CHADEMA: Hatutashiriki Kongamano la Amani la TCD, limefadhiliwa na CCM! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA: Hatutashiriki Kongamano la Amani la TCD, limefadhiliwa na CCM!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by CHADEMA, Jul 8, 2013.

 1. CHADEMA

  CHADEMA Verified User

  #1
  Jul 8, 2013
  Joined: Apr 13, 2013
  Messages: 426
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  Ndugu waandishi wa habari,

  Tumewaiteni hapa mchana huu kwa dharura, kutokana na kujitokeza kwa jambo moja muhimu sana katika mustakabali wa chama chetu na taifa kwa ujumla. Jambo lenyewe ni hili:

  Kwa muda wa siku mbili, kuanzia kesho– tarehe 9 Julai 2013 hadi 10 Julai – kutakuwa na "KONGAMANO LA AMANI" lililoitishwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania – Tanzania Center For Democracy (TCD).

  Kongamano hilo litajadili na kutafakari Amani ya Taifa, litafanyika kwenye hoteli ya White Sands ya jijini Dar es Salaam. Litafuguliwa na Mwenyekiti wa TCD, Mbunge wa kuteuliwa na Rais, Mheshimiwa James Mbatia na litafungwa na Rais Jakaya Kikwete.

  Baadhi ya washiriki, ni pamoja na mawaziri, viongozi wakuu wa vyama vyenye wabunge ambavyo ni wanachama wa TCD – Chama Cha Mapinduzi (CCM), Chama cha Wananchi (CUF), United Democracy Party (UDP), Tanzania Lebour Party (TLP), NCCR- Mageuzi na CHADEMA.

  Aidha, chama cha UPDP nacho kitashiriki mkutano huo kwa niaba ya vyama vingine ambavyo havina wabunge.

  Ndugu waandishi wa habari,
  CHADEMA kikiwa mmoja wa wadau wakubwa wa TCD, kimepokea mwaliko wa mkutano huo. Hata hivyo, tunapenda kutumia nafasi hii, kupitia kwenu, kuutangazia umma na Watanzania wote wanaotutakia mema na kulitakia mema taifa hili, kwamba hatutashiriki mkutano huo kwa sababu zifuatazo:

  Kwanza, Mwenyekiti wa TCD, Mheshimiwa Mbatia kwa makusudi amekiuka maazimio ya kikao ya kuteuwa Mwezeshaji wa mkutano huo na badala yake akafungamana na CCM kuteuwa watu wanaowataka wao.

  Pili, CHADEMA haitashiriki mkutano huo kwa kuwa Amani haijadiliwi. Amani inatengenezwa na kuwapo kwa mazingira ya haki na usawa; na kwamba aliyebobea katika uvunjaji wa haki hizo, ni serikali yenyewe.

  Katika mazingira haya, CHADEMA inaona hakuna umuhimu wa kushiriki kwenye mkutano ambao washiriki ni wale wale wanaotuhumiwa kuvunja haki za binadamu.

  Tatu, Amani siyo ya vyama vya siasa pekee yake. Amani inahusisha wadau mbalimbali wakiwamo viongozi wa kidini, taasisi za kiraia na mashirika yasiokuwa ya kiserikali. Taarifa zilizopo, ni kwamba mkutano huu haukushirikisha viongozi wa kidini, na hivyo, tunadhani kuwa siyo jambo zuri kama kweli tunataka kutafuta amani ya taifa.

  Nne, CHADEMA haitashiriki mkutano huo kwa kuwa aliyepanga, aliyefadhili na aliyeitisha mkutano huo kwa mgongo wa TCD, ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, Mizengo Kayanza Peter Pinda, ambaye ndani ya nafsi yake, haonekani kuwa na dhamira ya dhati ya kuwapo amani katika taifa letu.

  Ndugu waandishi wa habari;
  Ninyi ni mashahidi wa jinsi Waziri Mkuu Pinda alivyo mstari wa mbele katika kuhubiri kauli za chuki, uhasama, uchochezi, ubabe na ukiukwaji wa haki za binadamu nchini. Siyo mara moja wala mbili, Waziri Mkuu Pinda amesikika, tena ndani ya Bunge, akihamasiha vyombo vya usalama kuvunja sheria kwa kupiga, kuteka na kung'oa meno watu wanaotumia haki zao za kikatiba kushinikiza serikali kuchukua hatua dhidi ya maovu.

  Tano, CHADEMA haitashiriki katika mkutano huo kwa kuwa Serikali ya CCM inayofadhili mkutano huu, imejaa unafiki kwa kuhubiri amani mchana, wakati usiku inachochea uhasama wa kidini, kisiasa na inawagawa Watanzania kwa misingi ya imani za kidini na vyama.

  CHADEMA inao ushahidi usio na chembe ya mashaka, kwamba mifarakano mingi inayotokea kwenye jamii, mapigano katika koo mbalimbali, ugomvi wa kugombea ardhi kati ya wakulima na wafugaji, machafuko kwenye mikutano ya hadhara ya vyama vya upinzani, sababisho lake kuu ni CCM kuvitumia vyombo vya dola, ili kukibeba chama hicho.

  Tunataka umma utuelewe, kwamba tuna dhamira ya dhati ya kuona Tanzania inakuwa kisiwa cha amani, lakini hatutakubali kushiriki katika vikao ambavyo wanaoviongoza hawana dhamira hiyo. Ili amani iweze kupatikana, ni sharti kuwepo mijadala inayoingia kwenye viini vinavyosababisha amani ikosekane na hatua hiyo ianze kuchukuliwa na ionekane inachukuliwa na serikali.

  CHADEMA iko tayari, kufanya kazi ya kutafuta amani na wale wanaopenda demokrasia. CHADEMA haifanyakazi na wanafiki wa amani.

  Imetolewa na:
  Benson Singo Kigaila,
  Mkurugenzi wa Oganaizesheni ma Mafunzo,
  Dar es Salaam
   
 2. Philip Dominick

  Philip Dominick JF-Expert Member

  #2
  Jul 8, 2013
  Joined: May 26, 2013
  Messages: 1,025
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Ahsante CHADEMA
   
 3. T2015CCM

  T2015CCM JF-Expert Member

  #3
  Jul 8, 2013
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 7,911
  Likes Received: 357
  Trophy Points: 180
  nyie ni washari watanzania tumeshawajua, hamuwezi kushiriki kujenga amani ya nchi
   
 4. k

  kajaji JF-Expert Member

  #4
  Jul 8, 2013
  Joined: Jan 7, 2013
  Messages: 201
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  safi sana achana na wapuuzi hao wakae wenyewe
   
 5. k

  kibaya-kenya JF-Expert Member

  #5
  Jul 8, 2013
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 650
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hili ni jambo jema ambalo mnafiki hawezi kuona kamwe, big up CHADEMA ndio maana tunasema nyie mnabeba matumaini mema ya Watz. Mungu awalinde daima
   
 6. Highlander

  Highlander JF-Expert Member

  #6
  Jul 8, 2013
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 3,094
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  I support motion
   
 7. T2015CCM

  T2015CCM JF-Expert Member

  #7
  Jul 8, 2013
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 7,911
  Likes Received: 357
  Trophy Points: 180
  TCD ni jumuiko la vyama vya siasa vyenye wabunge unaposema haikushirikisha taasisi za dini unamaanisha nini??? acheni uzuzu chadema
   
 8. T2015CCM

  T2015CCM JF-Expert Member

  #8
  Jul 8, 2013
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 7,911
  Likes Received: 357
  Trophy Points: 180
  chama cha vurugu na mauaji na maandamano na matamko na shari
   
 9. kiagata

  kiagata Senior Member

  #9
  Jul 8, 2013
  Joined: Jan 12, 2012
  Messages: 192
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Mzuieni Mh.Mbowe asihudhurie kama kule Ikulu siku ile alipo kuja Rais Obama.Tangazeni kabisa kuwa Mbowe hata kuwepo ili akija afukuzwe.
   
 10. habariyamujini

  habariyamujini JF-Expert Member

  #10
  Jul 8, 2013
  Joined: May 16, 2013
  Messages: 3,095
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  CHADEMA INAPENDA MAMBO YA SHARI SHARI KAMA HAYA HAPA
  MFUASI WA CCM AMWAGIWA TINDIKALI NA WAFUASI WA CHADEMA IGUNGA


  [​IMG]

  [​IMG]

  [TABLE="class: cms_table_tr-caption-container, align: center"]
  [TR]
  [TD][​IMG][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: cms_table_tr-caption"]Mfuasi wa CCM, Mussa Tesha (24) akiwa katika hospitali ya wilaya ya Igunga mkoani Tabora, leo. Tesha ameungua usoni na sehemu kadhaa mwilini baada ya kumwagiwa tindikali usiku wa kuamkia leo na watu wanaodaiwa kuwa ni wafausi wa CHADEMA, ambapo inaelezwa kuwa walimwagia tindikali hiyo alipokuwa katika harakati za kubandika mitaani mabango ya mgombea wa Ubunge jimbo lgunga kwa tiketi ya CCM. Tesha alitarajiwa kuhamishiwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dar es Salaam leo kwa gharama za CCM. Anayemtazama ni Daktari wa hospitali hiyo, Selemani Masinga. (Na Mpigapicha Wetu)

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

   
 11. successor

  successor JF-Expert Member

  #11
  Jul 8, 2013
  Joined: Oct 25, 2012
  Messages: 1,471
  Likes Received: 1,629
  Trophy Points: 280
  Nimeelewa
   
 12. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #12
  Jul 8, 2013
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,605
  Likes Received: 6,107
  Trophy Points: 280
  CHADEMA ishashiriki kongamano la amani Ikulu Mbowe alipoenda kula na kunywa katika dhifa ya Obama, kwa hiyo hawahitaji kushiriki tena /s.
   
 13. B

  Bangoo JF-Expert Member

  #13
  Jul 8, 2013
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 5,594
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Napenda kuwapongeza kwa uamuzi mzuri, wanauwa raia, wanapiga raia, ALAFU WANALETA UNAFKI WAO..SAFI SANA.. Alutha continua...
  wanafki wakae na wanafki wenzie...MUME NA WAKE ZAKE!
   
 14. l

  lupe JF-Expert Member

  #14
  Jul 8, 2013
  Joined: Apr 1, 2013
  Messages: 5,659
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  :peace:
   
 15. Simiyu Yetu

  Simiyu Yetu JF-Expert Member

  #15
  Jul 8, 2013
  Joined: Apr 29, 2013
  Messages: 18,900
  Likes Received: 1,551
  Trophy Points: 280
  Bora msiende tu make mtaanza kutukana tu hatimaye kuharibu mkutano,vipi mandamano hamtafanya make ndiyo zenu.
   
 16. habariyamujini

  habariyamujini JF-Expert Member

  #16
  Jul 8, 2013
  Joined: May 16, 2013
  Messages: 3,095
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Hebu tupime hizi kauli za viongozi wa chadema
  1.NCHI HAITATAWALIKA
  2.kaskazini ijitenge
  3.hadi damu imwagike

  hizi ndio kauli za shari, ubabe, vitisho na zinazotishia usalama na amani ya nchi
   
 17. NAPITA

  NAPITA JF-Expert Member

  #17
  Jul 8, 2013
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 5,072
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Majanga!!!
   
 18. Simiyu Yetu

  Simiyu Yetu JF-Expert Member

  #18
  Jul 8, 2013
  Joined: Apr 29, 2013
  Messages: 18,900
  Likes Received: 1,551
  Trophy Points: 280
  Kwanza kunawengine wanatembea na sumu bora wasiende ili wasiende kudhuru watu wasiokuwa na hatia kwanza hata mngeenda mkeongea nini wakati hamna hoja zaidi ya matusi.
   
 19. habariyamujini

  habariyamujini JF-Expert Member

  #19
  Jul 8, 2013
  Joined: May 16, 2013
  Messages: 3,095
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  mtu aliyejaa chuki fitna na mpenda vurugu utamjua matendo yake tu, amejaa unafki na amevaa sura ya kondoo wakati ndani ni muuaji. huwezi kususia kongamano la amani ukaendelea kujiita ww ni chama cha kuhubiri amani na demokrasia
   
 20. T2015CCM

  T2015CCM JF-Expert Member

  #20
  Jul 8, 2013
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 7,911
  Likes Received: 357
  Trophy Points: 180
  tumeshawaju wazee wa maandamano na mauaji.
   
Loading...