Inashangaza sana kusikia watu wanavyoishutumu CHADEMA hawna nidhamu, ooh wanasambaratika mara Zitto anajitoa CHADEMA,mara oo mpasuko ndani ya CHADEMA na blah blah nyingi 2. Ikumbukwe chadema ni chama kilichozaliwa kipindi cha mfumo wa vyama vingi, tusiifananishe na CCM iliyozaliwa enzi za chama kimoja, enzi za kuchagua kati ya kivuli na binadamu wakati wa kupiga kura. Kipindi hicho watu wakiwa na akili mgando zenye mtazamo mmoja, hii ilikuwa rahisi sana kwa chama kukubalika na kuota mizizi na kustawi. Kipindi hiki cha CHADEMA ni kipindi kigumu cha purukushani nyingi kiasi kwamba si ajabu kusikia kiongozi kajitoa, mara kasaliti si ajabu. Kwani hao CCM ni wangapi wasioafikiana na maamuzi ya wakubwa zao? Mbona ni wengi tu? Mimi maoni yangu ni kwamba CHADEMA haina tatizo lolote na chini ya mpiganaji MBOWE tutafight mpaka mwisho. Viongozi wa CDM wanajitahidi sana kuwaweka pamoja viongozi wake na hata wanachama. Kutofautiana ni ki2 cha kawaida. Ni chama gani cha upinzani kiliwahi kuwa na mafanikio na umoja wa aina hii katika nchi hii? CHADEMA is still strong na wasifikiri itaishia hapa , we wont stop mpaka haki itakapopatikana.