Chadema hawana vikao vya Chama?

Sokomoko

JF-Expert Member
Mar 29, 2008
1,915
127
WanaJF,

Nimekuwa nikifuatilia mwenendo wa chama kikuu cha upinzani kabla na baada ya uchaguzi nimegundua kuwa uamuzi mwingi wa chama unatoka kwenye forum yetu yaani JF mfano.

1.Gari la Azania uzushi uliozushwa hapa JF na Slaa kuudaka juu kwa juu
2.Kugomea matokeo ya uchaguzi, ikumbukwe kuwa ni sisi wanaJF tuliopendekeza Slaa agomee matokeo na kweli akagomea.
2.Barua za waliokacha siku ya walk out Bungeni dodoma, sijui ila inaonyesha hata Mwenyekiti wa Chadema bwana Mbowe hakujua kama kuna wabunge hawaku "walk out" siku ile wabunge wa CDM walipotoka. Ila baada ya moto uliowashwa hapa na ushauri tuliotoa hatimae chama kikatusikiza na kuwaandikia wabunge ambao hawaku"walk out"

Sisi tunaweza ndio tukawa waamuzi wa hichi chama je mnalionaje hili wadau?
 
ni kweli kabisa usemayo mkuu. pia kua ile barua iliyodaiwa kuandikwa na wilson kbwe wa mwanza ya kuchakachua matokeo ilianbandiwa hapa , baadaye gazeti lao la tz daima. lakini iko wazi kuwa baadhi ya viongozi waandamizi wa chadema ni wanachama wa JF, hivyo hakuna kosa kuchota hapa hekima
 
Sokomoko umeanza kuonyesha rangi zako halisi nilifikiri wewe ni mwanamapinduzi - hata hivyo kuna vitu vingi vya kujadili hivi vya chadema havikujengi wewe kisaikologia waache wenyewe na chama chao wana uongozi na muongozo wao kama chama
 
Chadema wanaleta mkwara kama wa mchicha vile, majani rundo ila ukibandikwa jikoni unanywea na kuelea kwenye sufuria. Yaani wingi wenuJF haututishi sie tusio kuwa na vyama kwasababu what matter ni point na facts tu.
 
Senior na wewe tena? angehoji hayo maswali kwa ccm ingekuwa haki, ila chadema waachiwe wenyewe? chama kinachokuja kushika nchi?

kuna wanachadema humu, watamjibu vizuri, na watampa ratiba za vikao na ataridhika! majibu kama yako ni kwa hawa juniors wanajua kupiga vijembe tu na hawana point yoyote!

so far kama alichosema ni kweli what your stand? Slaa vitu vingi alivichukua humu na that alone was disqualifying him from power
 
Mimi ni mwanamapinduzi ila nakereka na tabia ya baadhi ya wanamapinduzi hawana muono kila kitu wanatetea. We fikiria wakati watu wanatakiwa kuangalia masuala ya kumkomboa masikini wao wanapika fitina hapa JF Zitto afukuzwe huo uwanamapinduzi gani mkuu? Fikiria mwenyewe.

Shy wewe ni shahidi juu ya post zangu za mwanzo naingia hapa JF nakumbuka kupambana na wewe sawia ila amini nakatishwa tamaa na uoinzani especial Chadema na nimekuja kugundua wana agenda zao nyingi za siri Mungu ameepushilia mbali hawakuchukua nchi saa hizi tungekuwa tunatafuta pa kukimbilia kama mambo yenyewe ndio haya ya kufukuzana.
 
Chadema wanaleta mkwara kama wa mchicha vile, majani rundo ila ukibandikwa jikoni unanywea na kuelea kwenye sufuria. Yaani wingi wenuJF haututishi sie tusio kuwa na vyama kwasababu what matter ni point na facts tu.

Je uliyoandika hapo juu ni facts
 
Senior na wewe tena? angehoji hayo maswali kwa ccm ingekuwa haki, ila chadema waachiwe wenyewe? chama kinachokuja kushika nchi?

kuna wanachadema humu, watamjibu vizuri, na watampa ratiba za vikao na ataridhika! majibu kama yako ni kwa hawa juniors wanajua kupiga vijembe tu na hawana point yoyote!

so far kama alichosema ni kweli what your stand? Slaa vitu vingi alivichukua humu na that alone was disqualifying him from power

Ni chama pekee kinachochukua utumbo kwenye forums duniani na kuziweka vipaumbele kwenye chama.
 
Wewe sokomoko usiwe mnafiki tangu lini wewe ukatoa ushauri kwa chadema kupitia jf? Usitake sifa ambayo huna, wewe ni mkulupukaji kila siku na matusi kwa strategy kwa chadema na wanachadema. Naomba nikuthibitishie kuwa pamoja na unafiki wa member wachache ndani ya jf, kimsingi jf imejaa wazalendo na wasomi ambao hutumika kupashana habari na elim ya uraia. Sasa yanayokuja jf siyo kwamba hayajafika au yameshafika ngome ya chadema. Chadema ni chama makini kinachosikliza na kufanya uchunguzi. Mambo mengi ambayo chadema imekuwa ikiyatoa kupitia makamanda wake mara zote wanafiki wamekuwa wakisema ni uongo lakini mwisho inajulikana ni kweli. Mifano michache ni hiyo uliyotoa
1. Kikao cha mwanza kama ingekuwa uongo dr slaa angekuwa mahakamani na wengine wote
2. Gari la adhani kama ingekuwa uongo adhani angeenda mahakamani, kwa taarifa yako karatasi hizo za kura zilikamatwa musoma

kwa hiyo usishangae mengi yanayojadiliwa humu yanafanyiwa kazi, hata leo asubuhi star tv imekiri kutumia michango ya wana jf, labda nikushauri tuu kwamba unapochangia ndani ya jf fikiri kwanza lakini kama umetumwa basi endelea na kazi yako. Ndio maana ccm imekutuma wewe, malaria sugu na weberoya ili kuthibitisha umuhim wa jf. Hongera jf kwa kazi nzuri sasa vita ni katiba mpya, tume huru ya uchaguzi, na tume huru ya uchunguzi.
 
WanaJF,

Nimekuwa nikifuatilia mwenendo wa chama kikuu cha upinzani kabla na baada ya uchaguzi nimegundua kuwa uamuzi mwingi wa chama unatoka kwenye forum yetu yaani JF mfano.

1.Gari la Azania uzushi uliozushwa hapa JF na Slaa kuudaka juu kwa juu
2.Kugomea matokeo ya uchaguzi, ikumbukwe kuwa ni sisi wanaJF tuliopendekeza Slaa agomee matokeo na kweli akagomea.
2.Barua za waliokacha siku ya walk out Bungeni dodoma, sijui ila inaonyesha hata Mwenyekiti wa Chadema bwana Mbowe hakujua kama kuna wabunge hawaku "walk out" siku ile wabunge wa CDM walipotoka. Ila baada ya moto uliowashwa hapa na ushauri tuliotoa hatimae chama kikatusikiza na kuwaandikia wabunge ambao hawaku"walk out"

Sisi tunaweza ndio tukawa waamuzi wa hichi chama je mnalionaje hili wadau?

crapist
 
kama wewe ni mwanamapunduzi ukweli vua hilo joho lako la jina bandia kuja na jina lako halisi halafu onge ulichoongea utasikilizwa kwa kuwa utakuwa na ushahidi lakini kwa njia hii usitegemee kupata kitu labda ni kuendeleza majungu tu - na waberoya unatakiwa ujue uchaguzi umeshakwisha waache wenye vyama hivyo waendeleze vyama kwa njia za amani na wanachama wao
 
Sawa mkuu,nimekusikia, nimekusoma na ninafuata ushauri wako kuanzia saa hii.

cheers
 
so far kama alichosema ni kweli what your stand? Slaa vitu vingi alivichukua humu na that alone was disqualifying him from power

Kikwete alichukua wapi pointi zake?

usitoe majibu kama juha

akili zako na za mbayuwayu sawasawa
 
Mhe. Sokomoko,

Why don't you become modest enough; by giving the leadership of Chadema the benefit of always thinking along the lines of JF members?

CDM leaders meet and discuss, they are in touch with one another continuously . They do not always read JF contributors.

And mind you, they do not always have to call press conferences to announce what they decide. CHADEMA is a dynamic political party.
 
Back
Top Bottom