CHADEMA hawana mpango wa kushinda uchaguzi 2010?

mwakatundu

Member
Jan 1, 2010
15
0
Hawa CHADEMA wamekata tamaa ya kuunda serikali hata kabla ya mpambano wenyewe? Afadhali chama wangemwachia Zitto kumbe.

Chadema yapania kunyakua majimbo 80

Daniel Mjema, Moshi

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimejiwekea mkakati wa kunyakua majimbo 80 katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu.

Tayari Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, ametangaza azma ya kugombea ubunge katika Jimbo la Hai.

Mkakati huo ulitangazwa juzi na Mbowe alipokuwa akifungua mkutano wa siku mbili wa madiwani wote wa Chadema kote nchini, waliokutana mjini Moshi.

Kwa mujibu wa Mbowe lengo la chama chake katika uchaguzi huo ni kupata angalau theluthi moja ya wabunge wote.

"Kama kuna eneo CCM inajidanganya ni Bunge la Jamhuri. Chadema mwaka 2010 lazima tuingize angalau theluthi moja ya wabunge ili tukate ngebe ya CCM katika maamuzi ndani ya chombo hiki muhimu,"alisema.

Mbowe alisema ana uhakika chama hicho kinaweza kunyakua majimbo 80 na kukifanya kiwe na nguvu katika maamuzi ya bunge kwa maslahi ya wananchi wengi.

"Kama CCM wanafikiri tunakwenda katika uchaguzi huu kuwasindikiza, wanajidanganya kwa sababu tuna uhakika wa wabunge 80 na hakuna mkoa ambao hautatoa madiwani wanaotokana na Chadema,"alisema Mbowe.

Alisema malengo ya chini ya chama chake ni kushinda na kushika hatamu ya kuongoza ya mabaraza ya madiwani katika halmashauri 30 na kwamba kinaweka wagombea wanaokubalika kwa wananchi.

Aliwahakikishia madiwani hao kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Hai anakokwenda kugombea ubunge na Halmashauri ya Manispaa ya Moshi, zitakuwa chini ya Chadema.

Alisema Chadema ni chama kinachokua ndani ya upinzani uliosinyaa na kutoa takwimu kuwa mwaka 1994 kilikuwa na madiwani 42 na idadi hiyo ikapanda mwaka 2000 na kufikia 56 na uchaguzi wa 2005 ikapata madiwani 103.

Hata hivyo alisema pamoja na mafanikio hayo lakini chama hicho kimekuwa kikipandikiziwa matatizo na mikasa mbalimbali ili kukidhoofisha.

"Mmesikia kwa muda mrefu kuwa Chadema ni chama cha Wachaga nawaambieni leo hii ni propaganda iliyopikwa na kupandikizwa ili kutugombanisha ndani ya chama lakini siku zote ukweli hudumu na uongo husinyaa"alisema.

Mbowe alisema anashangazwa na kauli hizo na kuwataka madiwani wa mkoa wa Kilimanjaro wanaohudhuria mkutano huo kusimama na waliposimama walifikia nane kati ya madiwani 103 nchi nzima.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Shirika la Ujerumani la Conrad Adeneur Stiftung (CAS), Anke Lensh alisema japokuwa mfumo wa vyama vingi nchini uliingia 1992 lakini baadhi ya Watanzania hawafahamu haki yao. "Japokuwa mfumo huu uliingia Tanzania mwaka 1992, lakini sidhani kama wananchi wamejengewa vya kutosha uwezo wa kuamua kwani bado wapo wanaoona kuchagua chama kingine nje ya CCM ni kusaliti nchi,"alisema.
 
Hawa CHADEMA wamekata tamaa ya kuunda serikali hata kabla ya mpambano wenyewe? Afadhali chama wangemwachia Zitto kumbe.
KWANINI KUKATA TAMAA, AU ulitaka wajilishe upepo kwa kuweka malengo mfu, hayo malengo ni yakinifu, na hakuna haja yakukuongopea, kua wanaweza kuchukua WABUNGE WANCHI NZIMA.
TATIZO LETU TUNAPENDA KUDANGANYWA NA KUONGOPEWA.
 
Hawa CHADEMA wamekata tamaa ya kuunda serikali hata kabla ya mpambano wenyewe? Afadhali chama wangemwachia Zitto kumbe.
Badilisha kichwa cha thread, hakiendani na maudhui. Kushinda uchuzi haimanishi Urais peke yake, hata kushinda wabunge 80 ni kushinda uchaguzi. Badili title ili iendane na hoja zako. By the way, CHADEMA are realistic on this, hawawezi kujifariji kwa kudai kwamba wanachukua nchi wakati ili hali wanafahamu fika kwamba hawajafanya kazi ya kutosha kuchukua serikali. Eti ohobora chama wangemuachia Zitto. Do you think CHADEMA inaendeshwa na mtu mmoja? Pole yako Mkuu.
 
They are telling people the truth, reality, hawana haja ya kuiga uongo watanzania wengi wamezoeshwa kuaminishwa uongo kiasi kwamba ukweli umekuwa uongo na uongo umekuwa ukweli wakiambiwa ukweli hawaamini wanaona mtu huyo si serious, ni kujidanganya kusema uchaguzi huu Chadema itaipiku CCM kwa wingi wa wabunge.

Wapo wengi sana wa type ya Mwakatundu ambao hawaamini ukweli na watu hawa ndio wale 70% ya watanzania wanaofuata upepo leo anaweza kuwa huku kesho akipewa kofia na kitenge anabadili mawazo bila kuangalia athari zake.
 
watanzania wa jana si waleo waleo awadanganyiki tena wanajua kuchambua mchele na chuya ole wao wanasiasa wasiosoma alama za nyakati wataipata fresh kwenye kampeni zao
 
Bunge kwanza, You know kwenye politics lazima uwe na plan. Ukiweza kulitikisa bunge ndiko populality na publicity inakoanzia. Wakiweza kweli kuwa na viti 50 lazima tukae. Kama leo wana idadi hiyo mambo yako hivi, je wakiwa 50?
 
I buy Mbowe's idea of getting at least one third of the parliament seats which is equivalent to wining in 80 constituency. Chadema has now started to prepare people psychologically the aftermath of general election that people should not expect wonders to be done by Chadema.

I think this it is a good thing to be done by any serious political party instead of giving people higher expectations that it cannot afford, that is why in contrary to other political parties Chadema is remaining even stronger after each general election.
 
I buy Mbowe's idea of getting at least one third of the pariament seats which is equivalent to wining in 80 constituency. Chadema has now started to prepare people psychologically the aftermath of general election that people should not expect wonders to be done by Chadema.

I think this it is a good thing to be done by any serious political party instead of giving people higher expectations that it cannot afford, that is why in contrary to other political parties Chadema is remaining even stronger after each general election.
hata ukiangalia mwenendo wa mambo namna CHADEMA INAVYOKUA, INAKUA IKIWA KWENYE MIZIZI yake, inakua kwa hatua, ni rahisi kumonitor mambo yanavyokwenda, hawana papara, wanashambuliwa ila wanasimama ,kisha wanasonga mbele.
 
Nakubaliana na Mbowe kabisa kwa asilimia 100 na pia Mungu awabariki sana katika msuala haya
 
hata ukiangalia mwenendo wa mambo namna CHADEMA INAVYOKUA, INAKUA IKIWA KWENYE MIZIZI yake, inakua kwa hatua, ni rahisi kumonitor mambo yanavyokwenda, hawana papara, wanashambuliwa ila wanasimama ,kisha wanasonga mbele.


Ni kweli kabisa kuna watu walikuwa wanasema Chadema kitakufa tu mara baada ya uchaguzi wa 2000 matokeo yake ndiyo kikapata nguvu zaidi, wakasema ngoja Chadema washindwe uchaguzi 2005 watasambaratika bado wapo tena ngangari zaidi.

Chadema wako makini viongozi wamejaribiwa kwa mbinu mbalimbali ili wagombane kimeitwa chama cha kikabila hadi sasa watu wameona ni upuuzi, hata sisi watu tulio nje ya chama tunaona tuna mifano halisi kama ule mgogoro wa NCCR ya Mrema na TLP. Chadema kimetulia hakina vurugu kilifanyiwa mizengwe tu Busanda kikanyamaza wakafaniwa tena Biharamulo Magh hawakufanya vurugu wala kwenda mahakamani, mimi nakuona huko ni kukomaa kwa chama.
 
Huo mkakati wa Chadema nimeupenda sana, Mungu awasadiye wafanikiwe. Ninatamani ndani ya hao 80 wawemo 'akina Slaa' watano hivi. Nakuambia mwaka 2015 tutaimba 'niagieni niagieni, niagieni ndg zangu mafisadi, niagieni ndg zangu walevi wa madaraka, niagieni ndg zangu wasojua kusoma alama za nyakati, niagieni ndg zangu walio waona watz kuwa ni vichwa mbofu, watu wa kudanganywa kwa khanga, skafu, kofia na TShirt; ili hali umaskini ukiwaandama mpaka kwenye fizi'. Naitamani siku hiyo.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom