CHADEMA Hamad Rashid akidondoka CUF mnyakueni, ili mzoe kura za visiwani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA Hamad Rashid akidondoka CUF mnyakueni, ili mzoe kura za visiwani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Jumakidogo, Jan 3, 2012.

 1. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #1
  Jan 3, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Upepo wa kisiasa unavuma vibaya kwa upande wa Mh Hamad Rashid wa CUF Unaweza kusababisha kumuengua kutoka ndani ya chama cha CUF.

  Bila ya shaka ikitokea hivyo atakuwa na chaguo la vyama viwili vya kisiasa vyenye nguvu ili asipotee katika siasa yaani CDM na CCM. Akitaka kubaki kwenye chati nzuri na umaarufu wa kisiasa chaguo zuri ni CDM. Hali itakayochangia chama hicho kuzoa kura za visiwani kama atagombea nafasi hiyo ya urais huko visiwani.

  Kwa upande wa CUF Hali inaweza kuwa mbaya na ikiwa hivyo pengine mwafaka sasa ukawa wa vyama vitatu baada ya uchaguzi. CDM, CUF na CUF.
   
 2. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #2
  Jan 3, 2012
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,153
  Likes Received: 1,249
  Trophy Points: 280
  Mh! Hamad kwenda Chadema mbona moyo wangu unanisuta kuwa huyu mtu hawafai chadema, mi nadhani ccm ndo kunamfaa zaidi
   
 3. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #3
  Jan 3, 2012
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Mara nyingi ajali za kisiasa zimekuwa na matokeo yasiyo tabirika japo mwathirika mara nyingi ni msababisha ajali.. ngoja tuone itakavyokuwa.
   
 4. k

  kkitabu Senior Member

  #4
  Jan 4, 2012
  Joined: Dec 27, 2011
  Messages: 122
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  HR njoo kwetu CHADEMA kwa sababu ukienda CCM itakuwa ndo mwisho wa upinzani kwa upande wa pili wa muungano yaani Tanzania visiwani
   
 5. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #5
  Jan 4, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  ngoja niendelee kupata staftahi:A S-coffee:
   
 6. Pelekaroho

  Pelekaroho JF-Expert Member

  #6
  Jan 4, 2012
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 1,502
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 160
  another Shibuda
   
 7. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #7
  Jan 4, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,271
  Trophy Points: 280
  Ni nani aliekwambia kwamba kuna Mtanganyika anaetaka kura za Wapemba? Watanganyika tupo kwenye mjadala wa kuuvunjilia mbali muungano na si vinginevyo.
   
 8. S

  SUWI JF-Expert Member

  #8
  Jan 4, 2012
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 548
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Hapana CDM wasimpokee kabisa,, kwanza jana nilimsikia kwenye taariya habari akisema hatajiunga na chama chochote kama atatemwa CUF bali wataanzisha chama chao.. anaonekana kuwa na tamaa ya pesa na madaraka. Anataka aanzishe chama ili awe mwenyekiti.. hafai huyo
   
 9. u

  utantambua JF-Expert Member

  #9
  Jan 4, 2012
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 1,373
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kwa vyama vya upinzani ambavyo kimsingi bado havijakuwa institutionalised kutegemea kura kwa sababu ya mwanachama mmoja si nzuri kwa afya ya muda mrefu ya chama. CDM wampotezee tu HR, wajijenge taratibu visiwani, ni bora wavune kura kiduchu zitokanazo na party institutionalisation kuliko kuvuna maelfu ya kura yatokanayo na mwanachama mmoja tu.
   
 10. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #10
  Jan 4, 2012
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Huyo Ziggo lisilobebeka linapenda uongozi tuuu
   
 11. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #11
  Jan 4, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,144
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  kesha sema hatajiunga na chama chochote, CDM wamchukue kwani yeye mzigo wa kubebeka usio na utashi?
   
 12. TOWNSEND

  TOWNSEND JF-Expert Member

  #12
  Jan 4, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,597
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  hata mimi namuona ni sumu kali kwa chadema, hata hivyo alishasema ataanzisha chama chake
   
 13. M

  Mkayah Member

  #13
  Jan 4, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hana issue atembee zake huko Pemba akalime Karafuu nasikia imepanda sana bei! anapenda sana kuongoza afu hapendi kabisa kuongozwa. Sasa CHADEMA atamuungoza nani?
   
 14. S

  Song'ito JF-Expert Member

  #14
  Jan 4, 2012
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 347
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  My take hii ni sumu kali ambayo chadema haipaswi kuigusa, huyu bwana hafai... ukiona ameanzisha moto katika nyumba aliyokuwa anaishi mwanzo, una hakika gani hataanzisha katika nyumba mpya atakayohamia?

  Chadema iachane na kuokoteza watu waliokuwa dumped kutoka vyama vingine kwa kuwa walionekana wana kasoro... ninaamini wapo watu wengi, vijana wenye moyo ambao wanaweza kuleta mabadiliko chanya katika chama... hata kama hawana nguvu sasa lakini taratibu chadema inaweza kuwajengea uwezo vijana hao na kuiambia jamii kuwa wanaweza... kwani kina Dr. Slaa na mbowe na zitto waliingia chadema tu na kujulikana papo kwa hapo?

  ila haya makapi ya kutoka CCM au CUF au chama kingine chochote sidhani kama yatakisaidia chama ila sana sana yatakiua tu... mmefanya kosa kwa shibuda naomba isijirudie tena kwa kumualika Hamad ndani ya chama, maana mnajua toka ndani ya mitima yenu jinsi huyu bwana asivyokubaliana nanyi katika sera zenu.
   
 15. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #15
  Jan 4, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,223
  Trophy Points: 280
  hapo mtakua mmebugi step
   
 16. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #16
  Jan 4, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,779
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  CDM isifanye kosa la kumchukua HR,huyu jamaa hafai,abakie huko CUF ama arudi nyumbani kwake CCM.
   
 17. KING COBRA

  KING COBRA JF-Expert Member

  #17
  Jan 4, 2012
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2,783
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  [h=2]Tamko la wanachama wa CUF mkoa wa DSM [/h]
  CUF – CHAMA CHA WANANCHI
  TAMKO LA WANACHAMA WA CUF MKOA WA DAR ES SALAAM JUU HALI YA KISIASA NDANI YA CHAMA.
  Sisi wanachama mkoa wa Dsm,baada ya kuona hali mbaya ya kisiasa ndani ya chama na mwelekeo wa kunyongwa kwa Demokrasia ambapo maamuzi kandamizi yamejitokeza na yanatarijiwa kufanyika katika vikao vinavyoendelea hivi sasa ambavyo mazingira ya kuitishwa kwake vinaashiria dhulma zidi ya haki na utekelezaji wa matakwa ya mtu binafsi, ambapo viongozi wakuu wanaolalamikiwa hawakotayari kukosolewa badalayake wanatumia mamlaka waliyonayo kutoa maamuzi kandamizi.
  Sisi kama wanachama na wapenda haki tungependa HAKI SAWA KWA WOTE ionekane ikitendeka na sio kutajwa kinadharia.​
  Kutokana na hali hiyo tumeona kubainisha madhaifu yaliyopo na madai yetu ya msingi tukitaraji Uziwi na Ukaidi wa Viongozi wetu utakoma hatimae Chama kuleta mvuto mpya:​
  A: MADAI YA MABADILIKO YA KATIBA
  1. Uwepo wa Makamu mwenyekiti bara​
  2. Mwenyekiti Taifa na Makamu wake wawili waingie kwenye Kamati Tendaji Taifa​
  3. Pasiwepo ubaguzi katika uwakilishi wa wajumbe wa Wilaya wanaounda Mkutano Mkuu wa Taifa ambapo ukiondoa wajumbe wanaoingia kwa nyadhifa zao ambao Zanzibar pia uzidi, wajumbe 20 wanatoka kila Wila ya Zanzibar wakati Tanzania Bara inatoa mjumbe mmoja tu.​
  4. Pawepo mabadiliko katika uwakilishi wa Wajumbe wa Balaza Kuu ambapo kwa sasa ,Wajumbe 25 wanatoka Katika Wilaya 123 za Bara na Wajumbe 20 Wanatoka katika Wilaya 10 za Zanzibar.Tofauti hii ya uwiyano na ugumu wa kuhudhuria vikaoni wajumbe wanaotoka TZ Bara kutokana ubovu wa miundombinu na umbali wa maeneo wanakotoka unatoa mwanya kwa Katibu mkuu kuitisha vikao kandamizi vyenye kupitisha matakwa binafsi ya Sefu Sharif na mfumo wa upendeleo wa Wapemba​
  5. Mfumo wa uteuzi wa viti maalum ubadilishwe kwa kuwa unaua bara , kutokana na kuzidi kujaza wabuge Zanzibar badala TZ Bara penye hitajio kubwa la wabunge wasaidie kujenga Chama na ikizingatiwa nafasi hizo ni hesabu ya kura tulizopigania watu wa Bara kwani Zanzibar kurazao ni chache.​
  6. Kuendelea kwa Chama kuitumia katiba ya zamani ya toleo la 2003 wakati mkutano mkuu wa taifa wa 2010 LAND MARCK HOTEL ulipitisha katiba iliyo na vipengele vipya haitumiki mpaka hii leo ni kuvunja sheria na ushahidi wa dharau kwa wajumbe wa mkutano mkuu na wanachama matawini.​
  B: UTAWALA NA UTENDAJI
  1. Mwenyekiti Taifa hana ofisi zanzibar wakati katibu Mkuu na makamu Mweyekiti wana ofisi Makao makuu Zanzibar na ofisi kuu bara.​
  2. Asilimia zaidi ya 80 ya ajira za madereva na wafanyakazi wengine wa ofisi kuu bara wanatoka zanzibar wakati hakuna madereva wanaofanya kazi zanzibar wanaotoka Bara.​
  3. Kuna matatizo ya mgawanyo wa raslimali za chama kati ya Bara na Zanzibar,mifano mgao wa Chama wa bajeti ya uchazi mkuu 2010 Zanzibar yenye wilaya 10 katika Mikoa 5 imepewa sh.500 milioni wakati Bara yenye wilaya 123 katika Mikoa 23 imepewa sh.70 milioni tu,fursa za Elimu na Mikopo,magali 5 ya Chama yameuzwa bila ya kufua taratibu za tenda.​
  C: UDHAIFU WA SEFU
  1. Amekua kiongozi hodari wa kufukuza au kusababisha kuhama kwa viongozi hodari wa Tanzania Bara kama:-​
  (a) Mhe. James Mapalala​
  (b) Mhe. Maiko Nyaluba​
  (c) Mhe. Slivesta Kasulumbai​
  (d) Mhe. Geoge Shambwe​
  (e) Mhe. Shaibu Akwilombwe​
  (f) Mhe. Richard Hiza Tambwe​
  (g) Mhe. Wilfred Lwakatare​
  (h) Mhe. Othman Dunga​
  (i) Mhe. Asha Ngende​
  (j) Mhe. Khamisi Katuga​
  (k) Mhe. Ashura Amazi​
  Kwa upande wa Zanzibar ni pamoja na​
  a.Naila Jilawi​
  b.Fatuma Magimbi​
  c.Juma Othuman​
  d.Salumu Msabaha​
  Watu wengi waliofukuzwa au kulazimika kuhama Chama ilitokana na mfumo wenye nguvu usio rasmi ndani ya Chama unaomkinga Maalim Sefu asikosolewe​
  2. Toka kuanzishwa CUF hajafanya ziara au vikao hata mara moja katika mikoa na wilaya nyingi za Tanzania Bora​
  3. Amekuwa bingwa wa kufanya maamuzi makubwa ndani ya Chama yeye binafsi nje ya katiba na utaratibu wa vikao mfano​
  Kumtambua Karume na kukiuka maamuzi ya Baraza kuu la Uongozi Taifa​
  (a).CUF imeambulia mawaziri 7 tu CCM ina mawaziri 9 lakini wakuu wa mikoa, wakuu wilaya na watedaji wote wa serikali ni wa CCM yeye analilridhia.​
  (b). Ilani ya inayo tekelezwa zanzibar ni ya CCM wakati inadaiwa ni serekali ya umoja wa kitaifa​
  (c).Ubaguzi wa upemba ndani ya chama.​
  Nahaya yanayoendelea Chama kumdhibiti Mh.Hamadi Rashidi ni uthibitisho juu ya Maalim Sefu kukiburuza chama anavyotaka ​
  a.Uundwaji wa kamati ya nidhamu na maadili kinyume na katiba ya chama.​
  b.kamati ya utendaji taifa imewajadili watuhumiwa bila kuwapa nafasi ya kujieleza ambapo ni haki yao kwa mujibu katiba​
  c.Kamati tendaji inaongozwa na Maalim Sefu akisaidiwa na wengi wa wajumbe wake ambao wameonyesha chuki za dhahiri na tayari wameshawahukumu watuhumiwa nje ya fikao mfano.E nail ya mwenye kiti wa kamati tendaji taifa sefu kwenda kwa mwenyekiti Prof.Lipumba ilishapanga namna ya kuwafukuza watuhumiwa ya 14.decembr 2012​
  d.Tamko la Naiba katiba mkuu bora julius mtatiro kwa press tarehe 13.12.2011 ofisi kuu buguruni la kuwatangaza watuhumiwa kuwa ni waasi na kuwapa kuwashuhulikia nje ya vikao katiba na taratibu za chama bila kuwapa nafasi ya kujieleza​
  e.Kauli za N.katibu mkuu Zanzibar Ismail Jusa makamu mwenyekiti Machano khamisi Ali katika maeneo mbalimbali na ofisi kuu kuwa tutawa wafukuza kama kama akina Mapalala​
  Hamad mwana wa haramu ni mwana wa haram tu,hata ukimuweka ndani ya chupa atatoa kidole nje ili aone kama!! Ambayo ni kashfa​
  c.Matumizi ya vitisho dhidi ya watuhumiwa yanadhihirisha kuwa wasioweza kutenda haki.​
  d.Kikao kilicho fanyika zanzibar cha kamati Tendaji ya Taifa inadhihirishwa kuwa lengo lake lilikuwa ni ubaguzi ilikikao kikifanyika yeye akawa hayupo basi kikao hicho kitaongozwa na Jusa Ismaili ambaye alisha watukana​
  Blue Guard Bara akiwemo mzee Juma wandwi kwamba wao ni mbwa wanatumiwa na watu wa Zanzibar katika ukumbi wa Diamond Tubilie,mwaka 2009 wakati wa mkutano mkuu​
  Baraza kuu limehitimishwa tarehe 4/01/2012 lina fanyika Zanzibar baada ya kikao cha kamati tendaji taifa tarehe 30 na 31 /12/2011 kutokana na mgawanyiko wa kijiografia wa wajumbe wa Baraza KuuTanzania​
  Baraza na hali ya miundo mbinu, Wajumbe wengi toka Tanzania Bara watashindwa kuhudhuria na hivyo kutoa nafasi ya wajumbe wa Zanzibar wanao muunga mkono sefu kufanya maamuzi kandamizi dhidi ya agenda za Tanzania bora​
  TAMKO LA WANACHAMA.
  Sisi wanachama, tuliokutana​
  Leo tarehe 1. 1. 2012 tuta hamasisha wanachama miko yote na hasa Tanzania Bara kuandamana kuelekea ofisi kuu ya CUF Buguruni kupinga mipango haramu ya kufukuzwa kwa wanachama wenzetu nje ya utaratibu wa kikatiba,​
  Tutachukua hatua za kisheria dhidi ya viongopzi wote wanao kiuka katiba halali ya chama.​
  Tunatoa rai kwa baraza kuu la uongozi Taifa kulimaliza suala hili kwa njia za kusuhulishana ndani ya vikao bila kufukuzana kwa njia zilezile zilizo tumika kukaa na wauji wa CCM serekali yake waliona wanachama wa CUF Bara na visiwani katika maandamano ya januari,26 na 27 na 2001 kuliko hatua wanazo tarajia kuzichukua za kufukuzana.​
  ................................................. …………………………………….
  Mwenyekiti Kamati ya Dharura Katibu Kamati ya Dharura
  Hamdan Ngulangwa (0715 552699)
  ...........................................................
  KATIBU KAMATI YA DHARURA
  Mpenda I. Mpenda (0715 664913)

  ……………………………………
  Mweka Hazina kamati ya dharura
  Leyla Husein (0719 827047)
   
 18. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #18
  Jan 4, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Jiwe linalokataliwa na waashi mara nyingi hugeuka jiwe la msingi
   
 19. Tz-guy

  Tz-guy JF-Expert Member

  #19
  Jan 4, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 439
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Naombeni msimfukuze Mh. Rashid, sisi CCM tunapenda kambi ya upinzani iwe na nguvu.
   
 20. L

  Luiz JF-Expert Member

  #20
  Jan 4, 2012
  Joined: May 23, 2011
  Messages: 342
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  naunga mkono hoja
   
Loading...