CHADEMA hii si ile iliyokuwa enzi za Dkt. Wilbroad Slaa

Bengal

JF-Expert Member
Aug 29, 2018
6,535
2,000
Watanzania sote ni mashahidi kwamba CHADEMA hii si ile iliyokuwa enzi za Dk wilbroad Slaa.
Chadema iliyokuwa ikibeba sera na hoja za kuupinga ufisadi uliokuwa ukifamywa na genge la wanamtamdao ndani ya CCM.

Sera na hoja zilizopelekea kutangazwa kwa list of shame pale kwenye viwanja vya mwembeyanga tarehe 4 ya mwezi Septemba 2007.

Mambo na hoja zile zilipelekea chadema kujizolea umaarufu nchini na hivyo kujipatia wafuasi wengi.
Na watu wengi walikuwa na imani kwa kutokana na aina ya viongozi wale kama kina Dk Kaborou,Dk Slaa,Proffesa Baregu,Proffesa Safari na kina Mabere marando kwa namna walivyokuwa wakiwakilisha hoja zao kwa uzalendo wa hali ya juu.

Wale na safu yao ikakipaisha chama huku kikiwa na vijana ambao tulitumaini watarithi siasa za watangulizi wao.

Mengi yametokea tangia hapo, baadae tulianza kuona chimbuko jipya la wanasiasa kizazi cha kina Zitto,Halima mzee,Tundu lissu ,John mnyika na Godbless lema nk.

Hawa nao waliendeleza kile walichokikuta,lakini wakiwa wamekaa kimaslahi binafsi na makundi kadhaa ya viongozi waandamizi ndani ya chama chao.

Makundi hayo yakaenda mbali zaidi kwa kufikia hatua ya wale waliokuwa nyuma ya mwenyekiti Mbowe wakijiona juu zaidi na kufikia hatua ya kuwakejeli wenzao hadharani.

Hata pale ambapo chadema ilipata viongozi wa wimbi la Lowassa kujiunga nacho.wale kundi Mwenyekiti waliendeleza dharau kwa viongozi waandamizi waliokuwa na maoni tofauti na mwenyekiti Mbowe.

Hatimae tulishuhudia kwanza kabisa chadema ile ya mwenyekiti Mbowe ikiwatimua kina Kitila Mkumbo,Samson Mwigamba na Zitto kabwe kwa makosa ya usaliti.kwamba walihoji raslimali za chama kutotumika kitaasisi zaidi ili kukiimarisha chama kitaifa,ikiwemo pia mgawanyo wa madaraka kitaifa zaidi na badala yake ikilenga zaidi wanachama wenye asili ya kaskazini.

Baadae tulishuhudia Muasisi na kiomgozi mwandamizi Dk Wilbroad Slaa, akilazimika kujiondoa chamani na kumpisha chaguo la mwenyekiti Mbowe kwenye ugombea urais wa mwaka 2015,Mzee Edward Lowassa aliekuwa ametimka kutoka CCM.

Tangia hapo ni kama chama kimekosa washauri wazuri kwa mwenyekiti na kinachoendelea sasa imekuwa ni chama cha matamko na uhamasishaji wa matukio kwa umma,ingawa umma huo umekuwa haukiungi mkono kwa kutokuwa tayari kuwaunga mkono kuanzia operesheni Sangara,operesheni Ukuta,Movement for change nk.

Sasa chadema imeparanyika mara wengine wanaitana covid19.
Wengine wamepiga kambi ughaibuni kazi yao ikiwa kuiombea mabaya Tanzania , na raia wake kwa wafadhiili na jumuia za kimataifa.
Ingawa nao wamegonga mwamba baada ya taasisi hizo kuamua kuendelea kufanya kazi kwa ushirikiano na Tanzania

Sasa mwenyekiti Mbowe ana kesi inayomkabili ya ugaidi inayoendelea huko mahakamani.

Cha kushangaza chadema inayoomba mabadiliko ya katiba mpya, wamegeuka wanasheria bila ya kuheshimu hata katiba hii iliyopo sasa.ambayo inatamka kuheshimu kutokujadili mjadala au kesi yoyote iliyoko mahakamani.

Kila mwana chadema amegeuka kuwa mwanasheria,viongozi waliopo kazi yao imegeuka kujadili watu badala ya hoja na sera.
Viongozi waandamizi wamegeuka watoa kashfa kwa viongozi waandamizi wa serikali huku wakiwaombea vifo.kisa uongozi na ulafi wa kuingia ikulu na hasira za kuwa nje ya Bunge.

Chadema imefikia mahali wanasherehekea vifo vya viongozi kwa kuitana kunywa bia na kuchoma nyama kwenye mabaa.Huku wakipongezana mitandaoni.

Je kwa hali hiyo mnatarajia CHAGGA DEVELOPMENT MANIFESTO (cha de ma).

Itaungwa mkono na kina nani kwa ujinga huu?
Lazima waungaji na wafuasi wenu wawe wameyumba madish!

Ni kama vile laana ya Dk Slaa inawatafuna taratiibu.
Je vipi ulinganifu wako kwa kijani ya enzi hizo na kijani mpya.
 
voicer

JF-Expert Member
Jul 13, 2020
652
1,000
CCM hii ndiyo ile CCM ya 1977 na waliyotaka kuiona waasisi wake!!?? Tuliokuwepo miaka hiyo hatuamini kama CCM ya sasa ni chama cha siasa sawasawa na kile cha mwaka 1977.
Chama chenye serikali kinakuwaje chama cha kijambazi/kimafia/kigaidi!!?? Ndio maono ya waasisi wake!!?
Hayo ni maoni na imani yenu chadema, lakini kwa kuwa wananchi wanaendelea kuiunga mkono CCM.

Chadema hamuungwi mkono na wananchi sababu ya kuishi kibange bange.
Hata hotuba zenu majukwaani hamna pozi.

Mnaongea kama ma MC!
 
Baba jayaron

JF-Expert Member
Jun 29, 2015
2,199
2,000
Watanzania sote ni mashahidi kwamba CHADEMA hii si ile iliyokuwa enzi za Dk wilbroad Slaa.
Chadema iliyokuwa ikibeba sera na hoja za kuupinga ufisadi uliokuwa ukifamywa na genge la wanamtamdao ndani ya CCM.

Sera na hoja zilizopelekea kutangazwa kwa list of shame pale kwenye viwanja vya mwembeyanga tarehe 4 ya mwezi Septemba 2007.

Mambo na hoja zile zilipelekea chadema kujizolea umaarufu nchini na hivyo kujipatia wafuasi wengi.
Na watu wengi walikuwa na imani kwa kutokana na aina ya viongozi wale kama kina Dk Kaborou,Dk Slaa,Proffesa Baregu,Proffesa Safari na kina Mabere marando kwa namna walivyokuwa wakiwakilisha hoja zao kwa uzalendo wa hali ya juu.

Wale na safu yao ikakipaisha chama huku kikiwa na vijana ambao tulitumaini watarithi siasa za watangulizi wao.

Mengi yametokea tangia hapo, baadae tulianza kuona chimbuko jipya la wanasiasa kizazi cha kina Zitto,Halima mzee,Tundu lissu ,John mnyika na Godbless lema nk.

Hawa nao waliendeleza kile walichokikuta,lakini wakiwa wamekaa kimaslahi binafsi na makundi kadhaa ya viongozi waandamizi ndani ya chama chao.

Makundi hayo yakaenda mbali zaidi kwa kufikia hatua ya wale waliokuwa nyuma ya mwenyekiti Mbowe wakijiona juu zaidi na kufikia hatua ya kuwakejeli wenzao hadharani.

Hata pale ambapo chadema ilipata viongozi wa wimbi la Lowassa kujiunga nacho.wale kundi Mwenyekiti waliendeleza dharau kwa viongozi waandamizi waliokuwa na maoni tofauti na mwenyekiti Mbowe.

Hatimae tulishuhudia kwanza kabisa chadema ile ya mwenyekiti Mbowe ikiwatimua kina Kitila Mkumbo,Samson Mwigamba na Zitto kabwe kwa makosa ya usaliti.kwamba walihoji raslimali za chama kutotumika kitaasisi zaidi ili kukiimarisha chama kitaifa,ikiwemo pia mgawanyo wa madaraka kitaifa zaidi na badala yake ikilenga zaidi wanachama wenye asili ya kaskazini.

Baadae tulishuhudia Muasisi na kiomgozi mwandamizi Dk Wilbroad Slaa, akilazimika kujiondoa chamani na kumpisha chaguo la mwenyekiti Mbowe kwenye ugombea urais wa mwaka 2015,Mzee Edward Lowassa aliekuwa ametimka kutoka CCM.

Tangia hapo ni kama chama kimekosa washauri wazuri kwa mwenyekiti na kinachoendelea sasa imekuwa ni chama cha matamko na uhamasishaji wa matukio kwa umma,ingawa umma huo umekuwa haukiungi mkono kwa kutokuwa tayari kuwaunga mkono kuanzia operesheni Sangara,operesheni Ukuta,Movement for change nk.

Sasa chadema imeparanyika mara wengine wanaitana covid19.
Wengine wamepiga kambi ughaibuni kazi yao ikiwa kuiombea mabaya Tanzania , na raia wake kwa wafadhiili na jumuia za kimataifa.
Ingawa nao wamegonga mwamba baada ya taasisi hizo kuamua kuendelea kufanya kazi kwa ushirikiano na Tanzania

Sasa mwenyekiti Mbowe ana kesi inayomkabili ya ugaidi inayoendelea huko mahakamani.

Cha kushangaza chadema inayoomba mabadiliko ya katiba mpya, wamegeuka wanasheria bila ya kuheshimu hata katiba hii iliyopo sasa.ambayo inatamka kuheshimu kutokujadili mjadala au kesi yoyote iliyoko mahakamani.

Kila mwana chadema amegeuka kuwa mwanasheria,viongozi waliopo kazi yao imegeuka kujadili watu badala ya hoja na sera.
Viongozi waandamizi wamegeuka watoa kashfa kwa viongozi waandamizi wa serikali huku wakiwaombea vifo.kisa uongozi na ulafi wa kuingia ikulu na hasira za kuwa nje ya Bunge.

Chadema imefikia mahali wanasherehekea vifo vya viongozi kwa kuitana kunywa bia na kuchoma nyama kwenye mabaa.Huku wakipongezana mitandaoni.

Je kwa hali hiyo mnatarajia CHAGGA DEVELOPMENT MANIFESTO (cha de ma).

Itaungwa mkono na kina nani kwa ujinga huu?
Lazima waungaji na wafuasi wenu wawe wameyumba madish!

Ni kama vile laana ya Dk Slaa inawatafuna taratiibu.
Kwendraaa ukoooo..... Kwani JK alikua anateka, kupiga risasi na kubambikia upinzani kesi za ugaidi?

Ungekua wewe ungeweza ??? Nyang'au mkubwa
 
voicer

JF-Expert Member
Jul 13, 2020
652
1,000
Umeshaeleza kuwa ..."alipokuwa Slaa"...!Sasa hayupo Slaa na bado unataka kifanane na alipokuwa Slaa?Mawazo ya wapi hayo?Slaa bado anaishi,mfuate.
Hata Mbowe aliwahi kutamka hivyo akimwambia Slaa,kwamba mzee atupishe.
Kibri ya pesa ya Lowassa ikiwa imemjaa kicjwani na rohoni.
Leo hii anajutia usiku na mchana.

Endeleeni kukaririshana ujinga tu.
 
Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
52,035
2,000
mazingira yamebadilika, utawala wa JK na wa dikteta ni vitu viwili tofauti, JK aliruhusu mijadala na wapinzani pamoja na mikutano ya hadhara, sasahivi hata vikao vya ndani ni dhambi kubwa, aje basi aitishe mkutano wa hadhara kama mpinzania akione cha moto
 
voicer

JF-Expert Member
Jul 13, 2020
652
1,000
Kwendraaa ukoooo..... Kwani JK alikua anateka, kupiga risasi na kubambikia upinzani kesi za ugaidi?

Ungekua wewe ungeweza ??? Nyang'au mkubwa
Wewe fala soma topic uielewe nimeongelea list of shame. Scandal kama Meremeta,Escrow na Epa...wewe unakurupuka eti fyo....fyo....fyo
Nani nchi hii hayajui madudu ya kikwete na genge lake?
 
Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
52,035
2,000
Najaribu kumfikiria Mwenyekiti anavyoupitisha usiku wake kule aliko.
Shauri ya kuukubali ushauri wa wafuasi wajinga wajinga kama nyie.
Mpuuzi kama wewe, magereza unaweza kupelekwa hata wewe, Mandela alikaa miaka 27 Mbowe ni nani asikae? ndiyo maana umeshindwa kuolewa mkuu mpaka leo sababu ya tabia zako za ajabu
 
Pac the Don

JF-Expert Member
Feb 17, 2021
1,212
2,000
Hizi 1.5trl alizochukua simlaumu maana kafanya au kujenga vitu vinavyoonekana kama vile Magufuli terminal pale mbezi luisi, stand ya treni ya kisasa ambayo itazinduliwa hivi punde, bara bara za njia 8 zilizokamilika na zile ambazo zimeshafikia hatua ya kukamilika kama vile morogoro road, kilwa road, bagamoyo road nk, daraja la mfugali, flyover, bwawa la kufufua umeme, ndege zetu wenyewe zilizopo na zile ambazo bado hazijafika ila zishalipiwa tayari, daraja la busizi, stand za mabasi za kisasa katika baadhi ya mikoa huku zingine zikiwa katika process ya kujengwa nk. Kifupi zile 1.5 T zimeenda katika matumizi sahihi ukilinganisha na yale mabilioni waliyokuwa wanakatwa wabunge, kile mwezi kwa muda wa miaka 5, mamilion ya ruzuku za chama, mamilioni ya hela za wafadhili kama vile kina Sabodo nk, michango tuliochangishwa kwenye kampeni nk ndio tunazoulizia zilipokwenda maana hakuna chama maana kilichofanyika ambacho anaweza kutuonesha kama alivyotuonesha wa 1.5 T. Ambapo matumizi yake yanaonekana kwa macho na sio porojo.
Sasa ndugu yang sisimizi.. kama ndivyo hivyo kulikua na ugumu gan kufanya analysis ya matumiz kama haya unayodai mpaka ikapelekea Mzee wa watu kutumbuliwa kisa kuhoji matumiz yake?
 
residentura

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
4,591
2,000
Hayo ni maoni na imani yenu chadema, lakini kwa kuwa wananchi wanaendelea kuiunga mkono CCM.

Chadema hamuungwi mkono na wananchi sababu ya kuishi kibange bange.
Hata hotuba zenu majukwaani hamna pozi.

Mnaongea kama ma MC!
Shida yenu "watoto wa shule za kata" ni kutotaka kuijua historia ya kweli ya inchi yenu.
Mmekaririshwa.
 
voicer

JF-Expert Member
Jul 13, 2020
652
1,000
Shida yenu "watoto wa shule za kata" ni kutotaka kuijua historia ya kweli ya inchi yenu.
Mmekaririshwa.
Mimi nakumbuka historia ya kifo chenye utata cha aliyekuwa mbunge wa Tarime enzi hizo marehemu Chacha Wangwe, baada ya kuhoji matumizi ya ruzuku ya chadema.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom