CHADEMA hali mbaya Kiteto, ofisi za Chama hicho ikiwemo ya Wilaya yafungwa zaidi ya miezi sita sasa

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,531
Wakati chama cha mapinduzi kikizidi kung'ara hapo Kiteto takribani wiki ya pili sasa baada ya Magufuli kuchaguliwa kupeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika October 25 mwaka huu, hali ya chama cha upinzani CHADEMA inazidi kuwa mbaya wilayani hapa baada ya wanachama wake kadhaa kurudi CCM kutokana na sababu mbalimbali na kupelekea ofisi za chama hicho wilayani hapa kutofunguliwa.

Ofisi ya wilaya CHADEMA hapa Kiteto ipo taabani, wakati viongozi wakuu wa chama cha CHADEMA wakiwa katika ombwe zito la kumpata mgombea wao pamoja na ukawa hali ya chamaa hicho wilayani imekuwa taabani na kubakia kuwa chama cha mijini na kwenye magazeti, tv pamoja na mitandao ya kijamii.

Hapa wilayani kiteto ofisi za CHADEMA ikiwemo ya wilaya na nyinginezo zina zaidi ya miezi sita haijafunguliwa kutokana na kudaiwa kuwa hali mbaya ya kisiasa ya chama hicho ambapo wana kiteto hususani hapa Kibaya makao makuu ya wilaya hawana mpango nacho kabisa.

Inasemekana kuwa sababu kubwa ya chama hicho kinachotishia kupotea wilayani hapa ni kukosekana kwa fedha za kulipia pango za frem wanazodaiwa na wenye nyumba waliokipangishia chama hicho.

Pia chama hicho kilikumbwa na kukimbiwa na wanachama wake hususani vijana ambao wengi wamekimbilia ACT-Wazalendo na wengine wengi kurudi CCM baaday ya uteuzi wa John Magufuli kuteuli wa kuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya CCM.

Badhi ya walikuwa wana chadema ambao leo hii wameungana na wana CCM wakiwa na mavazi ya njano na kijani katika uchaguzi wa wa ndani wa kutafuta viti maalum wamesema kuwa wamechoka kutoa fedha zao za mifukoni na kuendesha chama wakati na chama hicho kinapata ruzuku, pia wameaamua kurudi CCM kuachana na ubabaishaji unaofanywa na vyama viongozi wa vyama vya upinzani kwa kuwa wamekuwa wakihubiri wasiyoyatenda.

Sababu nyingine wamesema kuwa CHADEMA kimebakia kuwa chama mijini na vyombo vya habari yakiwemo magazeti na tv na hata mitandao ya kijamii wakati hali halisi wilayani hali mbaya hususani hapa Kiteto hakina nafasi kabisa si kwa chama hicho wala UKAWA
 
  • Thanks
Reactions: gsu
Kaka mkulima usharamba za wagombea nasikia wanagawa ubwabwa was kutisha huko..maana kama masikini kupata ugombea ndani ya Chama Chetu sahau
 
mkulimawakiteto

sio kiteto tu hata huku, pwani sehemu kama kiparang'anda, Kimazinyana, Mvuti, na sehemu nyoingi tu chadema hawaijui kabisa tena hata ofisi hamna
 
Last edited by a moderator:
mkulimawakiteto

Hata ulichokiandika chenyewe hakieleweki,mara ofisi zimefungwa zaidi ya miezi,mara wamehama baada ya ccm kumteua magufuri,mara wamehamia act,rudi kajipange ndio uje kivingine
 
Last edited by a moderator:
sio kiteto tu hata huku, pwani sehemu kama kiparang'anda, Kimazinyana, Mvuti, na sehemu nyoingi tu chadema hawaijui kabisa tena hata ofisi hamna

Uwache uwongo kudanganya watu kimanzichana,mkuranga yote,bigwa,mwanambaya,mlamleni, koote cdm imeenea na ina shine
 
sio kiteto tu hata huku, pwani sehemu kama kiparang'anda, Kimazinyana, Mvuti, na sehemu nyoingi tu chadema hawaijui kabisa tena hata ofisi hamna

huko pwani vp hali ya madarasa, watoto bado wanapata maisha bora ya kusoma chini ya miti?

Najua kutofika kwa elimu ni mikakati maalum ya ccm kwa ajili yenu
 
na lowasa angepita vita ya wakulima na wafugaji isingeisha kiteto ingekua kama somalia
 
mkulimawakiteto

Ni vizuri mkajua kwamba siyo lazima kusimamisha mgombea kila mahali. Lazima kuwa strategic wakati mwingine. Lakini mtu wa pwani kama bado anangangania ccm wakati pwani hakuna lolote basi atakuwa mwehu
 
Last edited by a moderator:
Danganya wajinga!!CCM kiteto imebaki vipande baada ya mzee mamvi kuwekwa kando!!Wengi kama siyo wote wako Chadema
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom