Ritz
JF-Expert Member
- Jan 1, 2011
- 46,903
- 32,312
Wanaukumbi.
Ninachotaka kuchambua katika huu uzi haina utofauti na mitazamo ya magwiji wa siasa pamoja na wasomi mbalimbali, mgongano wa fikra, kimaono na kimtazamo ambao kwa sasa umeikumba Chadema, ni kiashiria tosha kwamba Chadema kama chama kinazamishwa na Chadema wenyewe.
Wasomi na wapenda amani ambao wapo mitaani na sehemu za kazi wakisema kwa nyakati tofauti kitendo cha Kamati Kuu ya Chadema kuwavua madaraka Zitto na wenzake hata bila kuwasikiliza ni kiashiria tosha kuwa chama hicho kinaelekea kufa kifo cha kawaida, Dr. Slaa alikaliliwaakisema hata katiba ya nchi ukihusika kutengeneza mbinu za siri lazima ushughulikiwe, hakuna katiba itayaruhusu kufanya mipango ya siri, naye Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu alikaliliwa akisema kuwa waraka huo unaeleza mbinu za uasi ambazo zililenga kufanya mabadiliko makubwa ya uongozi wakati wa uchaguzi mkuu wa ndani wa chama hicho jambo ambalo ni kinyume na katiba, sheria na itifaki za Chadema.
Kinachoonekana hapa si uhaini kama viongozi wa Chadema walivyotaka kuaminisha jamii bali ni mbinu za kutaka kudumisha uongozi wa kimla, usultani, udikteta, ukanda na kudhoofisha wanachama wa chama hicho amabao wanapigana kwa nia ya kupanua uwigo wa demokrasia ndani ya Chadema, Lissu anajaribu kuingiza vitendo vya malumbano ya kisheria ya mahakama na kuyapeleka kwenye chama, tumeona matokeo ya Kamati Kuu kule Kigoma yaliyomkuta Dr.Slaa na wapambe wake wameishia kupopolewa mawe na kukaribishwa na mabango.
Chadema lazima mkubali inapokalibia uchaguzi wowote ule wagombea wanaowania kuwaondoa walioko madarakani ni lazima watumie ushawishi au utaratibu wa kisiri ili mikakati yao isijulikane kwa wale waliopo madarakani, ni vigumu kuwakuta viongozi wa juu wa chama chochote cha siasa wakijadili maendeleo ya chama huku wamejiachia barabarani.
Tundu Lissu, anachofanya ni kulazimisha taaluma yake ya uanasheria iwe fimbo ya kutishia wanachama, wanachofanya ni kutaka kuwafunga midomo wanachama ambao walikuwa na ndoto za kuwania nafasi za juu wasithubutu.