Mohamedi Mtoi
R I P
- Dec 11, 2010
- 3,321
- 6,327
Tangu kale katabia ka wanasiasa kuhama chama kimoja na kujiunga na chama kingine ni jambo la kawaida sana katika siasa.
Duniani kote wanasiasa huyumba hufuata upepo wa kisiasa. ikiwa upepo utaonesha chama fulani kina mvuto, basi wengi watajiunga, lakini upepo huo wa kisiasa ukisimama au kubadili uelekeo nao pia hubadilika.
upepo wa kisiasa kuwakumba wanasiasa vibaraka, vigeugeu na wasaliti ambao ni rahisi kurubuniwa au kuhongwa na vyama nyenye ukwasi. Vibaraka huwa hawana msimamo, wao hufuata mkumbo au watu ila wenye msimamo hufuata sera za chama.
Ndiyo maana hatushangai hiki kinachoonekana katika chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kwa baadhi ya wanachama kujiondoa na kujiunga na CCM. Kati ya mwaka 2010 na 2012 tena baada ya CCM kupata ushindi mnono, tulishuhudia mamia kwa maelfu ya wanasiasa wakihama na kujiunga na CHADEMA.
Tulidhani, wakati ule walikuwa wanafuata sera za chama hicho, lakini baada ya kuzuka usaliti ndani ya chama na wasaliti kuondolewa tumeshuhudia watu wakihama CHADEMA na kujiunga na CCM.
Hiyo ni haki yao ya kidemokrasia lakini hali ilivyo inaelekea CHADEMA ilikuwa imebeba mamluki, wasaliti na vibaraka. Maana kama si vibaraka inakuwaje kusimamishwa (Sio kufukuzwa) viongozi watatu kuibue wimbi la wanachama kujitoa na kujiunga na CCM?
Je, viongozi hao wakikiri makosa wakasamehewa na kurejeshewa vyeo hao waliojiunga na CCM watarudi tena CHADEMA? Haiwezekani siyo?
Kama si vibaraka ni nani? kwa nini waliohama wanatoa matamko ya kuzuia ziara za mikoani zilizoandaliwa na viongozi na viongozi wa CHADEMA makao makuu wakati hawahusiki?
Kama si vibaraka ni nani? kwa nini waliohama wanatoa matamko ya kuzuia ziara zinazoandaliwa na viongozi wa CHADEMA makao makuu wakati hawahusiki?
Kama si vibaraka kwa nini waliohama wako mstari wa mbele kuandamana na kutishia kuwadhuru viongozi wa chama kisichowahusu?
Kama CHADEMA kimekwisha hakina sera kwa nini waliohama wanavamia na kuchoma ofisi za chama kilichokwisha?
Mwanachama anayejua anachosimamia hawezi kuwa mgomvi, kuanzisha vurugu kufanya hujuma kama kuchoma ofisi. hujuma hizi zinawafunua kuwa wao ni vibaraka.
CHANZO: Mawio Uk 6.