CHADEMA hawana uwezo wa kuchukua nchi. Wakikamiwa wanapoa Kama uji wa dundi

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,337
51,848
Salama Wakuu!

Kwa jinsi mambo nilivyoyakuta na yalivyosasa kuhusiana na Siasa za nchi hii, nadiriki kusema kuwa CHADEMA bado Sana katika kuchukua nchi.

Nimeanza kufuatilia Siasa mwaka 2005, mpaka sasa ni miaka 16. Sio miaka mingi ila pia sio michache Sana. Inatosha Kueleza Jambo.

Nikiwatazama CHADEMA, kisha nikiwaangalia Watanzania, alafu nikamalizia na CCM wenyewe. Ni wazi kuwa, CHADEMA bado Sana kuchukua nchi hii.

Hawana uwezo Kwa sababu, hawana uwezo wa kukaza, hawana uwezo wa mapambano makali ya Muda mrefu.
CHADEMA ni Kama watoto, ambao Sisi wanafasihi tunasemaga Ngoma ya watoto haikeshi.

Kama ni kwenye riadha CHADEMA wanaziweza mbio fupi za Mita Mia, hapo wanaouwezo wa kukimbia Kwa Kasi kubwa wakashinda. Lakini mbio ndefu hakika CHADEMA wamethibitisha kuwa hawaziwezi. CCM wao wamejithibitishia kuwa wao ni mabingwa wa mbio ndefu.

CHADEMA kwenye Uwanja WA vita wapo kwenye kundi ambalo wanapenda ukanda wenye mashambulizi yaliyopoa, hawahimili ukanda wenye mashambulizi makali yasiyokoma.

CHADEMA wamepoa Kama uji wa dundi.
Mengi wanayoyapigania wameshindwa kuyapata, wanaishia kulalamika tuu.

Siku zote kwenye maisha, ukishakuwa upande wa mlalamikaji basi jua umekwisha.

CCM wao ni watu wakuchukua hatua. Hawalalamiki.

CHADEMA mkiendelea hivi kuwa Kama uji wa dundi, mtakatika vipande vipande.

Nawasilisha
 
Mnyika alituambia tujiandae kwa makongamano ya katiba pale alipoishia Mbowe wao wataendeleza, tena alisema ni maagizo ya kamati kuu, Heche naye akakazia, inapita mwezi now wote wapo kimyaa! Mnyika sijui hata huko Ufipa anaenda siku hizi, Heche yeye yupo busy kukamua maziwa ng'ombe wake!!

Lissu akasema hawatamuwekea wakili Mbowe, wala kumuombea dhamana, vilevile hataongea chochote, leo hii Mbowe ana mawakili zaidi ya 5, na kila siku watu wake wanampigia magoti Mother aongee na DPP aifute kesi!! CDM sijui hata wanasimamia nini kwa sasa kwenye siasa za TZ
 
Salama Wakuu!

Kwa jinsi mambo nilivyoyakuta na yalivyosasa kuhusiana na Siasa za nchi hii, nadiriki kusema kuwa CHADEMA bado Sana katika kuchukua nchi...
Sawa,endelea kutazama Huo uji usimwagike ukaunguza makada kwenye kitengo.ISPOILER][/ISPOILER]
 
Uzi wa Kipopomarism...kwaakili yake ndogo anafikiri CHADEMA ni Mbowe Myika Sugu nk Chadema ni beyond those...
 
Mnyika alituambia tujiandae kwa makongamano ya katiba pale alipoishia Mbowe wao wataendeleza, tena alisema ni maagizo ya kamati kuu, Heche naye akakazia, inapita mwezi now wote wapo kimyaa! ...
Kama wangeweza mapambano makali yasiyokoma pengine Kwa sasa wangeheshimiana.
 
chadema siasa zimeshawashinda hawana organize nzuri waropokaji tu kama kina pambalu sasa hapo kuna nini
 
Kama wangeweza mapambano makali yasiyokoma pengine Kwa sasa wangeheshimiana.
Kuna njia nyingi za kuheshimiana ukiacha hayo mapambano makali, unaweza ukafanya siasa za kistaarabu, ukawa really na ukaheshimika sana tu. Tatizo linakuja pale ambapo watu wavivu na wajanja wajanja wanapojiingiza kwenye siasa kwa nia yakujipatia kipato kingi na kwa urahisi, Mifano ni Mingi michache ni hawa akina Mdee, Katambi, Mwita, Gekul, nassari....Wananchi wanawapigania, wanahatarisha maisha yao kupambana na vyombo vya dola kuhakikisha wanatangazwa, mwisho wa siku wanaacha ubunge wenyewe wanaamia CCM! And ukiwauliza viongozi wanatoa jibu rahisi tu, eti wamenunuliwa hao!!!!! Sasa kama watu waliopo chini ya uongozi wako wananunuliwa na wewe unaona jambo la kawaida tu, nani atakuamini wewe na chama chako siku za mbeleni?
 
Njaa.
Njaa.
Njaa.

Wenye Uzalendo WA kweli ni wachache sana
 
ROBERT HERIEL, tangu nimeanza kukusoma post zako nimegundua kuwa wewe ni mweupe sana kichwani. Nyuzi zako zote zinahusu Chadema.

Tushakuambia mara milioni, kwamba ccm ilishajifia kitambo. Haipo tena, Chadema inafanya shughuli zake katika mazingira magumu ya kisiasa. Na wewe unajua.
Mizani ya ushindani kati ya the so called ccm na Chadema si sawa. Ccm wanatumia njia zote ovu, wanavunja sheria na hakuna mtu wa kuwawajibisha. Unatakaje hawa washinde kwenye mazingira kama haya?
Siasa ni majukwaani na mabarabarani hii ni kauli ya mwalimu nyerere. Chadema wamekatazwa majukwaani na mabarabarani pia. Unapataje wanachama wapya? Unafikishaje sera za chama kwa watu?

Jiangalie mdogo wangu. Usipokuwa makini nitakutukana.
 
Wapinzani bado Sana.
 
😃😃😃

Mkuu hitimisho lako limenichekesha Sana.

Mimi nimeandika ninavyoona tuu, inaweza kuwa sahihi au sio sahihi.

Kuhusu mizania baina ya CCM na Upinzani naungana na wewe.

Sasa swali linakuja, Upinzani wafanyeje?
Je waendelee kulalamika?
Au wachukue hatua, je ni hatua zipi??

Upinzania umeshindwa kuwashawishi Watanzania, niamini Mimi.
 
Nimeipenda hii Siku zote kwenye maisha, ukishakuwa upande wa mlalamikaji basi jua umekwisha. Ni hitimisho la uwezo wa viongozi wa CHADEMA na wafuasi wao. Mlalamikaji mara nyingi ni bingwa wa kulaumu na kukosoa tu
 
Back
Top Bottom