CHADEMA: Hatutikisiki | Wasema Cuf ni CCM B, Lipumba anatekeleza mradi

Chama changu chadema kimenifurahisha sana! Hili jibu lao limeonesha ujasiri, kupevuka na umakini wa hali ya juu sana. Tunaenda vzur sana na kwa huu mwendo tutafika mbali sana! Mapambano yanaendelea. Hao tumeshawajua. Tunabadili mbinu maana maadui wameongezeka. Cha msingi ni kwamba HAKUNA KULALA HADI KIELEWEKE!. .
 
CHADEMA: Hatutikisiki
• Wasema Cuf ni CCM B, Lipumba anatekeleza mradi

na Betty Kangonga

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema kamwe hakitishwi na propaganda zinazofanywa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kushirikiana na mamluki wake, zenye lengo la kukichafua na kujenga uhalali wa kuzuiliwa kwa maandamano na mikutano ya chama hicho.
Akizungumza na Tanzania Daima jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa masuala ya Bunge na Halmashauri wa CHADEMA, John Mrema, alisema vyama vidogo vya Cuf, NCCR-Mageuzi, TLP na UDP vimo katika utekelezaji wa mkakati huo wa CCM, kwa kushirikiana na kikundi maalumu kilichoundwa kwa ajili hiyo, kinachopachikwa jina la ‘vijana wapenda amani.'
Alisema mwanzoni mwa mwaka huu walitoa taarifa kwa umma wakieleza kuwa Chama cha Wananchi (CUF) si chama cha upinzani, kwa kuwa kinashirikiana na CCM na sasa ushahidi unazidi kujionyesha waziwazi, kwa mwenyekiti wake, Profesa Ibrahim Lipumba, kutoa matamko ya kuunga mkono propaganda za CCM zinazoituhumu CHADEMA kuwa inahatarisha amani ya nchi.
"CUF wamefunga ndoa na CCM, hivyo si chama cha upinzani …ni CCM B, kwa hiyo hatushangai kuona chama hicho na mwenyekiti wake wakiishambulia CHADEMA…wanatekeleza mkakati wao wa pamoja.
"CHADEMA ni chama makini kinasimamia na kutekeleza majukumu yake kwa umakini, hivyo hivi vyama vingine vinavyojiita vya upinzani tulishavitilia shaka muda mrefu hata wakati wa kuunda kambi ya upinzani tulibaini hawana dhamira ya kweli," alisema.
Alisema kwa sasa CCM imepoteza mwelekeo na imedhohofika ndiyo maana inafikia hatua ya kutumia watu mbalimbali ili waisaidie kuishambulia CHADEMA inayoungwa mkono na wananchi wengi.
Alisema haiingii akilini kuona vijana wanaotaabika na hali mbaya ya maisha wakinunuliwa kufanya maandamano na mikutano yao inayolenga kuwatetea, na kwamba wana taarifa kuwa kikundi hicho kimenunuliwa na kina uhusiano wa karibu na vigogo.
"Hivi kweli linajitokeza kundi la vijana na kudai wanaandaa maandamano ya kuunga mkono hotuba ya Rais Kikwete aliyoitoa Februari wakati leo tupo mwezi Machi? Wananchi wajiulize kwanini …sisi tunajua yote yanayoendelea," alisema Mrema. Alisisitiza kuwa CHADEMA hawababaiki na hatua hiyo bali kwa sasa wanajipanga zaidi katika kuhakikisha wanasema ukweli kwa kufanya maandamano na mikutano katika maeneo mengine ya nchi. Alisema chama hicho(CHADEMA) kipo katika hatua za mwisho kuhakikisha wanamalizia vikao vilivyobaki, ikiwa ni pamoja na kutoa ratiba ya wapi wanaelekea baada ya kumaliza maandamano yao katika maeneo ya Kanda ya Ziwa.

Source: TanzaniaDaima March 17,2011
 
Jamani mikakati hii mwishowe itakuwa ni ya kuimaliza CCM yenyewe, kwani inaratibiwa na watu wenye uwezo mdogo sana wa kufikiri, kama Ridhwan Kikwete, Makamba baba na mwana n.k.....
Waacheni waendelee kujimaliza kwa mbinu za kijinga!!......mtu gani mwenye akili atawakubali?
CCM haina watu wa kufikiri hivyo kadri wanavyovinunua vyama vya upinzani ndivyo Chadema kinavyobaki pekee yake na kuonekana wazi, kwa hali ilivyo sasa ni vigumu sana kwa mtu kama Lipumba, Cheyo, Mbatia wala Mrema ku convince watu wajiunge na vyama vyao kwa hiyo in a long run hii yote inakuwa faida kwa CDM lakini wao CCM hawaangalii huko wanaangalia faida ya siku moja ili waonyeshe kwenye TBC Mrema kasema nini basi.
 
Hizi ndo siasa za Tizedi tunataka tu kuwaonyesha wale walioanza kufuatilia kuanzia 2013
 
hahahaa naona mmekuja na mbinu za kuibua nyuzi za zamani ili kuchonganisha UKAWA. Jitahidini mwaweza fanikiwa.
 
Ndiyo maana wengine ushabiki wa vyama tumekaanao mbali kabisa,siwezi kuchezewa akili na wanasiasa.
 
Jaman tuwemakini na hivi vyama na wenyeviti wake kweli nimeamini vyama vyote vya kisiasa hapa kwetu ni udanganyifu ulaghai uroho havina nianjema kabisa na RAIA wake kila siku tunaimba tutajiondoaje kwenye utumw wa ccm Bali CHADEMA tu ndo imebaki kuhangaikia haki za RAIA ndio wanao taka kuiondoa ccm ila wengine wako kimaslahi2
 
Hii ndio JF ukweli unapatikana humuhumu haihitaji kutoka nje.
 
Hivi vyama vya upinzani ni vya kinafiki na wezi tu,watanzania tufungue macho tuone tunavyoendeshwa kama mang'ombe kwa manufaa yao binafsi,Mbowe mwizi,Lipumba mnafiki,Mbatia ndo msaliti mkubwa katika nchi hiii
 
Jamani mikakati hii mwishowe itakuwa ni ya kuimaliza CCM yenyewe, kwani inaratibiwa na watu wenye uwezo mdogo sana wa kufikiri, kama Ridhwan Kikwete, Makamba baba na mwana n.k.....
Waacheni waendelee kujimaliza kwa mbinu za kijinga!!......mtu gani mwenye akili atawakubali?
Waache waendelee na propaganda zao zisizokuwa na kichwa wala miguu.Tunawajua sana,elimu zao za kununua mitihani toka kidato cha nne,sita hadi chuo Kikuu( watoto wa wakubwa hawafeli)
 
Hiv leo kuna kampeni ya kufufua threads za zamani humu jf inajishushia heshima kwa kweli, hivi hayo ambayo vyama vya upinzani viliwahi ongea ndo iwe sababu ya kuvihukumu mbona watu huweka nadhiri makanisani na wanazivunja nyie ambao mnawaita wanafiki ndio wanafiki wakubwaa hawa wameungana kwa sababu wamemaliza tofauti zao achen maneno ya ajabu
 
Mbona nyie mnafufua kila leo hamuulizwi au kwa vile mna penda kusikia yale mnayoyapenda tu
 
tuwe tunaangalia post ni ya mwaka gani , watu wengine wanalipwa humu kubadilisha watu akili hii post ni ya tarehe 16 march mwaka 2011
 
Kuweni makini the uzi huu ulianzishwa na ni hoja ya mwaka 2011! Msomaji na mchangiaji changia ukijua fika kuwa uzi na hoja yake viko outdated! Uliwekwa kabla UKAWA haijafikiriwa kuwepo!
 
Ila inashangaz mno kuona vyama vya upinzani vinazomeana kunyosheana vidole ni upuuzi mkubwa unadhan kwa mtindo huu ccm na ufisadi wake watatoka hii in sawa na vita vya panzi furaha ya kunguru na kunguru huyo ni ccm
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom