CHADEMA hamishieni majeshi vijijini vinginevyo ukumbozi wa nchi hii ni ndoto

JERRY

JF-Expert Member
Feb 18, 2009
628
497
Mbali na mapungufu mengi sana ya mfumo wa uchaguzi na TUME YENYEWE YA UCHAGUZI ambavyo vimekuwa vikilalamikiwa sana kutaka kubaka demokrasia nchini lkn ikweli ni kwamba bado moto wa mabadiliko ktk nchi hii haujafika vijijini na ndo maana chaguzi nyingi matokeo ya vijijini yanakuwa yanaibeba sn ccm,Kule makatibu kata, wenyeviti wa vijiji na seikali za mitaa ndo waratibu wa madhambi mengi ya wizi wa kura.

HIVYO NASHAURI HUU NDO WKT MUAFAKA WA CDM KUHAMISHIA MAPAMBANO HUKO VIJIJINI VINGINEVYO VUGUVUGU HILI LITAISHIA MAENEO YA MIJINI KAMA ILIVYO SASA, WKT HUKO VIJIJINI ccm tayari wana mtaji wao wa muda mrefu,
wkt ni sasa 2015 panapo majaliwa si mbali
 
mmbangifingi

JF-Expert Member
Mar 9, 2011
2,839
554
Mkuu uko sahihi. hata tukio la kukamatwa mjumbe Igunga akinakili shahada za wenzie ni kielelezo tosha kwamba wajumbe/makatibu kata vjjini ndo wanatumiwa cause hawajatembelewa na dhana ya mabadiliko. So lazima CDM wajikite sana huko vjjini kuanzia sasa, 2015 wanamalizia mijini
 
CHUAKACHARA

JF-Expert Member
Jun 3, 2011
12,365
6,404
Mbali na mapungufu mengi sana ya mfumo wa uchaguzi na TUME YENYEWE YA UCHAGUZI ambavyo vimekuwa vikilalamikiwa sana kutaka kubaka demokrasia nchini lkn ikweli ni kwamba bado moto wa mabadiliko ktk nchi hii haujafika vijijini na ndo maana chaguzi nyingi matokeo ya vijijini yanakuwa yanaibeba sn ccm,Kule makatibu kata, wenyeviti wa vijiji na seikali za mitaa ndo waratibu wa madhambi mengi ya wizi wa kura.

HIVYO NASHAURI HUU NDO WKT MUAFAKA WA CDM KUHAMISHIA MAPAMBANO HUKO VIJIJINI VINGINEVYO VUGUVUGU HILI LITAISHIA MAENEO YA MIJINI KAMA ILIVYO SASA, WKT HUKO VIJIJINI ccm tayari wana mtaji wao wa muda mrefu,
wkt ni sasa 2015 panapo majaliwa si mbali

Waheshimiwa viongozi wa Chadema, hasa mtendaji mkuu Dr. Slaa, hakikisha at least kila kata ina ofisi ya CDM. Surely you will notice the difference. Can you imagine kama CDM mgekuwa na mtaji vijijini Igunga ingetokea nini. People would be happy by now.
 
FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
27,779
30,318
taratibu kaka, hata Roman empire haikujengwa siku moja - na ndiyo maana tunasema CDM sasa imekamilika na inaaminiwa na wananchi wa tanzania kwa zaidi ya 65% up to 75%.

We angalia statistics za jimbo la igunga oct 2010 uchaguzi mkuu - CDM Diwani mmoja - Mbunge hakugombea kabisaa.
Leo hii tuna wapiga kura wapya zaidi ya 23,000. ongezeko hili ni prove tosha kwamba CDM sasa ni chama ambacho kinaweza kuongoza dola hata leo hii.

Sibishi wazo lako ni zuri lakini nafikiri CDM is already doing that na kuhakikisha hilo ni uchaguzi huu wa igunga.
 
Godlisten Masawe

JF-Expert Member
Jul 20, 2011
738
281
Naunga mkono HOJA 100% mkuu, muda ndio sasa.
Niliposikia CDM wamepeleka IGUNGA vijana 200, nilifurahi sana. Ni vema wakafanya ivyo ivyo kubeba makundi ya vijana wa CDM wenye uelewa mpana wa hari ya sasa na kuwasambaza mkoa kwa mkoa, wilaya kwa wilaya, vijiji kwa vijiji, vitongoji kwa vitongoji. Ifahamike vijana tupo tayari kufanya kazi iyo.
 
ismathew

JF-Expert Member
May 18, 2011
253
38
Hoja hii ni muhimu sana kwa CDM natumaini na wao wameshaliona hili, sasa hivi ni hatua ya kung'oa mizizi ya Ccm vijijini
kwenye watanzania ambao kwa kila kitu ulazimishwa kwa itikadi za Ccm,
 
salesi

Member
Jul 27, 2011
35
5
wazo zuri,waelekeze nguvu vijijini sio kusubiri wakati wa uchaguzi ndio wafike vijijini! kama kweli wanataka kuchukua dola.wakiweza watumie hata shilingi yao ya mwisho kufika vijijini!
 
nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,779
Sio lazima kuhamishia Vijijini; Mijini ndio kuna wapiga kura msijidanganye wapiga kura waliojiandikisha walikuwa 171,000 waliopiga kura ni 50,000 asilimia 80 ya hao ni wa mjini kwahiyo ni kuhamasisha woote wa mjiji kupiga kura

Na woote wa mjini wanaipenda CHADEMA; MSIJISIMBUE NA VIJIJINI ANGALIA WOTE WA MJINI
 
salesi

Member
Jul 27, 2011
35
5
kiingine kilichosaidia kuongeza kura igunga ilikua udhibiti wa wizi wa kura baada ya kukubaliwa kwa mawakala kutoka nje ya igunga, in the geraral election is difficult coz every where needs attention of theft
 
mozze

Senior Member
Aug 27, 2010
185
28
Hoja hii ni muhimu sana kwa CDM natumaini na wao wameshaliona hili, sasa hivi ni hatua ya kung'oa mizizi ya Ccm vijijini
kwenye watanzania ambao kwa kila kitu ulazimishwa kwa itikadi za Ccm,

Pamoja na umuhimu wake lakini nadhani CDM wawe makini wasije poteza nguvu na resources zao kufuata vijiji wakati wakiwawekawatu sawa mijini inatosha kabisa. Yunajua kabisa katika sehemu za mijini au karibu na miundo mbinu ndio kuna watu wengi, sehemu kama wilayani au Kwenye kata.
Unajua CCM wamekuwa wakitumia hii propaganda kuwa wanapata kura nyingi vijijini ili ku-justify wizi wa kura. Ukweli unaonekana kutokana na idadi ya wapiga kura. Mimi siamini kama kweli number inayotolewa na tume ni sahihi. Kwa mfano igunga wanasema kuna wapiga kura zaidi ya 171,000 wakati tumeona ukweli kuwa 2010 na Tarehe 2 OCt idadi inakaribiana. Hiyo idadi iliyozidishwa ndio ya kubalance pale matokeo yakiwa tofauti na matarajio ya CCM kwa kisingizio kuwa CCM mtaji wake vijijini......
CCM wanajua vyama vya upinzani havina rasilimali za kutosha kuwafikisha vijiji vyote, hivyo inakuwa rahisi sana wao kuongza kura kidogo kujiwekea ushindi.

Chadema hakiwezi kuwa na uwezo wa kufika vijiji vyote, ni bora kuwekeza mijini ili effect yake isambae kwenda vijijini. CCM wanatumia viongozi wa serelakali kama viongozi wa serekali za vijiji kitu ambacho Chadema au chama kingine cha upinzani ni vigumu, unless kama watakuwa na uwezo wa kupandikiza watu wao ambao ndio watakuwa muhimili wa kuwafkia wananchi huko vijijini. May be CDM wajaribu kupenyeza wanachama wao au watu wenye mapenzi nao wafikie ungozi wa vijiji (bila CCM kutambua) na hivyo pindi ikifika wakati wa uchaguzi basi watakuwa angalau na watu wa kuwaamini kuwa watasimamia maslahi yao!
Narudia tena Chadema wasipoteze resources zao na nguvu kufikiria vijiji ila watumie akili zaidi na hizo resources wahakikishe wanawaweka sawa watu wa maendeo ya mijini na yanayofikika kwa urahisi...ikiwamo kuwahimiza wajiandikishe na kutunza Kadi zao!
 
Mkulima mimi

JF-Expert Member
Dec 12, 2009
233
30
siyo kuhamishia vijijii tu CHADEMA wanahitaji kubadili mfumo wao wa kampeni.

1)kampeni za jukwaani wanazofanya kwa sasa zinavuta makundi makubwa ya vijana ambao wengi ni rahisi kubadilishwa misimamo kama chadema yanyewe ilivyoweza kuwabadili pia inonesha vijana wanahamasika kwenye mkutano lakini hamasa inashuka haraka kampeni zinapofungwa kiasi wengi huwa hawaendi kupiga kura( kama siku ya kupiga kura ingeruhusiwa kuendele kuhamasisha watu kwa mkutano huennda chadema ingeshinda sehemu kubwa)
2)kipindi cha maandamano yanayofanyika makundi ya wazee, watu wazima na waanawake huona kama ni vurugu ingawa chadema na vijana huona kama ni mwamko, hili linaushahidi wa wawazi ndiyo maana ccm wanaimba chadema na maandamano wanataka kuvuruga amani ya nchi inawezakana madhara ya kauli kama hizi yasionekane au chadema waka yapuuza lakini ile hamasa wanayokuwa nayo vijana kwenye maandamano na mikutano ukijumlisha propaganda za ccm impact yake kwa haya makundi hasa ya vijijini siyo haba!!
USHAURI
CHADEMA kabla hawaja panda jukwaani au hawajafanya maandamno wanatikiwa kuandaa mikutano ya ndani kukutana na wazee na akina mama kwa nyakati tofauti, mfano chukulia mbowe ameenda mbeya kwenye kampeni za udiwani majengo siku moja baaada ya soko kuungua alionekana kihutubia watu aliokutana nao pale soko lilipo ungua iingekuwa busara sana kama muhehimiwa angehakikisha baada ya mkutano wauzinduzi wa kampeni au hata kabla angeomba kukutana na wazee wa mkoani mbeya wazee siyo wengi ila wanushawishi mkubwa kwa vijijini!! (sina uhakika kama alikutana naao au hakukutana nao wazunumze na haya makundi vizuri wayaeleweshe kwa undaninini hasa shabaha yao!! lugha za jukwaani kwa haya makundi haijalishi una sera nzuri kiasi gani huwa hawaielewi viizuri kama siyo kuwa haileweki kabisa!!
kwa kufanya itasaidia angalau haya makundi yakaanza kuwaona chadema kama wenzao ila kwa sasa propaganda za kwamba vyama vya upinzani vinalengo la kuleta vurugu haita isha!!
 
Ngonini

JF-Expert Member
Sep 1, 2010
2,023
562
chadema wanahitaji kuinvest sana kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa 2014. Hili ni daraja muhimu sana la uchaguzi mkuu. Siku zote wapinzani huwa hawatumii nguvu nyingi kataika uchaguzi huu. Hapa ccm ndo huwa wanawapigiga bao maana wakishajenga kule vijijini inakuwa vigumu kwa asiye na viongozi kuwafikia wanakijiji maana wanakuwa kama wako chini ya viongozi wa mitaa na mabalozi wa ccm.

Inashangaza sana watu bado wanawatambua mabalozi kama ndo viongozi wa serikali. Ndiyo wanaohhamasisha hata ulinzi wa mitaa,michango ya maendeleo. Kwa mtindo huu mzee akifUatwa na balozi na kuambiwa kura ya raisi na ubunge sisi ubalozi wetu tunampigia fulani hawezi kukataa kwa maana ndiye kiongozi wa karibu anayemfahamu na ndiye huwa anamfuata akiwa na shida za kiserikali.

Chadema amkeni mabalozi wanatuumiza huko vijijini!
 
Sir R

JF-Expert Member
Oct 23, 2009
2,175
297
Dr Slaa pole kwa shughuli ya kampeni.

Leo nileta kwako ombi maalum la vijana wanamageuzi wenye nia njema ya kukomboa nchi hii mikono mwa watawala wasiozingatia kanuni ya utawala bora. Vijana wengi tumehamasika sana na siasa ya chama chako CDM.

Tuanzie wapi ili tuweze kushiriki katika kazi ya ukombozi, vijijini watu wameanza kuelewa maana demokrasia lakini bado kuna tatizo la udanganyifu linalofanywa na watawala. Tungependa CDM iwe na mifumo mizuri vijijini ili wakati wa kampeni kazi iwe rahisi.

Mijini watu wana uelewa wakutosha kuhusu maana ya demokrasia ya vyama vingi.

Naomba mwongozo wako katika hili.
 
dedam

JF-Expert Member
Jan 5, 2011
845
164
ile kampeni ya washa taa ingeimarishwa ili kuweza kuwasha taa vijijin mbinu iliyotumika igunga zambazen sehemu zingine
 
Sir R

JF-Expert Member
Oct 23, 2009
2,175
297
ile kampeni ya washa taa ingeimarishwa ili kuweza kuwasha taa vijijin mbinu iliyotumika igunga zambazen sehemu zingine

Ahsante mkuu, ningetamani Dr Slaa aje hapa atushirikishe, tuna wajibu kati hili ila tunahitaji mwongozo pa kuanzia.
 
Mzee

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
13,536
5,642
Dr Slaa pole kwa shughuli ya kampeni.

Leo nileta kwako ombi maalum la vijana wanamageuzi wenye nia njema ya kukomboa nchi hii mikono mwa watawala wasiozingatia kanuni ya utawala bora. Vijana wengi tumehamasika sana na siasa ya chama chako CDM.

Tuanzie wapi ili tuweze kushiriki katika kazi ya ukombozi, vijijini watu wameanza kuelewa maana demokrasia lakini bado kuna tatizo la udanganyifu linalofanywa na watawala. Tungependa CDM iwe na mifumo mizuri vijijini ili wakati wa kampeni kazi iwe rahisi.

Mijini watu wana uelewa wakutosha kuhusu maana ya demokrasia ya vyama vingi.

Naomba mwongozo wako katika hili.

hebu pitia vizuri ulichoandika.!!
 
politiki

JF-Expert Member
Sep 2, 2010
2,376
1,504
Muda wa kukaa maofisini kwa chadema sasa umekwisha karibu kunakucha kuingia 2015, kuna vijana wengi nchi wenye uchungu na nchi hii kuna haja ya chadema kuwapa crash course ya miezi miwili au mitatu ya sera, muongozo na imani za chadema ili waingie vijijini kuwasha moto ktk kuwaelimisha wanavijiji kuhusu nia na madhumini ya chadema.

Hii itawasaidia ktk nyanja mbili:

Kwanza ujumbe wenu wa kutoa ajira kwa vijana utakuwa siyo theory tena bali ni practical.

Pili ni kwamba badala ya kuendesha siasa maofisini sasa mutakuwa mumewafikia wananchi wa vijijini na kukaa nao chini na kuwasikiliza matatizo yao na kuwapa mawazo wanavijiji hao kuwaonyesha nini mtafanya endapo chadema ikiingia madarakani badala ya CCM.

Huu ndio wakati mzuri wa kukaa na wanavijiji na siyo wakati wa uchaguzi kwani unakuwa na muda mzuri wa kubadilishana nao mawazo kwa upana hiyo itawaondolea dhana baadhi wa wanavijiji kuwa labda chadema ni chama cha watu wasiotakia mema nchi.

Kazi kuu ya akina DR.Slaa na Mhe. Mbowe itabakia ni kuwafuatilia makamanda hao huko vijijini na kufungua matawi na kutoa kadi kwa wanachama wapya kwani hawana muda wa kuweza kuhaha vijijini na at the same time kushugulikia kazi za jimbo na chama kwahiyo kwa mgawanyo huu kazi mtakuwa mmejiraisishia kazi nyie wenyewe.

Najaribu kufikiria kama chadema ingekuwa na timu hii ninayopendekeza ya vijana kama 15 au 20 halafu wangepita mahala kama igunga kabla kabisa ya uchaguzi halafu waka spend 10 to 20 days ktk moja ya hizi kata tulizopoteza probably that would have make a difference.

Kwahiyo chadema tuache siasa za maofisini, vijana wako tayari kuingia uwanja wa mapambano mapema na tuache kusubiri mpaka uchaguzi ufike ndio tunaanza kuwaingia wana vijiji watatuona sisi ni kama CCM tu tunasubiri uchaguzi ndio tunaonekana tuanze leo tusisubiri kesho.

Kwa professional yangu naweza kuwaandalia mtaala mdogo simple wa namna ya kuwaelimisha makamanda ili wabebe ujumbe huko simple, clear na pia straightforward.

MHESHIMIWA HECHE NAKUOMBA UTUFIKISHIE UJUMBE WETU VIJANA KWA WAHUSIKA NAAMINI WANAPENDA KUPATA USHAURI KUTOKA KWA VIJANA WENZAKO.
 
hahoyaya

Member
Apr 24, 2011
89
11
Mkuu umenena,hymambo ya kusubiri mpaka uchaguzi yana gharama zake ambazo nadhani ni unnecessary.Chadema nadhani hamjaelewa kuwa watanzania wanataka kuwakabidhi nchi sasa lazima muwafikie mapema na kuuza sera zenu ili wajenge imani,maana sio chama cha msimu na watu wanalitambuwa hilo.Imani ya watanzania kwenu wameionyesha igunga majuzi,pamoja na nguvu zote za serikali na vyombo vyake bado wananchi wameonyesha imani kubwa kwenu.Hamtakiwi kupumzika kabisa , 2015 haiko mbali km mnavyodhani!
 
Massenberg

JF-Expert Member
Jun 4, 2011
1,173
1,370
Muda wa kukaa maofisini kwa chadema sasa umekwisha karibu kunakucha kuingia 2015, kuna vijana wengi nchi wenye uchungu na nchi hii kuna haja ya chadema kuwapa crash course ya miezi miwili au mitatu ya sera, muongozo na imani za chadema ili waingie vijijini kuwasha moto ktk kuwaelimisha wanavijiji kuhusu nia na madhumini ya chadema.

Hii itawasaidia ktk nyanja mbili:

Kwanza ujumbe wenu wa kutoa ajira kwa vijana utakuwa siyo theory tena bali ni practical.

Pili ni kwamba badala ya kuendesha siasa maofisini sasa mutakuwa mumewafikia wananchi wa vijijini na kukaa nao chini na kuwasikiliza matatizo yao na kuwapa mawazo wanavijiji hao kuwaonyesha nini mtafanya endapo chadema ikiingia madarakani badala ya CCM.

Huu ndio wakati mzuri wa kukaa na wanavijiji na siyo wakati wa uchaguzi kwani unakuwa na muda mzuri wa kubadilishana nao mawazo kwa upana hiyo itawaondolea dhana baadhi wa wanavijiji kuwa labda chadema ni chama cha watu wasiotakia mema nchi.

Kazi kuu ya akina DR.Slaa na Mhe. Mbowe itabakia ni kuwafuatilia makamanda hao huko vijijini na kufungua matawi na kutoa kadi kwa wanachama wapya kwani hawana muda wa kuweza kuhaha vijijini na at the same time kushugulikia kazi za jimbo na chama kwahiyo kwa mgawanyo huu kazi mtakuwa mmejiraisishia kazi nyie wenyewe.

Najaribu kufikiria kama chadema ingekuwa na timu hii ninayopendekeza ya vijana kama 15 au 20 halafu wangepita mahala kama igunga kabla kabisa ya uchaguzi halafu waka spend 10 to 20 days ktk moja ya hizi kata tulizopoteza probably that would have make a difference.

Kwahiyo chadema tuache siasa za maofisini, vijana wako tayari kuingia uwanja wa mapambano mapema na tuache kusubiri mpaka uchaguzi ufike ndio tunaanza kuwaingia wana vijiji watatuona sisi ni kama CCM tu tunasubiri uchaguzi ndio tunaonekana tuanze leo tusisubiri kesho.

Kwa professional yangu naweza kuwaandalia mtaala mdogo simple wa namna ya kuwaelimisha makamanda ili wabebe ujumbe huko simple, clear na pia straightforward.

MHESHIMIWA HECHE NAKUOMBA UTUFIKISHIE UJUMBE WETU VIJANA KWA WAHUSIKA NAAMINI WANAPENDA KUPATA USHAURI KUTOKA KWA VIJANA WENZAKO.

Umenena Politiki, mimi si Heche lakini tuwasiliane 0712 785 695, thanks.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

3 Reactions
Reply
Top Bottom