiti wa chama fulan cha upinzani ametumia mamilioni ya ruzuku ya chama, mamilioni ya makato ya wabunge wa chama chake, mamilioni ya pesa za misaada ya wahisani, mamilioni ya shilingi aliyopokea kutoka kwa Sabodo, mamilioni ya mshahara wake alikuwa anakusanya kila mwezi kama mbunge na mamilioni ya hela za michango ya kwenye uchaguzi. Kajineemesha yeye na familia yake kama vile kwenda Dubai na Afrika kusini kula bata, huku genge lake akina Mmawia akili laghai kwa viela vidogo vidogo vya kununua unga na samaki wa kukaanga ili vimpambanie humu mitandaoni. Jamaa kakaa bungeni zaidi ya miaka 20, lkn hakuna cha maana alichofanya kwa wapiga kura wake mpaka ikafikia wapiga kura hao kukosa uvumilivu na kumtupia chupa za maji, kumzomea na kumshusha jukwaani.

images (16).jpeg
 

Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
112,251
2,000
Ya bora umekiri mwenyewe kuwa hayati Magufuli alitumia kodi za wananchi kujenga miradi mikubwa yenye tija na faida kwa nchi. Sasa kuna yule mwenyekiti wa chama fulan cha upinzani ametumia mamilioni ya ruzuku ya chama, mamilioni ya makato ya wabunge wa chama chake, mamilioni ya pesa za misaada ya wahisani, mamilioni ya shilingi aliyopokea kutoka kwa Sabodo, mamilioni ya mshahara wake alikuwa anakusanya kila mwezi kama mbunge na mamilioni ya hela za michango ya kwenye uchaguzi. Kajineemesha yeye na familia yake kama vile kwenda Dubai na Afrika kusini kula bata, huku genge lake akina Mmawia akili laghai kwa viela vidogo vidogo vya kununua unga na samaki wa kukaanga ili vimpambanie humu mitandaoni. Jamaa kakaa bungeni zaidi ya miaka 20, lkn hakuna cha maana alichofanya kwa wapiga kura wake mpaka ikafikia wapiga kura hao kukosa uvumilivu na kumtupia chupa za maji, kumzomea na kumshusha jukwaani.

View attachment 1985402
Hujajibu swali wewe lumumba
 

Larry barrice

Senior Member
Sep 17, 2021
112
250
Watanzania sote ni mashahidi kwamba CHADEMA hii si ile iliyokuwa enzi za Dk wilbroad Slaa.
Chadema iliyokuwa ikibeba sera na hoja za kuupinga ufisadi uliokuwa ukifamywa na genge la wanamtamdao ndani ya CCM.

Sera na hoja zilizopelekea kutangazwa kwa list of shame pale kwenye viwanja vya mwembeyanga tarehe 4 ya mwezi Septemba 2007.

Mambo na hoja zile zilipelekea chadema kujizolea umaarufu nchini na hivyo kujipatia wafuasi wengi.
Na watu wengi walikuwa na imani kwa kutokana na aina ya viongozi wale kama kina Dk Kaborou,Dk Slaa,Proffesa Baregu,Proffesa Safari na kina Mabere marando kwa namna walivyokuwa wakiwakilisha hoja zao kwa uzalendo wa hali ya juu.

Wale na safu yao ikakipaisha chama huku kikiwa na vijana ambao tulitumaini watarithi siasa za watangulizi wao.

Mengi yametokea tangia hapo, baadae tulianza kuona chimbuko jipya la wanasiasa kizazi cha kina Zitto,Halima mzee,Tundu lissu ,John mnyika na Godbless lema nk.

Hawa nao waliendeleza kile walichokikuta,lakini wakiwa wamekaa kimaslahi binafsi na makundi kadhaa ya viongozi waandamizi ndani ya chama chao.

Makundi hayo yakaenda mbali zaidi kwa kufikia hatua ya wale waliokuwa nyuma ya mwenyekiti Mbowe wakijiona juu zaidi na kufikia hatua ya kuwakejeli wenzao hadharani.

Hata pale ambapo chadema ilipata viongozi wa wimbi la Lowassa kujiunga nacho.wale kundi Mwenyekiti waliendeleza dharau kwa viongozi waandamizi waliokuwa na maoni tofauti na mwenyekiti Mbowe.

Hatimae tulishuhudia kwanza kabisa chadema ile ya mwenyekiti Mbowe ikiwatimua kina Kitila Mkumbo,Samson Mwigamba na Zitto kabwe kwa makosa ya usaliti.kwamba walihoji raslimali za chama kutotumika kitaasisi zaidi ili kukiimarisha chama kitaifa,ikiwemo pia mgawanyo wa madaraka kitaifa zaidi na badala yake ikilenga zaidi wanachama wenye asili ya kaskazini.

Baadae tulishuhudia Muasisi na kiomgozi mwandamizi Dk Wilbroad Slaa, akilazimika kujiondoa chamani na kumpisha chaguo la mwenyekiti Mbowe kwenye ugombea urais wa mwaka 2015,Mzee Edward Lowassa aliekuwa ametimka kutoka CCM.

Tangia hapo ni kama chama kimekosa washauri wazuri kwa mwenyekiti na kinachoendelea sasa imekuwa ni chama cha matamko na uhamasishaji wa matukio kwa umma,ingawa umma huo umekuwa haukiungi mkono kwa kutokuwa tayari kuwaunga mkono kuanzia operesheni Sangara,operesheni Ukuta,Movement for change nk.

Sasa chadema imeparanyika mara wengine wanaitana covid19.
Wengine wamepiga kambi ughaibuni kazi yao ikiwa kuiombea mabaya Tanzania , na raia wake kwa wafadhiili na jumuia za kimataifa.
Ingawa nao wamegonga mwamba baada ya taasisi hizo kuamua kuendelea kufanya kazi kwa ushirikiano na Tanzania

Sasa mwenyekiti Mbowe ana kesi inayomkabili ya ugaidi inayoendelea huko mahakamani.

Cha kushangaza chadema inayoomba mabadiliko ya katiba mpya, wamegeuka wanasheria bila ya kuheshimu hata katiba hii iliyopo sasa.ambayo inatamka kuheshimu kutokujadili mjadala au kesi yoyote iliyoko mahakamani.

Kila mwana chadema amegeuka kuwa mwanasheria,viongozi waliopo kazi yao imegeuka kujadili watu badala ya hoja na sera.
Viongozi waandamizi wamegeuka watoa kashfa kwa viongozi waandamizi wa serikali huku wakiwaombea vifo.kisa uongozi na ulafi wa kuingia ikulu na hasira za kuwa nje ya Bunge.

Chadema imefikia mahali wanasherehekea vifo vya viongozi kwa kuitana kunywa bia na kuchoma nyama kwenye mabaa.Huku wakipongezana mitandaoni.

Je kwa hali hiyo mnatarajia CHAGGA DEVELOPMENT MANIFESTO (cha de ma).

Itaungwa mkono na kina nani kwa ujinga huu?
Lazima waungaji na wafuasi wenu wawe wameyumba madish!

Ni kama vile laana ya Dk Slaa inawatafuna taratiibu.
Hicho chama mpaka atoke huo mchaga hapo....apewe mtu wa tabora , mara , shinyanga au mwanza......ila kikiwa cha wachaga tu.....msahau kuingia ikulu
 

domokaya

JF-Expert Member
Apr 22, 2010
3,545
2,000
Tubu na umuombe Mungu akuongoze uasirudie hiyo dhambi.
Mabadiliko sio dhambi, ni vipindi tu vya Mungu. 1977 isingekuwa rahisi kuwa na mbunge shoga ambaye video yake akishughulikiwa itambe halafu chama kibaki nae na mpaka leo adumu akikisemea chama akiwa kaolewa ughaibuni. Lakini sasa imewezekana.

Isingekuwa rahisi, ulaya hata Marekani, nini Tanzania kuwa na wabunge wasagaji, wakiishi pamoja na kuwa na nyadhifa za juu chamani. Lakini nyakati hizi imewezekana. Kama wewe ni hodari wa kuwashauri watu watubu ungeanza na wale.

Kila muda una mahitaji yake, waliokuletea dini unayoiamini wanaoana, unaowaamini na kuwaabudu wameolewa. Wewe utachomokea wapi? Ni suala la muda tu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom