Wana CHADEMA wenzangu kabla ya yote niwakumbushe nini kilitokea kwenye ule mchakato wa katiba mpya pale Dodoma kwenye Bunge la Katiba, laiti tungekubali japo nusu ya mapendekezo ya ile katiba kupita leo hii tungekua kwenye hatua kubwa kuelekea michakato huru ya siasa zetu lakini kutaka kupata yote imetufanya tukose vyote.
Kwa utangulizi huo turudi kwenye hii hoja ya wabunge wetu kwenda bungeni. Katika hili nashauri tupate wapambanaji wachache waende, tukumbuke CCM walitaka asipatikane hata mbunge mmoja aliye mpinzani halisi lakini mipango ya Mungu imetubeba wanyonge sisi.
Wabunge hawa watasaidia sana kupush hoja zetu kuelekea mapambano mengine ya kidemokrasia la sivyo tutakua tumekosa vyote kama tulivyokosa Katiba mpya.
Mwenyezi Mungu awaongoze katika tafakari yenu pengine mtapata tafakari bora kuliko hii yangu.