CHADEMA hawataki kusikia mema yanayotendwa na Serikali

Zee la kitaa

JF-Expert Member
Oct 25, 2017
403
211
Vyama vya upinzani havimaanishi uadui na chama tawala bali vyote vinatakiwa kujielewa kuwa vipo kwa ajili ya kuleta maendeleo katika taifa la Tanzania.

Imefikiwa wakati CHADEMA hawataki kusikia mazuri yanayotekelezwa na serikali na bahati mbaya vijana wa CHADEMA wamejikita kueneza mabaya bila kutambua hata jema linalotekelezwa na Serikali. Ukiwa kiongozi ndani ya chadema we sifia serikali utaitwa kila aina la jina.

Umenunuliwa; unataka kujiunga na CCM na mambo mengine kadhaa. Kuwa upinzani hakumaanisha ni kupinga kila kitu bali kuwa watch dog to the ruling part na kupaza sauti kwa jema na zuri; kuhusu baya ni kuleta njia bora ya kufikia maendeleo ya taifa hili.

Ikumbukwe Tanzania itabaki kuwa Tanzania bali vyama vitapita na kupotea.

Ni wakati vyama vikatambua kushirikiana vizuri na serikali kujenga taifa letu kwa kizazi cha sasa na badae.
 
Mbona ccm ikifanya vzr tunaisifia sana tu;
hata wabunge walioliingiza taifa hasara kubwa na kurudia tena chaguzi kwa fedha ambazo ni 'uhujumu uchumi' ccm inastahili sana kusifiwa.
Pia wale wengine woote waliondoka Upinzani na kujiunga ccm kwa 'ahadi' mbalimbali ccm pia inahitaji sifa sana mkuu.
 
Huwezi kujenga Taifa wakati amani haipo! tuache kuuana ndipo tutapata msingi amani yenye kuelekea kwenye maendeleo
Nani anaua wengine. Ujambazi unatakiwa kupingwa na kila MTU na kila chama. Hakuna chama kinachotaka watu wake wauwawe. Hoja ya msingi ni kushirikiana na kujenga taifa.
 
Mbona ccm ikifanya vzr tunaisifia sana tu;
hata wabunge walioliingiza taifa hasara kubwa na kurudia tena chaguzi kwa fedha ambazo ni 'uhujumu uchumi' ccm inastahili sana kusifiwa.
Pia wale wengine woote waliondoka Upinzani na kujiunga ccm kwa 'ahadi' mbalimbali ccm pia inahitaji sifa sana mkuu.
Hapa ndio msingi kiongozi ukaelewa. Acheni kujenga uadui ama kuwaona wabunge wenu wakisifia ama kupongeza jambo jema kama wanawahujumu. Juzi tu hapa Maneno ya Lowasa yalileta gongana katika chadema matamko kibao ya vijana wa chadema. Mkiacha hayo hakuna wabunge watakaohama. Bali watabaki na kuendelea kushirikiana na serikali.
 
Acheni kutumia ushawishi wa 'ile kitu iliyo ktk damu yenu' muone kama kuna kiumbe chochote hai kitapiga hodi ktk nyumba yenu.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Vyama vya upinzani havimaanishi uadui na chama tawala bali vyote vinatakiwa kujielewa kuwa vipo kwa ajili ya kuleta maendeleo katika taifa la Tanzania. Imefikiwa wakati chadema hawataki kusikia mazuri yanayotekelezwa na serikali na bahati mbaya vijana wa chadema wamejikita kueneza mabaya bila kutambua hata jema linalotekelezwa na serikali. Ukiwa kiongozi ndani ya chadema we sifia serikali utaitwa kila aina la jina. Umenunuliwa; unataka kujiunga na ccm na mambo mengine kadhaa. Kuwa upinzani hakumaanisha ni kupinga kila kitu bali kuwa watch dog to the ruling part na kupaza sauti kwa jema na zuri; kuhusu baya ni kuleta njia bora ya kufikia maendeleo ya taifa hili. Ikumbukwe Tanzania itabaki kuwa Tanzania bali vyama vitapita na kupotea. Ni wakati vyama vikatambua kushirikiana vizuri na serikali kujenga taifa letu kwa kizazi cha sasa na badae.
Acha uongo, siyo kweli kuwa chadema haiyaoni mazuri yanayofanywa na serikali yapo tu tena mengi, mfano rais amerudisha nidhamu kwa watumishi wa umma, anapambana na kutetea raslimali za nchi, anaboresha sekta ya afya na elimu, chadema wanachokipinga nipate tu mh rais anapoikanyaga katiba ya nchi na wakati mwingine matamko yake yanakuwa juuu ya katiba, lakini pia chadema wanapinga tu pale mh anapotumia dola kuwatisha watu ili asikosolewe.
 
msingetoa matamko ya kumpinga Lowasa alipompongeza rais. mkaanza kuleta hoja za kijinga.
 
Kwani vijana wa CCM walishawai lini kusifia mazuri yanayofanywa na upinzani?, mboni badala ya kuwasifia wanawachapa lisasi 38?
 
Vyama vya upinzani havimaanishi uadui na chama tawala bali vyote vinatakiwa kujielewa kuwa vipo kwa ajili ya kuleta maendeleo katika taifa la Tanzania. Imefikiwa wakati chadema hawataki kusikia mazuri yanayotekelezwa na serikali na bahati mbaya vijana wa chadema wamejikita kueneza mabaya bila kutambua hata jema linalotekelezwa na serikali. Ukiwa kiongozi ndani ya chadema we sifia serikali utaitwa kila aina la jina. Umenunuliwa; unataka kujiunga na ccm na mambo mengine kadhaa. Kuwa upinzani hakumaanisha ni kupinga kila kitu bali kuwa watch dog to the ruling part na kupaza sauti kwa jema na zuri; kuhusu baya ni kuleta njia bora ya kufikia maendeleo ya taifa hili. Ikumbukwe Tanzania itabaki kuwa Tanzania bali vyama vitapita na kupotea. Ni wakati vyama vikatambua kushirikiana vizuri na serikali kujenga taifa letu kwa kizazi cha sasa na badae.

Umenena vyema, CHADEMA na upinzani kwa ujumla hupenda kusikia mabaya na hata kama hayapo basi hutunga, mfano wa haraka ni mpika takwimu Zitto Kabwe aliyekuwa akilazimisha kuwa makusanyo ya kodi yameshuka na nk.
 
Je serikali inataka kusikia mema ya upinzani, na kufanyia kazi?
With examples convince me
Kiongozi hata mbowe amekiri kuwa mambo mengi walioyokuwa wanayapigia kelele upinzani yanafanyiwa kazi. Sasa ukisema serikali haisikii unamaanisha nini.
 
Vyama vya upinzani havimaanishi uadui na chama tawala bali vyote vinatakiwa kujielewa kuwa vipo kwa ajili ya kuleta maendeleo katika taifa la Tanzania. Imefikiwa wakati chadema hawataki kusikia mazuri yanayotekelezwa na serikali na bahati mbaya vijana wa chadema wamejikita kueneza mabaya bila kutambua hata jema linalotekelezwa na serikali. Ukiwa kiongozi ndani ya chadema we sifia serikali utaitwa kila aina la jina. Umenunuliwa; unataka kujiunga na ccm na mambo mengine kadhaa. Kuwa upinzani hakumaanisha ni kupinga kila kitu bali kuwa watch dog to the ruling part na kupaza sauti kwa jema na zuri; kuhusu baya ni kuleta njia bora ya kufikia maendeleo ya taifa hili. Ikumbukwe Tanzania itabaki kuwa Tanzania bali vyama vitapita na kupotea. Ni wakati vyama vikatambua kushirikiana vizuri na serikali kujenga taifa letu kwa kizazi cha sasa na badae.

Umeshasema UPINZANI sasa wakifanya hiko unachotaka ww wafanye watakuwa sio wapinzani tena

Ndio maana ya upinzani, jambo ambalo ww unaona ni jema wao wanaona lingefanyika kwa njia nyingine lingekuwa ni jema zaidi,
Kumbe ni kuleta changamoto kutekeleza mambo katika njia inayotakiwa. Tatizo kila jambo mnapinga bila kuleta njia mbadala ama suluhisho. Huu ndio upinzani wa bongo
 
Back
Top Bottom