CHADEMA: Hatutikisiki | Wasema Cuf ni CCM B, Lipumba anatekeleza mradi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA: Hatutikisiki | Wasema Cuf ni CCM B, Lipumba anatekeleza mradi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Mar 16, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Mar 16, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema kamwe hakitishwi na propaganda zinazofanywa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kushirikiana na mamluki wake, zenye lengo la kukichafua na kujenga uhalali wa kuzuiliwa kwa maandamano na mikutano ya chama hicho.

  Akizungumza na Tanzania Daima jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa masuala ya Bunge na Halmashauri wa CHADEMA, John Mrema, alisema vyama vidogo vya Cuf, NCCR-Mageuzi, TLP na UDP vimo katika utekelezaji wa mkakati huo wa CCM, kwa kushirikiana na kikundi maalumu kilichoundwa kwa ajili hiyo, kinachopachikwa jina la ‘vijana wapenda amani.'

  Alisema mwanzoni mwa mwaka huu walitoa taarifa kwa umma wakieleza kuwa Chama cha Wananchi (CUF) si chama cha upinzani, kwa kuwa kinashirikiana na CCM na sasa ushahidi unazidi kujionyesha waziwazi, kwa mwenyekiti wake, Profesa Ibrahim Lipumba, kutoa matamko ya kuunga mkono propaganda za CCM zinazoituhumu CHADEMA kuwa inahatarisha amani ya nchi.

  "CUF wamefunga ndoa na CCM, hivyo si chama cha upinzani …ni CCM B, kwa hiyo hatushangai kuona chama hicho na mwenyekiti wake wakiishambulia CHADEMA…wanatekeleza mkakati wao wa pamoja.

  "CHADEMA ni chama makini kinasimamia na kutekeleza majukumu yake kwa umakini, hivyo hivi vyama vingine vinavyojiita vya upinzani tulishavitilia shaka muda mrefu hata wakati wa kuunda kambi ya upinzani tulibaini hawana dhamira ya kweli," alisema.
  Alisema kwa sasa CCM imepoteza mwelekeo na imedhohofika ndiyo maana inafikia hatua ya kutumia watu mbalimbali ili waisaidie kuishambulia CHADEMA inayoungwa mkono na wananchi wengi.

  Alisema haiingii akilini kuona vijana wanaotaabika na hali mbaya ya maisha wakinunuliwa kufanya maandamano na mikutano yao inayolenga kuwatetea, na kwamba wana taarifa kuwa kikundi hicho kimenunuliwa na kina uhusiano wa karibu na vigogo.

  "Hivi kweli linajitokeza kundi la vijana na kudai wanaandaa maandamano ya kuunga mkono hotuba ya Rais Kikwete aliyoitoa Februari wakati leo tupo mwezi Machi? Wananchi wajiulize kwanini …sisi tunajua yote yanayoendelea," alisema Mrema. Alisisitiza kuwa CHADEMA hawababaiki na hatua hiyo bali kwa sasa wanajipanga zaidi katika kuhakikisha wanasema ukweli kwa kufanya maandamano na mikutano katika maeneo mengine ya nchi.

  Alisema chama hicho kipo katika hatua za mwisho kuhakikisha wanamalizia vikao vilivyobaki, ikiwa ni pamoja na kutoa ratiba ya wapi wanaelekea baada ya kumaliza maandamano yao katika maeneo ya Kanda ya Ziwa.
   
 2. Pelosi

  Pelosi Member

  #2
  Mar 16, 2011
  Joined: Jul 22, 2010
  Messages: 83
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mheshimwa Lipumba atoe ushahidi wa hao walionunuliwa kufanya maandamano na pia atuthibitishie kuwa CUF sio CCM B, hayo mengine ni mazungumzo baada ya habari!
   
 3. k

  kalechee Member

  #3
  Mar 16, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 85
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mapambano yanaendelea
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Mar 16, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Kundi hili ni watchdogs wa Ufisadi, na ni maiti zinazotembea...
  Kauli hii ya cdm ni ya kiume, na inamsisimua mwanamapinduzi yeyote!...keep us alive cdm!
   
 5. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #5
  Mar 16, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Ngoma imepata mpigaji......
   
 6. Smartboy

  Smartboy JF-Expert Member

  #6
  Mar 16, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,110
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Aibu yao wenyewe.
   
 7. Piere. Fm

  Piere. Fm JF-Expert Member

  #7
  Mar 17, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,194
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Njaa inawasumbua hao nawamefadhiliwa na baba yao Jk msimtafute mchawi nani. Na bado wataendelea kugeuzwa kalai ambalo linaonekana muhimu wakat wa ujenz lakin baada ya hapo hata chooni halifai kukaa.
   
 8. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #8
  Mar 17, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  LICHA YA ADUI HATARI ITAKAYOIUA CCM KWA HARAKA ZAIDI NDANI KWA NDANI HIVI KARIBUNI, CHAMA HIKI KIKO MBIONI KUJITWISHA MIZIGO MIPYA KUMBEBA LOWASA NA HASA KUFANYA MAUAJI YA SAUTI PINZANI KISIRI KUSAFISHA NJIA

  Kama uliwahi kufikiria kwamba CHADEMA ndicho adui mkubwa itakayoiua CCM basi kumbe kweli huelewi kabisa siasa za taifa hili zilivyo lakini hivi sasa kundi dogo ndani ya CCM linaloshikilia uhai wa chama hiki kiko mbioni 'KUSAFISHA NJIA KWA NAMNA YOYOTE ILE mmoja wao kushaka dola 2015.

  Kwa wadadisi wa mambo, adui mkubwa zaidi na wa kutisha ajabu tayari yuko chumbani kwao CCM na hivi karibuni italipuka kuliko KINU CHA NYUKLIA CHA JAPAN na kutuma mionzi itakayoifuta kabisa CCM bukia chama cha upinzani namba 4 baada ya NCCR-Mageuzi hapa nchini.

  Kwa kugusia tu kwa uchache; adui namba moja na hatasri mno hadi hivi, kwa haki kabisa kwa misingi ya kichama walichojiwekea, ni kwamba kule Wa-Tanzania Visiwani wanakiona CCM kama Chama kilichowasaliti kushika dola baada ya Mhe Benjamin Mkapa.

  Hakika jambo hili la USALITI WA CCM KWA WATANZANIA VISIWANI ni tishio kubwa hivi sasa ambapo majina zaidi kutoka Bara yaendelea kutajwa KUMRITHI Mhe Kikwete ambaye naye kwanza hata hatima yake bado haiko wazi kwa umma wa Tanzania.Kwa jinsi mambo yalivyo nchini itakavyolipua Naona baada ya CCM kuwatapeli Wa-Tanzania Visiwani nafasi ya kugombea Urais, katika ule mpango wao maalum wa SIASA ZA KUKABIDHIANA UONGOZI WA NCHI KWA ZAMU KWA WATOTO WA WAKUBWA tu Bara na Visiwani.

  Kitendo cha kikundi fulani kujipenyezea fedha haramu kupitia kwa akina Rostam Aziz na Edward Lowasa katika dakika za majeruhi kushawishi maamuzi kumtosa Mhe Salim Ahmed Salim (ambaye alipendwa sana bara na kuaminiwa mno na CCM-Mwalimu Nyerere) kule Dodoma, ndipo jini dume lenye vichwa viwili lilipozaliwa na kuleta salamu za maangamizi kwa hiki chama kilichowahi kupata umaarufu wa miaka mingi sana na kuaminiwa wa wengi nchini.

  Miongoni mwa hizo salamu ni pamoja na (1) Wana-Mtandao badala ya Wana-CCM (ambao nao walikujakugawanyika mbele ya safari na kuwa (i) Wanamtandao Walaji (MAFISADI WA HIVI LEO) na Wanamtandao Waliwa ambao nao mahasibu yao mazito na yanayo nuka mno tutakuja kuyaelezea siku nyingine humu, (2) Wana-CCM Bara ambao lao ni kuwatumia baadhi ya Wana-CCM maswahiba kutoka Visiwani wakiwachezesha kama mchezo wa CHESS au DRAFT KISIASA ili kuzuia Wa-Tanzania wa kawaida Bara na Visiwani kuwa na maamuzi yoyote juu ya nani awaongoze isipokua tu maamuzi yote yatatoka siku zote kwa hii CCM Bara tu kwa sura zima ya Jamhuri yetu ya Muungano Tanzania.

  Sasa kwa ujio wa CHADEMA na kuendelea kupendwa sana kwa chama hiki na azma yake ya KURUDISHA UONGOZI WA NCHI MIKONONI MWA WANANCHI WENYEWE kote Bara na Visiwani, na haya madai Moto Moto ya sisi Vijana kutaka Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi kote ndani ya taifa letu tayari zimekua ni mwiba mchungu katika ngozi ya kikundi hiki cha WAJANJA WACHACHE Wana-CCM Bara ambao mpaka hivi sasa, kwa mujibu wa habari nyeti za ndani sana chumbani mwao, kila ramani ya kisiasa wanalolichora linagoma kabisa, fedha walizokwisha wekeza kwenye juhudi hizi zote Bara na Visiwani zakumbwa na hatari za wazi mno na migawanyiko kuongezeka kila kukicha kati yao.

  Hata nako ndani ya kikundi hicho cha hao Wajanja wachache Wana-CCM kumeibuka nako Migawanyiko mikali ya KI-KANDA kwa namna ambayo hata juhudi gani zifanyike hakuwezekani kupatanishwa kitu hata wakafanya kazi kwa pamoja.

  Kwa mujibu wa vyanzo vya ndani ya CCM katika ujumla wake, hali si shwari hata kidogo mle!! Wapo hata wale ambao, kwa ufinyu tu wa mawazo, wamefikia mahala wamependekeza MAJINA 15 ya baadhi ya watu mashuhuri na tishio kwa maslahi yao KUUAUA. Lini wauawe na kwa MTINDO GANI usioweza kuleta tafrani kwa kile wanachokiita 'Tishio la Nguvu ya Umma' kutokuweza kuwakumba.

  Japo tatizo letu Wa-Tanzania tuliowengi ni mpaka tushikishwe jambo kiganjani ndio tuamini na wakati mwingine kugutuka kukiwa kumechelewa sana, miongoni mwa HAYO MAVUNO YA MIKONO YA KI-SHETANI tayari wameorodheshwa baadhi ya vinara wa kupinga madhambi ya CCM kwa njia mbali mbali nchini.

  Kati ya watu wanaolengwa wamo (i) baadha ya viongozi tishio kwa kinyang'anyiro cha kiti cha urais 2015 waliomo ndani na nje ya hicho kikundi cha Rostam Aziz na Edward Lowasa. Pia, (ii) wapo baddhi ya viongozi wa serikali za wanafunzi nchini, (iii) baadha ya Wana-JF ambao wametajwa kama 'wakorofi na waharibifu', (iii) baadhi ya viongozi wa dini katika kanda fulani ambao wameelezewa kuwa na 'vinywa pana' na kuonekana kukisaidia CDM, (iv) wafanyabiashara wanaohofiwa kukifadhili CHADEMA hivi sasa na (v) na baadhi Wanataaluma wanaoonekana kujitolea kukisaidia CDM ki-mikakati ambayo hadi sasa yaelezewa KUKIDHOOFISHA MNO hiki chama tawala.

  Sasa chama hiki chaonekana kubuni (1) mkakati mpya wa UONZOZI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA kukabidhiwa kwa zamu ile ile ila safari hii ni NDANI KWA NDANI TANZANIA BARA na vile vile ni (2) kwa KUZINGATIA AMA URAFIKI, UJIRANI AU UDINI kufanya hivyo.

  Hata hivyo nako mambo si yenyewe baada ya wale wafadhali wa Uarabuni (Libya, Misri na Iran) nazo kukumbwa na matatizo kibao, yale yanayoendelea na yale ambayo yatalipukia kwao miezi michache ijayo; kikundi hiki ndani ya CCM kimechanganyikiwa kupindukia kwani kwani ufadhili wao hauna uhakika tena huku wananchi tukiendelea kulishikilia bando DOWANS na mianya mingine itakayotumika kuchota kodi zetu kuyatekelezea haya yote.

  Dawa ya yote haya wanayopangwa kutekelezwa kwa mikono ya giza ni (1) kuhakikisha kwamba kila mmoja wetu anageuka kuwa mlinzi wa mwenzie dhidi ya juhudi hizi hatari, (2) kusimama kidete kwa KUSISITIZA Katiba Mpya ya Wananchi na Tume Huru ya Uchaguzi kupitishwa Bungeni mwezi ujao, (3) kuendelea kuhakikisha kwamba UTEUZI WA JOHN MIMOSE CHEYO kushika tena ile kamati kule bungeni haiwi tena kichochoro tena cha Mafisadi kujichotea fedha kununulia kura na kutekelezea mambo machafu huku Cheyo akijifanya hajaona kitu kwenye vitabu vyetu!!

  Maandamano sasa ndio yataendelea kama kazi mpaka MAFISADI wakimbie nchi wenyewe; ni haki ya kikatiba.
   
 9. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #9
  Mar 17, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,937
  Likes Received: 12,207
  Trophy Points: 280
  Right answer at right time, Lipumba alizoea kuheshimiwa, watu walikuwa wanamwonea aibu sasa wanamwambia ukweli kweupe kabisa. Chadema hongera sana kwa hilo hata ningekuwa mimi ningesema hivyo hivyo asitegemee tena kuonewa aibu kajidhalilisa mwenyewe.
   
 10. Click_and_go

  Click_and_go JF-Expert Member

  #10
  Mar 17, 2011
  Joined: Nov 21, 2010
  Messages: 451
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  hao wapuuzi wachache wanataka kupoteza dira ya maendeleo,,,,,,,i hate this,,,,,,CHANGES ARE INEVITABLE!!!

  KAMA ZILIVYOANGUKA DOLA KUBWA KAMA ZA BABELI,,,,UAMEDI NA UAJEMI NDIVYO CCM ITAKAVYOANGUKA TENA KWA KISHINDO!!!
   
 11. Naloli

  Naloli JF-Expert Member

  #11
  Mar 17, 2011
  Joined: Aug 26, 2010
  Messages: 416
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  LIPUMBA jukumu lake kuu ni kugombea URAIS kupitia CUF haya mambo mengine anayoyafanya sasa ni kusukuma siku tu hadi 2015 ifike aendelee na jukumu lake. Mwacheni aendelee kupayuka bila kufanya siasa hizo za maji taka mtajuaje kuwa bado yupo?mwenzenu hataki kusahaulika.

  Na mkumbuke alimkabidhi JK ILANI ya Uchaguzi ya CUF kwa ajili ya utekelezaji na JK aliipokea. Hivyo sasa hivi ni ILANI ya CCM na CUF ndio zinaendesha nchi sasa mnashangaa nini yeye kuinuka na kukemea kuwa maandamano yataondoa serikali yao isiyo rasmi.Prof kesha kuwa kibaraka wa CCM kapigana zaidi ya miaka 12 sasa kasalimu amri kachukuliwa mateka na JK anaendesha sera ya MTUMIKIE KAFIRI UPATE MRADI WAKO.

  Huu ni mwanzo tu tutasikia mengi miaka hii ya kuelekea 2015
   
 12. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #12
  Mar 17, 2011
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 2,185
  Likes Received: 233
  Trophy Points: 160
  Lipumba anaongea pumba kama jina lake mwenyewe!,kamegewa pesa za kifisadi amevimbiwa. Fikiria kama huyu angepewa urais wakati ana mawazo ya utata ingekuwaje? ndo maana nchi nyingi zinapata un compentent leaders, afu mambo yanaenda mrama. Huyu ni bure ndo maana keshagombea mara chungu nzima bila kuambulia kitu, hata mrema amemzidi kufikiri kabaki peke yake na anatarajia kugombea 2015!
   
 13. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #13
  Mar 17, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  nashindwa kutofautisha comment zako na za mlevi kwani kabla ya kura za maoni zanzibar chadema waliongoza kongamana huko zanzibar na la kuwashawishi wananchi kupiga kura ya ndiyo kwenye serikali ya umoja wakitaifa na wakijua fika chama chochote kitakachopata 5% au zaidi ya kura wataunda serikali ya umoja wakitaifa na chadema wakiwa mstari wa mbele, lakini kwa sababu hawakupata ndo maana hawapo, KWANINI SASA WANAPINGANA NA KILE WALICHOKIHUBIRI. CHADEMA AKA POPO.
   
 14. S

  SUTU BUTUGURI Member

  #14
  Mar 17, 2011
  Joined: Mar 8, 2011
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CCM i mahututi, inakufa. CDM siyo wanaoiua. CCM inauawa na wanaCCM ejusdem generis wanaofikiri kuwa CCM haiumwi ...
   
 15. B

  B4U Member

  #15
  Mar 17, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa jinsi mambo yanavyokwenda kimantiki tu inaonyesha ni kweli CDM ilishinda uchaguzi na kama kilishinda maana yake ni chama tawala hivyo kupata upinzani kwa vyama vingine vyote vikiongozwa na mpinzani mkuu yaani CCM.
   
 16. AK-47

  AK-47 JF-Expert Member

  #16
  Mar 17, 2011
  Joined: Nov 12, 2009
  Messages: 1,381
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Nilipomsikia Kamanda Kova anatoa maelezo yale ya kuzuia maandamano ya vijana wanaojiita wapenda amani nikajua kabisa hili ni igozo linalolenga kuivunja nguvu CHADEMA kufanya maandamano maana nao watapewa sababu hizo hizo za kuzuia maandamano yao badala ya zile za kiitelejensia kugutukiwa..sasa wamekuja na hili igozo ili CHADEMA wakikaidi waonekane wakorofi.
   
 17. m

  mndeme JF-Expert Member

  #17
  Mar 17, 2011
  Joined: Sep 2, 2008
  Messages: 322
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  kikundi cha wapenda amani (ambacho ni cha ccm) kwa taarifa zisizo rasmi ni kuwa kimetengewa zaidi ya mil. 100 kuzunguka nchi nzima.......jana manzese walizomewa nadhani hata mikoani watakutana na nguvu ya umma
   
 18. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #18
  Mar 17, 2011
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,501
  Likes Received: 1,082
  Trophy Points: 280
  Jamani mikakati hii mwishowe itakuwa ni ya kuimaliza CCM yenyewe, kwani inaratibiwa na watu wenye uwezo mdogo sana wa kufikiri, kama Ridhwan Kikwete, Makamba baba na mwana n.k.....
  Waacheni waendelee kujimaliza kwa mbinu za kijinga!!......mtu gani mwenye akili atawakubali?
   
 19. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #19
  Mar 17, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,381
  Likes Received: 3,141
  Trophy Points: 280
  Hivi hawa cuf (ccm-b/taasisi ya dini) wataendelea kuwepo tunakoelekea kweli?......tusubiri ila siamini km wanaweza kuffika popote zaidi ya kulamba miguu visiwani na kuleta majungu bara....hatari sana hii
   
 20. CPU

  CPU JF Gold Member

  #20
  Mar 17, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Lilianza la "Wapinzani wataleta vita" ikiwapamoja na kuremba kurasa za mbele za magazeti yao kwa Mafuvu ya Kimari, LIKASHINDWA
  Likaja la Ukabila (Eti CDM ni wachagga pyua), LIKASHINDWA
  Likaja la udini (Chama cha Maaskofu, wakristo) LIKASHINDWA
  Likaja la Uhaini kuipindua nchi (Hotuba ya Mkwere mwezi Feb) Likashindwa

  Sasa naona dalili zote hilo la Maandamano litakavyododa na kuzidi kukitafuna chama
  Hivi kweli wanaandamana eti kuunga mkono Maisha Magumu???

  My Nyweleeeeee:smash::smash::smash:
   
Loading...