CHADEMA: Hatumlipi yeyote kuandamana; maandamano hayo ni harakati za wananchi kudai haki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA: Hatumlipi yeyote kuandamana; maandamano hayo ni harakati za wananchi kudai haki

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Mar 16, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Mar 16, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesikitishwa na kauli kinazodai ni propaganda za CCM kuwa kinatumia fedha kuwalipa wananchi kuandamana.

  Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Chadema, Bw. Antony Komu alisema chama hicho haimlipi yeyote kuandamana, haijafanya wala haitafanya hivyo kwani wanaamini kuwa maandamano hayo ni harakati za wananchi kudai haki zao.


  "Kwetu sisi haingii akilini kuwa yupo mwananchi anayeweza kufikiria kulipwa ili adai haki zake, tunasisitiza kuwa tutaendelea kuratibu maandamano haya nchi nzima," ilisema taarifa ya Bw. Komu.


  Alisema Chadema itachukua maoni yote yanayotolewa katika maandamano na mikutano wanayofanya kwa kuwa ni maoni ya wenye nchi yao na ni lazima yasikilizwe na serikali yoyote inayotaka uhalali kwa watu wake.


  Alisema uvumi mwingine unaoenezwa kuwa Chadema inapewa fedha na mataifa ya nje kuendesha maandamano kwa lengo la kuvunja amani hayo ni mawazo yenye lengo la kukidhoofisha chama hicho.


  Alitoa wito kwawa wale ambao maandamano hayajafika kwao kujitokeza kwa wingi na kwa amani siku yakiwafikia, huku akiwataka kukwepa mtego wa wanaotaka kufanya fujo kuchafua mpango huo.


  Bw. Komu alisema ili kuthibitisha kauli za mawaziri watatu kuwa Chadema inawalipa watu kuandamana zifanyiwe kazi na Jeshi la Polisi ili kupata ukweli wa tuhuma zilizoelekezwa kwa Chadema.


  Alisema Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Bernard Membe, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Bi. Sophia Simba na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu, Bw. Stephen Wassira kudai kuwa Chadema inalipa wananchi fedha kufanya maandamano ni upofu.


  Alisema inashangaza kuona Idara ya Usalama wa Taifa, Polisi na Majeshi yahusike kupata ukweli badala ya kukaa kimya wakati kauli hizo zinayumbisha watu na kuiletea Tanzania maswali mbele ya jamii ya kimataifa.


  Bw. Komu alisema Chadema inaona kuwa wao ni wazalendo wanaoipenda nchi na kuitaka iongozwe vizuri na watu wenye hadhi na mapenzi ya nchi na watu wake.
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Mar 16, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Wenye nchi tunasema tutaendelea kusema ukweli na tutaendelea kuandamana hadi watuelewe...ujue ukiwa umezoea kufanya hivyo wanajua wote wanafanya hivyo...hatuhitaji kulipwa ili tuandamane...
   
 3. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #3
  Mar 16, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,604
  Likes Received: 4,723
  Trophy Points: 280
  Iwe jua iwe mvua lazima kuandamana kudai haki yetu, hao wote wanaofikiri kuwa watanzania wanalipwa na chadema ili kudai uwajibikaji wa serikali ni wapuuzi kabisa.

  Hivi unapolipa nauli kwenye basi na umepewa tiketi inayoonyesha namba ya kiti na ukaingia kwenye basi ukakuta kuna mtu amekalia siti hiyo na wewe ukakosa pa kukaa, utahitaji mtu akulipe hela ili udai haki yako ya kukaa kwenye kiti ulicholipia nauli?

  CCM wacheni kuweweseka, kumekucha Tanzania watu tunataka serikali inayowajibika kwa walipa kodi wake, tumechoka na serikali ya kishikaji ya Kikwete.
   
 4. Zegreaty

  Zegreaty JF-Expert Member

  #4
  Mar 16, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 638
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hatulipwi na hatutaacha kuandamana mpaka kieleweke kama nyie ccm hamuwezi kujibu hoja basi jiandaeni kutunga ngonjera zenu zaidi na zaidi
   
 5. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #5
  Mar 16, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,143
  Trophy Points: 280
  Mkiacha kutulipa na kama hamtaki kutulipa hatuji kwenye maandamano, tumenyeke bure bure? wakati nyie mnachukuwa marupurupu bungeni na mifedha ya wafadhili, yote inaenda wapi, mtupe japo perdiem ya elfu ishirini ishirini tukija kuandamna, mnhhhh, kuna vibomu vya machozi, basi tupate hata kununulia maji na maziwa ya kupunguza ukali wakuwashwa mwili na macho, vipi sasa mnatukatisha tamaa mapema.

  Juzi tu, mmechukuwa zaidi ya Billioni mbili (2,000,000,000?= +), mmezipeleka wapi. Msiwe na roho za korosho, nasie tunaeteseka mitaani mtukatie japo kidogo.
   
 6. F

  Froida JF-Expert Member

  #6
  Mar 16, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Senti tano moja hatulipwi tutaandamana tu hatujali maneno yenu ya propaganda tunatuma salamu wananchi sasa hivi tunajua haki zetu na tunaiunga mkono Chadema kwa nguvu zetu zote,tupo tayari kuandamana kuinyoosha serikali ya mazuzu na kizembe ya CCM mpaka itakaponyooka mstari na kutanguliza maslahi ya wananchi mbele badala ya matumbo yao.
   
 7. s

  seniorita JF-Expert Member

  #7
  Mar 16, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 674
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  mfa maji lini akaacha kutapatapa? It is not easy to die without struggles of some kind....dalili nzuri CDM, chapa kazi WAtanzania waliona na nia njema wako nanyi....yanayosemewa CDM ndio yanayofanywa na hao magwiji wa CCM.....
   
 8. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #8
  Mar 16, 2011
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Nakubaliana na CHADEMA: Hawamlipi muandamaji yeyote... bali hakuna njia nyingine ya kula ruzuku itokanayo na kuwa na idadi hiyo ya wabunge usipokuwa na justification ya kusafiri kwa ajili ya maandamano and the like.... wajinga ndio waliowao!!! ahahaha.... nawahurumia wananchi wa Tanzania sana... maana they can be manupulated in different angles....
  Per dieeeeeeeeemmmmmmmmmmmsssss
   
 9. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #9
  Mar 16, 2011
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Kama CHADEMA ni wazalendo naomba waombe matumizi ya kusafirisha viongozi kwa ajili ya maandamano... na kwenye mchanganuo watuonyeshe wamewapa nini kule wilayani na kwenye matawi............ i hate politics.
   
 10. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #10
  Mar 16, 2011
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  fisadi mkubwa wewe!!!
   
 11. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #11
  Mar 16, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,143
  Trophy Points: 280
  Kama we utaandamana bila posho, nenda mwenyewe, mie akuuuuuu, bila malipo siendi kula mkong'oto.
   
 12. s

  sawabho JF-Expert Member

  #12
  Mar 16, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,504
  Likes Received: 946
  Trophy Points: 280
  Tuwe wavumilivu, jana Mkuu wa nchi ameelekeza Watoza Ushuru waangalie namna ya kurekebisha mambo. CHADEMA ni daraja la kufikisha malalmiko ya wananchi kunakohusika, ina maana Umma umepata sehemu ya kuonyesha kilicho moyoni mwao. Na hii iwe somo kwa viongozi kuwa hali si shwari. Hata kama CDM wasingeanzisha hayo maandamano watu wangekuja kushtuka tu, ndio maana wanajitokeza kwa wingi ili kuonyesha hisia zao.
   
 13. s

  sawabho JF-Expert Member

  #13
  Mar 16, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,504
  Likes Received: 946
  Trophy Points: 280
  Mbona siku zote mimi na wewe hatuendi, lakini wanakuwa wengi? Waache waende hutuwezi kupingana na wakati.
   
 14. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #14
  Mar 16, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280


  Wao wamezoea kuwalipa wananchi ili wawaunge mkono kwa kuwavisha Tshirt na Kofia kwa mabilioni ya shiringi na hasa wamewa target wananchi walio vijijini maana ndiko huvaliwa sana Tshirt na kofia za chama hata kama kampeni zimekwisha. Kuna tetesi katika bajeti yao ya kampeni walitengeneza Tshirt na kofia za kutosha watu milioni10 nchi nzima, ukipiga hesabu kwa kila Tshirt ni Tshs5000 na kofia Tshs3000 (yaani10,000,000x5000+10,000,000x3000) utapata jumla ya pesa iliyotumika kuhonga wananchi ni Bilioni80, hizi pesa mpaka sasa haijulikani walizipata wapi? au ndo hizo wanataka kuzirudisha kupitia Downs'?
   
 15. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #15
  Mar 16, 2011
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wajinga ndio waliwao kila siku
   
 16. mbogo31

  mbogo31 JF-Expert Member

  #16
  Mar 16, 2011
  Joined: Nov 28, 2008
  Messages: 687
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Nilitaka na nyie muandamane, lakini mmeshindwa kwa kigezo cha foleni. waulize CCM watumia vipi mabilioni wanayokwapua Serikalini!
   
 17. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #17
  Mar 16, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  hivi kule CCM huwa mnalipwa kiasi gani?
   
 18. D

  Divele Dikalame Member

  #18
  Mar 16, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 77
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ah chedema tupeni hozo posho mlizotenga bilioni 2 nasi tule acheni uchoyo
   
 19. D

  Divele Dikalame Member

  #19
  Mar 16, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 77
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  chadema kazi kweli kweli!
   
 20. MduduWashawasha

  MduduWashawasha JF-Expert Member

  #20
  Mar 16, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 1,567
  Likes Received: 407
  Trophy Points: 180
  Ndo siasa hizo mjomba.jipangeni
   
Loading...